Udhu Baada ya Upasuaji wa Leza na Upasuaji wa Macho
Question
Nimefanyiwa upasuaji wa jicho kwa njia ya leza ili niweze kuona vizuri, na daktari bingwa amenikataza kufikisha maji ndani ya jicho na juu ya jicho kwa siku kadhaa. Naomba maelezo ya kisharia kuhusu namna ya kupata udhu katika hali hii.
Answer
Kutia udhu kwa aliyefanyiwa upasuaji kwa njia ya leza au upasuaji wa kawaida wa macho kuna hali tatu:
Hali ya Kwanza: Ikiwa hatadhurika kwa kumiminia maji juu ya jicho lake huku likiwa limefumbwa, basi inamtosheleza kumiminia maji kwa namna hiyo bila ya kulazimika kulifungua jicho.
Hali ya Pili: Ikiwa atadhurika kwa kumiminia maji juu ya jicho lake hata likiwa limefumbwa, lakini haidhuru akilipangusa, basi inamlazimu kulipangusa moja kwa moja endapo anaweza kufanya hivyo, au kulipangusa juu ya kizuizi kilichowekwa, kama plasta ya kitabibu na mfano wake.
Hali ya Tatu: Ikiwa atazuiwa kufikisha maji kabisa, iwe kwa kuosha au kwa kupangusa, basi kupangusa kunaondoka kama ilivyoondoka kwa kuoga kwa sababu ya dharura. Inatakiwa aoge au apanguse sehemu zilizo karibu na jicho lake katika sehemu ya uso iliobaki kwa kadiri anavyoweza na uwezo wake.
Maelezo
Imethibiti kisharia kwamba udhu ni sharti miongoni mwa masharti ya kusihi kwa Swala, na kwamba kuosha uso ni nguzo miongoni mwa nguzo zake ambazo Swala haiwi sahihi bila ya hilo. Hili limethibiti katika Qur’ani Tukufu, Hadithi za Mtume (S.A.W) na Ijmaaʿ:
Kutoka katika Qur’ani Tukufu ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. } [Al-Maida: 6].
Na kutokana katika Hadithi: Hadithi iliyopokelewa na Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Uthman bin Affan (R.A): “Kwamba aliletewa chombo cha udhu, akamimina maji yaliyomo kwenye chombo hicho juu ya mikono yake, akaosha mara tatu, kisha akaingiza mkono wake wa kulia kwenye maji ya udhu, kisha akasukutua, akavuta maji mdomoni na puani na kuyatoa, kisha akaosha uso wake mara tatu, na mikono yake mpaka kwenye kongo mbili mara tatu, kisha akapaka kichwa chake, kisha akaosha kila mguu mara tatu. Kisha akasema: Nimemuona Mtume (S.A.W) akitia udhu mfano wa udhu wangu huu, na akasema: Atakaye tia udhu mfano wa udhu wangu huu, kisha akaswali rakaa mbili bila kujisemeza moyoni mwake, Mwenyezi Mungu atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia.”
Na imepokelewa kwa makubaliano (Ijmaa) kuwa kuosha uso ni faradhi miongoni mwa faradhi za udhu [1]
Kiwango cha uso kinachowajibika kuenezwa kwa kumiminia maji wakati wa kutawadha ni kuanzia maoteo ya nywele hadi kidevuni kwa urefu, na baina ya vinyama viwili vya masikio mawili kwa upana.
Na ndani ya mipaka ya uso huingia sehemu ya juu ya jicho ikiwemo kope na nyusi za macho, na ni lazima maji yazipate sehemu hizi zote wakati wa kutia udhu. Hili limekubaliwa na wanazuoni wa Fiqhi.
Kope ni wingi wa neno hudb nalo ni nywele zinazoota pembezoni mwa nyusi, na kope ni kifuniko cha jicho na kile kinachoonekana wakati wa kufumba macho.
Na pamoja na makubaliano ya wanazuoni kuwa sehemu ya juu ya jicho ni katika sehemu zinazowajibika zipate maji kwa kuoshwa hata kama ni ndani: wamesema wazi kuwa ndani ya jicho – ambalo hufunikwa na kope wakati wa kufumba macho – si wajibu kwa mwenye kutawadha kufikisha maji humo; kwa sababu kutia udhu kumejengeka juu ya kufikisha maji kwenye sehemu za nje ya mwili, na ndani ya jicho si katika sehemu za nje.
Na makusudio ya uso ni kile ambacho mtu hukabiliana nacho, na ndani ya jicho si sehemu ya uso inayokabiliana na mtu, pamoja na kwamba kufikisha maji ndani yake kunaleta taabu na mashaka makubwa.
Na kama ni hivyo, inaonekana kuwa iwapo mtu aliyefanyiwa upasuaji kwa njia ya leza au upasuaji wa kawaida wa jicho atawajibika kutia udhu au kuoga, lakini ikashindikana kwake kufikisha au kumimina maji juu ya sehemu ya juu ya jicho kwa muda fulani, na kwa mujibu wa ushauri wa daktari anayemhudumia ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea na kujikinga na athari za zinazoweza kutokea: Basi ni miongoni mwa kanuni zilizothibiti katika sheria ya Kiislamu kuwa madhara yameondolewa, na kwamba nafsi haikalifishwi isipokuwa kadri ya uwezo wake. hivyo, yeyote anayekalifishwa jambo miongoni mwa mambo ya faradhi kisha likawa gumu kwake kulitekeleza kwa dharura ya udhuru kama ugonjwa au mfano wake, kupitia ugumu huo atapewa wepesi ama kwa kupunguzwa kadri ya uwezo wake, au kwa kuruhusiwa kuliacha; kwa kuwa imeamuliwa kwamba “mashaka huleta wepesi”, na kwamba “kile kinachowezekana hakibatilishwi na kisichowezekana”, na kwamba “nyudhuru huathiri kwa kuleta wepesi katika ibada”. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: " Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo." {: Al baqara:286]
Na amesema: "Hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini." {Al Haj: 78}
Na kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A) kwamba Nabii Muhammad (S.A.W) amesema: “Nikikuamrisheni jambo, leteni (lifanyeni –kadiri ya ) muwezavyo.” wameipokea Hadithi hii Al-Bukhārī na Muslim.
Na kutoka kwa Abū Umāmah (R.A) kwamba Nabii Muhammad (S.A.W) amesema: “Nimetumwa kwa dini yenye unyofu na wepesi.” Ameipokea Imamu Ahmad katika Musnad.
Ama kuruhusiwa kwa kupunguza kwa yule anayeshindwa kumimina maji juu ya kiungo miongoni mwa viungo vya udhu: basi maandiko na mapokezi yanaleza kwamba mwenye kutokwa na udhu na akashindwa kumimina maji juu ya kiungo miongoni mwa viungo vya udhu au sehemu yake kwa sababu ya jeraha au ugonjwa uliompata, basi inamtosheleza katika hali hiyo kupangusa juu yake moja kwa moja au juu ya kile kilichowekwa juu yake kama plasta au kizuizi, pamoja na kuosha vilivyosalia miongoni mwa viungo vya udhu.
Na ipokewa Hadithi kutoka kwa Jābir bin ‘Abdillāh (RA) kwamba amesema: “Tulitoka katika safari, mtu mmoja kati yetu akapigwa na jiwe likampasua kichwa, kisha akapatwa na janaba, akawauliza wenzake: Je, mnanipatia ruhusa ya kutayamamu? Wakasema: Hatupati ruhusa kwako ilhali una uwezo kutumia maji. Basi akaoga, akafa. Tulipofika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) ikaelezwa habari hiyo, akasema: Wameua na Mwenyezi Mungu awaue! Kwa nini wasiulize walipokuwa hawajui? Hakika dawa ya kutojua ni kuuliza. Ilikuwa inamtosheleza kutayamamu, kisha akakamua au kufunga bandeji juu ya jeraha lake, kisha akapangusa juu yake na kuosha sehemu iliyosalia ya mwili wake.” Ameipokea Al-Dāraqutnī katika Sunan.
Na wameeleza wazi Jamhuri ya Wanazuoni wengi kutoka Madhehebu ya Imamu Hanafi, Maliki na Hanbali kwa kauli sahihi kwamba mwenye kuogopa madhara iwapo maji yatapita juu ya jeraha lake au sehemu ya ugonjwa wake wakati wa kutia udhu: basi inamtosheleza wakati huo kupaka juu ya sehemu hiyo au juu ya kilichoambatana kama plasta au kifuniko /kizuizi kingine, na ataosha sehemu iliyo salama ya kiungo hicho pamoja na viungo vingine vyote ambavyo ni lazima kuvisafisha. Na wamesema Imamu Hanafi katika kauli ya Madhehebu na Maliki kwamba sharti ni kwamba kiasi ambacho kitapakwa kiwe kidogo kuliko kiungo kitakachooshwa katika viungo vingine vinavyowajibika kuoshwa, kama katika suala letu hili; ambapo inashindikana kwake kuosha macho yake tu. Wala haijumuishwi wakati huo kati ya kutayamum na kutumia maji; kwa sababu vyote viwili ni mbadala, na havikusanywi pamoja.
