Kufunga kwa lengo la kupunguza uzito
Question
Nina uzito kupita kiasi na nimeanza kutumia mfumo wa lishe (diet) ili kupunguza uzito. Moja ya mambo ninayofanya ni kufunga siku moja na kula siku nyingine, nje ya mwezi wa Ramadhani. Je, nitapata thawabu kwa kufunga huku, japokuwa nia yangu si ibada bali kupunguza uzito?
Answer
Mtu anayefunga kwa ajili ya lishe anapaswa kuambatanisha Nia ya ibada na kutarajia thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, pamoja na nia ya kupunguza uzito. Kwa sababu: Mtu akifunga kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu pamoja na Nia ya kiafya au matibabu – basi saumu yake ni sahihi na atarajiwe kupata thawabu.
Maelezo:
Mwenyezi Mungu ameifanya Nia kuwa sharti la kukubaliwa kwa matendo, usahihi wake, na kupata thawabu. Nia inapokuwa sahihi na matendo hukubaliwa ama inpokuwa mbaya na matendo huharibika. Mtume (S.A.W) amesema: “Hakika matendo yote yanategemea Nia, na kwa kila mtu ni vile alivyoikusudia. Kila aliyekuwa kuhama kwake kwa ajili ya dunia ili aipate, au kwa ajili ya kuoa mwanamke, basi kuhama kwake itakuwa kwa kile alichokuwa amekikusudia." — (Bukhari na Muslim, na tamko ni la Bukhari)
Mtu akifunga bila Nia ya kujikurubisha kwa Allah, yaani bila Nia ya ibada, hapati thawabu yoyote ya saumu hiyo. Wanazuoni wote – wa Madhehebu ya Imamu Hanafi, Maliki, Shafi na Hanbali – wamekubaliana kuwa Nia ni sharti la usahihi wa saumu, iwe ni ya faradhi au ya Sunna.
Kuhusu kupokelewa na thawabu, imethibitishwa kwamba suala la thawabu — ambalo ni jambo la akhera — linategemea usahihi au uharibifu wa Nia.
Kwa hakika, mtu anapofunga kwa ajili ya kudumisha afya (hifadhi ya mwili), anapaswa kuikusudia pia ibada na kupata thawabu pamoja na lengo la kupunguza uzito. Kwa hivyo, mtu anapofunga kwa Nia ya kumkaribia Mwenyezi Mungu na kwa madhumuni ya afya au tiba, saumu yake ni sahihi, na inategemewa kwake thawabu.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia;
Mwenyezi Mungu ameifanya Nia kuwa msingi wa kukubalika kwa matendo na thawabu zake.
Nia ni sharti la kusihi kwa swaumu, na ikiwa mtu anafunga bila Nia ya kumkaribia Mwenyezi Mungu, saumu yake haitakuwa sahihi.
Mtu aliyekalifishwa anayefunga kwa ajili ya afya na kupunguza uzito anapaswa kuikusudia pia ibada, ili kupata matokeo ya kiafya na thawabu ya kiroho yote pamoja.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
