Urafiki na Wasio Waislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Urafiki na Wasio Waislamu

Question

Tangu miaka mingi iliyopita nina rafiki yangu mpenzi, naye ni mkiristo. Niliposilimu na kuwa Muislamu, rafiki yangu aliendelea kuwa na urafiki kwangu kutokana na jambo hilo, na wala hakubadilisha mtangamano wake wa upendo nami. Na mimi nimesoma katika Qur’ani Tukufu kwamba Muislamu haruhusiwi kuwa na urafiki na Mkristo, ni nini hasa maana ya neno la Kiarabu “wali” katika muktadha huu?

Sitaki kuvunja urafiki kwa sababu mbili:

Kwanza: sisi tupo moja tangu tulipokuwa wadogo, na si rahisi kuweka uhusiano kama huo kando. Hisia za kweli, za dhati zina nafasi kubwa hapa.

Pili: mimi katika urafiki huo, nina nafasi ya kuzungumza naye kuhusu Uislamu. Iwapo nitakatisha uhusiano huo sasa, rafiki yangu atahuzunika sana na anaweza kuwa na mtazamo mbaya na kuhusu Waislamu. Hii ina maana kwamba ninaweza kuokosea Uislamu kwa kuukata urafiki huo.

Pia nimesoma kwamba Mtume Muhammad hakuwahi kukata uhusiano wake na ami yake Abu Talib hadi kifo chake na kwamba alimpenda, ingawa hakusilimu.

Kwa hivyo basi, namomba mnijulishe kama inajuzu kuendelea urafiki na mkiristo huyo au hapana?

Natanguliza shukrani kwa jibu lenu, na nawatakia kila la kheri.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

        Ewa ndugu yetu:

Kwa hakika, asili ya hukumu katika uhusiano baina ya Waislamu na wasio Waislamu ni kuishi pamoja na wala sio mgongano na uadui, na jambo hili linakusanya aina zote za mahusiano ya kibinadamu, kama vile kushirikiana na kusaidiana kiujenzi ngazi ya mtu mmoja mmoja na ngazi ya watu wote.

        Ama kwa upande wa ukaribu uliozuiliwa na Mwenyezi Mungu kwa wasiokuwa Waislamu ni ule ambao unakusanya mapenzi ya dini ya asiyekuwa Muislamu. Ama kwa upande wa mtangano mzuri, wema na ukarimu pamoja na tabia njema, hivi vitu ni katika mambo ambayo Muislamu ameamrishwa kujipamba nayo na kuwatendea walimwengu wote.

        Na kwa hivyo basi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Qur`ani Tukufu: {Na semeni na watu kwa wema} [AL BAQARAH 83], Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema pia: {Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.(8). Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu. (9)} [AL MUMTAHINAH 8,9]

        Basi ewe ndugu yangu, endeleza urafiki wako na rafiki yako mkiristo, na uzifanye tabia zako za kiislamu kuwa ndizo unazozitumia pale unapouzungumza naye kuhusu Uislamu kama walivyokuwa wakifanya wale wema waliotutangulia.

        Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas