Kuswali kwa kukaa bila udhuru

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuswali kwa kukaa bila udhuru

Question

Je, inajuzu kwa mtu kuswali akiwa amekaa bila ya kuwa na udhuru unaomzuia kusimama wakati wa Swala?

Answer

Swala tano ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu ambazo ni lazima kwa Muislamu kuzichunga na asizicheleweshe kutoka katika wakati wake; Mwenyezi Mungu anasema: “Na wale ambao Swala zao wanazilinda” [Al-Mu’minun: 9].

Kusimama katika Swala za faradhi ni nguzo miongoni mwa nguzo za Swala, na haijuzu kwa mtu kuiacha bila udhuru. Hata hivyo, inajuzu kuacha kusimama katika Swala za faradhi kwa sababu ya udhuru kama vile ugonjwa au mashaka makubwa yasiyovumilika. Vilevile, inajuzu katika Swala za Sunna kuswali ukiwa umeketi, lakini mtu hupata nusu ya dhawabu za aliyesimama ikiwa ana uwezo wa kusimama.

Maelezo

Ni jambo lililothibiti kisharia kuwa Swala ndiyo nguzo ya Uislamu na ni nguzo ya pili baada ya Shahada mbili. Mwenyezi Mungu Anasema: {Na simamisheni Sala (Enyi Mayahudi) na toeni Zaka na inameni pamoja na wanaoinama (yaani kuweni Waislamu)}[AL Baqara:43:] na Mwenyezi Mungu Anasema: {Mwishapo kuswali kuweni mnamkumbuka Mwenyezi Mungu (vile vile) – msimamapona mkaapo na (mlalapo) ubavu. Na mtakapopata amani (mkawa katika salama, hapana vita), basi simamisheni Swala (kama desturi). Kwa hakika Swala kwa Waislamu ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi}[An-Nisaa: 103], Kutoka kwa Abdullah bin Umar (R.A). amesema: Mtume (S.A.W). amesema: ((Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kuhiji (Makkah), na kufunga mwezi wa Ramadhani) Imepokelewa na Bukhari.

Ni makubaliano ya Wanachuoni kuwa kusimama ni nguzo katika Swala ya faradhi kwa yule mwenye uwezo; kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu: "Na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu" [Al-Baqarah: 238].

Ama kuacha kusimama katika Swala kwa udhuru hukumu zake ni hizi:

Kwanza : Kunajuzu kuacha kusimama katika Swala kwa udhuru, katika hali zifuatazo:

Ikiwa mtu hawezi kusimama au kunakuwa uzito kwake  inajuzu kwake kuswali akiwa ameketi. Kutoka kwa Imran bin Husain (R.A). amesema: "Nilikuwa na ugonjwa wa bawasiri, nikamuuliza Mtume (S.A.W). kuhusu Swala, akasema: 'Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi ukiwa umeketi, na usipoweza basi kwa kulalia upande mmoja'" (Imepokelewa na Bukhari).

Katika Swala za Sunna : Inajuzu kuswali Swala za Sunna ukiwa umeketi; iwe ni chini au juu ya kitu kilichoinuka (kama kiti).  Kutoka kwa Amiri bin Radbia (R.A). amesema: “Nilimuona Mtume (S.A.W). anaswali juu ya mnyama wake, eneo aloelekea”. Hata hivyo, mwenye kuswali Sunna akiwa ameketi na hali ana uwezo wa kusimama, anapata nusu ya dhawabu za aliyesimama.

Pili: Haijuzu kuacha kusimama katika Swala ya Faradhi bila udhuru:

Hii ni kwa sababu asili ni kwamba mtu ni lazima atekeleze namna aliyoamrishwa kisharia kulingana na uwezo wake katika kila nguzo ya Swala. Kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A). (Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W). aliingia Msikitini, kisha akaingia mtu mmoja na kuswali, kisha akaja na kumtolea salamu Mtume (S.A.W). naye akaitikia salamu yake na kusema: "Rudi ukaswali, kwani hakika wewe hujaswali." Yule mtu akarudi na kuswali kama alivyoswali mara ya kwanza, kisha akaja na kumtolea salamu Mtume (S.A.W). naye akasema: "Rudi ukaswali, kwani hakika wewe hujaswali" - akamwambia hivyo mara tatu. Yule mtu akasema: "Naapa kwa Yule aliyekutuma kwa haki, mimi sijui vizuri zaidi ya hapa, basi nifundishe. Mtume (S.A.W). akasema: "Unaposimama kwa ajili ya Swala, piga Takbira (Allah Mungu Akbar), kisha soma kile kilicho chepesi kwako katika Qur`ani. Kisha rukuu mpaka utulie katika rukuu yako, kisha inuka mpaka ulingane sawa ukiwa umesimama, kisha sujudu mpaka utulie katika sijda yako, kisha inuka mpaka utulie ukiwa umeketi, na ufanye hivyo katika Swala yako yote.")) Imepokelewa na Al-Bukhari.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Swala tano ni nguzo ya Uislamu: Ni lazima kwa Muislamu kuzilinda na asizicheleweshe kutoka katika wakati wake. Mwenyezi Mungu anasema: “Na wale ambao Swala zao wanazilinda” [Al-Mu’minun: 9].

Kusimama ni Nguzo: Katika Swala ya faradhi, kusimama ni nguzo na haijuzu kuiacha bila udhuru.

Urahisi wa Sharia: Inajuzu kuacha kusimama katika Swala za faradhi kwa sababu ya udhuru kama ugonjwa au mashaka yasiyovumilika.

Swala za Sunna: Inajuzu kuswali Swala za Sunna ukiwa umekaa, lakini utapata nusu ya dhawabu za aliyesimama ikiwa una uwezo wa kusimama.

Share this:

Related Fatwas