Kuvunja Ahadi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuvunja Ahadi

Question

Nina kampuni, na nimemuahidi mshirika wangu kutekeleza baadhi ya mambo yanayohusiana na kazi, lakini baada ya muda nilishangaa kuona kwamba mshirika wangu huyo amevunja ahadi na amekiuka baadhi ya yale tuliyoyakubaliana, na nilipomwuliza juu ya jambo hilo akanielezea msimamo wake kwamba haiwezekani kuyatekeleza masharti yote ya ahadi hiyo, na nilipomkumbusha kwamba Mwislamu havunji ahadi yake, aliniambia kuwa kuvunja baadhi ya masharti ya ahadi siyo kama kuvunja ahadi nzima, na ameusisitizia mtazamo wake kwamba Mtume S.A.W. katika Mkataba wa Al-Hudaibiya baada ya kukubaliana na Maqureshi kwamba yeyote atakayekuja kwake kutoka kwao atamrudisha kwao hata akiwa ni Mwislamu, alivunja sehemu ya ahadi hiyo katika wanawake waumini kwa kuzingatia amri ya Allah: {Enyi mlio amini! Wakikujieni wanawake Waumini waliohama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri.} [AL-MUMTAH'INAH: 10], tafadhali naomba unionyeshe palipo na haki katika jambo hili?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ahadi ina maana nyingi katika lugha, na miongoni mwa maana zake ni: usalama, dhima, kiapo, na yote ambayo Mwenyezi Mungu ameahidiwa juu yake, na kila kitu kati ya watu miongoni mwa mikataba ni ahadi. Na ahadi ni wasia na amri, inasemwa kuwa: amemwahidi kama akimwusia au akamwamuru. Na kuvunja ahadi ina maana ya kuipoteza na kutotimiza na inaitwa uhaini. [Taji Al-Arusi 8/454 kwa 455.13 / 203 Dar Al-Hidaya].

Uislamu umesifu kutimiza ahadi na umewasifu watu wanaoitimiza ahadi kwa sifa nzuri, kama kuwa mkweli na kumcha Mungu, na umezidisha cheo chao katika dunia na Akhera, na haukuusifu uhaini na watu wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {na wanaotimiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio waliosadikisha, na hao ndio wajilindao.} [AL-BAQARAH: 177], na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema pia: {Wenye akili ndio wanao zingatia. Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji maagano} [AR-RAA’D: 19.20], na akasema: {Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao. Na ambao Sala zao wanazihifadhi Hao ndio warithi. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.} [AL-MUUMINUN 8-11], Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamuru kutimiza ahadi, hata pamoja na wasio-Waislamu, akasema: {Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa} [AL-ISRAA: 34], na akasema: {Isipo kuwa washirikina ambao mliahidiana nao kisha wasikupunguzieni chochote, wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi hao watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha-Mungu.} [AL-TAWBA: 4], na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Itakuwaje iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake, ila wale mlio ahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu} [AL-TAWBA: 7]. Mwenyezi Mungu Mtukufu amelaani Wayahudi na makafiri kwa ajili ya kuvunja maagano yao, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Hakika vinyama vilio viovu kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao kufuru, basi hao hawaamini. Wale ambao miongoni mwao umepatana nao ahadi, kisha wanavunja ahadi yao kila mara, wala hawamchi Mungu.} [AL-ANFAL: 55.56], {Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini.} [AL-BAQARAH: 100].

Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. ni mfano mtukufu wa kiutu ambaye ni mkamilifu na ambaye Mwenyezi Mungu amekusanya sifa nzuri na maadili bora na heshima katika yeye, na Mwenyezi Mungu akasema kuhusu yeye S.A.W.: {Na hakika wewe una tabia tukufu.} [Al-Qalam: 4], {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.} [Al-Ahzab: 21]. Na imepokelewa na Imam Ahmad katika Musnad wake kutoka kwa Saad bin Hisham bin Amer, alisema: ((nilikwenda kwa Bi Aisha, nikasema: Ewe Mama wa Waumini, niambie kuhusu tabia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., akasema: tabia yake ilikuwa ikifuata Qurani)).

Maana ya hayo ni kwamba hakuna sifa nzuri zilizoamuriwa katika Qurani Tukufu ambayo ilikusanya sifa zote nzuri, isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad S.A.W. amesifiwa kwa sifa hizo, na hakuna sifa mbaya ambazo ni haramu, isipokuwa Mtume S.A.W. alikuwa mbali nazo kuliko watu wote. Kwa hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. ametimiza kila ahadi, na hata imepokelewa na yeye kulaani na kukanusha dini kwa wale ambao hawatimizi maangano yao, akasema: "Hakuna imani kwa wale ambao hawana Uaminifu, wala hakuna dini kwa wale ambao hawatimizi maagano yao". [Imepokelewa na Imam Ahmad katika Musnad wake].

Na Mtume S.A.W. amesema kwamba uhaini na kuvunja ahadi ni sifa miongoni mwa sifa za wanafiki ambazo muumini wa kweli anapaswa kuziepuka. Imepokelewa na Abdullah bin Amr R.A. kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Sifa nne anayekuwa nazo sifa hizi atakuwa mnafiki sana: kama akisema uongo, na kama akiahidi na kisha akavunja ahadi yake, na kama akiaminiwa kisha akafanya hiana, na kama akiwa mgomvi anadhulumu, na yule ambaye ana sifa miongoni mwa sifa hizo, ana sifa za unafiki mpaka atakapoziacha". Maimamu wawili (Al-Bukhari na Muslim) wamekubaliana katika hadithi hii.

Na kutokana na hayo, Waislamu na kila mwenye akili timamu wanalazimishwa kusema kwa imani kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alikuwa akitimiza maagano yake zaidi kuliko watu wote, na pia Manabii wengine S.A.W., na ni lazima kuamini kwamba wao wanaepukana na makosa yote, na uhaini au kuvunja ahadi ni miongoni mwa sifa mbaya sana.

Na katika majadiliano marefu ambayo yalifanyika kati ya Abu Sufyan - kabla ya kuingia katika Uislamu- na Heraql, wakati alipomuuliza kuhusu Mtume S.A.W. ili athibitishe unabii wake, Heraql akamwambia Abu Sufyan: "Na nilikuuliza je, anafanya hiana?, ukasema hapana, na hivyo ndivyo ilivyo kwamba mitume hawahaini ... na nimekuuliza: Je anakuamrisheni, ukasema kwamba anakuamrisheni kumwabudu Mwenyezi Mungu pekee yake, na kwamba hakuna mwengine aliye pamoja naye, na anakukatazeni kuhusu miungu wanaoabudiwa na baba zenu, na anakuamrisheni swala, sadaka, usafi wa moyo, na kutimiza ahadi, na utendaji wa uaminifu. Akasema, na hizo ni sifa za Mtume, nilijua kwamba atakuja, lakini sikudhani kwamba atakuwa miongoni mwenu, lakini kama kweli uliyoyasema, atakaribia kumiliki nafasi ya miguu yangu, na kama nikitarajia nifike kwake, nitavumilia shida ya kukutana naye, na kama nitakuwa pamoja naye nitaiosha miguu yake." Imepokelewa na Imam Al-Bukhari katika Sahih yake.

Na miongoni mwa mifano ya kutimiza ahadi ya Mtume S.A.W. ni: kutimiza yaliyomo kwenye hati, ambayo aliifikia pamoja na Maqureshi katika kuwekeana Mkataba wa Al-Hudaibiya, na ambao unasema kuwa Mtume S.A.W. anatakiwa kumrudisha yeyote atakayekuja kwake hata akiwa ni Mwislamu kwa Maqureshi. Suhail bin Amr –amabye ni Balozi wa Maqureshi katika kuuandaa Mkataba huo - akasema, "na kwa mujibu wa Mkataba huu, hakuna yeyote miongoni mwetu atayekuja kwako, isipokuwa umrudishe kwetu hata kama ataiingia dini yako." Imepokelewa na Imam Al-Bukhari katika Sahih yake.

Na katika hadithi: "Kisha wakati wake waumini walipokuja kwake, Aya hii ikateremshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Wakikujieni wanawake Waumini walio hama, basi wafanyieni mtihani} [Al-Mumtahina: 10]. Kisha Mtume S.A.W. akarudi Madina. Abu Basir –ambaye ni miongoni mwa Maqureshi- akaja kwake Mtume, naye alikuwa Mwislamu, wakawapeleka watu wawili kwa ajili ya kumwuliza mtu yule, wakasema: tunauliza kuhusu ahadi ambayo umetufanyia, basi Mtume akawapa mtu yule".

Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. hakuwahi kuvunja ahadi yake yoyote pamoja na Maqureshi katika Mkataba wa Al-Hudaibiya, lakini uhaini na uvunjaji ahadi ulifanywa na Maqureshi tu. Na jambo hilo lilikuwa sababu ya kuiteka Makkah. Kwa hivyo basi, kama kutoruwadisha wanawake Waumini kungetokea, ingekuwa ni kuvunja ahadi kwa upande wa Waislamu, jambo ambalo Maqureshi walikuwa wakilikana hilo na walikuwa wakitangaza haki yao katika vita, lakini hakuna chochote miongoni mwa hicho kilichotokea mpaka Maqureshi wakavunja ahadi wao wenyewe, ukawa ushindi dhahiri kwa upande wa waislamu.

Ibn Battal alisema katika "Sharhu Sahihi Al-Bukhariy" [8/90, Maktaba ya Al-Rushd - Riyadh: (“na kwa mujibu wa hayo, hakuna yeyote miongoni mwetu anayekuja kwako, isipokuwa umrudishe kwetu hata kama akiwa amekwishaingia dini yako.”) na hakutaja wanawake, kwa sababu hiyo kumchukua binti yake Hamza kulikuwa sahihi. Je, huoni kwamba amemrudisha Abu Jandal kwa baba yake, naye ndiye aliyeleta madai hayo?.

Al-Aini alisema katika kitabu chake “Umdatu lQarii Sharhu Sahihil Bukhari” [13/277, Daru Ihiyaa Al-Turathu Al-Arabi]: “ukisema: binti yake Hamza alitoka pamoja naye? Nimesema kwamba wanawake hawakuingia katika ahadi, na sharti lilikuwa likihusiana na wanaume tu, na Al-Bukhariy ameeleza hivyo katika kitabu cha “Masharti” baada ya hayo, na katika baadhi ya njia zake, Suhail akasema: na kwamba na hakuna yeyote miongoni mwetu anayekuja kwako, isipokuwa umrudishe kwao hata kama akiingia dini yako. na hakutaja wanawake, kwa ajili ya sababu hiyo kumchukua binti yake Hamza kulikuwa sahihi, je, huoni kwamba amemrudisha Abu Jandal kwa baba yake, naye ndiye aliyefanya madai hayo.

Wanavyuoni wametofautiana kuhusu majibu yao katika suala la kuacha kuwarudisha wanawake waumini kwa makafiri katika Mkataba wa Al-Hudaibiya, inaasemekana: kwamba ni kama kuondoa sehemu ya mkataba huo, yaani kuvunja ahadi hiyo. Ikasemwa pia: ni ubainishaji jumla unaodhaniwa au ni ubainishaji wa neno ndani ya Mkataba. Na ikasemwa: lakini wanawake hawakuingia katika matini ya Mkataba huo tangu mwanzoni, na Mwenyezi Mungu amewasahaulisha Maqureshi kuwataja wanawake wote kwenye Mkataba huo.

