Hukumu ya kusherehekea siku ya Sham An-Nasim
Question
Je! Inajuzu kusherehekea siku ya Sham An-Nasim?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Sham An-Nasim ni desturi ya kitaifa ya Wamisri ambayo haina chochote cha matambiko yanayokiuka Sharia ya Kiislamu. Imekubalika kuwa mila na desturi zinajuzu maadamu hazipingani na misingi ya Sharia ya Kiislamu. Na kuhusu yanayosemwa kuwa sherehe hii ina asili zinazopingana na Uislamu – hilo halina athari yoyote katika hukumu ya sasa; kwa kuwa asili hizo zimesahaulika, na kilichosalia ni desturi ya furaha, matembezi, kufurahisha familia, na mengineyo yasiyokiuka Sharia ya Kiislamu.
Kilichoharamishwa ni yale yanayotokea katika baadhi ya mambo yanayoambatana na furaha hizi, kama kupitiliza mipaka ya Sharia ya Kiislamu na kutoka katika maadili ya Kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
