Malipo ya pesa kwa ajili ya Ruqyah ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Malipo ya pesa kwa ajili ya Ruqyah (kutibu) kwa Quraani

Question

Ni ipi hukumu ya kulipwa fedha kwa ajili ya kutibu kwa Quraani?

Answer

Shukrani anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na rehma na amani ziwe juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, watu wake, masahaba wake, na waliomfuata. Baada ya hayo,
Maana ya Ruqyah katika lugha ni: kujilinda, Ibn Al-Athir anasema: Ruqyah ni ni kinga ambayo mtu anaitumia ili kujikinga kutokana na maradhi kama kama vile homa, kifafa na mengine mengi. [Lesan Al-Arab 20/1711 , Dar Al-Maarif.]
Katika istilahi Al-Adawi anaieleza katika kitabu chake: Ruqyah ni kitu kinachotibu kama vile dua ambayo huwa maombi ya uponyaji. [Hashita Al-Adawi ala Kifayat Al-Talib Al-Rabani 2/489 , Dar Al-Fikr.]
Wanavyuoni wanasema Ruqyah inaruhusiwa kwa kila ugonjwa aupatao binadamu kwa sharti moja tu, nalo ni kuwa dua hiyo kwa maneno ya Mwenyezi Mungu, au majina yake na sifa zake. Na iwe kwa lugha ya Kiarabu, au kwa maneno mengine yanayofahamika. Na tuamini kwamba Ruqyah haiathiri peke yake, lakini huathiri kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na uwezo wake, kutokana na Hadithi iliyopokelewa na Muslim kutoka kwa Auf bin Malik R.A. anasema: (Tulikuwa tukifanya Ruqyah katika zama za ujinga na tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unalionaje jambo hilo? Mtume S.A.W akasema: Nioneshe Ruqyah yenu, hakuna kitu kibaya katika jambo hilo kama hakuna ushirikina).
Katika kitabu cha Al-Um: (Al-Rabii anasema: Nilimuuliza Al-Shafii kuhusu Ruqyah akasema: Kama mtu anatibu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu na anayoyajua miongoni mwa yale ya kumtaja Mwenyezi Mungu, basi hakuna kitu kibaya katika jambo hilo). [ 7/241 , Ch. Dar Al-Maarifa.]
Ama kuhusu hadithi zinazozuia kufanya Ruqyah zinakusudiwa kama ikiwa Ruqyah bila ya majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, au ilikuwa kwa lugha isiyo ya Kiarabu, au ikiaminika kuwa Ruqyah peke yake ndio inayoathiri .
Ama kuhusu kulipwa pesa kwa ajili ya kufanya Ruqyah (kutibu kwa Quraani), wanavyuoni wengi wanasema ni halali. Na wanathibitisha hivyo kwa hadithi ya Abu Saed Al-Khudaryi R.A iliyopokelewa katika Bukhari na Muslim, akisema: (tulikuwa katika safari, Tukashuka, basi mtu mmoja akaja, akasema: bwana wa eneo hili ameumwa na nge, na sasa hakuna mtu wa kumtibu, je, kuna yoyote miongoni mwenu anaejua kutibu kwa mfumo wa Ruqyah? akasimama mtu ambae hatukujua kuwa alikuwa ana uwezo wa kutibu kwa Ruqya, na akamtibu na mtu yule akapona. Basi mtu yule akaaamrisha zitolewe kondoo thelathini (kama zawadi) na akatunywesha maziwa. aliporudi yule mganga, tukamuuliza: je, ulikuwa unaijua vizuri Ruqyah, au ulikuwa ukifanya Ruqyah tu? akasema: Hapana, nilifanya Ruqyah kwa Quraani tu, tukasema: msifanye kitu chochote mpaka tufike nyumbani, na tumwulize Mtume S.A.W., na tulipofika Madina tulimtaja mtu huyo kwa Mtume S.A.W., akasema: Yule mtu alijuaje kwamba hiyo ni Ruqyah? gawanane zawadi ile na mimi mnipe sehemu yangu.
Badr Al-Din Al-Inyi anasema: (Ruqyah ni aina ya dawa, na kinachochukuliwa kutokana na Ruqyah ni kama zawadi, na inaruhusiwa kupokea malipo kwa ajili ya kutibu. [Al-Binayah Sharhu Al-Hidayah 10/281, Ch. Al-Maktaba Al-Elmiyah].
Shihabuddin Al-Nafrawi Al-Malikyi anasema: (Inaruhusiwa kuchukua malipo kwa ajili ya Ruqyah, kama katika kisa maarufu -katika sehemu ya zawadi- cha mtu aliyeumwa na nge, basi mmoja wa masahaba alimfanyia Ruqyah). [Al-Fawakeh Al-Dawani Sharhu Resalatu Al-Qayrawanyi 2/340, Ch. Dar Al-Fikr).
Ibn Hajar alisema: (Inaruhusiwa kutoa zawadi iliyo halali kwa ajili ya Ruqyah kama yalivyotangulia juu, pia kwa ajili ya kumuuguza mgonjwa na kutoa dawa kwake, hata ikiwa ni mnyama, na pakiainishwa kitu kama vile kupona na mgonjwa akapona, basi hili linastahiki kilichoainishwa, au malipo ya kawaida. [Tohfatu Al-Muhtaj Fi Sharhi Al-Minhaj 6/372, Ch. Al-Maktaba Al-Tujariya Al-Kubra].
Ibn Qudaamah anasema: "Kuhusu kupokea malipo kwa ajili ya Ruqyah, Imam Ahmed alichagua kwamba jambo hilo linaruhusiwa, na akasema hakuna kitu kibaya ndani yake. Na ametaja hadithi iliyopokelewa na Abu Saed. Tofauti kati yake na yale waliotofautiana wanazuoni katika ile Hadithi ni kwamba Ruqyah ni aina ya matibabu. Na kinachopokelewa kutokana nayo ni zawadi. Na inaruhusiwa kuchukua zawadi kwa ajili ya kutibu. Na zawadi ni pana zaidi kuliko malipo. Kwa hivyo inaruhusiwa pamoja na kutojua kazi inayofanyika na muda wake. Mtume S.A.W. anasema: (Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Quraani) kinastahili kulipwa kuliko kitu kingine chochote), pia ina maana ya kuruhusiwa kuchukua malipo kwa ajili ya Ruqyah; kwa sababu imesemwa hivyo katika hali ya Ruqyah". [Al-Mughnyi 5/412, Ch. Maktabat Al-Kahira].
Eltahawy alisema: "Si kosa kukodisha Ruqyah na matibabu kwa ujumla, ingawa tunajua kwamba pengine mpangaji atafanya Ruqyah kwa Quraani, kwa sababu siyo wajibu kwa watu kufanya hivyo kwa kila mmoja, basi kama wakipanga kwa ajili ya kufanya kitu fulani kisicho wajibu juu yao, basi hivyo inaruhusiwa". [Sharhu Maani Al-Athar 4/127, Ch. Dar Al-Maarifa].
Ibn Hazm alisema: "inaruhusiwa kukodisha kwa ajili ya kufundisha Qurani, na elimu kwa jumla, na yote ni halali, na kuhusu kufanya Ruqyah, na kunakili kwa Quraani, na vitabu vya maarifa; kwa sababu hakuna matini kutoka Qurani au hadithi za Mtume zinazohusu kukataza jambo hilo, lakini yaliokuja na kupokelewa yanahusu uhalali wa jambo hilo, ni maoni ya Imam Malik, Shafi'i, na Abu Sulaiman". [Al-Mahalyi kwa Ibn Hazm 7/18, Ch. Dar Al-Fikr.]
Al-Sanaani alisema: "Al-Bukhari kutaja kisa cha Abu Saed ni ushahidi kuwa inaruhusiwa kuchukua malipo kwa ajili ya Quraani, kwa ajili ya kuunga mkono malipo kwa ajili ya kusoma Quraani, kwa ajili ya kuifundisha au vinginevyo, na hakuna tofauti kati ya kusoma Quraani kwa ajili ya kuifundisha na kuisoma kwa ajili ya kutibu". [Subl Al-salam kwa Sanaani 2/117, Ch. Dar Al-Hadith].
Kwa mujibu wa yaliyotangulia: inaruhusiwa kuchukua malipo kwa ajili ya kufanya Ruqyah kwa Quraani tukufu, kwa kila ugonjwa, sharti iwe ni kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu, au kutoka katika majina na sifa zake, na kwa lugha ya Kiarabu, au kwa yale yanayojulikana maana yake, na kuamini kwamba kufanya Ruqyah hakuathiri peke yake, lakini anayeathiri ni Mwenyezi Mungu mwenye kutibu kwa upole mkubwa na uwezo wake. Na tunapaswa kujihadhari na waganga ambao wanadanganya watu na wanachukua malipo kwa udanganyifu wakidai kwamba hii ni Ruqyah. Ni bora kwenda kwa watu wema ambao wanajulikana kwa uaminifu na uadilifu wao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas