Kutenga dua maalumu kwa kila siku y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutenga dua maalumu kwa kila siku ya Ramadhani

Question

Ninashirikiana na wenzangu kazini, katika kikundi kwenye programu moja ya mitandao ya kijamii, na wakati mwingine, mmoja wetu huchapisha hekima, Hadithi, dua, au jambo kama hilo. Siku chache kabla ya kuanza kwa Ramadhani, mmoja wa washiriki katika kikundi alichapisha makala ndefu yenye kichwa: "Dua Thelathini za Siku za Ramadhani." Tulipoisoma, tulipata dua ya siku ya kwanza, kisha dua ya siku ya pili ... na kadhalika hadi siku ya thelathini. Mmoja wa wenzangu alikemea hilo, akidai kwamba kutenga dua maalumu kwa kila siku ni uzushi ambao haukupokewa katika Hadithi. Je, ni nini hukumu ya Sharia katika hilo?

Answer

Kuandika kwa baadhi ya watu dua ya mwezi wa Ramadhani kwenye vikundi vya mitandao ya kijamii, katika mfumo wa dua ya kila siku, ili kuwakumbusha washiriki kuhusu ibada ya dua- inaruhusiwa na Sharia wakati wote na katika hali zote.

Maelezo

Dua ni mojawapo ya ibada bora na ni miongoni mwa ibada tiifu inayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamuru waja wake waumini kutakasa dua zao kwake yeye pekee, akasema: {Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni} [Ghafir 60].

Hakuna shaka kwamba dua ni kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtaja kumeamriwa wakati wote na katika kila mahali, katika aina zote, na katika hali zote. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mkisha Swali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala.Na mtapo tulia basi shikeni Swala kama dasturi. Kwani hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu.} [An Nisaa 103]

Na kuhusu yailiyotajwa katika swali, kwamba baadhi ya watu huandika dua kutokana na dua zilizotajwa katika Qur’ani Tukufu au Hadithi tukufu za Mtume (S.A.W), au dua za wema waliotangulia, kila siku miongoni  mwa siku za Ramadhani kwenye vikundi vya mitandao ya kijamii ili kuwakumbusha watu kuhusu tendo hilo la ibada, hilo ni tendo bora kutokana na Sharia ya Kiislamu, na lina msingi katika Sunna za Mtume (S.A.W) kutenga baadhi ya siku kwa ibada maalumu, Imepokewa Hadihi kutoka kwa Abdullah Ibn Omar R.A., alisema: “Mtume (S.A.W.), alikuwa akija Msikiti wa Qubaa’ kila Jumamosi, akitembea na wakati mwingine akiwa amepanda farasi.” Abdullah Ibn Omar R.A., alikuwa akifanya vivyo hivyo. (Hadithi hii imepoklewa na Bukhary na Muslim). Kauli yake, “kila Jumamosi,” inaonesha ruhusa ya kutenga siku fulani kwa kutembelea na kufanya matendo mema, na kudumu katika kufanya hivyo.

Baadhi ya watu kukemea ruhusa ya kutenga dua maalumu kila siku miongoni mwa siku za Ramadhani ili kuwakumbusha watu kuhusu ibada hiyo, kwa kudai kwamba ni uzushi ambao haujatajwa katika Hadithi, si sahihi na hakukubaliki.

Wanazuoni walipozungumzia kuhusu uzushi wamesema kwamba ni jambo ambalo limezuka miongoni mwa mambo amabayo hayana asili katika Sharia ya Kiislamu unaoliashiria, ama kuhusu lile ambalo lina asili katika Sharia ya Kiislamu unaoliashiria, si uzushi kisharia, hata kama litaitwa Bidaa (uzushi), katika lugha.

Wanazuoni waliochunguza jambo hilo wamegawanya Bidaa nzuri na Bidaa mbaya, au: katika Bidaa potofu na Bidaa ya uongofu. Bidaa ya uongofu ni ile inayolingana na mafundisho ya Uislamu na Misingi ya Sharia, na hiyo ndio maana ya Hadithi ya Jarir Bin Abdullah, R.A, kutoka kwa Mtume (S.A.W.), ambaye amesema: "Yeyote anayeanzisha Sunna nzuri katika Uislamu, na ikaitendwa baada yake, atapata thawabu kama ile ya wale wanaoitenda, na hakitakapunguzwa katika thawabu zao chochote." Imepokelewa na Muslim.

Na ama kuhusu Bidaa ya upotovu, ni ile ambayo haiendani na makusudio ya Sharia na misingi yake, na ndio ambayo Mtume, (S.A.W), aliikusudia aliposema: “Yeyote atakayeanzisha Bidaa mbaya katika Uislamu, na ikafuatwa baada yake, atakuwa na dhambi kama zile za wale wanaoufuata, na hakitapunguzwa katika dhambi zao chochote.” Imepokelewa na Muslim.

Vile vile, katika Hadithi ya Al-`Irbaadh Ibn Sariyah R.A., kutoka kwa  Mtume (S.A.W) amesema: "Jihadharini na mambo yaliyozushwa, kwani kila jambo lilizushwa ni  Bidaa na kila Bidaa ni upotovu." Hadithi hii imetolewa na At-Tirmidhi katika kitabu chake cha Al-\Jamii. Ni kwa uelewa huo wa Hadithi zilizotajwa hapo juu, na kwa ujumaisho na kuafikiana kwa matini zake, ndio wamefuata Maimamu wa Uislamu na Wanazuoni wa Umma huu.

Na yayofanywa na baadhi ya watu ikiwemo kuandika machapisho kwenye vikundi vya mitandao ya kijamii yanayojumuisha hekima, Hadithi, au dua- kama vile “Dua Thelathini za Siku za Ramadhani,” kama ilivyo katika swali-  inazingatiwa ni miongoni mwa mambo yanayopendeza katika Sharia ya Kiislamu, na ni Bidaa nzuri yenye msingi katika Sharia ya Kiislamu, inayowakumbusha watu kuomba dua, kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumkaribia zaidi.

Na hilo ni muhimu hasa kutokana na watu na kujishughulisha na kazi, kutimiza mahitaji yao, na kukabiliana na mzigo wa maisha. Na kitendo kinachopendekezwa kisharia ambacho mtu hulipwa thawabu. Abu Mas'ud Al-Ansariy R.A., anasimulia: "Mtu mmoja alimjia Mtume (S.A.W.) na kusema: “Nimekatikiwa safarini kutokana na kifo cha ngamia[1].; tafadhali nipe ngamia.' Mtume akajibu, 'Sina kitu.' Kisha mtu mwingine akasema, 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, naweza kumwonesha mtu anayeweza kumpa ngamia.' Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akasema, 'Yeyote anayemwongoza mtu katika jambo jema atapata thawabu sawa na ile ya yule anayeyafanya.'" (Imepokelewa na Muslim). Hadithi hii inaangazia wema wa kuwaongoza wengine kwenye mema, kuwavutia watu kuyazingatia, na kuwasaidia wale wanaoyafanya. Pia inaonesha wema wa kufundisha maarifa na wajibu wa ibada, hasa kwa wale wanaoyafanya sana, miongoni mwa ibada na wengineo.

Tunapata faida Kutokana na yaliyotangulia:

Dua ni miongoni mwa ibada tukufu zaidi na inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kufanya dua maalumu kila siku miongoni mwa siku za Ramadhani ili kuwakumbusha watu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ni jambo linalojuzu na kupendekezwa.

 

[1] - Yaani, nilikatishwa na usafiri kutokana na kifo au udhaifu wa ngamia.

Share this:

Related Fatwas