Dhamana//Uwajibikaji wa wakala kuhu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhamana//Uwajibikaji wa wakala kuhusu mali ya Zaka

Question

 Kuna kijana aliteuliwa na dada yake kuwa wakala wa kugawa mali ya Zaka yake. Siku ile ile aliyopokea fedha hizo, nyumba yake iliibiwa usiku wake, na kati ya vitu vilivyoibiwa ni pamoja na hiyo mali ya Zaka. Je, kwa mujibu wa Shaia ya Kiislamu, anawajibika kulipa fidia? Na ikiwa hatowajibika, je, dada yake anapaswa kutoa tena Zaka hiyo? Ijulikane kwamba alikabidhi fedha hizo kwa kaka yake mwishoni mwa mwaka wa zaka bila kuchelewa.

Answer

Mtu aliyeteuliwa kugawa mali ya Zaka (wakala), na mali hiyo ikaibiwa kutoka kwake, hawajibiki kulipa mali hiyo, isipokuwa kama itathibitika kwamba alifanya uzembe au alivuka mipaka katika kuitunza; kwa sababu wakala ni mwaminifu, na mwaminifu hawajibiki kulipa mali isipokuwa kwa uzembe. Na kigezo cha uzembe ni kushindwa kuuweka mahali salama kama inavyostahiki, au kwa njia ambayo watu hutumia kawaida kuweka mali zao. Kwa hiyo, dada aliyekabidhi Zaka hatotakiwa kutoa tena Zaka hiyo, kwa kuwa alikabidhi kwa wakati, bila kuchelewa, na hakufanya uzembe wala kosa juu ya mali hiyo baada ya kuikabidhi kwa kaka yake. Kwa hivyo, hana dhambi wala lawama.

Maelezo

"Wakala" ni jina la kitendo cha kumkabidhi mtu kazi fulani kwa niaba yako.

Na katika Sharia: Ni kumpa mtu jukumu maalumu la kushughulikia jambo fulani kwa niaba ya mwingine, iwe kwa sababu ya kutopatikana au udhaifu wa mwenye jukumu.

Imethibiti katika Sharia ya Kiislamu kwamba inaruhusiwa kumteua wakala wa kutoa Zaka kwa niaba ya mwingine, na huu ndio mtazamo wa Wanazuoni wengi kutoka Wanazuoni Imamu Abu Hanifa, Maliki, Shafi na Hanbali, kwa sababu ni ibada ya kifedha ambapo uteuzi unaruhusiwa[1].

Na kwa kuwa uteuzi wa wakala wa kulipa Zaka kwa niaba ya mwingine ni halali kulingana na Wanazuoni, basi mkono wa wakala juu ya mali za Zaka zaka ni mkono wa uaminifu mradi tu asizembee katika kuzihifadhi. Akizembea, mkono wake hubadilishwa kutoka kwenye amana hadi kuidhamini, na hii ni kama mali zingine. Wanazuoni wamesema kwamba wakala ni mwaminifu kuhusu mali ambazo mwakilishi wake amempatia, kwa sababu yeye ni mwakilishi wake katika umiliki na utumiaji. Kwa hivyo, hana jukumu la kulipa dhamana kwa kile kilichopotea au kilichoharibiwa mkononi mwake isipokuwa akikiharibu na kuzembea katika kukihifadhi, kwa sababu uharibifu unaotokana na mkono mwake ni kama uharibifu wa aliyemuwahilisha.

Hivyo, jambo la kutoa na kusambazwa kwa Zaka kwa wakili litachunguzwa - kama ilivyo katika suala letu hili - ikiwa amezembea katika kuhifadhi mali za Zaka au kuzifuja, atawajibika kwa hilo atalipa dhamana, na kisha lazima alipe mfano wake. Lakini ikiwa itathibitishwa kwamba hakuzembea au hakupuuza katika kuzihifadhi, basi hakuna chochote dhidi yake, kwa sababu yeye ni mwaminifu, na imethibitishwa kwamba mwaminifu hana jukumu la kulipa dhamna isipokuwa kwa uzembe au ukiukaji. Kigezo cha uhifadhi na uzembe kwa wakili—yaani, mwaminifu - mdhamini—kinapimwa kutokana na wadhamini wengine katika kulinda amana na miliki zao. Nacho ni kiwango cha Kiwango kinachojulikana kikawaida cha uhifadhi, au kile ambacho ni desturi miongoni mwa watu katika kulinda mali zao. Ingawa wakala hutofautiana na amana kwa kuwa amana haiwezi kutumiwa, na wakala huthibiti kwa mwakilishi uwezo wa kutumia ndani ya mipaka aliyoekewa na anayemwakilisha. Isipokuwa, hizo zote zina sifa moja ya kuwa ni amana; ikiwa mdhamini ni mzembe basi atawajibika, na ikiwa si mzembe basi hatowajibika. Na Wanazuoni wengi wanakubali kwamba ikiwa aliyepewa amana akiihifadhi ipasavyo, kasha ikatokezea kuharibika bila ya kuihujumu au kwa matumizi mabaya, basi hatowajibika kuidhamini.

 Kuhusu jambo la mmiliki wa pesa (dada aliyetoa Zaka zaka), alichofanya katika kutenga kiasi cha Zaka baada ya kufikia kiwango cha kisharia ambacho kilizidi kwa mahitaji yake ya msingi, nako ni kukamilika kwa mwaka au siku moja au mbili baada yake – kwa kuzingatiwa kwamba "kile kilicho karibu na kitu ndicho kinachopewa hukumu yake." Kisha akamkabidhi kaka yake (wakala) ili aitowe kwa wale waliostahiki kwa niaba yake, na ikaibiwa kutoka kwake usiku alioipokea, bila ya uzembe wowote kutoka kwake wakati wa kuwajibika kutolewa. Kwa hivyo, halazimiki kutoa kile kilichopotea katika mali ya Zaka iliyotajwa, kwa sababu hakuzembea au kupuuza kuigawa kwa wakati wake, Vile vile, hakumtendea vibaya baada ya kumkabidhi kwa kaka yake (wakala).

Na maelezo yake ni kuwa; Kupotea kwa mali ya Zaka baada ya kuitoa, baada ya kukamilika mwaka kwa siku moja au mbili, au wakati wa kukamilika kwake, bila ya kuzembea kutoka kwa mwenye kutoa Zaka zaka, wala bila ya kuvuka mipaka katika kuifikisha mali hiyo kwa mafakiri — hakumfanyi awe mwenye kuwajibika kuilipa tena; ili zisikusanyike juu yake hasara mbili: hasara ya kupotea mali baada ya kuitoa, na hasara ya kulazimishwa kulipa badala yake hali hakufanya uzembe, wala kosa, wala kuvuka mipaka kwake.

Ama iwapo itathibitika kuwa kuna uzembe kutoka kwa mwenye kutoa Zaka, au kosa, au kuvuka mipaka katika mali ya Zaka — kama kuchelewesha kuikabidhi kwa wakala baada ya kukamilika mwaka kwa siku nyingi, au kuwa na ushiriki katika kuibwa kwake — basi anawajibika kuilipa Zaka hiyo, na haitomwondokea, ili kulinda haki ya masikini ambayo aliipuuzia. Na uzembe huo unahesabiwa kuanzia wakati wa kukamilika mwaka, kama ilivyobainishwa awali, si kabla ya hapo; kwa sababu Zaka haiwi deni katika dhima ya mwenye kutoa Zaka ila baada ya kukamilika mwaka. Hivyo, kama alifanya uzembe kabla ya kukamilika mwaka, basi uzembe huo unahusiana na mali yake mwenyewe kabla ya wajibu wa zaka kutimia juu yake, si katika mali yenyewe ya Zaka; kwani bado haijawa wajibu. Huu ndio msimamo wa Madhehebu ya Imamu Maliki, nao hii ndio iliochaguliwa kwa ajili ya kutoa Fatwa.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia;

Wakala wa Zaka hawezi kuwajibishwa kulipa mali iliyopotea isipokuwa kama alifanya uzembe au kosa katika kuitunza.

Kigezo cha uzembe ni kukosa kuihifadhi mali katika sehemu salama au kutofuata desturi za watu katika ulinzi wa mali.

Mtoa Zaka (dada) hatalazimika kutoa tena Zaka ikiwa alikabidhi kwa wakati, na hakufanya kosa au kuchelewa. Hana dhambi wala lawama.

 

[1] Tazama: “Al-Bahr Al-Raiq” cha Imam Zayn Al-Din Ibn Nujaym Al-Hanafi (2/226, chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islami), “Minah Al-Jalil” cha Sheikh Alish Al-Maliki (6/357, chapa ya Dar Al-Fikr), “Al-Tanbih Al-Shiraip, Al-Shirazi 18 Chapa ya Alam Al-Kutub), na “Sharh Muntaha Al-Iradat” cha Imam Abu Al-Sa’adat Al-Buhuti Al-Hanbali (2/184, chapa ya Alam Al-Kutub).

Share this:

Related Fatwas