Kutoka Katikati ya Swala ya Faradhi kwa Sababu ya kubanwa na Haja Ndogo au Kubwa
Question
Nilikuwa safarini, na njiani gari lilisimama mahali pa kupumzika. Abiria walishuka ili kutekeleza ibada ya Swala, na nilikuwa nikihisi haja ya kwenda chooni, lakini niliiahirisha kutokana na msongamano katika vyoo. Hivyo, niliingia msikitini ili kuwahi Swala ya faradhi ya jamaa. Wakati wa Swala, sikuweza tena kujizuia, na unyenyekevu wangu katika Swala uliondoka kabisa. Hivyo, nilitoka kwenye Swala nikiwa nimeshikwa na dharura, nikaenda chooni. Je, ni ipi hukumu ya kutoka kwenye Swala kwa sababu hii?
Answer
Kuswali huku ukizuia haja ndogo au kubwa ni jambo linalochukiza (makruhu) ikiwa linamfanya mswaliji kukosa unyenyekevu na utulivu katika swala. Lakini, ikiwa mtu ameingia kwenye Swala ili kuwahi jamaa na akaweza kujizuia, na hali yake ilikuwa nyepesi, Swala yake ni sahihi. Lakini katika hali ambapo mtu hawezi kujizuia kabisa, ni lazima avunje Swala hiyo kutokana na dharura hiyo, kisha aende chooni na aswali tena Swala baada ya hapo. Hakuna dhambi juu yake kwa kuwa alikatisha Swala ya jamaa au hata kama muda wa Swala utakuwa umeisha, kwani anaudhuru wa kisharia.
Maelezo
Ni jambo lililokubalika kisharia kwamba kutekeleza Swala ya faradhi kwa kukamilisha nguzo na masharti yake yote kunafanya Swala hiyo kuwa sahihi kisharia. Allah Amesema katika kitabu chake kitukufu: "HAKIKA wamefanikiwa Waumini (1) Ambao ni wanyenyekevu katika Swala zao(2)." [Al-Mu'minun: 1-2]. Na unyenyekevu katika Swala hauwezi kupatikana isipokuwa akili ya mswaliji iwe huru kutokana na mambo yanayomshughulisha.
Kwa sababu hiyo, Wanachuoni wa Imamu Hanafi wameeleza kuwa Swala ya mtu ambaye anazuia haja mbili (ndogo na kubwa) au moja wapo, ni makruhu tahrim (chukizo la uharamu), iwe kabla au baada ya kuanza Swala. Wameamua kwamba ikiwa jambo hilo linamshughulisha na Swala, anaweza kuikata ili kuepuka tofauti za kisharia, mradi tu haogopi kupitwa na wakati wa Swala. Na akimaliza Swala katika hali hiyo, anapata dhambi[1].
Wanachuoni wa Maliki wameeleza kuwa swala ya mtu anayezuia haja ni batili ikiwa jambo hilo linamletea shida au kumshughulisha. Lakini ikiwa ni jambo jepesi lisilomsumbua, haliathiri kusihi wa Swala[2].
Wanachuoni wa Imamu Shafi (katika na kauli maarufu) na Imamu Hanbali wameeleza kuwa Swala ya mtu anayezuia haja ni sahihi pamoja na kuchukiza. Kuchukiza huku ni pale anapoanza Swala akiwa katika hali hiyo. Lakini ikiwa hali ya kuzuia haja inamtokea akiwa tayari yuko kwenye Swala, hana ruhusa ya kutoka isipokuwa akihisi kupata madhara kwa kujizuia. Hata hivyo, wanachuoni wa Imamu Shafi wameamua kuwa inapendekezwa aende kujisaidia ikiwa muda wa Swala unaruhusu, hata kama atakosa Swala ya jamaa. Na imetajwa pia kauli katika madhehebu yao kuwa inafaa kufanya hivyo hata kama wakati wa Swala ukimpita[3].
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kisharia, kutekeleza Swala ya faradhi kwa kukamilisha nguzo na masharti yake huifanya iwe sahihi.
Sharia ya Kiislamu imejengwa juu ya wepesi, na haimtwishi mwanadamu mzigo unaomzidi uwezo wake.
Kuswali ukiwa unazuia haja kubwa au ndogo ni makruhu ikiwa inakuletea ukosefu wa unyenyekevu. Lakini ikiwa umeingia kwenye Swala ili kuwahi jamaa na hali hiyo ni nyepesi, Swala yako ni sahihi.
Ikiwa mtu hawezi kabisa kujizuia, ni lazima akate Swala hiyo kutokana na dharura, kisha aende aianze tena Swala.
[1]“ Wir Al Mukhtar Alaa Al Dar Al Mukhtar” 1/654. Dar Al Fikri Publishers.
[2] Ala Nawadir, 1/241. Daar Al Magrib Publishers.
[3] Al Mughny Al Muhtaj, 1/422.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
