Hukumu ya Kupeana Mikono Baada ya Swala
Question
Je, nini hukumu ya kupeana mikono baada ya Swala baina ya waumini? Wapo baadhi ya watu wanaosema kuwa ni bid‘a kwa madai kwamba haikupokelewa kutoka kwa Mtume (S.A.W) wala Maswahaba zake watukufu, na kwamba inamshughulisha mswaliji na dhikiri za kumalizia Swala.
Answer
Kupeana mikono kumesuniwa kiasili katika Sharia tukufu, na kutekelezwa kwake baada ya Swala kumeingia katika ujumla wa uhalali huu; kwa hivyo ni jambo linaloruhusiwa au linalopendelewa. Hata hivyo si sehemu ya kukamilisha Swala. Na yule anayefuata rai ya kukarahishwa asizingatie tofauti za kifiqhi kwa namna inayozua fitna, kuwagawa Waislamu au kueneza uadui kwa kutopeana mikono na yule anayemnyooshea mkono wake baada ya Swala.
Maelezo
Imewekwa kisharia kuwa kusalimiana kwa kupeana mikono ni katika Sunna, ambayo dhambi hufutwa na madhambi husamehewa kwa tendo hilo.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Baraa’ bin ‘Azib (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: (Hakuna Waislamu wawili wanaokutana na kusalimiana kwa kupeana mikono, isipokuwa husamehewa kabla hawajafarakana) [Imepokewa na Ahmad, Abu Dawud, Tirmidhiy na Ibn Majah].
Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfa bin Al-Yaman (R.A) kwamba Mtume (S.A.W)) amesema ((Hakika Muumini anapokutana na Muumini mwenzake, akamsalimia na akashikana naye mikono, madhambi yao hupukutika kama yanavyopukutika majani ya mti) [Imepokewa na At-Tabaraniy na wengine].
Na imepokelewa pia kutoka kwa Mtume (S.A.W): (Salimianeni kwa kupeana mikono, chuki itaondoka; na peaneni zawadi, mtapendana na uadui utaondoka) [Imepokewa na Malik].
Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattab (RA) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: (Waislamu wawili wanapokutana na mmoja akamsalimia mwenzake, basi mpenzi zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni yule aliye na uso bora zaidi kwa mwenzake) [Imepokewa na Al-Bayhaqiy].
Dalili Hizi kwa pamoja zinathibitisha sunna ya kusalimiana kwa kupeana mikono na kuhimiza juu yake, na hili ndilo lililo juu ya rai ya wanazuoni wengi tangu zamani hadi sasa.
Kuhusu hukumu yake maalumu baada ya Swala: kwa kuwa amri ya kisharia imetaja ujumla wa Sunna kusalimiana kwa kupeana mikono kati ya watu kila wanapokutana, bila kuifungamanisha na muda fulani, inayoifanya hukmu hii kuingia katika kupeana mikono baada ya Swala tano au kila Swala. Na hili ndilo lililofahamika kwa Waislamu na kufanyiwa kazi na vizazi baada ya vizazi, bila kukemewa, na maneno ya Wanazuoni wa Madhehebu makuu yamethibitisha Sunna hii.
Ama kauli ya kutokuruhusiwa kwa madai ya kuwa ni bid‘a, hii ini kauli isiyokubalika kwa kuwa Wanazuoni wametofautiana katika maana ya bid‘a.
Baadhi, kama Imam ‘Izz Ad-Din bin ‘Abd As-Salam, wameona kwamba jambo lolote ambalo Mtume (S.A.W) hakulifanya ni bid‘a, na akalifanya linazunguka pamoja na hukumu tano (Wajibu, Haramu, Sunna, Makruh, Mubah).
Wengine wamehusisha bid‘a na ile tu iliyo haramu; nayo ni yale yasiyo na asili yeyote katika Sharia.
Hivyo basi, hata kama tukikubali kimjadala kwamba kupeana mikono baada ya Swala ni bid‘a, basi ni katika bid‘a iliyo nzuri au inayopendeleza, kwa kuwa kiasili kusalimiana kumesuniwa bila kikomo cha wakati.
Aidha, imepokelewa katika Hadithi kuwa Maswahaba walikuwa wakimsalimia Mtume (S.A.W) kwa kupeana mikono baada ya Swala, naye hakuwakataza. Mfano: Hadithi ya Abu Juhayfa (R.A) na Yazid bin Al-Aswad (RA) ambapo Maswahaba walikuwa wakishika mkono wa Mtume (S.A.W) baada ya Swala na kujipangusa nao.
Na kwa kuwa salamu na mapokezi baina ya Waislamu ni amri kila wanapokutana, basi hali ya anayeswali baada ya kuhitimisha Swala ni kama vile mtu aliyekutana na mwenzake tena baada ya kutengana; kwa hivyo kusalimiana kwa kupeana mikono kunasuniwa katika hali hii.
Wanazuoni waliosema ni chukizo walifanya hivyo kwa ajili ya kufunga njia ya watu kuamini kuwa ni sehemu ya Swala. Lakini hata wao wamethibitisha kuwa ukinyoshwa mkono basi haifai kukataa, kwa sababu ya kuvunja moyo wa Muislamu.
Imepokewa pia kuwa Mtume (S.A.W) amesema: (Hakuna Waislamu wawili wanaokutana, mmoja akashika mkono wa mwenzake na wakaomba dua pamoja, isipokuwa Mwenyezi Mungu huwa anakubali dua zao na hawaachani mikono yao mpaka awasamehe)) [Imepokewa na Ahmad na wengine].
Hii ndiyo ada iliyoenea kwa Waislamu – kuunganisha baina ya kusalimiana kwa kupeana mikono na dua baada ya Swala, kama kusema: Haramān au Jama‘an, au Taqabbala Allahu minnā wa minkum. Vyote hivi vina asili katika sharia na vimekusudiwa kueneza upendo na mapenzi baina ya Waislamu.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kusalimiana kwa kupeana mikono kumesuniwa kiasili katika Sharia.
Kusalimiana kwa kupeana mikono na kuomba dua baada ya Swala – kwa maneno kama Haramān, Jama‘an, au Taqabbala Allahu minnā wa minkum – vyote vina asili ya kisharia na vimependekezwa kwa lengo la kueneza mapenzi na kuimarisha undugu.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
