Kukusanya Swala kwa Sababu ya Mvua
Question
Ni ipi hukumu ya kukusanya Swala kwa sababu ya Mvua?
Answer
Fatwa iliyotolewa ni kujuzu kukusanya kati ya Swala ya Adhuhuri na Alasiri, na kati ya Swala ya Magharibi na Isha katika wakati wa kwanza ya moja zao kwa sababu ya mvua kubwa; ili kuondosha uzito na kero, na pamoja na kuchunga sharti ambazo ni: Kuwepo mvua wakati wa kwanza wa Swala mbili na kuendelea kwa mvua hiyo mpaka wakati wa Swala ya pili, na kuwa mvua ambayo inasababisha uzito kwenda Msikitini ikiwa inanyesha, na kuwa kukusanya wakati wa Swala kwanza, kukusanya hali ya kutanguliza (Jam’u Taqdiim) si kuchelewasha (Jam’u Ta’khiir), na kuhudhurisha Nia ya kukusanya wakati wa Swala ya kwanza na wakati wa kuanza Swala ya pili, na kuwa Swala ya jamaa katika Msikiti, na kufululiza, kwa kutokuwa na kitambo kirefu kati ya Swala mbili.
Maelezo
Asili ni kupasa kusimamisha Swala ndani ya wakati wake pasi na kuchelewesha au kuitanguliza, Mwenyezi Mungu anasema: }Kwani hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu{ [Annisaa:103], kukusanya kati ya Swala linakuwa jambo la dharura, na inakuwa kwa sababu ya udhuru.
Na kukusanya ima kunakuwa kwa kutanguliza kati ya Swala mbili za Adhuhuri na Alasiri katika wakati wa Adhuhuri, na kukusanaya kati ya Swala mbili za Magharibi na Isha katika wakati wa Magharibi, au kukusanya kwa kuchelewesha kati ya Swala mbili za Adhuhuri na Alasiri katika wakati wa Alasiri, na kukusanaya kati ya Swala mbili za Magharibi na Isha katika wakati wa Isha.
Miongoni mwa udhuru za ambazo zinaruhusu kukusanya Swala ni: Mvua kubwa unaosababisha uzito Kwenda msikitini kukiwa na mvua hiyo, kwa namna kunakuwa na ugumu kurudi tena wakati wa Alasiri au Isha, na Wanazuoni wa Fiqhi wametofautiana katika hukumu ya huko kukusanya.
Madhehebu ya Imamu Malik na Madhehebu ya Imamu Hanbali wanasema kujuzu kukusanya kati ya Magharibi na Isha tu, kukusanya kwa kutanguliza (Jam’u Taqdiim) si kati ya Swala ya Adhuhuri na Alasiri[1].
Madhehebu ya Imamu Shafi wamejuzisha kukusanya kati ya Udhuhuri na Alasiri na kati ya Magharibi na Isha katika nyakati za Swala zao za kwanza, na hali hii pia katika Madhehebu ya Hanbali ameichagua Abou Khattab miongoni mwa Wanazuoni wao[2].
Na Madhehbu ya Imamu Hanafi yamekataza kukusanya kati Swala kwa kutanguliza (Jam’u Taqdiim) au kwa kuchelewesha (Jam’u Ta’khiir) kwa sababu ya mvua au baridi, na wameruhusu kukusanya katika maeneo mawili tu: Muzdalifa na Arafa[3].
Na Fatwa tunayoichagua ni: Ile iliyotolewa na madhehebu ya Imamu Shafi na waliokubalina naye katika kujuzu kukusanya wakati wa Mvua kati ya Adhuhuri na Alasiri na kati ya Magharibi na Isha katika wakati wao wa kwanza; kwa Hadithi sahihi kutoka Ibnu Abbas amesema: (Mtume S.A.W aliswali Madina Adhuhuri na Alasiri zote na Magharibi na Isha zote), na Muslim amezidisha: (Si wakati wa hofu wala safari) Imamu Maliki na Imamu Shafi wameona kwamba hii ilikuwa kwa udhuru wa mvua.
Na imethibiti pia kwamba Ibnu Abbas na Ibnu Omar (R..A) walikuwa wakikusanya Swala kwa sababu ya mvua; kwa sababu ni kuwepo sababu ambayo ni mvua sawasawa usiku au mchana, lakini lazima kuchunga sharti za kukusanya katika hali iliyoelezwa na Madhebu ya Imamu Shafi, nayo ni: Kuwepo mvua katika mwanzo wa Swala mbili na kuendelea mpaka wakati wa Swala ya pili, na kuwa mvua inayolowesha nguo, kwa maana kwamba inafanya uzito Kwenda msikitini inapokuwa inanyesha, na kukuwa kukusanya wakati wa Swala ya kwanza wa Swala mbili hizo (Jam’u Taqdiim) si kuchelewasha (Jam’u Ta’khiir), na kuhudhurisha Nia ya kukusanya Swala katika wakati wa Swala ya kwanza, na wakati wa kuanza Swala ya pili, na kuwa Swala ya jamaa msiktini, na kufululiza kwa kutokuwa na kitambo kirefu kati ya Swala mbili.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
asili ya hukumu ni wajibu wa kusimamisha Swala katika wakati wake pasi na kuchelewesha wala kutanguliza.
Kunajuzu kukusanya wakati wa mvua kati ya Swala ya Adhuhuri na Alasiri na kati ya Swala ya Maghraibi na Isha katika nyakati zao za kwanza.
Ni lazima kuchunga masharti ya kukusanya Swala ambayo ni:
Kuwepo mvua wakati wa kwanza wa Swala mbili na kuendelea kwa mvua hiyo mpaka wakati wa Sawla ya pili.
kuwa mvua ambayo inasababisha uzito Kwenda Msikitini inaponyesha
Kuwa kukusanya wakati wa Swala ya kwanza, kukusanya hali ya kutanguliza (Jam’u Taqdiim) si kuchelewasha (Jam’u Ta’khiir).
Kuhudhurisha Nia ya kukusanya wakati wa Swala ya kwana na wakati wa kuanza Swala ya pili, na kuwa Swala ya jamaa katika Msikiti.
Kufululiza, kwa kutokuwa na kitambo kirefu kati ya Swala mbili
[1] Al Sharh Al Kabeer 1/370, Al Kashaf Al Qinaa 2/7.
[2] Rawdha al Talibeen 1/ 399.
[3] A Dar Al Mukhtar uk 55.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
