Kufunga Maduka ya Biashara Wakati w...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufunga Maduka ya Biashara Wakati wa Sala ya Ijumaa

Question

Maduka ya biashara wakati wa Sala ya Ijumaa tunatakikana tuyafanye nini? Je tuyafunge ili kuheshimu alama za dini (ibada) au inatosha kusitisha uuzaji na ununuzi wakati wa sala?

Answer

Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., watu wake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:
Siku ya Ijumaa ni moja ya matukio maalumu ya aina yake kwa umma wa Mtume Muhammad S.A.W., imepokewa hadithi ya Mtume s.a.w isemayo " Mwenyezi mungu hakuijaalia siku ya Ijumaa kwa watu waliotutangulia, mayahudi siku yao maalum ilikuwa Jumamosi na manasara ikawa Jumapili. Allah alipotuleta sisi (Umma wa Muhammsd S.A.W.) siku yetu maalumu alituongoza kuelekea siku ya Ijumaa, akazijaalia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuwa ni zetu, na wao (Mayahudi na Manasara) wakawa ni wafuasi wetu mpaka siku ya Kiyama, sisi ni wa mwisho duniani na ni wa mwanzo kuhukumiwa siku ya kiyama kabla ya viumbe vyote" [Imepokelewa na Muslim].
Aidha, siku ya Ijumaa ni Idi kwa waislamu, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. [Ameitoa Ahmad], na Ijumaa ni siku bora kuliko siku zote za wiki. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameichagua siku ya Ijumaa kwa kuijaalia sifa kemkem kutokana na ubora wake na daraja yake. Muslim amepokea kutoka kwa Abu Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. alisema: "Sala tano, na Ijumaa mpaka Ijumaa ni kafara yenye kufuta madhambi yaliyo baina yake madamu hayakufanywa madhambi makubwa" [Imepokelewa na Muslim], Na kutoka kwa Abu Huraira R.A. alisema: Mtume S.A.W. alisema: "Siku bora ya kuchomoza jua ni siku ya Ijumaa; katika siku hiyo Adam aliumbwa, katika siku hiyo aliingizwa peponi na katika siku hiyo alitolewa peponi na Kiyama hakitosimama isipokuwa katika siku ya Ijumaa", [Imepokelewa na Muslim].
Na atakayekufa siku ya Ijumaa au katika usiku wake, Mwenyezi Mungu mtukufu amemkinga na fitina ya kaburi. Kutoka kwa Abdullahi Ibn Amro R.A. alisema: Mtume S.A.W. alisema: "Hakuna Mwislamu yoyote anaekufa siku ya Ijumaa au katika usiku wake, ila Mwenyezi Mungu Mmtukufu amemkinga na fitina ya kaburi" [Imepokelewa na Ahmad na Al Tarmaziy].
Na kutokana na ubora huu, basi siku ya Ijumaa inasifika kwa fadhila mbalimbali, inapendeza kwa (ni sunna) mwislamu asighafilike nazo, na miongoni mwa mambo ya Sunna katika siku ya Ijumaa ni kuoga, kuvaa nguo nzuri na safi hasa nguo nyeupe, kutia manukato, kukithirisha kumsalia na kumtakia rehma Mtume S.A.W. na kusoma surat AL KAHF, na miongoni mwa mambo ya Sunna katika siku ya Ijumaa ni kwenda msikitini mapema kwa ajili ya Sala ya Ijumaa. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Huraira R.A. kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Atakayeoga siku ya Ijumaa kama anavyooga janaba, kisha akaenda (msikitini) saa ya kwanza (mapema sana), atakuwa ni kama aliyetoa sadaka ya ngamia. Na atakayeenda katika saa ya pili, atakuwa ni kama aliyetoa sadaka ya ng'ombe. Na atakayeenda katika saa ya tatu, atakuwa ni kama aliyetoa sadaka ya kondoo mwenye pembe. Na atakayeenda katika saa ya nne, atakuwa ni kama aliyetoa sadaka ya kuku. Na atakayeenda katika saa ya tano, atakuwa ni kama aliyetoa sadaka ya yai. Tambueni Imamu anapopanda juu ya mimbari, Malaika wanahudhuria ili kusikiliza mawaidha." [Bukhari na Muslim].
Ni wajibu juu ya kila inayomlazimu Sala ya Ijumaa kuiharakia, kwa lengo la kuitikia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; { Enyi mlioamini! Inaponadiwa (adhana ya) Sala ya Ijumaa, kimbilieni kwenye dhikri ya Allah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.}, [AL JUMUA,9].
Al Qurtubiy anasema: "Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {kimbilieni kwenye dhikri ya Allah } yaani Sala. Na wapo waliosema maana yake ni hotuba ya Ijumaa na mawaidha, Said Bin Jubair Ibn Al Arabiy alisema hayo. Na kauli yenye nguvu yote ni wajibu (sala, hotuba na mawaidha), na katika mstari wa mbele ni hotuba. Wanavyuoni wetu walisema kauli hiyo pia, isipokuwa Abdulmalik Bin Al Majeshon aliyesema kuwa ni Sunna. Na dalili ya uwajibu wake ni kwamba Sala ya Ijumaa inaharamisha kuuza, na laiti kama si uwajibu wake basi sala isingeharamisha kuuza, kwani jambo la Sunna haliharamishi jambo halali. Na tukisema kuwa maana ya Dhikri katika aya hiyo ni Sala basi hotuba ni sehemu ya Sala" [18/107, Ch. Dar Al Kotoob Al Masriya].
