Kutazama Yaliyoharamishwa

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutazama Yaliyoharamishwa

Question

Je, ni haramu kutazama yaliyoharamishwa?, kama vile mtu kumwangalia mtu mwingine anafanya jambo la haramu, au kutazama kitu ambacho ni haramu kukitengeneza kama sanamu inayofanana na mwenye roho, au kuangalia kitu ambacho ni haramu kukinywa kama ulevi.

Answer

Sifa zote njema anstahiki Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., watu wake, masahaba wake na waliomfuata, ama baada ya hayo:

Haramu katika lugha ni kila kinachokatazwa, Al-Fayoumi amesema: “Kitu kikiharamishwa, itakuwa haramu kukikaribia … kama sala ikiharamishwa, itakuwa haramu ikisaliwa katika wakati maalumu … na marufuku katika lugha ni haramu” [Al Misbah Al Munir, 1/131, Al- Maktaba Al-Elmiya].

Haramu katika istilahi ya wanachuoni wa Fiqhi na elimu ya Usuulu Fiqhi” ni hukumu ya kisheria inayoambatana na kitendo cha mtu baleghe “mukalaf” ambacho sheria inakataza kukikaribia na imeandika adhabu kali juu ya yule anayekitenda huko Akhera au kuekewa kisasi na kutekeleza adhabu na kutia adabu katika maisha ya hapa duniani. Mwanachuoni Taf-tazaniy alisema: “mwenye kufanya haramu anaadhibiwa” [Al-Talweeh, 2/252, ch. Mat-ba’at Subeeh]. Naye Al-Zarkashiy alisema: “Haramu ni kile kitendo ambacho mwenye kukitenda analaumiwa kisheria na miongoni mwa majina yake ni kitendo kibaya, kinachokatazwa na marufuku” [Al Bahr Al Muheet, 1/337, ch. Dar Al Kotubiy].

Asili ni kwamba vitu havisifiwi kuwa ni halali au haramu katika dhati yake, lakini kitendo huitwa hivyo kulingana na kuchuma, kama kula, kunywa na kuvaa n.k. kwa mfano: kuvaa nguo ya hariri ni haramu kwa mwanamume, lakini inajuzu kwa mwanamke kuvaa nguo ya hariri. Kwa hiyo nguo kama nguo si haramu.

Mwislamu analazimishwa kujiepusha na mambo yaliyoharamishwa na mabaya, tena ni juu yake akiona kitu kibaya akichukie na awe tayari kujitahidi kukiondoa anavyoweza. Mtume S.A.W. anasema: “Yoyote atakayeuona uovu auondoe kwa mkono wake na kama hawezi, auondoe kwa ulimi wake na kama hawezi hilo pia, auchukie moyoni mwake, na hiyo ndiyo hali dhaifu zaidi ya imani” [Imepokelewa na Imamu Muslim].

Imamu Al Nawawiy alisema: “Maneno yake S.A.W. “moyoni mwake”; auchukie moyoni mwake, na hivyo haimaanishi kuundoa na kuubadilisha uovu lakini inamaanisha kwamba amefanya analoweza kufanya, aidha maneno yake S.A.W. “na hiyo ndiyo hali dhaifu zaidi ya imani” maana yake ina faida iliyo ndogo zaidi. Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi” [Sharh Sahih Muslim, 2/25, ch. Dar Ihiyaa’ Al Turath].

Imamu Ibn Taymiya alisema: “Mwislamu ni juu yake kuamrisha mema na kukataza mabaya kadiri ya uwezo wake. Mtume S.A.W. alisema: “Aonaye ubaya auondoe kwa mkono wake, na kama hawezi, aundoe kwa ulimi wake, na kama hawezi hilo pia, auchukie moyoni mwake, na hiyo ndiyo hali dhaifu zaidi ya imani”. Basi analazimishwa kufunika utupu, na akishindwa, ni juu yake ainamishe macho” [Ibn Taymiya, Al Fatawa Al Kubra, 1/300, Ch. Dar Al Kutoob Al Elmiya].

