Kupeleka chakula kwa familia ya Maiti
Question
Jirani yetu mmoja alikufa, basi, niliamua kuwatengenezea familia yake chakula na kuwapelekea, kwani walishughulikia majonzi ya maiti wao. Ni ipi hukumu ya Kiislamu juu ya hili? Je, nitapata thawabu kwa hilo?
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Answer
Kutayarisha chakula kwa ajili ya familia ya maiti na kuwapelekea kutoka kwa majirani, kwa kuzingatia kwamba wanajishughulisha na kutayarisha mazishi ya marehemu wao na kupokea rambirambi, au kwamba wanasitasita kuandaa chakula kutokana na huzuni yao, ni jambo ambalo limependekezwa kwa sharia ya Kiislamu, kwa mujibu wa makubaliano ya Wanachuoni, na linaleta thawabu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maelezo
Chakula cha rambirambi: Chakula kilichopelekwa na majirani na ndugu kwa familia ya marehemu ili kuwafariji kutokana na kuhangaika na msiba walioupata. kwani huzuni inawashughulisha na kujitengenezea chakula, au kwa sababu nafsi zao zinasitasita kufanya hivyo kutokana na ukuu wa msiba.
Chakula cha rambirambi ni miongoni mwa dalili za kuimarisha mahusiano ya kijamii, msaada wakati wa shida na misiba, mapenzi na huruma, na kwa mbinu hiyo, mazoeano yanaimarishwa na mshikamano unaimarishwa kati ya watu, rika baada ya rika.
Na dalili ya Uhalali wake kutoka Sunna: Mtume (S.A.W.) aliamrisha wakati habari za kifo cha Jafar bin Abi Talib (R.A.):
Basi kutoka kwa Abdullah Bin Ja’far, ambaye alisema: ilipokuja Habari ya kifo cha Jafar (R.A)., Mtume (S.A.W.) akasema: “Waandalieni chakula watu wa Jafar, kwani limewajia jambo litakalowashughulisha.” Imtolewa na Imam Al-Shafi katika Al-Musnad, Abu Dawud katika Al-Sunan, At-Twabarani katika Al-Mu’jam Al-Kabir, na Al-Baihaqiy katika Ma’rifat Al-Sunan wa Al-Athar. Katika simulizi yenye maneno: "Tengeneza." Imetolewa na Imamu Ahmad katika Al-Musnad, Ibn Majah, na At-Tirmidhiy katika Al-Sunan.
Na akasema, "Hadithi Hasan na sahihi." Na inchukuliwa faida kutoka katika Hadithi hiyo: kupendekezwa matayarisho ya chakula kwa ajili ya familia ya marehemu, iwe maiti yupo au habari ya kifo chake imefika, hiyo kwani familia hushughulishwa kwa habari ya kifo chake au hali yake. Hali iliyotajwa katika Swali inaitwa "wadhimah," ambacho ni chakula cha mazishi, au chakula kilichoandaliwa inapotokea msiba au kifo. Wanachuoni wa Fiqhi wameeleza kuwa, inapendekezwa kwa majirani na ndugu wa mbali wa marehemu kupeleka chakula kwa familia hiyo, hasa mchana na usiku wa maziko.
Ama thawabu wa chakula hicho: ni dhihirisho miongoni mwa madhihirisho ya Sunna ya "kuwalisha masikini chakula." Matini za Qur’ani Tukufu na Sunna ya Mtume (S.A.W) yameeleza mara kwa mara kwamba kulisha masikini ni miongoni mwa matendo yanayopendwa sana na Mwenyezi Mungu na yenye uwezekano mkubwa wa kukubaliwa, hadi akaifanya kuwa ni miongoni mwa sababu za kupata Pepo. Amesema Mwenyezi Mungu akiwasifu waja wake walioamini: {Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake,masikini, na yatima, na wafungwa.} [Al Insaan 8]
Kutoka kwa Abdullah Ibn Amro (R.A.) kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume (S.A.W) “Je, Uislamu upi ulio bora zaidi?” Akasema: "Kuwalisha masikini chakula na kuwasalimu mnaowajua na msiowajua." Mutafak.
Kutoka kwa Amiri wa wanaamini Ali Bin Abi Twalib R.A. amesema: Mtume (S.A.W.) amesema: “Hakika Peponi kuna vyumba ambavyo migongo yao inaonekana kutoka ndani na ndani yake huonekana kutoka kwenye migongo yao. Bedui mmoja akasimama na kusema: “Nani ana vyumba hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Alisema: “Kwa yule anayezungumza maneno mema, huwalisha watu, hufunga mara kwa mara, na huswali usiku wanapolala watu.” Imepokewa na Imam Ahmad katika “Al-Musnad,” Al-Twabarani katika “Makarim Al-Akhlaq,” Al-Baihaqiy katika “Al-Ba’th wa An-Nushur,” na Al-Hakim ameithibitisha katika “Al-Mustadrak.”
Hilo linathibitisha kwamba Kuwalisha walio karibu na walio mbali, waliohudhuria na wasafiri, waliohuzunika na majirani, kwa lengo la kuimarisha vifungo vya mazoea na urafiki, au kufariji huzuni na kusaidia, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutafuta radhi Zake, na kuharakisha katika kutenda mema na kujitokeza kwenye baraka Zake - huchukuliwa kuwa ni miongoni mwa matendo bora ambayo Muislamu humkaribia Mwenyezi Mungu Mtukufu nayo; kwa sababu yana thawabu kubwa na malipo makubwa, pamoja na maana za kijamii zinazooneshwa na matendo mema haya kama vile ushirikiano, mshikamano, kukidhi mahitaji, na kusaidiana baina ya watu wote.
Tunafpata faida kutokana na yaliyotangulia:
Chakula cha rambirambi ni mojawapo ya mbinu za kuimarisha mahusiano ya kijamii na kusaidiana wakati wa shida na misiba.
Majirani na jamaa wa mbali wa marehemu kuwapelekea chakula familia ya marehemu, hasa siku ya maziko na usiku wake, ni miongoni mwa matendo mema anayoyapenda Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yanayotegemewa kukubaliwa, na ni sababu ya kushinda Pepo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu nj Mjuzi zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