Na mtu inayomlazimu Sala ya Ijumaa, ni haramu kwake kuuza katika wakati wa Sala hiyo, Sheikh wa Uislamu Zakariya Al Ansariy alisema: "Ni haramu kwa inayomlazimu Ijumaa kufanya kazi kama kuuza, ufundi n.k, kazi ambayo itamshughulisha mpaka aghafilike na Sala ya Ijumaa baada ya kuanza adhana ya hotuba. Mwenyezi Mungu mtukufu amesema: {Inaponadiwa (adhana ya) Sala siku ya Ijumaa, kimbilieni kwenye dhikri ya Allah na acheni biashara.}. Yaani mwuache kuuza, na kitendo cha amri hapa kinamaanisha ni lazima kuacha kuuza , basi inaharamishwa kuuza. [Sharh Al Manhaj pamoja na Hashiat Al Bijiamiy, 2/54, Ch. Dar Al Fikr].
Ni wajibu juu ya mtu inayomlazimu Sala ya Ijumaa asishughulishwe na kuuza au mfano wake kiasi ambacho akakosa kuhudhuria Sala, na inakusudiwa baada ya adhana ya pili. Wanachuoni wa Fikhi walihitilafiana katika usahihi wa mkataba katika wakati wa katazo unaofanywa na mtu inayomlazimu Ijumaa.
Ama kuhusu Sala la kufunga maduka ya biashara wakati wa Sala ya Ijumaa basi Sala hili haliingii katika kipengele cha kubeba jukumu kisheria kwa kuwajibisha au kuharamisha, na mtu anayefuatilia kauli za wanachuoni wa madhehebu hawezi kutoa uamuzi wa mwisho kwamba kufunga maduka ya biashara wakati wa Sala ya Ijumaa ni miongoni mwa mambo yanayokubaliwa na wanavyuoni na hayana hitilafu, pia tukisoma kauli za wanachuoni tunaweza kusema kwamba kufunga maduka ni kwa ajili ya maslahi ya pamoja na kuzuia madhara, haya yanadokezwa na kauli za Msomi wa madhehebu ya Malik..
Al Disuqiy anasema katika [Hashia yake juu ya Al Sharh Al Kabeer] kwenye kauli yake: " Wamiliki wa soko wafunge soko kwa yule ambaye Ijumaa inamlazimu au kwa yule isiyomlazimu, wakati wa sala", " Na inapendeza kwa mtu isiyomlazimu Ijumaa kufunga duka hata kama ni kafiri ili asije akawashughulisha watu ambao Ijumaa kwao ni lazima, kwani yule ambaye asiyelazimika kuswali sala ya Ijumaa kama atafungua duka wakati wa sala ya Ijumaa atakuwa anakusanya faida jambo ambalo litamdhuru yule anaelazimika kuswali Ijumaa. Kwa hiyo na yeye ingawa Ijumaa si lazima kwake basi anatakikana afunge duka ili kuchunga maslahi ya wengi", [1/382, Ch. Dar Al Fikr].
Al Kharashiy alisema katika kitabu cha [Manh Al Jalil]: "Imamu anawaamrisha wamiliki wa soko kuacha kuuza na kununua kwa watu ambao Ijumaa inawalazimu, hali hii inaambatana wa wakati wa hotuba ya Ijumaa yaani tangu pale Imamu anapokaa juu ya mimbari hadi kumaliza sala kwa kutoa salamu, Na isiyomlazimu Ijumaa afunge duka ili asije akamshughulisha mtu inayomlazimu, kwani isiyomlazimu kama atafungua duka wakati wa sala ya Ijumaa atakuwa anakusanya faida jambo ambalo litamdhuru inayomlazimu Ijumaa hiyo. Kwa hivyo na yeye isiyomlazimu Sala ya Ijumaa anatakikana afunge duka ili kuchunga maslahi ya wengi. [1/437, Ch. Dar Al Fikr].
Na kuna tofauti baina ya kufunga maduka ya biashara na kutojuzu kuuza wakati wa Sala ya Ijumaa. Inajuzu kufungua maduka lakini shughuli za kuuza zikasita wakati wa Sala, na inajuzu kwa mtu isiyomlazimu Ijumaa kuuza kwa mfano mwanamke, na hivi ndio baadhi ya watu wanavyofanya. Maalikiya wanasema ni vizuri na inapendeza Imamu kuwalazimisha wamiliki wa masoko kufunga maduka kwani kufanya hivyo ni maslahi ya umma.
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu, mtu inayomlazimu Ijumaa ni wajibu kwake kutouza na kutonunua wakati wa adhana ya pili na wakati wa sala. Ama mtu isiyomlazimu Ijumaa ni sunna kwake asimuuzie mtu inayomlazimu Ijumaa kwa sababu mmoja hapa ni wajibu kwake faradhi lakini anashughulishwa na mtu mwingine.

Ama kufunga maduka wakati wa sala ya Ijumaa si wajibu wa kidini bali ni jambo linalomhusu Imamu. Na huachwa kwa ajili ya maslahi ya jamii ambayo hubadilika kwa mujibu wa nchi husika. Matamshi haya hayamaanishi kupuuza utekelezaji wa sala ya Ijumaa au ishara ya kuharibu alama za dini (ibada).
Na Mwenyezi Mungu mtukufu ni mjuzi wa yote.
 

Share this:

Related Fatwas