Nia ya Kufunga kafara na nadhiri pa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Nia ya Kufunga kafara na nadhiri pamoja na Saumu ya Ramadhani

Question

 Nina deni la kufunga baadhi ya siku kwa ajili ya kafara ya kiapo, na pia nilimuahidi Mwenyezi Mungu (niliweka nadhiri) kufunga siku tatu. Kisha mwezi wa Ramadhani ukaingia, na nikakusudia kufunga Ramadhani pamoja na kufunga kafara na nadhiri hizo. Je, swaumu yangu hii ni sahihi au hapana?

Answer

Haijuzu kwa anayefunga Ramadhani kuunganisha nia ya kufunga Ramadhani na nia ya kufunga wajibu mwingine kama kafara au nadhiri.  Ikiwa atafanya hivyo (yaani, kuunganisha nia mbili), basi swaumu yake itahesabiwa kwa Ramadhani pekee, kwa sababu muda wa Ramadhani umewekwa mahsusi kwa ajili ya saumu ya Ramadhani, na hauwezi kubeba saumu nyingine.

Maelezo

Miongoni mwa saumu za wajibu ni: Saumu ya Ramadhani, nadhiri, na kafara. Na ingawa saumu katika hakika yake ina sura moja — nayo ni kujizuia na vitu vinavyofunguza — lakini kinachotofautisha aina hizi ni nia.

Na mtu aliyekalifishwa anaweza kutekeleza ibada moja kwa nia zaidi ya moja, jambo ambalo Wanazuoni wanalita “kushirikisha nia.” Ikiwa ibada mbili ni za wajibu, kama kukusudia kufunga kwa nia ya kutekeleza saumu ya Ramadhani na kwa nia ya kafara au nadhiri, basi Wanazuoni wengi kutoka Madhehebu ya  Imamy Maliki, Shafi na Hanbali wamesema kwamba haijuzu kuunganisha saumu ya Ramadhani na saumu nyingine ya wajibu, kama saumu ya kulipa (kadhaa), au kafara, au nadhiri. Kwa kuwa saumu ya Ramadhani ni ya wajibu, basi akikusudia nayo saumu nyingine ya wajibu, itakuwa amezikusanya pamoja, na haijuzu kuunganisha na kushirikisha kati ya faradhi mbili[1].

🔸 Kauli ya Wengi wa Wanazuoni:

Wanazuoni wa Malikiya, Shafi’iya, na Hanbaliyya wamesema kuwa haijuzu kuchanganya nia ya Ramadhani na nia ya faradhi nyingine (kama kafara au nadhiri).

Kwa hivyo, ukichanganya nia, saumu yako itahesabiwa ya Ramadhani pekee, na bado unadaiwa kafara na nadhiri zako.

🔸 Kauli ya Imamu Hanafi:

Ikiwa mtu ana afya njema na yuko nyumbani, kisha akaunganisha nia ya Ramadhani na kafara - nadhiri: Basi swaumu hiyo itahesabiwa kwa Ramadhani. Ikiwa ni msafiri: Sahibayn (Wanachuoni wawili wa Madhehebu) wanasema: inahesabika kwa Ramadhani. Imamu Abu Hanifa anasema: inahesabiwa kwa ile ibada aliyoikusudia (kafara au nadhiri)[2].

Hii ikiwa na maana: Saumu katika hali hii ni sahihi, awe mkazi au msafiri; jambo la msingi ni tofauti ya maoni kuhusu namna inavyohesabika ikiwa ni msafiri. Hivyo basi, mwenye kufunga akikusudia (akinuia) pamoja na saumu ya Ramadhani saumu nyingine ya wajibu, kama kafara au nadhiri, basi saumu yake inahesabika kuwa ni ya Ramadhani pekee; kwa sababu wakati wa Ramadhani umewekwa mahsusi kwa ajili ya saumu ya Ramadhani, na hauwezi kubeba saumu nyingine.

Tunapata faida kutokana ana yaliyotangulia:

Haijuzu kwa mwenye kufunga katika mwezi wa Ramadhani kuunganisha pamoja na nia ya saumu ya Ramadhani nia ya saumu nyingine ya wajibu.

Akiwa amefunga na akanuia kuunganisha baina ya nia mbili katika saumu ya Ramadhani, basi saumu yake inahesabika kuwa ni ya Ramadhani pekee; kwa sababu wakati wa Ramadhani umewekwa mahsusi kwa ajili ya saumu ya Ramadhani, na hauwezi kubeba saumu nyingine.

 

[1] “Manḥ al-Jalīl” cha al-‘Allāmah ‘Alīsh al-Mālikī (Juzuu ya 2, uk. 161, chapa ya Dār al-Fikr), na “al-Majmū‘” cha Imām an-Nawawī ash-Shāfi‘ī (Juzuu ya 6, uk. 299, chapa ya Dār al-Fikr), na “Kashshāf al-Qinā‘” cha al-‘Allāmah al-Buhūtī al-Ḥanbalī (Juzuu ya 2, uk. 359, chapa ya Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah).

[2]“Badā’i‘ as-Ṣanā’i‘” (Juzuu ya 2, ukurasa wa 84, chapa ya Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah)

Share this:

Related Fatwas