Eda ya mwanamke wa Ahlu Kitabi (wat...

Egypt's Dar Al-Ifta

Eda ya mwanamke wa Ahlu Kitabi (watu wa kitabu – waliopewa Taurat na Injil)

Question

Ni ipi eda ya mwanamke wa Ahlu kitabi kama ameachwa na mumewe Mwislamu na anataka kumrejea, au kama Mwislamu mwingine anataka kumwoa?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Baadhi ya Waislamu wanamwoa mwanamke Mkristo au Myahudi, kisha pengine wanaachana. Swali ni: Je, mke huyu wa Ahlu kitabi ana eda?

Kwa mujibu wa sheria, tunaona kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameruhusu kuwaoa wanawake waliopewa kitabu: kama mayahudi au manasara; kama ilivyoelezwa katika Quraani tukufu: {Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini bila shaka amali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.} [Al-Maidah: 5].
Mume na mke inawezekana kutengana, siyo kwa talaka tu, lakini kwa talaka, inawezekana kwa kuibatilisha ndoa, na pia kwa kifo, na katika kila hali zilizotangulia mke ana eda.

Eda katika lugha imechukuliwa kutoka neno idadi; kwa sababu mara nyingi inahusiana nayo, Al-Azhari alisema: “Eda ya mwanamke ni miezi au Kuruu, au kuzaa mimba ya mume anayemkalia eda”.

Ama eda katika sheria ya Uislamu ni kama alivyosema Sheikh Zakaria Al-Ansari: “Ni muda ambao mwanamke hukaa nyumbani mwake kwa ajili ya kujua kilichomo ndani ya fuko la uzazi, au kwa ajili ya kuabudu, au kwa ajili ya huzuni yake juu ya mumewe” (Ansa Al-Matalib 3/389, Dar Al-Kitab Al-Islamiy).

Kuhusu uamuzi wa kisheria juu ya suala hilo ni: mke aliyepewa kitabu ni wajibu kukaa eda iwapo kaachwa au kwa jambo jingine kama ilivyotangulia hapo juu.

Dalili ya hayo ni dalili za ujumla zilizomo katika milango ya eda katika vitabu vya Fiqhi, kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu talaka: {Na wanawake walioachwa wangoje peke yao mpaka tohara (au hedhi) tatu zipite. Wala haifai kuficha alichoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.} [Al-Baqarah: 228], na katika kauli ya Mwenyezi Mungu kuhusu kifo: {Na wale miongoni mwenu wanaokufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi minne na siku kumi.} [Al-Baqarah: 234]. Ushahidi: matini hazikutofautisha kati ya mke Mwislamu na mke aliyepewa kitabu.

Neno "au" katika kuainisha maana ya eda halizuii ukusanyaji wa aina mbali mbali zilizotajwa, Al-Bujayrimiy anasema katika kitabu chake “Al-Iqnaa”: kauli yake: “(kwa ajili ya kujua kilichomo ndani ya fuko lake la uzazi) yaani ni nani yule atakaezaliwa.Na kauli yake: "au" kwa ajili ya huzuni yake... nk. yaani: kwa kufiwa kwake. Mifano hiyo iko kila sehemu ikiwa peke yake. Na huwenda ikakusanyika -katika tamko hilo- kuabudu na huzuni katika hali ya kifo kwa asiyetarajia kuzaa mtoto au kabla ya kuingiliwa, na pengine hukusanyika pamoja katika kujua kilichomo ndani ya fuko la uzazi na huzuni kwa anayetarajia kuzaa mtoto kwa sababu ya msiba uliotokea. Na pengine mambo matatu hukusanyika pamoja kama ilivyo katika mfano huo, kwa sababu eda ina aina ya kuabudu daima, na kukusanyika sehemu zenyewe kwa zenyewe kunachukuliwa kutokana na kutajwa neno “au” kwa sababu neno hilo linazuia kutokuwepo kwa mambo yote, lakini linaruhusu kuyakusanya mambo hayo pamoja. [Hashiat Al-Bujayrimi alaa Al-Iqnaa fi Hal Alfadh Abi Shujaa lelkhatib Al-Sherbini 4/41, Dar Al-Fikr]. Na hali hiyo inazuia kwamba ibada ni mahitaji ya kisheria tu, na kauli ya Mwenyezi Mungu inaelezea hivyo: {basi hamna eda juu yao mtakayo izingatia} [Al-Ahzab: 49] Allah s.w amejaalia eda kuwa ni haki ya mume.

Inawezekana eda ni haki ya waja au ni kuabudu, na haki za waja zinamlazimu mwanamke Mwislamu na aliyepewa kitabu kuzifanya, kwa hiyo, inamlazimu mwanamke aliyepewa kitabu kutekeleza eda.

Imamu Shafiy anasema: “Mwanamke huru na aliyepewa kitabu ni sawa kama mwanamke mwislamu huru hawatofautiani kuhusu eda, matumizi, na makazi akiwa mume mwislamu amemtaliki au amekufa, basi kila yanayomlazimu mwanamke mwislamu yanamlazimu aliyepewa kitabu kama vile kuomboleza nk., na akisilimu katika muda wa eda kabla ya kuimaliza, basi anaendelea kuimaliza eda yake, na pia kama mume aliyepewa kitabu akimtaliki au akifa, na mke akitaka kutoka nyumbani katika muda wa eda, basi mume wake akiwa na uhai anaweza kumzuia kutoka, na akiwa amekufa, basi wenye kumrithi mumewe wanaweza kumzuia mke kutoka kama wanaweza kumzuia mwanamke mwislamu sawasawa hakuna tofauti baina yao katika chochote isipokuwa mke aliyepewa kitabu hamrithi mumewe mwislamu wala yule mumewe mwislamu hamrithi mkewe aliyepewa kitabu.” [Al-Om 5/230, Dar Al-Maarifa].

Al-Kasaani anasema: “Iwapo mwanamke Mwislamu au aliyepewa kitabu ameolewa na mume Mwislamu, basi mwanamke Mwislamu huru ni sawa na mwanamke huru aliyepewa kitabu na mwanamke Mwislamu mtumwa ni sawa na mwanamke mtumwa aliyepewa kitabu, Kwa sababu eda inalazimika kwa haki ya Mwenyezi Mungu, na kwa haki ya mume, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {basi hamna eda juu yao mtakayo ihisabu} [Al-Ahzab: 49] Na mwanamke aliyepewa kitabu analazimishwa kwa haki za waja, na pia analazimishwa eda kwa ajili ya haki ya mume na ya mtoto, kwa sababu mwanamke aliyepewa kitabu ni miongoni mwa wanaotekeleza haki za waja”. [Badaai Al-Sanaai 3/191, Al-Maktaba Al-Elmiya].

Ibn Qudamah anasema: “Eda inamlazimu mwanamke wa dhimma aliyeolewa na mume wa dhimma au Mwislamu, Abu Hanifa anasema: “Akiwa mwanamke huyo ana dini nyingine tofauti na mume, basi haimlazimu, kwa sababu wao hawasemeshwi kwa matawi ya dini, na tuna aya kwa ujumla, na kwa sababu mwanamke yule ameachika kwa, basi ni sawa na mwanamke Mwislamu, na eda yake ni kama eda ya mwanamke Mwislamu, kwa mujibu wa maoni ya wanavyuoni miongoni mwao ni Maliki, Al-Thawri, Al-Shafii, Abu Obaida, na wenye maoni na wanaowafuata, isipokuwa ilivyopokelewa kwa Malik anayesema: Eda ya kifo ni hedhi moja, lakini sisi tunashikilia kauli ya ujumla ya Mwenyezi Mungu: {Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi minne na siku kumi.}. [Al-Baqarah: 234], na kwa sababu yeye ana eda kwa ajili ya kifo, basi ni kama mwanamke Mwislamu”. [Al-Mughni 8/96, Maktabat Al-Qahira].

Kwa mujibu wa yaliyotangulia hapo juu inaonekana kwamba mke aliyepewa kitabu akitalikiwa na mumewe Mwislamu, basi mwanamke huyo analazimika kukaa eda kama wanawake Waislamu, na pia anapewa matumizi na makazi kama wanawake Waislamu, jambo hilo linatofautiana kwa mujibu wa tofauti ya hali, basi akiwa miongoni mwa wenye hedhi, eda yake itakuwa kuoga mara tatu, au akiwa siyo miongoni mwa wenye hedhi, eda yake itakuwa miezi mitatu, na akiwa na mimba, basi eda yake itakuwa mpaka pake atakapojifungua.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas