Kuweka kzuizi (Kitu chenye urefu wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuweka kzuizi (Kitu chenye urefu wa futi moja) mbele kwa anayeswali.

Question

Mtu yupo dukani anaswali peke yake, anauliza: je, analazimika kuweka kizuizi mbele yake akiwa anaswali?

Answer

Kunapendeza kwa mtu anayeswali kuweka kizuizi mbele yake akihofia kupita mtu mbele yake akiwa anaswali hali ya kuwa peke yake au yeye ndiye Imamu, asipohofia kutpita mtu mbele yake akiwa anaswali basi anaweza kuswali bila ya kuweka kizuizi, na hana dhambi na wala hakuna ubaya katika hilo.

Maelezo

Ni Sunna kwa anaeswali kuweka kizuizi mbele yake ili asipite mtu mbele yake; kwa Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Abou Saeed Al Khudry (R.A) amesema: amesema Mtume (S.A.W): “Akiswali mmoja wenu basi aswali na kizuizi, na akaribie” imetolewa na Maimamu wa Hadithi: Abou Daoud, Ibnu Majah, Bayhaqy katika Al Sunan.

Na imepokewa kutoka kwa Twalha bin Ubaydillah R.A amesema: Amesema Mtume (S.A.W): “Mmoja wenu akiweka mbele yake mfano wa kibao cha kukalia juu ya mnyama basi na aswali, wala asijali wanaopita nyuma ya kibao hiko” imetolewa na Imamu Muslim katika Sahihi yake.

Na imepokewa kutoka kwa Abouhurayra (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “atakaposwali mmoja wenu basi aweke mbele yake kitu, akikosa basi achomeke fimbo, akikosa basi achore mstari, kisha haidhuru atakaepita mbele yake” imetolewa na Maimau Hamdy, Is’haq na Ahmad katika Al Musnad, na Abou Dawoud na Ibnu Majah katika Al Sunan.

Wanazuoni wa Fiq’hi wamekubaliana kupendeza kuwaka Sutra mbele ya anayeswali ikiwa anaswali peke yake au anaswalisha watu akiwa Imamu, sawasawa alikuwa mkazi au msafiri, na baadhi yao wamenukuu makubalino ya hilo. Bidayat Al mujtahid, Al Majmouu.

Na Wanazuoni wa Fiqhi wametofautisha kati ya anayeswali anahofia kupita mtu mbele yake akiwa anaswali peke yake au Imamu, na yule asiehofia hilo:

Madhehebu ya Imamu Hanafi ambayo ni maarufu zaidi kuliko Madhdhebu ya Malik wanasema kwamba kunapendeza kuweka kizuizi ikiwa kunahofiwa kupita mtu mbele ya anayeswali, na hakuna ubaya kuacha kufanya hivyo ikiwa akuhofiwi kupita mtu mbele ya anayeswali, kama kuwa sehemu ambayo hakuna mtu yeyote zaidi yake, au katika sehemu ya mbele ambayo hawezi kupita mtu yeyote mbele yake[1].

Madhehebu ya Imamu Shafi na Hanbali na Malik katika kauli ya pili wanaona kunapendeza kuweka kizuizi katika hali yoyote, sawasawa kukikohofiwa kupita mtu mbele yake wakati wa Sawla au hakukohofiwa hilo[2].

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kupendeza kuweka kizuizi mbele kwa mtu anayeswali ikiwa anaswali peke yake au anaswalisha watu, kukihofiwa kupita mtu mbele wakati anaswali, kusipohofiwa kupita mtu mbele yake akiwa katika Swala yake, basi anaweza kuswali bila ya kuweka kizuizi na hakuna dhambi wala si vibaya.

 

[1] Ak Hidaya 1/63. Al Mawahib Al Jalil 1/532.

[2] Mawahib Al Jalil 1/532. Al Majmou 3/461.

Share this:

Related Fatwas