Je, dhambi huongezewa katika mwezi wa Ramadhani?
Question
Kuna mazungumzo yaliyojiri kati ya marafiki kuhusu kuongezwa dhambi kwa kufanyika mabaya/maovu katika mwezi wa Ramadhani, kama ilivyo katika kuongezwa mema kwa kufanya mema. Je, hili lina ukweli gani?
Answer
Dhambi huongezewa kama ilivyo kwa mema katika nyakati bora, kama mwezi wa Ramadhani, isipokuwa kwamba mema huongezewa kwa namna na kwa idadi, wakati dhambi huongezewa kwa namna bila ya kuongezewa kwa idadi. Yaani, katika ubora na uzito wake bila ya kuongezewa kwa idadi na kiasi.
Maelezo:
Hekima na Sunna (utaratibu) wa Mwenyezi Mungu umejiri katika kuvipendelea baadhi ya viumbe juu ya wengine. Amependelea jinsi ya mwanadamu, kutoka kwa wana wa Adam, juu ya viumbe vyake vingine, amemjaalia mwenye heshima na anayetunzwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.} [Al-Israa: 70]. Kisha akawachagua miongoni mwa kizazi cha Adam Manabii na Mitume, akawatumia Ufunuo wake na Ujumbe wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.} [Aali Imran: 33]. Upendeleo huo haukuishia kwa watu, bali ulijiri pia katika maeneo. Mwenyezi Mungu Ameipendelea Makka tukufu juu ya sehemu nyingine za ardhi, akaifanya kituo cha ardhi, na sehemu bora zaidi na tukufu zaidi. Na katika nyakati, kama siku ya Ijumaa, miezi Mitukufu na Mwezi wa Ramadhani. Na imewekwa kisharia kwamba mema huongezewa kwa anayeyafanya, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi} [Al-Baqarah: 245], na kauli yake Mtukufu: {Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi} [Al-An'aam: 160]. Na kuongezewa huzidi na thawabu huongezeka katika maeneo na nyakati bora kama Mwezi wa Ramadhani, kama walivyokadiria Wanachuoni wa Fiqhi kwamba dhambi pia huongezewa kwa sababu ya wakati na mahali bora kama mema.
Na hilo ni kwa kile kilichosimuliwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alisema: ((Hakika umati wangu hautaaibika maadamu wataisimamisha Saumu ya Ramadhani)). Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni aibu zipi katika kuupoteza Mwezi wa Ramadhani? Akasema: ((Kuvunja vitu vilivyoharamishwa ndani yake. Yeyote anayefanya uzinifu ndani yake au kunywa pombe, Mwenyezi Mungu anamlani, na kila aliyepo mbinguni mpaka mfano wake katika mwaka mzima. Na akifa kabla ya kuufikia Mwezi wa Ramadhani, hatakuwa na mema yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu ambayo atajikinga nayo na moto. Basi uogopeni mwezi wa Ramadhani, kwa sababu mema huongezewa ndani yake kiasi kisichoongezewa katika miezi mingine, na kadhalika madhambi)). Imepokelewa kutoka kwa At-Tabarani katika "Al-Mu'jam Al-Awsat" na "Al-Mu'jam Al-Sagheer", na Ibn Shahin katika "Fadhail Ramadhani", na Al-Asbahani katika "At-Targhib wal Tarhib". Isipokuwa kwamba mema huongezeka kwa namna na idadi, wakati dhambi huongezeka kwa namna bila ya idadi. Yaani, huongezeka katika ubora wake tu, na huwa zito katika maeneo na nyakati bora. Basi anayefanya dhambi katika Msikiti Mtukufu au katika mwezi wa Ramadhani, dhambi yake inakuwa nzito.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia;
Kwamba mema huongezewa kwa anayeyafanya, na kuongezewa huzidi na thawabu huongezeka katika maeneo na nyakati bora kama Mwezi wa Ramadhani.
Wanachuoni wa Fiqhi waliamua kwamba dhambi pia huongezewa kwa sababu ya wakati na mahali bora kama mema.
Mema huongezewa kwa namna na idadi, wakati dhambi huongezewa kwa namna bila ya idadi, yaani katika uzito wake bila ya kiasi na idadi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
