Kufunga mirija ya uzazi
Question
Ni nini hukumu ya kufunga mirija ya uzazi ili kuzuia mimba?
Answer
Mchakato wa kufunga sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke ikiwa itasababisha asiweze kupata mimba tena haijuzu katika sharia ya Kiislamu, kwa sababu ni kukata ukoo ambao umeamriwa uhifadhiwe, ambao ni mojawapo ya mambo muhimu matano ambayo dini zote yamekuja nazo.
Ama kukiwa na ulazima wa kufunga sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke, kama vile ikiwa maisha yake yako hatarini kufa ikiwa atapata mimba katika siku zijazo, au ikiwa na ugonjwa wa kurithi ambao unahofiwa kuambukizwa kwa mtoto wa tumboni, basi inaruhusiwa kufunga katika hali hiyo, na anayeamua jambo hili ni daktari anayeaminika na mtaalamu.
Wanazuoni wamekubaliana kwamba ni haramu kabisa kwa mtu kutumia chochote kinachoweza kuzuia uzazi wake, na kwamba inaruhusiwa kutumia madawa ya kuchelewesha ujauzito ikiwa kuna udhuru kama vile kulea watoto na kadhalika.
Maelezo
Uislamu unahimiza ndoa na kuifanya kuwa moja ya Suna za manabii na mitume, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wakezenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri} [Ar Ruum 21]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kablayako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya} [Ar Ra’d 38]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiriMwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua} [An Nuur 32].
Na Mtume (S.A.W.) amesema: “Enyi vijana, yeyote kati yenu anayeweza Al Ba’ah (Uwezo wa kimwili na kifedha wa kuoa.), basi afanye hivyo, kwani ni bora zaidi katika kupunguza macho na kulinda tupu. Na yeyote asiyeweza kumudu, basi afunge, kwani itakuwa “Wijāa’: (Usafi wa mwili na ulinzi kwa mtu dhidi ya kuanguka katika uzinzi).” (Imepokelewa na Muslim)
Hadithi hii inaonesha kwamba ndoa ndiyo njia halali ya kukidhi matamanio ya kimwili, tofauti na njia nyingine zilizokatazwa. Kwa hivyo, Mtume (S.A.W) aliwaamuru wale ambao hawawezi kuoa kufunga, kwa sababu inadhoofisha matamanio na kumlinda mtu aliyefunga kutokana na kuanguka katika fitina na matendo yaliyoharamishwa.
Sharia Tukufu imefanya mchakato wa kustarehe na kukidhi mahitaji ya kimwili kupitia tendo la ndoa kati ya wanandoa, na imeuweka kwenye uhusiano huo, na imepiga marufuku njia au mfumo wowote mwingine isipokuwa ndoa.
Uislamu umeweka malengo mengi katika ndoa, muhimu zaidi ni kuhifadhi kizazi, kupitia kupata watoto; kwa hivyo, Mtume (S.A.W) alituhimiza kuoa mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa. Imepokewa kutoka kwa Ma’qel Bin Yasaar amesema: “Mtu mmoja alimjia Mtume wa Mungu, (S.A.W.) akasema: Ewe Mtume wa Mungu, nimempata mwanamke wa ukoo mtukufu, mwenye hadhi ya juu, na utajiri, lakini hawezi kuzaa watoto. Je, nimwoe? akamkataza. Kisha akamjia mara ya pili, naye akamwambia vivyo hivyo. Kisha akamjia mara ya tatu, akasema: Oeni wanawake wenye wzuri na wanaozaa sana, kwani nitajivunia idadi kubwa ya umma kupitia kwenu.” [imepokelewa na Abu Dawud]
Na kutoka kwa Anas R.A., amesema: “Mtume (S.A.W.) alikuwa akiamuru ndoa na kukataza vikali kutooa (useja) kukataza kwa ukali, na anaesema: ‘Oeni wanawake wazuri wanaozaa sana, kwani mimi nitajivunia idadi yenu mbele ya manabii Siku ya Kiyama.” Imepokelewa na Abou Dawoud.
Hadithi zilizotangulia ni ushahidi wa kupendeza Ndoa ya mwanamke anayezaa watoto wengi, kwa sababu kupata watoto ni lengo la asili la kisheria, kuendelea maendeleo ya dunia na urithi wake.
Mchakato wa kufunga sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke ikiwa itasababisha asiweze kupata mimba tena haijuzu katika sheria ya Kiislamu, kwa sababu ni kukata ukoo ambao umeamriwa uhifadhiwe, ambao ni mojawapo ya mambo muhimu matano ambayo dini zote zimekuja nayo.
Ama ikiwa na haja ya kufunga sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke, kama vile ikiwa maisha yake yako hatarini kufa ikiwa atapata mimba katika siku zijazo, au akiwa na ugonjwa wa kurithi ambao unahofiwa kuambukizwa kwa mtoto tumboni, basi inaruhusiwa kufunga katika hali hiyo, na anayeamua jambo hili ni daktari anayeaminika na mtaalamu.
Wanazuoni wamekubaliana kwamba ni haramu kabisa kwa mtu kutumia chochote kinachoweza kukata kizazi chake, na kwamba inaruhusiwa kutumia madawa ya kuchelewesha ujauzito ikiwa kuna udhuru kama vile kulea watoto na kadhalika.[1] Na hayo ni Fatwa ya Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misri.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Hakujuzu kufunga sehemu yoyote ya mfumo wa uzazi wa mwanamke ikisababisha kukata kizazi moja kwa moja.
Ikiwa kuna haja ya kufunga sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke, kama vile ikiwa maisha yake yako hatarini kufa ikiwa atapata mimba katika siku zijazo, au kiungo miongoni mwa viungo vyake, au kumuambukiza ugonjwa mtoto wa tumboni, basi inaruhusiwa kufunga katika hali hiyo.
[1] - Kitabu cha “Hasheatu Al-Jamal ala Mahaju At Twlaab" (4/447), na Kitabu cha: "Al-Kafi Fii Feqh ya Imam Ahmad" na Ibn Qudamah (4/93).
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
