Kutangaza Kifo na Mazishi kwa Kutumia Vipaza Sauti vya Misikiti.
Question
Katika baadhi za nchi jirani, ilikuwa ni ada kwa watu, inapotokea kifo, hutumia vipaza sauti vya Misikiti kutangaza kifo hicho kwa majirani wa marehemu. Hii ilifanyika ili idadi kubwa ya watu iweze kuhudhuria Swala ya mazishi na kutoa rambirambi. Je, Ni Nini hukumu ya jambo hili katika Uislamu?
Answer
Inaruhusiwa kutangaza kifo cha marehemu kwa kutumia njia zilizo rahisi, kama vile vipaza sauti vya Misikiti;
Hii ni kwa sababu inasisitiza kutekeleza haki yake, kwa kuhudhuria mazishi yake, kuswali juu yake, kumsindikiza, kumzisha, kumwombea, na kuwafariji ndugu zake.
Yote hayo ni matendo mema yanayohimizwa na sharia za dini. Na kile kinachopelekea kwenye wema, basi ni wema. Kwa sharti kwamba tangazo hilo lisifuatane na matendo ya zama za ujinga, kama vile kulalamika, kulia kwa sauti, kuchochea huzuni, na kuonesha dalili za kupinga uamuzi wa Mwenyezi Mungu, kwani haya ndiyo yaliyokatazwa kisharia. Hali kadhalika, inapaswa kuzingatiwa kutowasababishia usumbufu watu, na vilevile, tangazo hili lisipingane na sharia na maelekezo ya mamlaka husika.
Maelezo
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Sheria Tukufu ya Kiislamu imehimiza sana kuhudhuria mazishi na kuongeza idadi ya watu wanaoswalia juu ya maiti, na imebainisha kheri nyingi zilizomo katika jambo hilo; kwa marehemu, anapata maombezi (shafa'ah) na msamaha, na kwa upande wa aliye hai, anapata thawabu nyingi.
Kutoka kwa Aisha (R.) anasema kwamba Mtume (S.A.W) alisema: "Hakuna maiti yeyote ambaye umma wa Waislamu unaomswalia, ambao wanafikia mia, wote wakimwombea (shafa'ah), isipokuwa maombi yao yanakubaliwa." (Hadithi hii imetolewa na Imamu Muslim katika kitabu chake cha "Sahih".)
Kutoka kwa Abu Hurairah (R.A) amesema kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: "Yeyote atakayehudhuria mazishi hadi aswali, atapata qirrat moja. Na yeyote atakayehudhuria hadi mazishi yakamilike, atapata qirrat mbili." Iliulizwa: "Qirrat mbili ni nini?" Akasema: "Ni kama milima miwili mikubwa." (Hadithi hii imekubaliwa na Al-Bukhari na Muslim)
Na kutangaza kwa wengine kuhusu kifo cha marehemu ni jambo linalohitajika kisharia; kwani ni sababu ambayo inamwezesha marehemu kupata haki zake, ambazo ni kuhudhuria mazishi yake, kuswaliwa, kusindikizwa, kuombewa, na ndugu zake kufarijiwa. Pia, wale walio hai hupata thawabu za kuhudhuria na kuswali juu ya maiti.
Na kwa sababu hiyo, hadithi nyingi tukufu za Mtume (S.A.W.) zimepatikana kuthibitisha uhalali wa kutoa tangazo la kifo.
Kutoka kwa Abu Hurairah (R.A.) kwamba mwanamume mweusi, au mwanamke mweusi, aliyekuwa akifagia Msikiti, alifariki. Mtume (S.A.W.) alimuulizia, na watu wakamwambia kuwa amefariki. Akasema: "Mbona hamkunijulisha? Nionyesheni kaburi lake." Basi, akaenda kwenye kaburi lake na akamswalia. (Mutafaq)
Na kutoka kwa Abu Hurairah R.A., kwamba Mtume (S.A.W.) aliomboleza kifo cha Najashi kwa watu siku ile aliyokufa. Aliwaongoza kwenda mahali pa kuswalia (Musalla) na akasema Takbira nne." Imekubaliwa na Al-Bukhari na Muslim.
Na inachukuliwa kutoka Hadithi, kupendedeza tangazo la kifo cha mtu. Na wengi wa Wanazuoni wa Fiqhi wanaruhusu kutangaza kifo cha mtu ili watu wahudhurie mazishi yake na kuswali Swalah ya Janazah. Na baadhi ya Wanazuoni wa Hanbali walisemea ni chukuzo kwa tangazo la kifo cha mtu, hasa ikiwa ni kwa njia ya kupaza sauti sokoni au kuzunguka katika vikao kama ilivyokuwa ikifanywa wakati wa Ujahiliyah (kabla ya Uislamu). Wao wanaruhusu tu kutangaza kwa ndugu, marafiki, na watu wenye heshima, bila kupiga kelele. Maoni mengine yanasema ni jambo la kupendeza. [1]
Na yaliyotaja katuka kukataza kutangaza kifo, makusudio yake ni vitendo vya zama za Ujahiliyah, kama vile kulia kwa sauti kubwa, kupiga kelele, na kuomboleza huku wakitaja sifa na matendo makuu ya marehemu, pamoja na malalamiko na kukata tamaa vinavyoambatana na kifo chake, na kudai kuwa kifo chake ni maangamizi, na kwa makusudi kuamsha huzuni na kuchochea kilio.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Sharia ya Kiislamu imehimiza sana kuhudhuria mazishi na kuongeza idadi ya waumini wanaoswali Swala ya maiti. Hili lina lengo la kumsaidia marehemu kupata maombezi na msamaha, na yule aliye hai kupata thawabu.
Kutangaza kifo cha mtu ni moja ya mahitaji ya kisharia kwa sababu inampa marehemu haki yake ya kuhudhuriwa mazishi yake, kuswaliwa, kusindikizwa, kuombewa, na familia yake kupata faraja.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
[1] - "Bada'i al-Sana'i" (1/299, iliyochapishwa na Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah), "Al-Istidhkar" (3/26, iliyochapishwa na Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah), "Al-Mughni" (2/425, iliyochapishwa na Maktabat Al-Qahirah), "Al-Adhkar" (uk. 154, iliyochapishwa na Dar Al-Fikr), "Al-Furu'" (3/273, iliyochapishwa na Mu'assasat Ar-Risalah).
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
