Hukumu ya kushiriki katika uchaguzi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kushiriki katika uchaguzi katika nchi zisizo za Kiislamu

Question

Hebu tafadhalini niambie kwa mfano Wanazuoni wa uraia mbalimbali walioruhusu kushiriki kwenye shughuli za Demokrasia na Uchaguzi, iwapo itachangia kukuza Uislamu!

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Hili ni suala linalohusiana na maslahi ambayo Waislamu wanaweza kuyapata kutokana na shughuli hizo, na Halmashauri ya Fiqhi ya Kiislamu lilitoa Fatwa iliyoandikwa na kutolewa katika toleo lake la 19 lililofanyika kwenye Makao ya Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu, mjini Makka, hapo tarehe 22-26 Shawali 1428 H.J. / 3-7 Novemba 2007 B.K., ambapo suala hilo la: “Hukumu ya Muislamu kushiriki kwenye uchaguzi pamoja na wasio Waislamu katika nchi zisizo za Kiislamu” nalo ni mojawapo ya masuala yaliyoahirishwa kutoka toleo la 16 lililofanyika hapo tarehe 21-26 Shawali 1422 H.J. kwa ajili ya kuendelea kulijadili, na baada ya kusikiliza uwasilishaji wa tafiti, mijadala na mahojiano yaliyotolewa kuhusu suala hilo, Baraza la Halmashauri lilipitisha yafuatayo:

Kushiriki kwa Muislamu kwenye uchaguzi pamoja na wasio Waislamu katika nchi zisizo za Kiislamu ni miongoni mwa masuala ya Siasa ya Kisharia ambayo hukumu yake inatakiwa kuzingatia kuhakikisha maslahi na kuzuia ufisadi, kwa hiyo Fatwa yake hutofautiana kutokana na kutofautiana kwa wakati, hali na mahali.

Muislamu anaye haki ya kutambuliwa kuwa ni mwananchi wa nchi isiyo ya Kiislamu anaruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi wa Bunge na mfano wake kwa kuwa maslahi yanatarajiwa kuhakikishwa kupitia kushiriki kwake ni kati ya maslahi yanayotarajiwa; kama vile; kutoa taswira sahihi ya Uislamu, kutetea masuala ya Waislamu katika nchi husika, kuchangia kuhakikisha maslahi ya walio wachache kidini na kidunia, kuimarisha nafasi na athari ya walio wachache katika jamii, kushirikiana na wenye misimamo wastani na wa kutetea haki kwa lengo la kuhakikisha ushirikiano wa kufanikisha haki na uadilifu, hayo kwa mujibu wa vidhibiti vifuatavyo:

Kwanza: Muislamu atakayeshiriki awe na nia ya kuchangia kuhakikisha maslahi ya Waislamu na kuwazuilia madhara na ufisadi.

Pili: Muislamu atakayeshiriki awe anataraji kupata faida kwake na kwa Waislamu nchini humo, kwa kuimarisha nafasi yao katika shughuli za kisiasa na za kijamii, na kufikisha matarajio yao kwa watunga sheria na watawala wa nchi, na kulinda maslahi yao ya kidini na kidunia.

Tatu: Ushiriki wa Muislamu katika uchaguzi huo kusisababishe awe na mapungufu katika dini yake.

 

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas