Hukumu ya kuachia mikono katika Swa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuachia mikono katika Swala

Question

Nilipokuwa naswali siku moja Msikitini nilikuwa naachia mikono nikiwa nimesimama, baada ya kumaliza kuswali akanijia mtu mmoja na akaniambia: kwanini huweki mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika Swala? Nikamwambia: mimi naswali hivi tangu nilipoanza kuswali. akasema: kufanya hivi ni kinyume na Sunna. Ni upi usahihi wa maneno haya? Je, Swala yangu ni sahihi?

Answer

Kuachia mikono miwili katika Swala kunajuzu kisharia, na hili ni katika Sunna, na hili ni katika mambo ya mwisho aliyokuwa akiyafanya Mtume (S.A.W) na watu wa madina wamefuata hilo, na hili linafuatwa na Madhehebu ya Maliki na wanaowaunga mkono, na si sahihi kauli ya kwamba ni kinyume na Sunna.

Maelezo

Matendo katika Swala yapo aina mbalimbali, miongoni mwao ni faradhi au nguzo, na miongoni mwao Sunna au yanayopendeza, na miongoni mwao ni fadhila ambazo yanajulikana kama mapambo. Ama faradhi: Ni zile ambazo zikiachwa kwa makusudi au kwa kusahau haziungwi na sijida ya kusahau, wala kitu chochote katika Sunna. Ama Sunna: Ni zile ambazo zinasuniwa ambazo hazilazimu sijida ya kusahau, na pia huitwa Sunna za Ab’aadh, ama fadhila au mapambo: Ni zile zinazosuniwa ambazo hazilazimu sijda ya kusahau, mwenye kuziacha kwa kusahau, hakuna wajibu wowote kwake.

Na miongoni kwa mapambo: Ni hali ya kuweka mikono miwili wakati wa kusimama kwa kusoma au kumsikiliza Imamu, na Wanazuoni wa Fiqhi ametofautiana katika hukumu yake na aina yake, na jamhuri ya Wanazuoni wa Fiqhi wa Imamu Hanafi na Shafi na Hanbali wamekubaliana kwamba hali ya kuweka mikono miwili wakati wa kusimama kwa kusoma au kumsikiliza Imamu, kukunja mikono, kwa maana kuweka mkono wa kuume juu ya mkono wa kushoto, kwa kutofautiana sehemu zake, juu ya kifua au chini yake, kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto au kuweka kwa hali yoyoyte na mfano wake.

Madhehehbu ya Imamu Maliki wameeleza kuwa hukumu ya kukunja mikono wakati wa kusimama kuna kauli nne:

Kwanza: Kwamba kuachia mikono ndio sahihi na kukunja mikono ni makuruhu katika Swala ya faradhi, na wamejuzisha katika Swala ya Sunna wakati wa kurefusha kisomo, na hili ndio linalofuatwa katika Madhehbu yao, pamoja na kutofautiana na ufafanuzi katika sababu ya kauli hiyo, je, chukizo kwa sababu ya kutopitishwa, au kwa kutofautiana itikadi ya namna yake na kupasa kwake kwa ujumla, au kuhofia kudhihiri kwa mandhari ya kukunyenyekea kwa kuzuia ria.

Pili: kwamba kunakatazwa kufunga Swala katika Swala ya faradhi na Sunna, na haya ni Madhehebu ya watu wa Iraq.

Tatu: kunajuzu kufunga Swala katika aina zote mbili, na hili wamekubaliania jamhuri ya Wanazuoni.

Nne: Ni chukizo katika Swala ya faradhi, na kunajuzu katika Swala ya Sunna ndefu au fupi[1].

Aboubarakat Al Derdeer ameeleza kwamba chukizo kukunja akiwa hakukusudia Sunna, akikusudia hilo na hakukusuidia kupitishwa basi si chukizo, na asili ya kauli ya Madehehbu ya Malik kuwa kunapendeza kuacahia mikono katika Swala ya faradhi. Chukizo ya kufunga  Swala: yaliyopokewa katika Hadithi ya Abou Hamid Al Saaidy (R.A) amesema “Mimi ni mjuzi zaidi kati yenu wa Swala ya Mtume (S.A.W,) wakasema: Kivipi? Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu hukuwa unafuatana zaidi na Mtume kuliko saisi na wala Sahaba wa zamani kuliko sisi, akasema: ni kweli, wakasama: eleza, akasema: “Mtume (S.A.W) alikuwa akisimama katika Swala ananyanyua mikono yake mapaka usawa wa mabega, kisha anasoma Takbira mpaka kila kiungo kitulie sehemu yake” Imetolewa na Maimamu wa Hadithi: Abou Daoud, Al tirmidhy na Ibnu Maja kati a Al sunan.

Sehemu ya dalili katika Hadithi hii ni kwamba baada kubainisha kunyanyua mikono miwili katika Takbiir Abou Hamdy Al Assdy amebainisha kuwa Mtume (S.A.W) alikuwa akirudisha kila kiungo katika sehemu yake, na sehemu asili ya mikoni miwili ni kuiachia usawa wa mapaja si kuikunja, hii imejulisha kwamba kitendo chake Mtume (S.A.W) kilikuwa ni kukunja.

