Kucheza mchezo ili kutimiza gharama za Hija
Question
Ni ipi hukumu ya kucheza mchezo ili kutimiza gharama za Hija? Pamoja na kujua kwamba mchezo huu utakuwa kati yangu mimi na rafiki zangu, na kila mmoja atatoa kiasi cha pesa kila mwezi kwa muda maalumu. Na kila mtu atakuwa na zamu maalumu ya kupokea pesa inayokusanywa kutoka kwa washiriki waengine kila mwisho wa mwezi ukiwa mchezo huo ni wa kila mwezi, kila mwezi anapokea mtu mpaka mshiriki wa mwisho, mimi nitakuwa mtu wa kwanza kupokea.
Answer
Hakuna ubaya kwa watu wanaojuana kucheza mchezo kwa ajili ya kupata gharama za Hija, na kufanya bidii ili kupata gharama za Hija kwa njia ya kucheza mchezo, hili ni jambo halali na halina ubaya kisharia, lakini si wajibu; kwani Hija ni wajibu wenye ruhusa ya kuchelewesha.
Maelezo
Hija ni wajibu kwa kila Muislamu mwenye uwezo katika Maisha yake yote mara moja kwa makubaliano ya Wanazuoni; hii kwa Ushahidi wa Hadithi iliyotolewa na Imamu Muslim kutoka kwa Abu Hurayra R.A. amesema: “Mtume (S.A.W) alituhutubia akasema: Enyi watu! Mwenyezi Mungu Amekufaridhishieni Hija, basi Tekelezeni Ibada ya Hija. Mtu mmoja akasema: je, ni kila mwaka ewe Mjumbe wa Allah? Mtume akanyamaza, akauliza mpaka mara tatu, akasema Mtume (S.A.W): Lau ningesema: Ndio ingekuwa wajibu (kila mwaka) na msingeweza”.
Na uwezo ni sharti katika kupasa Hija kwa mtu mwenye kukalifishwa na Sharia, Mwenyezi Mungu Anasema: (Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea)[Aal-Imran: 97].
Na imepitishwa kisharia kwamba uwezo ni sharti katika Hija, miongoni mwa uwezo kumiliki gharama za Hija ambazo ni maandalizi na kipando, na hizi ni sharti za kupasa, dhima inakuwa kwa sababu ya kupata sifa hizo, na kunapasa kufanya jitihada ili kutekeleza Ibada ya Hija, na dhima inaondoka muda wa kutopata sifa hizi, pia haipasi Hija kwa mtu mwenye kukalifishwa na sharia ima kwa kuwa vitu hivyo havipo kwenye uwezo wake, au kwa kuwa sharia haikumuwajibisha kwake.
Hivyo maana ni: Mtu kutomiliki mali wakati wa Hija unapelekea kutopasa ibada hii kwake, kwa namna kwamba akihiji wakati huo hana dhambi; kwa sababu kilichotangulia wajibu ambacho ni kupatikana mali au kuweka akiba kwa ajili ya kutimiza gharama za Hija si wajibu kama ilivyopitishwa na Wanazuoni wa Usuul Al-Fiqhi.
Ama kucheza mchezo – kama ilivyo kweye swali- kwa watu kujikusanya na kila mmoja anatoa kiasi maalumu cha pesa kila mwezi na kwa muda maalumu, na kila mmoja wao ana zamu maalumu ya kupokea pesa kila mwezi, ikiwa mchezo huo ni wa mwezi. Mpaka mwisho wa mchezo.
Mchezo ni katika miamala inayojuzu kisharia; kwa sababu ni katika njia za ushirikiano kwa wema na uchamungu, Mwenyezi Mungu Anasema: (Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui)[Al-Maidah: 2].
Tunaweka wazi kwamba: Washiriki katika muamala huu wanamtanguliza mtu mwenye uhitaji zaidi, kisha anayefuatia katika uhitaji, na kama hivyo, hii inaonesha makusudio ya asili ambayo ni kutoa katika njia ya kukopesha, na si kupata faida, na inajulikana kuwa kujitolea huhitaji msamaha na wepesi, na humo husamehewa mambo ambayo hayasamehewi katika mikataba ya kubadilishana (ya kibiashara). Baadhi ya Wanazuoni wa Fiqhi wa sasa wameeleza kujuzu kwa muamala huu.
Hivyo basi: kufanya juhudi kwa ajili ya kupata gharama za Hija kwa njia ya mchezo ni jambo la halali halina ubaya kisharia, lakini si wajibu; kwa sababu Hija wajibu kwa nafasi.
Na Sharia tukufu haikuondoa ibada kwa asiye na uwezo isipokuwa kwa kufanya wepesi na huruma, pamoja na hayo mtu akijikalifisha Hija pamoja na kufanya hivyo si wajibu kwake- kunamtosha kwa faradhi aliyotekeleza ikiwa imekamilika nguzo na sharti zake. Na ni sharti kwa mtu huyo kuacha pesa kwa jamaa zake na familia yake kipindi chote atakachokuwa katika ibada ya Hija; kwa sababu ghara hizi ni za lazima kwa uharaka, ikiwa kuzitanguliza ni bora na muhimu; kwa Hadithi iliyotolewa na Annasaaiy katika kitabu chake cha Sunan kutoka kwa Abdullah bin Amru R.A. amesema: “Inatosha mtu kupata dhambi kuwaacha na njaa wanaomtegemea”.
Na kwa haya ikiwa muulizaji ndio mtu wa kwanza kupokea pesa katika mchezo, kunapasa kwake kulipa pesa zote za mchezo kwa mpangilio, kwani desturi imehalalisha kutumia mali yote kwa kila mmoja wao baada ya kupokea, muda wa kuwa wanalazimika kulipa pesa ya mchezo kila mwezi kwa mujibu wa hali- na ameacha matumizi kwa watu anaowajibikia kuwagharamia, muda wa kuwa amewaeleza jamaa zake kuwa anacheza mchezo, kwa namna akifa jamaa zake watamalizia nafasi yake katika mchezo.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kucheza mchezo kwa ajili ya kupata gharama za Hija ni jambo linalojuzu kisharia
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
