Tofauti kati ya Bahashishi na Rushw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti kati ya Bahashishi na Rushwa

Question

Baadhi ya watu huwapa pesa baadhi ya wafanyakazi kwa ajili ya kutoa huduma nzuri kwao, au kwa sababu wanajua ufukara wao na haja yao, hasa kwa sababu siku hizi imeenea hali ya kazi bila ya malipo kutoka kwa mwajiri, lakini kazi ni kwa bahashishi tu. Na pengine mtu anaweza kutoa bahashishi kwa ajili ya kujiepusha na uchoyo. Je, kuna tofauti kati ya bahashishi na rushwa katika hukumu ya kisheria?

Answer

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfua, na baada ya hayo:
Rushwa katika lugha ni pesa zinazotolewa kwa mtu mwenye cheo au kwa mtu yoyote kwa ajili ya kupata kile mtu anachokikusudia. [Al Misbahu Al Muniir kwa Al Fayiumiy kidahizo cha: (Rushwa)].
Maana ya neno hilo katika istilahi haiko mbali na maana yake katika lugha; inasemwa kuwa ni: “ni kile kinachotolewa kwa ajili ya kuvuruga haki au kwa ajili ya kurekebisha batili.” [Al- Tarifaat kwa Jerjaniy uk. 111, Ch. Dar Al Kutub Al- Elmiya]. Na inasemwa kuwa ni: “kile anachofanyiwa mtu ili ahukumu kinyume na haki, au kwa ajili ya kuepusha hukumu ya haki” [Mughni Al Muhtaj Sharhu Al Minhaj 6/288. Ch. Dar Al-Kutub Al- Elmiya].
Lakini neno la “bahashishi” siyo miongoni mwa maneno fasaha ya Kiarabu; kwa sababu kidahizo chake hakifahamiki katika lugha ya Kiarabu. Mwanachuoni wa lugha Abu Bakr Ibn Duraid anasema katika kitabu cha [Gamhartu Al Lugha 1/344, kidahizo cha: (bahashishi), Dar Al Ilmu lell Malayiin: “neno la bahashishi siyo miongoni mwa maneno fasaha ya Kiarabu”.
Na maana ya bahashishi kwa kawaida: inalinganishwa na zawadi; kwa sababu hutolewa bila ya kupokea chochote. Mwanachuoni Ibn Al Athiir anasema katika kitabu cha [Al-Nihaya fii Ghariib Al-Hadith wa Al-Athar 5/231, Al Maktabatu Al Elmiya]: “Zawadi ni: kila kinachotolewa bila malipo na malengo yoyote.”
Imamu Al Nawawi anasema katika kitabu cha [Al Minhaj 3/558-559, Ch. Dar Al-Kutub Al Elmiya - kwa ufafanuzi wake: Mughni Al Muhtaj -]: “kummilikisha mtu kitu chochote bila ya malipo ni zawadi”.
Hii ni kuhusu maana, na kuhusu hukumu: Rushwa ni haramu bila ya upinzani. Nayo ni miongoni mwa madhambi makubwa. Zimekuja dalili nyingi kuhusu jambo hilo, miongoni mwake ni: kauli ya Mwenyezi Mungu inawasema vibaya baadhi ya watu wa kitabu: {Hao ni wasikilizaji wa uwongo, na ni walaji mno vya haramu!} [AL MAIDA 42], Al Hassan na Saeed bin Jubair walisema: “ni Rushwa”.
Mwenyezi Mungu anasema: {Wala msiliane mali zenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua} [AL BAQARAH 188], na dalili katika aya hiyo ni dhahiri, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anakataza tendo hilo, na analielezea kuwa ni batili na dhambi.
Imepokelewa na Abdullah bin Amr R.A. anasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amemlaani mwenye kutoa rushwa na anayeichukua” [Imepokelewa na Abu Dawud na Al Tirmidhiy, na anasema: “Hiyo ni hadithi NZURI na SAHIHI”]; na dalili katika hadithi hiyo ni: kumlaani anayetenda hivyo, na kulaani kitendo hicho kama ni miongoni mwa alama za madhambi makubwa.
Ama kuhusu kile watu wanachokiita bahashishi: asili yake ni kutoa kitu kwa hiari, na moyo safi, na hujumuisha kila aina ya zawadi ambayo inakusudiwa heshima kwa anayechukua zawadi hiyo -na Sadaka- ni ile ambayo hukusudiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu -nayo kwa njia hii, inaruhusiwa kisheria. [Tahkiku Al Qadhiya baina Al Rushwa na Al Hadiya kwa Nabulsi uk. 138, Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Mfalme Abdul Aziz. Dalili za kuruhusiwa kwa zawadi au hiba zimefupishwa na mwanachuoni Al Khatib Al Sherbini katika kitabu cha [Mughni Al Muhtaj 3/558, Ch. Dar Al-Kutub Al Elmiya], akisema: “Asili yake -yaani zawadi- kabla ya makubaliano ya wanavyuoni: ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha} (na kauli yake), {na anawapa mali, kwa kupenda kwake} (na kauli yake), {Na mnapoamkiwa kwa maamkio yoyote} Inasemwa: inakusudiwa zawadi.
Al Bukhari na Muslim wamepokea hadithi: (Jirani hadharau chochote kwa jirani yake, hata ikiwa kwato ya kondoo). Makubaliano ya wanavyuoni yamependezesha kila aina ya zawadi; Mwenyezi Mungu anasema: {Na saidianeni katika wema na uchamungu} na zawadi: ni wema, kwani inasababisha upendo pamoja na kupendana; na Mtume S.A.W. anasema: “peaneni zawadi mtapendana”, Mtume S.A.W. mwenyewe alikubali zawadi ya Al Muqawqis aliyekuwa kafiri, alifurahishwa kwa kuwepo Mariiya Al Qibtiya na akazaa naye. Alikubali zawadi ya Al Nagashiy aliyekuwa Mwislamu na aliitoa kama zawadi pia”.
Tofauti kati ya rushwa na bahashishi inaonekana kwa maudhui na lengo. Wanavyuoni wameeleza jambo hilo wakati wakizungumzia tofauti kati ya rushwa na zawadi.
Kinachotolewa kwa watawala na wenye nyadhifa mbali mbali kwa mtindo wa rushwa hakijuzu. Ama kuhusu hiba na zawadi na mfano wa hivyo, ambavyo hutolewa kwa wafanyakazi mafukara na maskini vinapendeza mno. Na mambo huambatana na makusudio yake. Kwa hivyo, nia ni dalili inayotofautisha kati ya mambo mawili yanayofanana kwa sura na umbile pamoja na tofauti zake katika hukumu au lengo, Imamu Ibn Qudamah katika kitabu cha [Al-Mughni 6/41, Ch. Maktabat Al Qahira] anasema: “Mtume S.A.W. alikuwa anakula zawadi wala hali Sadaka, na akasema kuhusu nyama aliyopewa Bariyrah kama Sadaka: “hiyo ni Sadaka kwake, na kwetu ni zawadi”.
Mwenyezi Mungu Mtumufu ni mjuzi zaidi ya yote.


 

Share this:

Related Fatwas