Al-Hafidh ibn Hajar alisema katika kitabu chake cha [Fathu Al-Bari, 9/419, Daru Al-Maarifa - Beirut]: “Kuhitilifiana katika kutorudisha wanawake kwa watu wa Makkah pamoja na kupatanisha baina yao na Waislamu katika Al-Hudaybiyah kwamba aliyekuja miongoni mwao kwa Waislamu wamrudishe, na aliyekuja kutoka kwa Waislamu kwao hawatamrudisha, je, hukumu ya wanawake imeondolewa kutoka katika mkataba huo, Waislamu wamekatazwa kuwarudisha? Au haukuingia katika Mkataba huo, au jambo hilo ni la ujumla linalokusudiwa jambo maalum.

Na amebainisha hivyo wakati wa kuteremshwa kwa Aya, na wanaosema mtazamo wa pili wameshikilia baadhi ya njia za hadithi hiyo kwamba hakuna mwanamume yeyote miongoni mwetu anaekuja kwako, isipokuwa umrudishe kwetu, inafahimika kwamba wanawake hawakuingia. Na imepokelewa na Ibn Abi Hatim kupitia Muqatil Ibn Hayyan: kwamba washirikina walimwambia Mtume S.A.W. umrudishe kwetu yeyote anayehamia miongoni mwa wanawake wetu, kwa sababu tumeweka sharti ya kwamba anayekuja kwako miongoni mwetu umrudishe kwetu. Akasema, sharti lilikuwa likihusiana na wanaume tu siyo wanawake. Na Hdithi hiyo ikithibitika itatatua tofauti hii, lakini Hadithi iliyotangulia mwanzoni mwa masharti inaunga mkono mtazamo wa kwanza na wa tatu kwamba Umm Kulthum binti yake Uqbah ibn Abi Muat alipohama, familia yake ikaenda Madina kwa ajili ya kumrudisha, naye Mtume S.A.W hakumrudisha kwao ilipoteremka aya hii: {Wakikujilieni wanawake Waumini waliohama}...

Mtazamo sahihi zaidi ni kwamba wanawake hawakuingia katika Mkataba huo tangu awali, kwa sababu ni lazima tuseme kwa kuondoa kile kinachothibitishwa mwanzoni kupitia kukiri kwa Waislamu, hivyo itakuwa uhaini na uvunjaji wa ahadi kwa mujibu wa mtazamo wa Maqureshi. Lakini Maqureshi hawakusema hivyo, basi siyo kweli kwamba wanawake walitajwa katika Mkataba huo.

Pia kauli ya kwamba matini ya mkataba ilikuwa kwa ujumla kwa kuwakusanya pia wanawake ndani yake, kauli hiyo siyo sahihi mno, kwa hivyo, Mtume S.A.W. amebainisha kwamba kauli hiyo kuwa wanaume hasa hasa ndio iwanatakiwa na wala siyo wanawake, kwa sababu kama kauli hiyo ni sahihi tofauti itaendelea kati ya pande mbili, Maqureshi wanasisitiza kwamba wametaka maana jumla, na Waislamu wansisitiza kwamba wametaka maana maalum, na kama Maqureshi wakihitaji kurudisha wanaume wakiwashindisha juu ya Waislamu, basi wanahitaji zaidi kuwarudisha wanawake kama wakipata sababu nzuri kwa mgogoro huo kama kusema kuwa wametaka maana ya ujumla kwa maneno yaliyotajwa katika hati ya upatanisho, na watachukua kauli hiyo kama kisingizio cha kuwashitaki Waislamu kwamba wao ndio wavunja ahadi, lakini jambo hilo halikutokea, hii inaonesha kwamba Maqureshi walifahamu kwamba wao hawana haki ya kudai kwa kuwarusdisha wanawake kwa mujibu wa agano hilo.

Al-Tahar Bin Ashour alisema katika tafsiri yake [Al-Tahrir wa Al-Tanwir, 28/155, Al-Dar Al-Tunisia Lel-Nashr- Tunisia]: “Mahitaji ya masharti ya Mkataba ni uwazi kwa ajili ya ukubwa wa Mkataba huo na haki inayotokana nao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasahaulisha washirikina sharti lao kwa ajili ya kuhurumia wanawake wahamiaji, ambapo amewatengenezea njia ya kutokea”.

