Kusoma kwa Sauti katika Swala ya Ku...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma kwa Sauti katika Swala ya Kusoma Siri au kusoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa sauti

Question

Nimeingia kuswali ya jamaa Msikitini Sawla ya Alasiri, nikakuta Imamu anasoma kwa sauti na hakusujudu sijida ya kusahau, je, hii ni Sahihi?

Answer

Imamu kusoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa sauti au kusoma kwa sauti katika Swala ya kusoma kwa siri kwa kusahau, hakubatilishi Swala kwa makubaliano ya Wanazuoni, na Wanazuoni wametofautiana kuwa anawajibu wa kusujudu sijida ya kusahau au laa, na tunaloshauri ni kuwa masuala kama haya yasiibue mgogoro na mfarakano kati ya Waislamu, hasa hitilafu katika masuala kama haya kunajuzu, na kuna nafasi ya kuchukua rai ya Wanazuoni wa Fiqhi hakuna ubaya wala kubana.

Maelezo

Hekima ya kusoma kwa Sauti na kusoma kwa siri katika sehemu zao: hii ni kwa kuwa usiku ni sehemu ya faragha, kunahitaji mkesha: kumeruhusiwa kusoma kwa sauti ili kutaka mja kumuomba Mola wake, na ni maalumu kwa rakaa mbili za kwanza ili wanaoswali wapate uchangamfu katika rakaa hizo, na mchana ni sehemu ya kushughulika na watu kuchanganyika kukatakiwa kusoma kwa siri kwakutofaa kwake kujitenga kwa kuomba, na Swala ya asubuhi imeunganishwa na Swala za Usiku kwa sababu wakatii wake sio wakati wa kushughulika kikawaida[1].

Wanazuoni wametofautiana katika umuhimu wa kusoma kwa sauti katika Sala ya kusoma kwa sauti na kusoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa siri, Imamu Hanbali na Malik waanaona kuwa kusoma kwa sauti katika Swala ya kusoma kwa sauti na kusoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa siri ni Sunna kwa Imamu na Muumini, na Imamu Shafi amewaunga mkono katika hilo kwa Imamu ni Sunna na Maamuma ni kipambo, hilo kwao wao ni Sunna na katika vipambo vya Swala kwa Maamuma.

Madhehbu ya Imamu Hanbali yanasema kwamba ni wajibu kwa Imamu kuchunga sifa za kisomo katika kusoma kwa sauti na kwa siri, na katika hilo: Imamu atakaposoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa sauti, au atakaposoma kwa sauti katika Sawla ya kusoma kwa siri kwa kusahau; Swala haibatiliki kwa makubaliano ya Wanazuoni, lakini je, analazimika kusujudu sijida ya kusahau au laaa? Wanazuoni wa Fiqhi wametofautiana.

Madhehebu ya Imamu Hanafi, na Hanbali katika moja ya mapokezi kwamba Imamu akisahau akasoma kwa sauti katika Swala ya kusoma kwa siri, au akasoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa sauti, basi ni wajibu kwake kusujudu sijida ya kusawau, na haya ndio Madhehebu ya Malik[2].

Madhehebu ya Imamu Shafi na Hanbali katika Madhehbu yaliyopitishwa wanona kwamba hakuna sijida ya kusahau kwa kusoma kwa sauti katika Swala ya kusoma kwa siri na kusoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa sauti[3].

Na dalili ya kuacha kusujudu sijida ya kusahau katika hilo ni kwamba Mtume (S.A.W)  alifanya hivyo; Anas bin Malik amepokea kutoka kwa Mtume (S.A.W)  kwamba wao walikuwa wakisikiliza sauti ya “Sabbihisma Rabbikal Alaa”, na “ Hal Ataaka Hadiithu Al Ghashiya” ameipokea Ibnu Khuzayma katika Sahihi yake,  na Al Muqaddasy katika Al Mukhtar.

Na kitendo hiki kimepokelewa katika Hadithi kadhaa kutoka kwa Masahaba kadhaa, akiwemo Umar, Abdullah bin Masoud, Khabbab bin Art na Saeed bin Al Aas R.A, pia imepokewa na Ibnu Abee Shaybah katia Mussnafihi na Al Bayhaqy katika Al Sunan Al Kubraa.

Tunaloshauri ni kuwa masuala kama haya yasiibue mgogoro na mfarakano kati ya Waislamu, hasa hitilafu katika masuala kama haya kunajuzu, na kuna nafasi ya kuchukua rai ya Wanazuoni wa Fiqhi hakuna ubaya wala kubana.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

 Imamu kusoma kwa siri katika Swala ya kusoma kwa sauti au kusoma kwa sauti katika Swala yakusoma kwa siri kwa kusahau, hakubatilishi Swala kwa makubaliano ya Wanazuoni, na wemetofautiana ikiwa je, anasujudu sijida ya kusahau au laa.

Hakutakikani kuwa masuala waliyotofautiana Wanazuoni kwa kuhitilafiana tofauti zinazojuzu kuibua mgogoro na taofauti kati ya Wanaoswali, hakujuzu kukemea kwa mwenye kuchukua rai ya aliyejitahidi katika wanaojitahidi wanaofuatwa.

 

[1] Hashiyat Al Bahramy alaa Sharh Al Khatib, 2/63.

[2] Al Mabsout.

[3] Al Shrah Al Kabeer 1/279. Al Masaail Al fiqhiyya. 122.

Share this:

Related Fatwas