Na miongoni mwa dalili zinaruhusu kuachia pia ni: Hadithi iliyotolewa na Bukhary na Muslim kutoka kwa Abouhurayra (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) aliingia Msiktini, akaingia mtu, akaswali, akamsalimia Mtume (S.A.W,) akamjibu na akasema” Rudia kuswali kwani haujaswali Swala sahihi” akarudia akaswali kama alivyosali, kisha, akamsalimia Mtume (S.A.W) akasema” Rudia kuswali kwani haujaswali Swala sahihi” akafanya hivyo mara tatu, kisha akasema: Naapa kwa aliyekutuma kwa Haki (Anaapa kwa Mwenyezi Mungu) siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivi, nifundishe, akasema: “Ukisimama kwenye Swala, soma Takbira, kisha soma sehemu ndogo ya Qur’ani, kisha rukuu mpaka utulizane, kisha nyanyuka mpaka usimame sawa, kisha sujudu mpaka utulizane, kisha nyanyuka mpaka utulizane, na fanya hivyo katika Swala yako yote”.

Sehemu ya kutolea dalili Hadithi hii ni kuruhusiwa kuachia mikono katika Swala na kutokunja: ni kwamba Mtume (S.A.W) hakumuamrisha Sahaba kukunja mikono baada ya Takbira ya kuhirimia wakati wa kuisoma, na lau kama kufunga Sala kungekuwa lazima au Swala haisihi isipokuwa kwa kufunga mikono, Mtume (S.A.W) angemuamrisha, kinyume na hivyo basi ingekuwa kuchelewesaha ubainifu wakati wa hitajio, na kumehukumiwa kutocheleweshwa ubainifu wakati wa haja, katika hili kumejulikana kuruhusiwa kuachia mikono.

Miongoni mwa dalili za kuachia mikono miwili na kutokunja katika Swala: Ni kitendoa cha watu wa Madina, na hii ni katika dalili zinazoshikwa katika Madhehebu ya Malik, imetolewa na Abou Zaraa Al Demeshqy katika Taariikhihi amesema: Ameniahadithia Abdurrahama bin Ibrahim, kutoka kwa Abdallah bin Yahyaa Al maafiriy, kutoka kwa huweya kutoka kwa Bakr bin Amru: kwamba yeye hakuwahi kumuona katu Abou Umama -akimaaaisha Sahl- akiweka mkono wake mmoja juu ya mwingine, wala mtu yeyote katika watu wa Madina, mpaka alipofika Sham, akamuona Awzaii na watu wengine wanafunga mikono yao” na dalili ya hilo pia: kauli ya Imamu Malik katika Al Madwana: “Na wala sijui hilo katika Swala ya faradhi, na alikuwa analichukia”.

Wala haipingwi hilo kwamba Imamu Malik amepokea kutoka kwa Abdul Kariim bin Abou Al Makhariq Al Basary amesema:  “ Katika maneno ya Mtume (S.A.W) ikiwa huoni haya basi fanya unachotaka, na kuweka mikono miwili mmoja juu ya mwingine katika Swala, ni kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto” na hii ni dalili ya kufunga Swala, kwani Imamu Malik amepinga kama haya katika  Maisha yake, na jambo hili haliishii katika Hadithi hii tu, kuna Hadithi isemayo: “Wawili wanaouziana wanahiayari” kwani ameipokea Hadithi hii na hakuifanyia kazi, mtu mmioja akamuuliza hilo, akamwambia: “ili mjinga kama wewe ajue kuwa mimi nalijua na nimeliacha”.

Na kwa hili kunabainika kwamba Imamu Malik hakuacha Hadithi hii isipokuwa baada ya kutambua kitendo cha watu wa Madina cha kuachia mikono, na kwahivyo akachukia katika Swala ya faradhi si katika Swala ya Sunna, kama ilivyobainika hapo nyuma.

Imamu Shai amejuzisha kuachia mikono katika Swala na si chukizo ikiwa hakufanya mchezo, kama alivyojuzisha Imamu Ahmad katika riwaya yake kwa hali yoyote, na katika riwaya nyingine: kujuzu kuachia mikono katika Swala ya Sunna, si faradhi.[2]

Pia kuachia mikono katika Swala ni kauli ya Imamu Al Lithy bin Saad, na kumepokewa kwa zaidi ya mtu mmoja katika wema waliotangulia, katika simulizi ya Imamu bin Mundhir katika Al Awsat, masuala haya ni masuala yaliyotofautiana Wanazuoni ambayo yapo katika sehemu ya ruhusa, na Daraja yake ya juu ni kupendeza.

Na kunatakikana kutoyafanya masuala waliyotofautiana Wanazuoni kuwa chanzo cha kugawanyika na kutohitalifiana kati yao, ili wasiingie katika mfarakano uliokatazwa kisharia, imeafikiwa kisharia kwamba hukemewa walilokubaliana na wala halikemewei walilohitalifiana, na usahihi katika hilo ni kuwaacha watu katika mazoea yao: Anaetaka akunje mikono, na anaetaka aachie, na wote wapo sawa.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Vitendo vya Swala haviko katika aina moja, vipo ambavyo ni faradhi au nguzo, vipo ambavyo ni Sunna au vinapendeza, na vipo ambavyo ni fadhila na pia vinazingatiwa kuwa ni mapambo.

Kuachia mikono katika Swala ni katika masuala waliyotofautiana wanazuoni ambayo yapo katika kuruhusiwa na kupendeza, na sahihi katika hili ni kuwaacha watu katika mazoea yao: anaetaka akunje na anaetaka aachie mikono na wote wapo sahihi.

 

[1] Al Madwana 1/169. Al Dhakhira 2/228.

[2] Mughny Al Muhtaj 1/391. Al Insaaf 2/46.

Share this:

Related Fatwas