Ama kuhusu maneno yaliyotajwa katika hadithi ya upatanisho huo, ambayo yalikuja mara kwa maana inayohusiana na wanaume, na mara nyingine inayonahusiana na wote, wanaume na wanawake, jibu kuhusu hali hiyo ni: kwamba tofauti hiyo ni pengine inatokana na tofauti ya waliosimulia hadithi hiyo; haiwezekani kuwa maneno haya yote tofauti kutajwa katika hati ya Mkataba huo, na maneno ya hadithi yaliyobainisha kwamba sharti lilihusiana na wanaume ni sahihi zaidi kwa ajili ya yaliyotangulia hapo juu, na pia haiwezekani kwamba Mwenyezi Mungu anamwamuru Mtume wake, S.A.W. kuvunja ahadi.

Imepokelewa na Al-Dhahhaaq, nae alisema: ilikuwepo ahadi kati ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. na washirikina: kwamba hakuna mwanamke yeyote asiye Mwislamu miongoni mwetu atakuja kwako, ila umrudishe kwetu, lakini kama ameingia dini yako, na ana mume, basi arudishwe kwa mume wake aliyrbeba jukumu la kumgharamia kwa kila kitu, na kwa Mtume S.A.W. kama kuna sharti hilo hilo. [Tafsir Roho Al-Maani kwa Al-Alusi, 14/271, Al-Maktaba Al-Elmiyah- Beirut]. Kutokana na hayo, kama washirikina wakipatanishwa na Mtume S.A.W. kuhusu kuwarudisha wanawake, basi inakusudiwa wanawake wa waashirikina wasio Waislamu tu, na hiyo inathibitisha kuwa wanawake Waislamu wahamiaji hawakutajwa kimaandishi ndani ya Mkataba huo.

Sheikh Mohammed Ali Al-Sais anasema katika “Tafsir Ayat Al-Ahkam” [1/759, Al-Maktaba Al-Asriya Lel Tibaa]: “Baadhi ya wanavyuoni wanaamini kwamba formula ya ahadi haikuwa kama ilivyotangulia hapo juu, nayo ilikuwa pamoja na matini maalum inayohusu wanawake, ambayo ina maana kwamba: Hakuna mwanamke yeyote asiye Mwislamu miongoni mwetu atakaekuja kwako, ila umrudishe kwetu, lakini kama ameingia dini yako, na ana mume arudishwe kwa mume wake mwenye jukumu la gharama zote kwake, na kwa Mtume S.A.W. sharti ni kama hilo hilo. Na kutokan an hayo, basi Aya inaafikiana na ahadi. Na mtazamo huo ni sahihi zaidi kuliko yote. Ama kuhusu mitazamo mingine iliyotangulia hapo juu ni kinyume na Uti wa mgongo wa sheria ya Kiislamu kwa upande wa kwamba kutimiza ahadi ni wajibu, na haipaswi kuwa upande mmoja miongoni mwa pande mbili kuainisha matini zake au kuziondoa pasipo na mwafaka wa upande mwengine, na unajua kwamba ahadi ya kuutekeleza Mkataba wa Al-Hudaybiyah haikuondolewa ila baada ya Maqureshi kuivunja kwa kwenda kinyume na viapo vyao.

Kulingana na yaliyotangulia hapo juu, na kwa mujibu wa swali lililoulizwa: haiwezekani kwa mshirika yeyote kuivuja ahadi mliyokubaliana kati yenu, wala haiwezekani kudai kwamba Mtume S.A.W. amevunja baadhi ya masharti ya mkataba wa Alhudaibiyah, uliouweka kati yake na Maqureshi, na hakuna tofauti yoyote katika kuvunja ahadi, kati ya kuvunja sharti moja au zaidi. Kwa hivyo basi, kukiuka baadhi ya masharti kunapelekea kuvunjika kwa ahadi nzima.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas