Hukumu ya kusherehekea siku maalumu ya upendo
Question
Ni nini hukumu ya kuhusisha siku iwe sikukuu ya upendo? Tunaomba jibu lililo wazi kuhusu suala hilo!
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Watu kutenga siku maalumu kwa ajili ya kufufua upendo wa halali kati ya waume na wake siyo jambo haramu kisharia, kwani hakuna katika Sharia ya Kiislamu kilichokataza hilo. Hata hivyo, haifai kuuita “sikukuu”, bali inaweza kuitwa kwa mfano: “Siku ya Upendo”.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
