Kujumuisha Pesa Taslimu na Bidhaa z...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kujumuisha Pesa Taslimu na Bidhaa za Biashara katika Zaka

Question

 Mtu anamiliki bidhaa za biashara, na ana pesa taslimu nyingine anazomiliki, na zote zimefikiwa na mwaka, lakini kila moja kati ya hizo hazifiki kiwango isipokuwa kwa kujumuisha na nyingine. Anauliza: Je, anajumuisha bidhaa za biashara na pesa taslimu na kuzitoza Zaka kama mali moja, au azitoe kila moja kwa Zaka yake pekee?

Answer

Anayemiliki bidhaa za biashara na ana pesa taslimu nyingine anazomiliki, na zote zimefikiwa mwaka, ni lazima akadirie thamani ya bidhaa za biashara alizonazo, na aunganishe na pesa taslimu alizonazo. Iwapo jumla ya vyote viwili itafikia kiwango cha Zaka, basi atoe Zaka ya pamoja kwa kiwango cha robo ya kumi (2.5%) ya jumla ya mali yote.

Maelezo

Neno ‘urūḍ” ni wingi wa ‘arḍ’ kilugha, nalo linamaanisha bidhaa au mali yeyote isipokuwa dirhamu na dinar, kwani hizo mbili huitwa ‘ayn’  (fedha halisi). Maana yake katika istilahi ya Kifiqhi haipishani na maana hiyo ya lugha iliyotajwa.

Wanazuoni wote wameafikiana kuwa bidhaa za biashara ni lazima zitolewe Zaka iwapo zitafikia kiwango na kupitiwa na mwaka mmoja kamili. (Tazama Ijmāʿ ya Ibn Al-Mundhir)

Na kiwango - Nisabu ya Zaka ya bidhaa za biashara ni kama kiwango cha dhahabu au fedha, kulingana na maoni ya Wanazuoni wengi. Na kiwango kinachotumika kwa wakati wetu ni: Kiasi kinacholingana na gramu 85 za dhahabu safi (yaani dhahabu safi ya kiwango cha karati 21).

Vilevile, wamekubaliana kuwa mwenye bidhaa za biashara na pesa taslimu nyingine, na zote zimepita mwaka, lakini kila moja kwa pekee haifiki nisabu ila kwa uunganishwa, basi: Hupaswa kukadiria thamani ya bidhaa za biashara na kuziunganisha na pesa taslimu, Iwapo jumla yake itafikia kiwango, basi atoe Zaka ya pamoja kwa vyote, kwa kuwa Zaka ya biashara inahusu thamani, hivyo inakuwa pamoja na pesa kama aina moja ya mali. Hili limepokewa kwa kauli ya wengi wa wanazuoni[1].

Tunafapata faida kutokana na yaliyotangulia;

Mwenye bidhaa za biashara pamoja na pesa taslimu nyingine, na zote zimepita mwaka, ni lazima, akadirie thamani ya bidhaa hizo, aziunganishe na pesa taslimu alizonazo, Akiona jumla inafikia kiwango basi atoe Zaka ya pamoja kwa asilimia 2.5 ( robo ya kumi) ya jumla ya mali yote.

 

[1] “Ma’alim al-Sunan” (2/16, kilichochapishwa na Al-Matba’ah Al-Ilmiyyah), “Al-Mughni” (3/36, kilichochapishwa na Maktabat Al-Qahirah).

Share this:

Related Fatwas