Hukumu ya mwanamke kufanya kazi kam...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya mwanamke kufanya kazi kama mwanamitindo (Model)

Question

Ni ipi hukumu ya mwanamke wa Kiislamu kufanya kazi kama mwanamitindo - Model)?

Answer

Hijabu ya mwanamke wa Kiislamu ni wajibu wa kidini anapofikia umri wa kuwajibika (baleghe), hivyo ni lazima asitiri mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono. Haijuzu kwa mwanamke kuvua nguo zake au kuvaa baadhi ya nguo zinazofunua mwili wake kwa hoja ya kufanya kazi ya Uana Mitindo au uonyeshaji mavazi (model). Lakini ikiwa kazi ya mwanamke ni uoneshaji wa mavazi ya stara (hijabu), hilo ni jambo linalojuzu kisharia, lakini ni lazima mavazi hayo yatimize masharti ya hijabu ya kisharia, na mwanamke afuate na adabu pamoja na hulka ya haya wakati wa kuonesha mavazi hayo.

Ama ikiwa kazi ya mwanamke ni uoneshaji wa mavazi yanayofunua sehemu za mwili wake, basi ni lazima yatimie masharti haya yote:

Mavazi hayo yawe ni yenye kusitiri maeneo ya tupu nzito ya mwanamke.

Onyesho hilo liwe mbele ya wanawake pekee bila wanaume.

Hairuhusiwi kupiga picha onyesho hilo na kulisambaza, kwani jambo hilo ni haramu kisheria.

Maelezo

Hijabu[1] ni wajibu kwa kila mwanamke aliyefikia umri wa kuwajibika (baleghe), na jambo hili ni kwa mujibu wa makubaliano (Ijmaa) ya Wanachuoni.

Na umri wa kuwajibika: Ni umri ambao mwanamke anaanza kuona damu ya hedhi; basi kuanzia hapo ni lazima asitiri mwili wake isipokuwa uso na viganja vya mikono, na juu ya hili ndivyo Waislamu walivyofanya katika karne zote tangu enzi ya bwana wetu Mtume (S.A.W).

Na wanachuoni wote wanaona kuwa mwanamke anapofunua kile ambacho ni wajibu kwake kusitiri, basi amefanya jambo la haramu, na ni wajibu kwake kutubu kwa Mwenyezi Mungu kutokana na jambo hilo. Hivyo, hukumu ya faradhi ya hijabu — kwa maana hii iliyotangulia — imekuwa miongoni mwa misingi thabiti ya dini ya Kiislamu ambayo haibadiliki katika zama zote.

Na ushahidi wa faradhi ya Hijabu kwa mwanamke aliyebaleghe ni kama ifuatavyo:

1- Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.}[2] [Al-Ahzab: 59].

Sababu iliyopelekea kuteremka kwa Aya hii ni kwamba wanawake walikuwa wakionesha nywele zao, shingo zao, na sehemu ya vifua vyao; basi Mwenyezi Mungu (S.W.) Akawakataza jambo hilo, na akawaamrisha kuteremsha majilbab juu ya maeneo hayo waliyokuwa wakiyafunua[3].

2-Kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao,na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao[4] juu ya vifua vyao[5], wala wasionyeshe uzuri wao ila kwawaume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, auwatoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, auwana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawakewenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, auwafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambaohawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chinimiguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Natubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ilimpate kufanikiwa} [Al-Nur: 31].

Aya hii tukufu imewakataza wanawake Waumini kuonyesha mapambo yao, na ikavua mapambo ya dhahiri ambayo inajuzu kwa mwanamke kuyafunua, nayo ni: Uso na viganja vya mikono[6].

3- Kutoka kwa Bi. Aisha (R.A.): “Kwamba Asmaa bint Abi Bakr al-Siddiq (R.A.) aliingia kwa Mtume (S.A.W) akiwa amevaa nguo nyepesi, Mtume (S.A.W.) akampa mgongo na akasema: Ewe Asmaa! Hakika mwanamke anapofikia umri wa kupata hedhi, haifai kuonekana kwake chochote isipokuwa hiki na hiki” na akaashiria uso wake na vitanga vyake vya mikono. (Imepokelewa na Abu Dawood).

4- Kutoka kwa Aisha (R.A.): “Kwamba Mtume (S.A.W) aliingia kwake, basi kijakazi wake mmoja akajificha. Mtume (S.A.W) akauliza: Je, ameshaanza kupata hedhi? Akasema: Ndiyo. Mtume akamchania sehemu ya kilemba chake na akasema: Jifunike kichwa kwa hichi” (Imepokelewa na Ibn Majah). Hadithi hizi mbili zinaonesha kuwa hijabu ya mwanamke ni wajibu wa kisheria kwake anapofikia umri wa kuwajibika.

5- Umma wa Kiislamu umekubaliana juu ya uwajibu wa hijabu kwa mwanamke aliyebaleghe, kwa kusitiri mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono. Hivyo basi, ushahidi huu wote wa kisharia unaonyesha kuwa hijabu ya mwanamke ni faradhi kwake pindi anapofikia umri wa kuwajibika (baleghe). Ama kuhusu kazi ya mwanamke kama mwanamitindo (model), jambo hilo lina ufafanuzi kama ifuatavyo:

Kwanza: Ikiwa kazi ya mwanamke ni uoneshaji wa mavazi maalumu ya stara (hijabu): Hukumu yake ni kwamba inajuzu na haina kizuizi, lakini ni lazima masharti yafuatayo yatimie:

Mavazi hayo yawe ni yenye kusitiri kile ambacho ni wajibu kwake kusitiri, kama ilivyokwisha bainishwa hapo awali.

Mavazi hayo yasiwe yenye kuchora umbo la mwili, kiasi kwamba yakawa yanakusudia kudhihirisha mapambo ya mwanamke kwa namna inayoharibu maana ya hijabu na lengo lake.

Mwanamke achunge na adabu pamoja na maadili wakati wa kuonesha mavazi hayo; hivyo haifai njia yake ya uonyeshaji iwe na aina yoyote ya uvunjifu wa hayaa, bali anapaswa kuwa na haya (staha) katika mwendo wake na mfano wa hayo.

Pili: Ikiwa kazi ya mwanamke ni uoneshaji wa mavazi yanayofunua mwili wake: Hukumu hapa inatofautiana kulingana na hali mbalimbali, kama ifuatavyo:

Hali ya Kwanza: Mavazi hayo yawe ni yenye kufunua mapambo na tupu ya mwanamke. Hukumu yake: Ni haramu kisheria; kwani hata maharimu wa mwanamke kama vile baba, mtoto wa kiume, na kaka hawaruhusiwi kuyaona maeneo hayo ya mwili wake, na badala yake inajuzu kuyafunua maeneo hayo mbele ya mume wake tu.

Hali ya Pili: Mavazi hayo yawe ni yenye kufunua baadhi ya sehemu za mwili wa mwanamke bila kudhihirisha mapambo yake (maeneo nyeti). Hukumu yake: Inajuzu kufanya hivyo mbele ya wanawake pekee bila wanaume, lakini ni lazima masharti yafuatayo yatimie:

Mavazi hayo yawe ni yenye kusitiri maeneo ya tupu nzito ya mwanamke.

Hairuhusiwi kupiga picha onyesho hilo na kulisambaza, kwani jambo hilo ni haramu kisheria.

Tunapata faidia Kutokana na yaliyotangulia:

1- Hijabu ya mwanamke wa Kiislamu ni wajibu wa kidini anapofikia umri wa kuwajibika (baleghe), nayo ni kusitiri mwili wake wote isipokuwa uso na vitanga vya mikono.

        2-Haijuzu kwa mwanamke kuvua nguo zake au kuvaa baadhi ya nguo zinazofunua mwili wake kwa hoja ya kufanya kazi ya uonyeshaji mavazi (model). Kwani hata maharimu wake kama baba, mtoto wa kiume, na kaka hawaruhusiwi kuyaona maeneo ya mapambo (fitna) mwilini mwake; bali hayo ni kwa ajili ya mume wake pekee, au kwa dharura kama vile matibabu mbele ya daktari mwaminifu na anayeaminika.

         3-Inajuzu kwa mwanamke kufanya kazi ya uonyeshaji wa mavazi ya stara (hijabu), lakini ni lazima masharti ya hijabu ya kisheria yatimie katika mavazi hayo anayoyaonyesha, na mwanamke achunge adabu pamoja na hulka ya hayaa wakati wa uonyeshaji wa mavazi hayo.

Haijuzu kwa mwanamke kufanya kazi ya uonyeshaji mavazi yanayofunua mwili wake mbele ya wanaume wa kando. Lakini inajuzu kufanya hivyo mbele ya wanawake pekee, kwa sharti la kutodhihirisha chochote katika tupu yake nzito (awra mughalladha), na kutotangaza wala kupiga picha onyesho hilo.

 

[1] «Hijabu»: Ni kile kinachositiri mwili wa mwanamke isipokuwa uso wake na vitanga vyake vya mikono.

[2] «Jilbab»: Nguo inayofunika mwili wa mwanamke.

[3] Tafsir Muqatil bin Sulayman (3/508).

[4] «Khimar»: Nguo ambayo mwanamke hufunika kichwa chake, wingi wake ni 'khumur'.

[5] «Juyub»: Yaani kifua na nahr (shingo), na nahr ni sehemu ya chini ya koo.

[6] Al-Hidayah ila Bulugh al-Nihayah cha Al-Qurtubi (8/5071).

Share this:

Related Fatwas