Matumizi ya Pembe na Mifupa ya Wany...

Egypt's Dar Al-Ifta

Matumizi ya Pembe na Mifupa ya Wanyama katika Kutengeneza Fimbo na Tasbihi.

Question

Nini hukumu ya kutumia pembe na mifupa ya wanyama katika kutengeneza fimbo na tasbihi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Tangu zamani za kale watu wanatumia mifupa na pembe katika kutengeneza baadhi ya zana mbalimbali, ama pembe inatumika zaidi kutokana na uzuri wake, na bado watu katika siku hizi wanatumia pembe katika utengenezaji wa funguo za piano na mpira wa biliadi, pia inatumika katika utengenezaji wa fimbo, sufuria na tasbihi.

Wanavyuoni walizungumza juu ya matumizi ya mifupa na pembe katika sehemu ya Tohara; wakazungumza katika sehemu ya maji kuhusu vyombo amabavyo vinawekwa maji yanayoathiriwa kutokana na kuwekwa ndani ya vyombo hivyo. Pia wamezungumza kuhusu jambo hilo katika sehemu ya biashara wanapozungumza juu ya kuuza najisi.

Hukumu ya matumizi ya mifupa na pembe ni Mubaha, basi hakuna kosa kutengeneza zana kutoka vitu hivyo, na pia inaruhusiwa kuchanganywa na vyingine, hata kama kuna na rutuba ya wastani.

Dalili ya kuruhusiwa ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika,} [Al-Anaam: 145].

Na hadithi iliyopokelewa kwa Ibn Abbas katika sahihi ya Al-Bukhari na Muslim inaiunga mkono aya hiyo, kwamba Mtume S.A.W., alimpitia mbuzi aliyekufa wa mtumwa wake Maimunah, basi Mtume S.A.W. akasema: “Wanaommiliki mbuzi huyu hawata kuwa na kosa lolote iwapo watachukua ngozi yake wakaisafisha na wakafaidika nayo, walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Munguuzi mbuzi amekufa! alisema, Kilichoharamishwa ni kula nyama yake (nyama ya mbuzi aliyekufa)”. Wanavyuoni wa hadithi walikubaliana kuhusu usahihi wa hadithi hiyo, na imebainisha madhumuni ya aya kuhusu kutoruhusu kula tu.

Al-Baghawi anasema: Katika kauli yake (Kilichoharamishwa ni kula nyama yake) ni dalili ya waliosema kwamba zisizokuwa sehemu zinazoliwa tu za nyamafu zinaruhusiwa kunufaika nazo, kama manyoya, meno na pembe n.k. Wanavyuoni wametofautiana kuhusu jambo hilo, baadhi yao wanasema kwamba vitu hivyo vina uhai, basi mnyama akifa, vitu hivi vinanajisi kama ngozi, na ikiwa ngozi ya mnyama aliyekufa itasafishwa na ina manyoya, basi manyoya hayatohiriki kwa kusafishwa, nayo ni kauli ya Imam Al-Shafii, wanavyuoni wengine wanasema kwamba manyoya hayana uhai, kwa hivyo hayanajisiki kutokana na kufa kwa mnyama. Na wameruhusu kusali kwa mayoya hayo, nayo ni kauli ya Hammad, Malik, na wenye maoni. Baadhi ya wanachuoni wanasema mifupa ina uhai kwa hivyo inakufa kutokana na kifo cha mnyama, na inanajisika kutokana na kunajisika kwa mnayama mwenyewe.

Ama kuhusu nyangumi, basi kifo chake ni halali, na mifupa yake ni safi baada ya kifo chake. Na wengine wanasema kwamba mifupa haina uhai, kwa hiyo, kifo hakihalalishi mifupa, nayo ni kauli ya wenye maoni, na wameruhusu kuitumia mifupa ya tembo. Al-Zahriy anasema kuhusu mifupa ya nyamafu: “Nimewawahi watu miongoni mwa wanavyuoni waliotangulia wanaichania nywele, wanatia mafuta, wala hawaoni ubaya”. Ibn Sirin na Ibrahim wanasema kuwa: “ hakuna dhambi kufanya biashara ya pembe”. Na dalili yao ni aliyoyapokelewa Thawbaan, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alimwambia mnunulie Fatma mapambo ya mikononi ya pembe), na wengine wamefahamu ni: mifupa ya kobe, siyo mifupa ya tembo”. [Sharhu Al-Sunna kwa Al-Baghawyi 2/101, Al-Maktab Al-Islamy].

Na kutoka kwa Abu Hurayrah R.A. anasema: "Mtume S.A.W. anasema kuwa: inzi akitumbukia katika kinywaji cha mmoja wenu, basi amzamishe ndani, kisha amtoe nje, kwa sababu katika moja ya mbawa zake kuna ugonjwa na jingine ni dawa". Imepokelewa na Al-Bukhari.

Baadhi ya wanavyuoni wanasema nyamafu asiyekuwa na damu ni tohara, Al-Hafidh Ibn Hajar anasema: “Hadithi hii ni dalili ya kwamba maji machache hayanajisiki kutokana na kuanguka kwa wasio na damu inayochuruzika ndani yake, kwa sababu Mtume S.A.W. haamrishi kuzamisha kinachonajisi maji akifa ndani yake, kwa sababu huo ni uharibifu” dalili hiyo imepokelewa na Al-Bayhaqiy kutoka kwa Al-Shafei. [Fath Al-Bari 10/251, Dar Al-Maarifa].

Hakuna shaka kwamba mifupa ambayo haina uhai na damu haichuruziki ndani yake inastahiki hukumu hii zaidi, ambayo ni tohara.

Kutoka Sunani ya Abu Dawuud (Kutoka kwa Thawbaan mtumishi wake Mtume S.A.W. alisema: Mtume S.A.W. alikuwa anaposafiri mtu wa mwisho katika familia yake kumwona ni Fatma, na akirudi mtu wa kwanza kuingia kwake ni Fatma, basi siku moja alirudi kutoka vita huku Fatma ametundika pazia juu ya mlango wake, na aliwavalisha Al-Hassan na Al-Hussein bangili mbili za fedha, akaja Mtume S.A.W. hakuingia nyumba ya Fatma, akadhani kwamba kile alichokiona Mtume ndicho kilichomzuia kuingia, basi akalikata pazia na akazikata bangili mbili hizo, basi watoto hawa wawili walikwenda kwa Mtume S.A.W. wanalia, Mtume S.A.W. akazichukua bangili hizo, akasema: Ewe Thawbaan nenda nazo hizi hadi jamaa wa mtu fulani katika nyumba moja mjini, hakika hawa ni jamaa wa nyumbani kwangu wanachukia kula vizuri vyao katika maisha yao ya dunia. Ewe Thawbaan! mnunulie Fatma mkufu wa mshipa na bangili mbili za pembe).

Hii ni wazi kuhusu uhalali wa kutumia pembe, nazo ni mifupa ya pembe ya tembo, kwa mujibu wa mtazamo sahihi, na wanachuoni waliotangulia wamesema mtazamo huo kama itakavyokuja.

Al-Bukhari anasema: “mlango wa najisi zinazoangukia katika maji na samli”. Al-Zahriy alisema: “Hakuna tatizo kuhusu maji ikiwa haikubadilisha ladha au harufu au rangi”. Hammad alisema: “hakuna tatizo kuhusu manyoya ya ndege waliokufa”. Al-Zahriy alisema: “Kuhusu mifupa ya nyamafu kama tembo na wengine: Niliwaona watu miongoni mwa wanavyuoni waliotangulia wanaichania, na wanaitumia kama mafuta yao, wala hawakuona kosa katika jambo hilo”. Ibn Sirin na Ibrahim wanasema: “Hakuna dhambi kufanya biashara ya pembe”.

Ibn Al-Munier anasema: “Nilisema: Mwenyezi Mungu akubariki, maana yake katika tafsiri kwamba kinachozingatiwa katika najisi ni sifa zake, basi manyoya ya ndege waliokufa hayabadiliki kwa kubadilika kwake, kwa sababu uhai wa ndege hawa hauyafanyi manyoya kuwa tohara, na kadhalika mifupa na maji yakichanganyika na najisi lakini hayajabadilika, na pia samli iliyo mbali”. [Al-Mutwari Ala Abwabi Al- Bukhari 1/72, Maktaba Al-Mualla – Al-Kuwait].

Ibn Battal alitaja madhehebu ya wanavyuoni kuhusu mifupa na pembe ya nyamafu, na mfano wake; ambapo alisema katika [Sharhu Al-Bukhari 1/351, Maktabatu Al-Rushd]: “Kuhusu manyoya ya ndege waliokufa na mifupa ya tembo na mfano wake ni tohara kwa mtazamo wa Abu Hanifa, lakini mtazamo wa Maliki na Al-Shafii ni najisi, wala haitumiwa kama mafuta wala haichaniwa, lakini Maliki, alisema: Kama tembo ni tohara, basi mifupa yake ni tohara, na Al-Shafii anasema kwamba: Hakika kuchinja wanyama pori hakuwafanyi kuwa halali. Al-Laithu na Ibn Wahb: Mifupa ikichemshwa kwa maji ya moto na ikitengenezwa, basi inaruhusiwa kutumiwa kama mafuta na inachaniwa. Orwah ameruhusu kuuza pembe. Ibn Al-Muwaz anasema: Maliki amekataza kuitumia mifupa ya nyamafu na tembo na kuitumia kama mafuta, na katazo hilo si kwa ujumla; kwa sababu Orwah, Ibn Shihab, na Rabia waliruhusu kuchania. Ibn Habib amesema: Al-Laithu, Ib Al-Magshun, Mutarrif, Ibn Wahb, na Asbagh waliruhusu kuchania na kupakia rangi, ama kuuza kwake hakuruhusu isipokuwa Ibn Wahb tu, aliyesema: Kama ikichemshwa inawezekana kuuzwa, na inakuwa kama ngozi ya nyamafu inayotengenezwa kwa ajili ya kuuzwa. Maliki, na Abu Hanifa walisema: Ikiwa tembo ni tohara, basi mifupa yake ni tohara. Al-Shafii anasema: Kuchinja wanyama pori hakuwafanyi halali, na anayeruhusu biashara ya pembe, basi mtazamo wake ni tohara. Sharhu Al-Bukhari kwa Ibn Batal.

Ibn Abdu Al-Barr anasema: “wanavyuoni walikubaliana kwamba inajuzu kukata sufi ya kondoo aliyehai, ama kuhusu kauli ya Mtume S.A.W.: (Msitumie nyamafu hata kama ngozi zake), maana yake ni mpaka mzisafishe kwa ushahidi wa hadithi za kusafisha ngozi, na tumeshaeleza suala hilo katika sehemu ya Zayd ibn Aslam, na tunamshukuru Allah S.W. Na aliyejuzisha mifupa ya nyamafu kwa kusema ni kama pembe ameifananisha katika kuchania na kulidai kwamba nyamafu anapitiwa na damu, na mifupa haiko hivyo. Na dalili zao ni kauli ya Mtume katika hadithi hii “lakini imeharamishwa kuliwa tu”, na mifupa siyo miongoni mwa vinavyoliwa, walisema: Kila kitu cha nyamafu kisicholiwa inajuzu kunufaika nacho, Mtume S.A.W. amesema: “lakini imeharamishwa kuliwa tu”. Na walioruhusu kutumia mashanuo ya pembe na vinavyotengenezwa kwa meno ya tembo na mifupa ya nyamafu ni Ibn Sirin, Orwah ibn Al-Zubayr, Abu Hanifa na wenzake, waliosema: “Inasafishwa kwa maji, watu hunufaika nayo, huuzwa na hununuliwa. Na amesema hivyo Al-Laithu Ibn Sad, lakini alisema: Inachemshwa kwa maji na moto hadi mafuta yaliyo ndani yake yanakwisha”. [Al-Tamhiid lima fi Al-Muwataa min Maani wa Asaaniid 9/52, Wizarat Umum Al-Awqaf wa Al-Shuun Al-Islamiya - Moroko].

Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi wanajuzisha kutumia mifupa ya nyamafu, Al-Kasaani alisema: “Kuhusu mifupa ya wanyama, mshipa wake, nywele zake, sufi yake, manyoya yake, na miguu yake inaweza kuuzwa na kutumiwa kwa mtazamo wetu, lakini mtazamo wa Shafii – R.A - haiwezikani, kwa sababu vitu hivi ni tohara kwetu, lakini kwake ni najisi, na dalili yake ni kauli ya Mwenyezi Mungu {Mmeharimishiwa nyamafu} na sehemu hizo ni miongoni mwa nyamafu; nazo ni marufuku hairuhusiwi kuuzwa, Mtume S.A.W. alisema “Msitumie ngozi ya nyamafu hata kama mshipa wake”. (Na kwetu) kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na Mwenyezi Mungu amekujaalieni majumba yenu yawe makazi} mpaka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kwa sufi zao na manyoya yao} Aya, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameeleza kwamba amefanya mambo hayo kwa ajili yetu na ametupa neema hiyo pasipo na kutenganisha kati ya mnayma aliyechijwa na nyamafu, na hii ni dalili ya kuthibitisha kuruhusiwa, kwa sababu katazo la nyamafu siyo kwa ajili ya kifo chake; kifo kipo katika samaki na nzige, na wawili hawa ni halali, Mtume S.A.W. alisema: “Tumehalalishiwa maiti mbili na damu mbili”, lakini kwa sababu ya rutuba ya majimaji. [Badaai Al-Sanaai 5/142, Al-Maktaba Al-Elmiyah].

Al-Mardaawi alisema: “Kauli yake (na mifupa, pembe yake na kucha yake ni najisi), na pia mshipa wake na miguu yake, inakusudiwa inanajisika kutokana na kifo chake. Na imepokelewa kwake kwamba vitu hivyo ni tohara, alitaja hivyo katika Al-Furuu na vitabu vingine. Alisema katika kitabu cha Al-Faiq: maoni ya Abu Al-Khattab ni tohara na Sheikh wetu ameyachagua, maana Sheikh Taqi Al-Din alisema maoni hayo. Baadhi ya marafiki walisema: kufuatana na hayo inaruhusiwa kuuzwa. Alisema katika kitabu cha Al-Furuu: ilisemwa kwa sababu haina uhai. Na ilisemwa: kwa kukosekana sababu ya kusababisha najisi, nayo ni rutuba, na kauli hiyo ni sahihi zaidi. Na katika asili ya suala hilo kuna rai kwamba kwa kawaida kinachoanguka kama vile pembe ya tawi ni tohara, na chengine ni najisi”. [Al-Insaaf kwa Mardaawi 1/92, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi].

Na wanavyuoni wa madhehebu ya Maliki wanatofautisha kati mnyama aliyechinjwa na asiyechinjwa; basi aina ya pili inachukiza sana na ya kwanza inachukiza kidogo, Al-nafrawi alisema: “(na haipendezi kutumia meno ya tembo, na wanavyuoni wametofautiana katika jambo hilo). Mambo yaliyotajwa miongoni mwa kutopendeza baadhi yao wamechukulia kuwa kuchukiza kwa sababu ya kuchukiza tu, na baadhi yao wamechukulia hivyo kwa sababu ya kukataza. Na kanuni iliyo wazi na karibu na maneno ya mwandishi kwamba mlango unaohusu “kilihochukuliwa kutoka kwa mzoga wa mnyama”; kwa kuwa tamko lililoandikwa ni: Nahukia mafuta yaliyopo katika meno ya tembo, kuchana nywele kwa meno hayo na kuyafanyia biashara; kwa sababu mnyama huyo ni mzoga kwahivyo karaha hapo inachukuliwa kama ni haramu, na miongoni mwavyo ni jino la tembo mfu ambalo liling’olewa wakati tembo huyo akiwa hai. Ama jino la tembo aliyechinjwa, basi linachukiza kwa namna yakujiepusha nalo. Na Mashekhe wametofautiana kuhusu unajisi wa mafuta yaliyotiwa katika chombo cha pembe, na ambayo ilielezwa na wanavyuoni wa madhehebu haya kwamba: kama ikiwa mafuta hayo hayatachanganyika na kitu chochote cha pembe hiyo na kwa kuwepo uhakika, basi itaendelea kuwa na usafi wake kama mifupa ya punda iliyochakaa, haikinajisi kile kilichotuka ndani yake. Na ikiwa kuna uwezekano wa kuchanganyika na chochote katika pembe hiyo basi hapana shaka yoyote kitu hicho kitakuwa najisi, na uangalia kigezo hicho kwa kila aina ya najisi kavu”. [Al-Fwakih Al-Dawaniy 1/388, Dar Al-Fikr].

Ibn Taymiyah alisema: “Inaonesha usahihi wa kauli ya wanavyuoni wengi: kwamba Mwenyezi Mungu ametuharimishia kumwaga damu, kama alivyosema: {Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilichoharimishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika} damu inayosameheka ni ile isiyochuruzika ingawa ni jinsi ya damu. Inajulikana kwamba Mwenyezi Mungu ametofautisha kati ya damu inayochuruzika na nyengine. Na ndiyo maana Waislamu wanatia nyama katika mchuzi na mistari ya damu katika sufuria inadhihirika, na walikula hivyo katika enzi ya Mtume Muhammad S.A.W. kama alivyosema Aisha, na kama ingekuwa haifai wangeliondoa damu kutoka katika mishipa kama wanavyofanya Wayahudi. Na Allah S.W amekataza kula nyamafu, pia ameharamisha mnyama aliyekufa kwa kunyongeka koo, aliyekufa kwa kupigwa, aliyekufa kwa kuanguka, na aliyekufa kwa kupigwa pembe. Mtume S.A.W. ameharamisha kinachowindwa kwa kulengwa shabaha, akasema: “Hakika mnyama huyo amekufa kwa kupigwa” kinyume na yule aliyewindwa kwa silaha yake, na tofauti kati yao ni kumwagika damu; hii inaonesha kwamba sababu ya najisi ni kumwagika damu, na ikimwagika vibaya kama kutaja jina lisilo la Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi ubaya hapa unakuwa katika upande mwingine, kwa sababu kuharamisha baadhi ya wakati kunakuwa kwa kuwepo damu, na wakati mwingine kwa kuchinja vibaya kwa mfano achinje Majusi, aliyeritadi. Uchinjaji katika hali hizi si mahala pake. Na kama mifupa, kucha, miguu, n.k haina damu inayomwaga, basi hakuna sababu ya kuwa ni najisi, na hii ni kauli ya wanavyuoni wengi waliotangulia. Al-Zahriy alisema watu mashuhuri wa taifa hili wanachana kwa mishanuo ya mifupa ya tembo. Imepokelewa kuhusu pembe hadithi Maarufu lakini haikuthibitishwa; lakini hatuna haja ya kuitoa hadithi hiyo kama dalili. Na pia imethibiti katika Sahihi ya Bukhari (Mtume S.A.W. alisema katika kondoo wa Maymuna: "Je, hamchukui ngozi yake kwa ajili ya kufaidika nayo? walisema: Ni nyamafu, Akasema lakini imekatazwa kuliwa tu". Na katika Sahihi ya Al-Bukhari hakuna neno Dibaghi (kusafisha ngozi za wanyama), na hawakulitaja wenzake Al-Zahriy, lakini imeelezwa na Ibn Uyaynah na ilipokelewa na Muslim katika Sahihi yake. Imamu Ahmad amekataa hayo, na akaonesha kosa aa Ibn Uyaynah, na alisema kuwa Al-Zahriy na wengine walikuwa wakijuzisha matumizi ya ngozi ya nyamafu bila ya hata kusafisha ngozi kwa mujibu wa hadithi hiyo”. [Majmuu Al-Fataawa, 21/99, Taasisi ya Al-Malik Fahd ya uchapishaji wa Msahafu Tukufu].

Kutokana na yaliyotangulia: Inajuzu kutumia mifupa na pembe za wanyama katika kutengeneza fimbo na tasbihi, na hakuna dhambi kufanya hivyo.
 

Share this:

Related Fatwas