Kuunganisha kati ya nia ya kulipa f...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuunganisha kati ya nia ya kulipa fuunga ya Ramadhani (kadhaa) na nia ya kufunga siku ya Ashuraa

Question

 Mwanamke ana deni la kufunga baadhi ya siku za mwezi wa Ramadhani, na wakati huo huo ameingia mwezi wa Muharram. Je, inajuzu kwake kuunganisha katika saumu hiyo nia ya kufunga kulipa mwezi wa Ramadhani na nia ya kufunga siku ya Tasu’a (9) na Ashuraa (10), au Ashuraa na siku ya 11 ya Muharram?

Answer

Inajuzu kwa mwanamke huyu kuunganisha nia ya kufunga siku za kulipa za Ramadhani na nia ya kufunga siku za Tasu’a na Ashuraa, au Ashuraa na siku ya 11 ya Muharram. Saumu hiyo itatosha kwa kulipa (kadhaa) na Sunna kwa pamoja, na atapewa thawabu ya funga zote mbili, lakini ilivyo kamilifu zaidi na lenye thawabu zaidi ni kufunga kila moja kwa nia yake pekee.

Maelezo

Siku ya Ashura ni miongoni mwa siku za Mwenyezi Mungu; siku ambayo Mwenyezi Mungu alimwokoa Bwana wetu Musa (A.S) na wale walio pamoja naye kutokana na mateso ya adui yao. Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi wana wa Israili, kwa hakika tumekuokoeni kutoka kwa adui yenu}  [Taha: 80].

Na kufunga siku hii ni Sunna ya Mtume (S.A.W) inayofuatwa. Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullāh bin ‘Abbās (R.A) kwamba alisema:

Mtume (S.A.W) alifika Madina, akaona Mayahudi wanafunga siku ya ‘Ashura. Akasema: “Ni nini hii?” Wakasema: “Hii ni siku njema; ni siku ambayo Mwenyezi Mungu aliwaokoa Wana wa Israili kutokana na adui yao, na Musa aliifunga.” Mtume (S.A.W) akasema: “Mimi nina haki zaidi na Musa kuliko ninyi.” Basi akafunga, na akaamrisha kufunga siku hiyo.) — Imepokelewa na Bukhari na Muslim.

Na kufunga siku ya ‘Ashura kikiwa kumeambatana na kufunga siku moja kabla au baada yake ni ni jmbo la lililosuniwa; kutokana na mapenzi makubwa ya Mtume (S.A.W) na akasisitiza jambo hilo. Kama ilivyo katika hadithi ya ‘Abdullāh bin ‘Abbas (R.A) ambapo Mtume (S.A.W) alisema: "Iwapo mwaka ujao, inshallah tutafunga siku ya tisa." Ibn ‘Abbas alisema: “Mwaka huo haukuja hadi Mtume (S.A.W) alipoaga dunia.” Muslim katika sahihi zake.

 

Pia, Mtume (S.A.W) alisema kuhusu kufunga ‘Ashura:
"Fungeni siku moja kabla yake au baada yake." (Imepokelewa na Imamu Ahmed, al-Bazzār katika Musnad, na Ibn Khuzaymah katika Sahihi).

Na katika riwaya iliyotolewa na al-Bayhaqī katika Shu‘ab al-Īmān, Mtume (S.A.W) alisema: "Iwapo nitabaki, nitaamrisha kufunga siku moja kabla yake au baada yake," akimaanisha siku ya ‘Ashura.

Kufunga siku ya ‘Ashura kuna baraka maalumu za kiroho, kwani hufutiwa dhambi za mwaka uliotangulia. Kama ilivyo kwa riwaya ya Abū Qatadah (R.A) Mtume (S.A.W) alisema: "Kufunga siku ya ‘Arafah, natumaini kwa Mwenyezi Mungu kufutisha dhambi za mwaka uliotangulia na mwaka ujao, na kufunga siku ya ‘Ashura, natumaini kwa Mwenyezi Mungu kufutisha dhambi za mwaka uliotangulia." — (Muslim katika sahihi yake)

Wanazuoni wametafautiana kuhusu uhalali wa kuunganisha nia ya kufidia saumu ya Ramadhani na nia ya saumu ya Sunna kama ile ya ‘Ashura, Tasu‘a, au siku ya kumi na moja ya Mwezi wa Muharram, jambo hili linategemea tofauti yao kuhusu uhalali wa “kushirikisha nia” katika ibada — yaani, “kuikusudia ibada nyingine iliyo sunnah pamoja na ibada ya wajibu”.

Kauli ya fatwa iliyochaguliwa ni kwamba kuunganisha nia hizi mbili inafaa kisheria, na inakidhi mahitaji ya saumu ya wajibu (kufidia Ramadhani) pamoja na saumu ya sunna (Tasu‘a, ‘Ashura, na siku ya kumi na moja). Huu ndio mtazamo wa Maliki na Shafi.

Zaidi ya hayo, baadhi ya wanazuoni walisema kwamba mtu anapofunga siku ambazo ni sunnah kufunga (kama ‘Ashura), hata kama amefunga kwa nia ya wajib tu, au kwa nia ya jumla bila kutofautisha sunnah, bado hupata thawabu ya sunna hiyo.

Pamoja na yote, lililo bora zaidi na la ukamilifu kabisa kwa mtu aliyekalifishwa ni kwa upande wa thawabu n malip ni kufunga siku za fidia za Ramadhani katika siku ambazo si za sunna, iwe ni zile za ‘Ashura au zile sunna nyingine;

Iwe ni kwa kufunga siku ya ‘Ashura au zile nyingine za sunna; kwa sababu kile kinachopatikana kwa kuunganisha nia zote mbili ni dhumini la kupata malipo, na haitowezekana kupata thawabu kamili, na wala hatopata thawabu kamili inayostahili kwa jambo analolihitaji.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kuunganisha nia ya kulipa ya Ramadhani na nia ya kufunga Ashuraa ni jambo sahihi na linajuzu kisheria, mwenye kufunga hivyo hupata thawabu zote kwa pamoja.

Kilicho kamili zaidi na chenye malipo makubwa ni kufunga kila ibada kwa nia yake pekee.

Share this:

Related Fatwas