Kumuingilia mke kabla ya harusi
Question
Ni ipi hukumu ya kisharia kwa anayetaka kujamiiana na mke wake au wakafanya hivyo kwa njia ya siri baada ya kufungwa ndoa mbele ya familia na marafiki kwa njia rasmi, lakini bado hakukufanyika sherehr za harusi, jambo linajulikana katika desturi ya watu leo “kuingilia" (dukhla)?
Answer
Haifai kisharia kwa mwanaume kuingia kwa mke wake aliyefunga ndoa ikiwa kulikuwa na makubaliano na walii wa mwanamke kwamba kuingilia kutakuwa siku ya harusi inayojulikana kwa watu kama siku ya kuingilia (dakhla). Ni wajibu kisharia kwa mume kutekeleza sharti aliloliweka walii wa mwanamke wakati wa kufunga ndoa, hivyo asimtake mke wake kujamiina naye mpaka harusi ifanyike na mke akae naye katika makazi ya ndoa.
Hivyo hivyo, kwa upande wa mwanamke, ni wajibu kwake kujizuia kujamiiana na mumewe baada ya kufunga ndoa mpaka wakati wa harusi – siku ya kuingilia – kama ilivyokubaliwa na walii wake.
Kumzuia mwanaume kujamii na mke wake kabla ya siku ya harusi – kuingilia – ni jambo linaloafikiana na makusudio ya kisharia ya kulinda heshima na kuheshimu mila na desturi za kijamii zinazofuatwa, na ndani yake kuna kulinda haki za pande zote mbili katika kuthibitisha talaka au kifo iwapo kuingia kutakanushwa.
Maelezo
Uislamu umekiri jambo na kuthibitisha ndoa na kuhimiza juu yake kwa kuwa ni Sunna ya Mitume, ni hitaji linalotakiwa na maumbile ya mwanadamu, na ni dharura kwa ajili ya kuendelea kwa kizazi duniani. Ndani yake kuna staha na usafi, na kuhifadhi macho na tupu dhidi ya kuangukia katika yaliyo haramu. Kutoka kwa Abdullah bin Mas‘ud R.A kwamba Mtume (S.A.W ) amesema: “Enyi vijana, mwenye uwezo miongoni mwenu wa gharama za ndoa[1] na aoe; kwa kuwa hiyo inafunika macho na inalinda tupu; na asiyeweza basi afunge, kwa kuwa hiyo ni kinga kwake[2].”[3]
Ina imethibiti kisharia kwamba mkataba wa ndoa lazima utimize masharti na nguzo zifuatazo:
Tamko la ndoa.
Mashahidi wawili.
Mahari.
Walii wa mwanamke kwa mujibu wa rai ya wanazuoni wengi; kutokana na Hadithi ya Al-Hasan R.A kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Ndoa haijuzu ila kwa walii, mahari na mashahidi wawili waadilifu.”[4]
Na madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, nayo ndiyo inayotolewa Fatwa na inayotekelezwa katika mahakama za Misri, hayashartishi walii kwa mwanamke mwelevu; hivyo mwanamke baleghe akijiozesha kwa mwanaume anayefaa[5] na kwa mahari ya mfano wake, ndoa yake huhesabika kuwa sahihi.
5- Kutokuwepo katika Mkataba wa ndoa vizuizi vya kisharia, kama vile mwanamke kuwa ni mwenye kuharamishwa kwake kwa nasaba, kunyonya au ukwe.
Nguzo na masharti haya yakitimia, ndoa huwa sahihi, na athari zake za kisharia hutimia; miongoni mwa zilizo wazi na muhimu zaidi ni kuruhusiwa kwa mwanaume kuingia kwa mke wake na kujamiana.
Lakini wakati mwingine familia za wanandoa hukubaliana juu ya tarehe maalumu ya kuingilia baada ya kufunga ndoa; na hapo ni wajibu kwa mume kutekeleza sharti hilo alilokubaliana na walii wa mwanamke aliyefunga ndoa, kwa sababu zifuatazo:
1- Sharia tukufu imekiri desturi na kuzizingatia katika hukumu za kisharia. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Shikamana na kusamehe, na amrisha kwa yaliyo mema kwa desturi, na jiepushe na wajinga} [Al-A‘raf: 199]. Na desturi imezoeleka kwamba kujamiana hakufanyiki isipokuwa baada ya harusi; hivyo ni lazima iheshimiwe na izingatiwe.
2- Haifai kumuingia mke bila kuwajulisha walii na kushuhudisha hilo; kwa kuwa kuingilia kunaleta hukumu nyingine ambazo mmoja wa wanandoa anaweza kuzikana, miongoni mwazo ni:
a) Mwanamke kustahiki nusu ya mahari kabla ya kuingiliwa, na mahari yote baada ya kuingilia.
b) Kunasibishwa watoto kwa mume ikiwa mwanamke atazaa kutoka kwake.
c) Kuhukumiwa mwanamke kuwa ni bikira au si bikira kunategemea ikiwa mume alimwingili au hapana.
3- Ikitokea kuingia kwa siri kati ya mke na mume, kisha jambo hilo likafichuka kwa watu kabla ya harusi; desturi hulichukulia hilo kuwa ni jambo la aibu[6] kwa wanandoa wote wawili, na ni kukosea heshima kwa familia linalohitaji kuomba radhi na kuonesha masikitiko. Mtume S.A.W ameusia kutotenda jambo linalohitaji kuombewa radhi. Kutoka kwa Ibn Umar R.A amesema: “Mtu mmoja alimjia Mtume (S.A.W) akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nieleze Hadithi na iwe fupi. Mtume( S.A.W) akamwambia: Sali Swala kana kwamba unaswali Swala ya mwisho, kwani ikiwa humwoni (Mwenyezi Mungu) basi Yeye anakuona; chukia[7] vilivyomo mikononi mwa watu utakuwa tajiri; na jiepushe na jambo linaloombewa radhi.”[8] Hadithi hii inaonesha onyo la Mtume (S.A.W) dhidi ya kufanya jambo linalohitaji kuombewa radhi[9].
4- Miongoni mwa sifa za muumini ni kushikamana na ahadi na makubaliano yake na watu; na kutimiza ahadi katika jambo la kuingilia kwa mke na kuhalalisha kujamiana naye ni muhimu zaidi na kubwa zaidi. Kutoka kwa Uqba bin Amir Al-Juhani R.A amesema: Mtume (S.A.W) amesema: “Sharti linalostahiki zaidi kutimizwa ni lile mlilohalalishia kwa hilo tupu.[10]” Maana ya hadithi ni kwamba sharti linalostahiki zaidi kutimizwa ni lile lililokuwa sababu ya kuhalalika kustarehe na mke; nalo ni sharti lililokubaliwa katika mkataba wa ndoa ikiwa halipingani na yaliyothabiti katika Kitabu na Sunna wala hayapingani na msingi wa kisheria.
5- Ikiwa mwanamke atapewa talaka baada ya kufungwa ndoa, na mumewe akawa amemuingilia kwa siri, hilo litasababisha maovu mengi, tuhuma na dhana mbaya juu ya mwanamke iwapo aliyefunga ndoa hatakiri kuingilia.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Baada ya ufafanuzi huu, yale yaliyopitishwa na Ofisi ya kutoa Fatwa ya Fatwa ya Misri ni kama ifuatavyo:
1- Haifai kwa mwanaume kumuingilia mke wake aliyefunganaye ndoa ikiwa kulikuwa na makubaliano na walii wa mwanamke kwamba kuingilia kutakuwa siku ya harusi inayojulikana kwa watu kama siku ya kuingilia (dakhla).
2- Ni wajibu kisharia kwa mume kutekeleza sharti aliloliweka walii wa mwanamke wakati wa mkataba wa ndoa, hivyo asimtake mke wake kujamiana naye mpaka harusi ifanyike na mke akae naye katika makazi ya ndoa.
Ni wajibu kwa mwanamke kujizuia kujamiana na mume wake baada ya kufunga ndoa mpaka wakati wa harusi – siku ya kuingilia – kama ilivyokubaliwa na walii wake.
Kumzuia mwanaume kujamiana na mke wake kabla ya siku ya harusi ni jambo linaloafikiana na makusudio ya kisharia katika kulinda heshima na kuheshimu mila na desturi zinazofuatwa, na ndani yake kuna kulinda haki za pande zote mbili katika kuthibitisha talaka au kifo iwapo kuingia kutakanushwa.
[1] Uwezo wa kimwili na kifedha juu ya kuoa.
[2] Usafi na ulinzi kwa mtu huyo dhidi ya kuanguka katika uzinzi.
[3] Imepokewa na Imam Muslim (2/1018).
[4] Imepokewa na Bayhaqiy katika Sunan Kubra (7/203).
[5]"Mwenza anayefaa": ni yule anayetaka kuoa mwanamke aliye karibu naye katika hali ya kitamaduni na kifedha.
[6] Linaloharibu heshima.
[7] Inamaanisha: kutojali kile ambacho wengine wanacho, na kukata tumaini na matarajio yako kwacho.
[8] Imeripotiwa na Al-Tabarani katika ‘Al-Mu’jam al-Awsat’ 4/358.”
[9] “At-Taysir bi Sharh al-Jami’ al-Saghir” cha Zainuddin al-Manawi 2/90.
[10] Imepokewa na Bukhary.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