Ama kuhusu ruhusa ya kuacha (kuosha): Ikiwa mwenye jeraha atashindwa kuweka kifuniko / kizuizi juu ya jeraha lake ili apanguse juu yake, inajuzu kwake kuacha kuosha sehemu hiyo ya kiungo, na udhu wake utakuwa sahihi kwa mujibu wa dhahiri ya maandiko na mapokezi, na huu ndio msimamo wa Imamu Hanafi.
Katika riwaya ya Ibn ‘Abbas (RA): “Kwamba mtu mmoja alijeruhiwa kichwani wakati wa Mtume (S.A.W), kisha akapatwa na janaba, akaamrishwa kuoga, akaoga, akapatwa na ugonjwa wa tetanasi na akafa. Tukamfikishia habari hiyo Mtume (S.A.W), akasema: Wamemuua, na Mwenyezi Mungu awaue! Je, si tiba ya ujinga ni kuuliza?!” ‘Ataa alisema: Na imetufikia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) alisema: “Lau angeuosha mwili wake, na akaacha kichwa chake mahali ambapo kilichojeruhiwa.” Na kuzāz ni ugonjwa unaotokana na baridi kali (Kifafa cha misuli), na imesemwa: ni baridi yenyewe. Wameipokea Hadithi hii Ma-Imamu: Abū Dawud na Ibn Majah katika Al-Sunan (na lafudhi ni ya Ibn Majah), na Ahmad na Abu Ya‘la Al-Mawṣili katika Al-Musnad, na Al-Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra na Al-Sunan As-Ṣughra, na Al-Ḥakim katika Al-Mustadrak.
Na kutoka kwa Nafi kutoka kwa Ibn ‘Umar (RA): kwamba alikuwa akisema: “Ikiwa hakuna bandeji juu ya jeraha, ataosha sehemu inayolizunguka na asioshe sehemu yenyewe.”
Ameipokea Al-Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra, na ametaja Al-Kirmani katika Masā’ilihi, na Ibn Al-Mundhir katika Al-Wasat.
Na wanazuoni wa Maliki wameafikiana na Hanafi hasa pale inaposhindikana kupaka juu ya kiungo kilichoathirika na kiungo hicho kikawa miongoni mwa viungo vya kutayammum, kama kope za jicho; kwa sababu kushindikana kupaka humo kunapatikana katika kutayamum kama ilivyo katika udhu, hivyo haimi katika kiungo hicho kwenda kwenye tayamum; kwani hali zote mbili zitakuwa pungufu, na udhu pungufu ni bora kuliko tayamum pungufu[3].
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kwamba udhu ni sharti miongoni mwa masharti ya kusihi Swala, na kwamba kuosha uso ni nguzo miongoni mwa nguzo zake na haisihi bila ya hilo.
Yeyote atakayepata madhara kwa kumiminia maji kwenye jicho lake hata akiwa amelifumba, basi ni wajibu kwake wakati huo kupaka jicho moja kwa moja iwapo ataweza kufanya hivyo, au kupangusa juu ya kuzuizi kilichowekwa juu yake kama plasta ya tiba au mfano wake.
Ikiwa daktari atamzuia mgonjwa kufikisha maji kabisa, iwe kwa kuosha au kupaka, basi hutoshelezwa kwa kuacha kupaka kama ilivyoachwa kuosha kwa dharura, na inapasa kuzingatia kuosha au kupaka sehemu zinazozunguka jicho kutoka katika sehemu ya uso kadiri ya uwezo wake na uweza wake wa kufanya hivyo.
[1] Ang. “At Tamhid” (4/31. Chapa Awqf Al Maghrib).
[2] Nyongo: ni kile kilicho ndani ya tumbo la kila kiumbe hai. Imeitwa hivyo kwa sababu ya uchungu wa maji ya kijani yaliyomo ndani yake. Ama kinachokusudiwa hapa ni kwamba aliifanya kama bandeji ya kidonda.
[3] Mawahib Jaleyl (1/363).
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
