Kushirikiana na asiye mwislamu kati...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushirikiana na asiye mwislamu katika Udh-hiya (Kuchinja mnyama wakati wa Eid El Adh-haa).

Question

Nini hukumu ya asiye mwislamu kushirikiana na mwislamu katika kuchinja ng’ombe au ngamia wakati wa Eid El Adh-haa?

Answer

Alhamdulilla, na sala na salamu ziwe juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, watu wake, masahaba wake na wafuasi wake. Baada ya hayo:

          Udh-hiya kisheria ni jina la mnyama anayechinjwa kama ngamia, ng’ombe na kondoo siku ya kuchinja na siku za Tashriki (siku tatu za sikukuu), kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Na Udh-hiya imewekwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwasaidia masikini wakati wa sherehe za Iddi kubwa. Na hii ni Sunna ya baba yetu Nabii Ibrahim, kama alivyoashiria Mtume Muhammad S.A.W. katika hadithi yake iliyopokelewa na Ahmad, Ibn Majah na Tirmidhiy kutoka kwa Zaid Ibn Arqam, mtu mmoja alisema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: hivi Vichinjo ni kitu gani? Mtume S.A.W akasema: (Sunna ya baba yenu Ibrahim), pakaulizwa: Tuna faida gani kutoka kwake?: akasema: (kila unywele mmoja ni jema moja), pakasemwa: Na sufi je? Mtume S.A.W akasema: “kila unywele mmoja unaotokana na sufi ni jema moja”.

         Kuchinja huku ni Sunna nzuri, wanachuoni wanahitalifiana katika kuwa kwake ni wajibu juu ya matajiri au ni Sunna. Al Nawawiy anasema: “Wanachuoni walihitalifiana katika wajibu wa Udh-hiya kwa mtu tajiri” Aghalabu ya wanachuoni wanasema: Udh hiya ni Sunna juu yake, akiacha bila ya udhuru hakuna dhambi juu yake, na halazimiki kulipa. Na miongoni mwa waliosema kauli hii ni Abubakar Siddiyq, Omar Ibn Al Khattab, Bilal, Abu Masoud Al Badriy, Said Ibn Al-Musib, Al Qamah Al Aswad, Ataa, Malik, Ahmad, Abu Yusuf, Ishaq, Abu Thawr, Al Mazeny, Ibn Mundhir, Daud, n.k. Ama Rabiyah, Al awzaiy, Abu Hanifa na Allayth walisema: Udh-hiya ni wajibu juu ya tajiri. Pia baadhi ya wafuasi wa Imamu Malik walisema kauli hii”. [Sharh Sahih Muslim, 13/110, Ch. Dar Ihyaa Al Turaath Al Arabiy).

         Na kuchinja (Udh-hiya) mbuzi mmoja inatosha kwa mtu mmoja au kwa familia yake. Na kuchinja (Udh-hiya) ng’ombe mmoja au ngamia mmoja inatosha kwa watu saba. Imamu Muslim amepokea kutoka kwa Jabir ibn Abdullah amesema: (Tulichinja pamoja na Mtume S.A.W. mwaka wa Al Hudaibiah, ngamia mmoja kwa watu saba, na ng’ombe mmoja pia kwa watu saba, na subuu (sehemu moja katika saba) ya kila mtu ni kama kondoo mmoja kwa kila mtu) .

         Na inajuzu kushirikiana katika kuchinja (Udh-hiya) kwa nia mbalimbali, kwa mfano baadhi nia yao ni kujikurubisha kwa Allah S.W, na baadhi wanataka nyama, hata kama atashiriki asiyekuwa mwislamu. Dalili ya haya ni kauli ya Mtume S.A.W “Hakika matendo yanafungamana na nia”.[Muslim na Bukhary].

         Al Zarkashiy amesema: “Inajuzu kushirikiana katika kuchinja (Udh-hiya), hata kama baadhi nia yao ni kutaka nyama na baadhi nia yao ni kutaka kujikurubisha kwa Allah S.W, basi inajuzu”. (Al Manthur fil Qawaid, 2/103, Ch. Wizara ya Al-awqaf, Kuweit).

         Na Al Bahutiy amesema: “Inajuzu kuchinja ngamia mmoja au ng’ombe mmoja kwa watu saba, imepokolewa hadithi ya Jabir kutoka kwa Ali, Ibnu Masoud, Ibn Abbas na Aisha “Tulichinja pamoja na Mtume S.A.W mwaka wa Al Hudaibiah, ngamia mmoja kwa watu saba, na ng’ombe mmoja pia kwa watu saba”. Imepokelewa na Muslim.

          Na kuchinja ngamia au ng’ombe inategemea na nia, Mtume S.A.W. anasema “Hakika matendo yanafungamana na nia”, sawa nia yao wote ni kujikurubisha kwa Allah S.W. au baadhi yao ndio wanataka kujikurubisha au baadhi yao wanataka nyama. Pia hata kama baadhi yao ni waislamu wanataka kujikurubisha kwa Allah S.W. na baadhi yao si waislamu, cha msingi kila mmoja ana nia yake, kwa sababu malipo ya mwenye kutaka kujikurubisha kwa Allah S.W. hayapungui kwa kushiriki asiye kuwa na nia kama hiyo. [Sharh Muntaha Al Iradat, 1/602, Ch . Alam Al Kutub).

Share this:

Related Fatwas