Kuzuia nafasi maalumu Msikitini
Question
Baahi ya watu katika Msikiti wa mji wetu wanaweka nafasi zao maalumu kwa kuweka msala au mfano wake, hasa katika safu ya mbele, kwa namna nafasi hiyo inakuwa ya kwao muda wowote wanapofika msikitini, je, inafaa kwao kufanya hivyo?
Answer
Baadhi ya watu kuzuia nafasi zao katika msikiti kwa kuweka msala au mfano wake ni haramu kisharia kwa makubaliano ya Wanazuoni wote wa Fiqhi, na bora zaidi kuacha kufanya hivyo isipokuwa kukiwa na manufaa yanayowapata Waislamu wote walio msikitini na hakuna madhara kwa yeyote kati yao, kama sehemu ya Imamu na muadhini, na vikao vya elimu na Fatwa na mfano wake, hapo hakutakuwa na ubaya.
Maelezo
Kisharia Misikiti ni watu wote na manufaa yake ni kwa Waislamu wote, hakuna tofauti katika hili kati ya anaeishi Jirani na Msikiti na mpita njia, wala kati ya mkazi na msafiri; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: (Kwa wakaao humo na wageni)[Al Hajj:24], na hii ni hukumu jumuishi katika Misikiti yote iliyotengenezwa kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Swala katika Msikiti huo,
Pia kunapendeza kuwahi Msikitini, Mwenyezi Mungu Anasema: (Na katika hayo washindanie wenye kushindana) [Al Mutaffifeen:26].
Kuzuia nafasi Msikitini kuna hali mbili:
Kwanza: Mwenye kufika Msikitini mapema, kisha akaenda kukidhi haja iwe kutawadha au jambo lingine, huyu anakuwa na kipaumbele cha nafasi yake hata kama hajaizuia, pia inaruhusiwa kwake kuizuia kwa kuweka kitu kitakachomuhifadhia haki yake katika nafasi hiyo, kuzuia nafasi katika hali hii ni bora zaidi ili kuondosha ugogoro na hitilafu katika Msikiti, imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Akisimama mmoja wenu katika kikao chake, kisha akarudi basi ana haki zaidi ya sehemu hiyo” imetolewa na Imamu Muslim katika Sahihi yake, Na hili ndio waliloeleza Wanazuoni wote.
Na ya pili: Mwenye kuzuia nafasi kwa kudumu kwa kuweka kitu kama msala na mfano wake maalumu kwa ajili yake, kwa namna anamuomba aliyetangulia kukaa hapo ampishe na kumuachia nafasi hiyo, kama ilivyo kwenye maudhui yetu hii, na aina hii ina mambo mawili: jambo la kwanza: Kuzuia nafasi kwa ajili ya mtu mwingine kwa njia ya kudumu, na ya pili: Kudumu katika sehemu hiyo katika Msikiti huo, haswali katika shemu nyingine.
Ama kumuwekea mtu mwingine nafasi kwa kudumu: Huko ni kuvunja haki ya wengine, kwani sehemu za Swala katika Msikiti ikiwemo safu ya kwanza ni katika maeneo ya wote kwa kila atakaye kuswali katika sehemu hiyo, na alietangulia ana haki zaidi; kwa kufanyia kazi kanuni iliyopitishwa na Wanazuoni wa Fiqhi kwamba “Ni halali kwa aliyetangulia.
Na hii ndio maana ya kauli ya Mtume (S.A.W): “Mwenye kutangulia katika ambacho hajakiwahi Muislamu basi ni haki yake” imetolewa na Imamu Dawoud katia Sunanih, na katika riwaya nyingine: “Mwenye kuwahi maji…” na hili linatiwa nguvu na kauli ya Abdullah bi Umar (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Akinyanyuka mmoja wenu sehemu yake asikae mtu mwingine” Imepokelewa na Bukhari na Muslim.
Wanazuoni wa Fiqhi wametofautiana katika masuala ya kuzuia nafasi Msikitini kwa kuweka msala au mfano wake katika ambavyo vinakuwa alama kuwa sehemu hii ya mtu Fulani:
Jamhuri ya Wanazuoni wa Malik, Shafi na Shekhe Ibnu Taymia katika Madhehebu ya Hanbali, wamesema kwamba kuzuia nafasi katika Msikiti kuwa ni mahususi kwa mtu Fulani ni haramu, na wala hakuthibishi haki kwa mtu aliezuia sehemu hiyo; kwa sababu sehemu ya Swala katika Misikiti ni ya watu wote hamilikiwi na Mtu yeyote, kuzuia nafasi kunakuwa ni kuvuka mipaka na kulazimisha, pia kumuwekea nafasi mtu ambaye hakufika Msikitini hakuna faida[1].
Madhehebu ya Imamu Hanafi na Hanabila katika njia nyingine kwa wote wawili, na Madhehebu Imamu Shafi katika isiyotegemewa: kwamba Sharia ya kuzuia sehemu Msikitini ikiwemo mtu kumuwekea mtu nafasi au kuweka nguo au mfano wake, kwamba hii ni sehemu ya kuwahi inathibiti kwake haki ya eneo hilo, kwa sharti ya kutochelewa Swala, au kuwavuka wanaosali, asipokuja basi mtu mwingine ana haki ya kuondoa alichokitoa kwa ajili ya kuzuia na atasawli sehemu yake, wala asiswali juu yake[2].
Madhehebu ya Imamu Hanaf wametofautisha kati ya Msikiti wenye nafasi na Msikti uliobana; kwamba anaweza kumuwekea nafasi katika Msikiti wenye nafasi na asisali sehemu hiyo mtu mwingine, na asimuwekee nafasi katika Msikiti mdogo; ili hilo lisipelekee madhara kwa Waislamu wengine[3].
Ama kulazimiana na sehemu moja kuswali katika Msikiti: Imepokewa kwa Mtume (S.A.W) amekataza, kutoka kwa Abdurrahman bin Shibil (R.A) “Kwamba Mtume (S.A.W) amekataza kujiwekea mtu nafasi katika Msikiti kama anavyojiwekea nafasi ngamia” Imetolewa na Ahmad, Ibnu Hibban na Al bayhaqy.
Na katika maelezo ya Jamhuri ya Wanazuoni wa Fiqhi ni chukizo; kwa sababu hilo linaondoa utulivu, na kwa sababu akifanya hivyo Swala kwake inakuwa ni kama tabia, na Ibada inapokuwa tabia basi inakuwa katika njia ya kuacha, pia hilo linahofiwa kwake kuwa ni ria, na fadhila ni kufanya Misikiti ni sehemu ya Swala na kumtaja Mwenyezi Mungu, si kwa lengo lingine katika malengo ya kidunia na maslahi binsfsi[4].
Pamoja na haya Jamhuri ya Wanazuoni wa Fiqhi wa Imamu Shafi Malik na Hanbali wameona kuwa inapendeza kuondolewa kuchukiza kwa Wanazuoni kulazimiana na sehemu moja, na wasomaji na mwenye kuwa na sehemu thabiti katika Msikiti ili kusomesha na kutoa Fatwa, kwa sharti watu wengine wafaidike, na hili linamjumuisha Imamu na Muadhini; kwa sababu hawa kudumu katika sehemu zao ili watu wawazoee na wafaidike nao, na hii ndio maana inayozingatiwa kisharia[5].
Sehemu za Swala Misikitini hazitoki katika sifa ya kuwa sehemu za wote katika hali ya kunufaika, na mwenye kutagulia katika sehemu hizo basi ana haki zaidi, vilevile akisimama kwa sababu ndogo na akarudi, basi hapa ana haki ya kuzuia sehemu hiyo.
Ama kuzuia nafasi kwa kudumu kwa mtu maalumu, si sahihi kwa Jamhuri ya Wanazuoni pasi na haja, nako ni aina ya kuvunja haki za watu wengine, kama walivyoeleza baadhi yao kuwa ni chukizo, pamoja na kudumu katika sehemu moja katika msikiti, na hili ndilo waliloeleza wanazuoni wa Fiq’hi, isipokuwa ikiwa kufanya hivyo kuna manufaa kwa watu kama kuwafundisha au kutoa Fatwa au mfano wake, na Wanazuoni walioeleza kuruhusu kuzuia nafasi Msikitini wameifunganisha na kutochelewa Swala, na kutopangua shingo za watu ili kufika sehemu yake, na kutomduhuru yeyote katika wanaoswali, na kutowasumbua, akichelewa vitaondolewa vitu vyake na ataswali Mtu Mwingine kama iliytotangulia kusemwa.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Mwenye kuwahi sehamu Msikitini, si sehemu iliyotengwa kwa ajili ya Imamu, akaweka msala au mfano wake, basi ana haki ya kukaa sehemu hiyo muda wakuwa Swala haijakimiwa, Ikikimiwa Swala basi ana haki na sehemu hiyo.
Kunatakikana kufuata yaliyopitishwa na pande husika katika jambo hili ikiwemo Wizara ya Mambo ya Dini; kwa kuwa ni pande inayohusika kupamgilia masuala ya Misikiti, na imepitishwa kisharia kwamba kiongozi kuweka vifungu vinavyoruhusiwa kwa ajili ya kufikia Maslahi na kuonda madhara.
[1] Manh Al Jaleel 6\318. Nihayat Al Muhtaj 2/339. Al Majmou Al Fatawa 22/193.
[2] Manh Al Jaleel 6\318. Nihayat Al Muhtaj 2/339. Al Majmou Al Fatawa 22/193. Chapa cha Mfalme wa Fahd
[3] Maraqi Al Falah Uk 228
[4] Tabyeen Al Haqaaiq cha Imamu Fakhrudeen Al Zaylaii 1/131. Al Mubdiii cha Imamu Burhan Al Deeeb ibnu Muflih 2/102. Al Bahr Al raaq cha Imamu Zaynuddeen Ibnu Nujaym 2/38. Mughny Al Muhtaj cha Imamu Shamsuddeen Al Khateeb Al Shirbiny 3/511, Al Misqat Al MAfatih cha Imamu Al Mulaa Ally Al Qaary 2/581.
[5] Ikmaal Al Muallim 7/71. Nihayat AL Muhtaji 5/345, Al Mubdii 2/102.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