Kutazama mambo yaliyoharamishwa kwa makusudi (yakiwa ni vitendo au vitu) bila ya kuwa mwenye kuyatazama anayachukia na kuwa tayari kuyaondoa ni haramu; kwani kuzoea kuyaangalia yaliyoharamishwa, kuna athari zake mbaya juu ya nafsi ya kibinadamu kwa kuwa kunaifanya kidogo kidogo kuzoea yale mambo na kuaathirika nayo. Tena kuzoea kuyaangalia yale yaliyoharamishwa bila ya kuyachukia ni sawa sawa na kukiri, kumhamasisha mtendaji aendelee na uovu na kupuuza uovu. Na hii ni njia ya kusaidia katika dhambi. Kauli hii ni ya madhehebu manne yanayofuatwa. Ibn Abdin amesema: “Yanayofanywa siku za mapambo kama kutandika hariri na kuweka vyombo vya dhahabu na fedha bila ya kuvitumia inajuzu kama hajakusudia kujifakhararisha kwa kutekeleza amri ya mtawala, ama kuwasha mishumaa na kandili mchana haifai kwa sababu ni kupoteza mali. Lakini mtu akifanya hivyo kwa kuogopa mateso ya mtawala basi hakuna kosa juu yake”(Rad Al Mukhtar, 6/354: 355, ch. Dar Al Kutoob Al Elmiya).

Sheikh Al Dardir mfuasi wa madhehebu ya Maalik alisema: “kuangalia lililoharamishwa ni haramu” [Al Sharh Al Kabir, 2/338, ch. Dar Ihiyaa’ Al Turath Al Arabiy].

Al Halabiy alisema: “kila lililoharamishwa ni haramu kuliangalia; kwani inakuwa sawa na kusaidia katika maasia” [Hashiyat Tuh-fat Al Muhtaj, 10/221, Ch. Dar Ihiyaa’ Al Turath Al Arabiy], na “ambalo asili yake ni haramu, inaharamishwa kuliangalia; kwani kuliangalia ni kama kulikubali” [Hashiyat Nihayat Al Muhtaj, 2/376, Ch. Dar Al Fikr].

Ibn Kudama Al Hanbaliy alisema: “kuona maovu ni sawa na kuyasilikiza, kama mtu hatakiwi kukaa katika mahali pa kuwepo muziki, aidha hatakiwi kukaa katika mahali pa kunywa ulevi na maovu mengine” [Al Mughniy, 7/218, ch. Dar Ihiyaa’ Al Turath Al Arabiy].

Ibn Mufleh alisema: “inachukizwa kuangalia mavazi ya hariri na vyombo vya dhahabu na fedha n.k. ikiwa mtu anayaangalia kwa matamanio ya kupata mapambo na kufakharishana. Aidha Ibn Ukeel alisema: harufu ya ulevi ni kama sauti za klabu, mtu akizoea harufu zake anakuwa kama kwamba anasikia sauti za klabu na kuzikubali. Kwa hiyo, inalazimika kuziba pua kama ilivyolazimika kuziba masikio. Kwa hiyo inaharamishwa kuangalia hariri na vyombo vya dhahabu na fedha ikisababisha kutamani kupata mapambo na kufakharishana” [Al Adab Al Shari’ya, 3/519, Ch. Alam Al Kutoob].

Kutokana na yaliyopita inabainika kuwa haifai kuviangalia vitendo na vitu vilivyoharamishwa bila ya kuwepo haja au dharura isipokuwa hali ya kuviangalia kwa lengo la kuvikataza na kuviondosha, mbali ya hivyo inakuwa haramu kuviangalia kama walivyoafikiana maimamu wa madhehebu na wanachuoni wanaofuatwa.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas