Mambo ya Sufi

Egypt's Dar Al-Ifta

Mambo ya Sufi

Question

Baadhi ya watu wanaibua fitna kwa kudhani kwao kuwa wafuasi wa Usufi wametamka maneno ya kikafiri yaliyo wazi, na kwamba wao ni makafiri kwa kutamka kwao maneno hayo ambayo kwayo wameudhihirisha ukafiri wao. Je ni upi ukweli wa jambo hili? Tunaomba mlitolee fatwa.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Sifa zote njema ni zake, rehema na amani zimfikie Mtume wetu yeye na jamaa zake, maswahaba wake na wafuasi wake.

Baada ya utangulizi huu.
Pamepokelewa kwa baadhi ya sufi wa kisasa kama vile Al Harawiy, Ibnu l Arabiy, Ibnu Sabiin, Afiifiy Atalmasaaniy, Ibnu-Lfaridh na wengine wengi miongoni mwao, bali hata waliowatangulia hawa kama vile Al Hallaaj aliyefariki mwaka (309 hijiria), na Al Bastwaamiy aliyefariki mwaka wa (261 hijiria) pamepokelewa maneno yenye mawazo tofauti yasiyoeleweka kwa mtu ambaye hakutaka kuangalia istilahi za watu hawa, isipokuwa kwa kuwa kwake maneno haya yana mawazo mengi na wala hayaeleweki hayamaanishi kuwa aliyeyasema amekufuru. Na hasa kwa kuwa maneno haya yana tafsiri yake kwa ajili ya kuitumia katika kuleta dhana nzuri kwa viongozi hawa. Lakini sisi hatutaingia katika ufafanuzi wa matamshi hayo na kutaja tafsiri zake, kwa sababu wanachuoni wengi wameandika vitabu vingi vinavyoyafafanua hayo, kama vile tafsiri ya Isitlahi za Sufi Shatbiy ya Ashaaraniy na Allam-u ya Siraaj na wengine wengi.

Sisi tunasema kuwa Mfuasi wa Usufi ameyapuuza mambo yote isipokuwa Mwenyezi Mungu, pale anapokuwa katika safari yake ya kukua kiroho na katika kupanda ngazi ya kimwenendo, na Moyo wake ukajisafisha na kilakisichokuwa na uhusiano na Mwenyezi Mungu, na akawa katika Ulimwengu wa uwepo uliio sawasawa, na ushuhuda ulio sawasawa na ibada iliyonyoofu, kasha ikmdhihirikia haki kwa mara ya kwanza na wala hakuweza kuvumilia kwa kile alihokiona, si hivyo tu, bali akjikuta akipiga kelele katika hali ya kuleweshwa na kile alichokiona: akasema: Mimi wewe! Hakika imemdhihirikia siri kuu, na wala hakuwa na nguvu za kutosha kuweza kuibeba amana katika undani wake, ulimi wake ukajaa ufasiri wa picha aliyoiona lakini ukashindwa kueleza kwa maneno ya Lugha inayoeleweka, na hapo ndipo anapoangukia makosani, mpaka pawepo katika hili njia ya kuondosha nguvu hiyo kubwa. Na hali hii huitwa tukio la Shathi, nalo ni “maneno yanayofasiriwa na ulimikutoka katika undani ambayo yanapindukia uwezo wake wa kimaumbile huku yakiambatana na wito” [Allam-u Lisiraj uk 346].

Na sisi tuna haja ya kuweka mfumo wa namna ya kuyachukulia maneno haya ya sufi wa kisasa kwa ujumla, na tumekikuta tunachokitaka, kwa mwanachuoni Ibnu Khaldun ambaye anasema:

“Kisha wengi miongoni mwa wanachuoni na watoa Fatwa wameamua kufuata njia ya kuwarudi hawa Sufi wa Kisasa katika Makala mbali mbali na mfanowe, na wakajumuisha upingaji huo kwa kila kilichoangukia mikononi mwao. Na ukweli ni kwamba maneno yao pamoja nao yanahitaji maelezo marefu. Ni kwamba maneno yao hayo yanagawanyika sehemu nne:

Ya kwanza: Maneno yanayohusu mapambano na yanayopatikana miongoni mwa vionjo na matukuzo na kuikanya Nafsi kutokana na vitendo, ili ivipate vionjo hivyo ambavyo hubadilika na kuwa maafikisho ambayo hupanda heo na kuwa kingine kama tulivyokwishasema.

Ya pili ni: Maneno ya Ufihuaji na Mambo ya kweli yanayopatikana katika Ulimwengu wa visivyoonekana, kama vile Sifa za Kiungu, Kiti cha Enzi, Malaika, Wahyi, Utume, Roho na Mambo ya kweli yanayohusu viumbe vyote visivyoonekana na vinavyoonekana, na miundo ya Ulimwengu wote tangu mwanzo wake kutoka kwa Muumba wake na aliyeutengeneza kama ilivyotangulia kuelezwa.
Na ya Tatu: Vitendo katika Maumbo mbali mbali ya Ulimwengu huu kwa aina za Makarama.
Na ya Nne: Maneno yasiyoeleweka uwazi wake yaliyosemwa na wengi miongoni mwa Maimamu wa Sufu, wanayatumia kwayo katika istilahi zao kama ni Shatahaati. Nazo huunda mionekano yake, na kasha kusababisha uwepo wa yanayokanwa, yanayoboreshwa, na yanayofasiriwa.

Na maneno kuhusu Mapambano na maafikio na yanayopatikana miongoni mwa vionjo na mazuri katika matokeo yake, na kuihunga nafsi katika kuzembea njia zake, basi jambo hili halina msukumo wa mtu yeyote yule, na vvionjo vyao ndani ya hali hii ni sahihi, na kuvifikia vionjo hivyo ndio hasa furaha yenyewe.

Ama maneno kuhusu makarama ya Sufi na wkujua kwao mambo yasiyoonekana na vitendo vyao katika viumbe mbali mbali, hili ni jambo lililosahihi lisilokanwa ingawa baadhi ya wanazuoni wanamili katika kulipinga, si haki katika hilo. Na hoja zilizotolewa na mwalimu Abuu Ishaaq Al-Isfaraaniy kutoka kwa Maimamu wa Ash-ariy kuhusu kulikana jambo hili kwa kuhusika kwake na miujiza, wahakiki wengi wa Sunna wametofautisha kati ya mawili haya kwa changamoto, nayo ni madai ya kutokea miujiza kwa mujibu wa aliyoyaeleza, wamesema; Kisha kutokea kwake kwa mujibu wa madai ya mwongo hakupewi uzito wowote, kwa kuwa Maana ya Muujiza ili uaminike ni ya kiakili, kwa hivyo sifa yake namna ilivyo ni ya kuamini, na kama ungelimtokea Muujiza huo mtu Mwongo basi sifa yenyewe ingelibadilika. Na jambo hili ni muhali. Na hili ni pamoja na kuwa Uwepo unashuhudia kutokea kwa makarama mengi ya aina hii, na kuyakanusha ni aina ya jeuri. Na mengi miongoni mwa makarama kama haya yaliwatokea maswahaba na Salaf wengi na jambo hili linajulikana na ni mashuhuri.

Na kuhusu Ufichuaji na kutoa maelezo ya mambo ya kweli ya Ulimwengu wa juu pamoja na mpangilio wa kuumbwa viumbe mbali mbali, mengi ya maneno yao katika jambo hili yana mkanganyo kwa kuwa ni ya undani wao, na yameukosa undani kwa kutengana na vionjo vya ndani yake.

Na Lugha hazitoi mweleweko wa wanayoyakusudia kwa kuwa Lugha hazikuwekwa isipokuwa kwa vti vinavyotambulika, na vingi kati ya vitu hivyo ni vile vinavyohisika. Ni bora tusiingilie maneno yao katika jambo hili, na tunaliacha katika yale tulioyaacha miongoni mwa yanayokanganya. Na yule mwenye kupewa na Mwenyezi Mungu ufahamu wa kitu katika maneno haya kwa namna ya kuwafikishwa kwa uwazi wa Sheria, basi kwayo ni furaha ya hali ya juu.

Na kuhusu matamshi yasiyoeleweka maana zake na ambayo wanayaita kuwa Shatwahaati, na watu wa Sheria wanawachukulia kwayo, jua kwamba uuwianishaji katika jambo la Sufi kwamba wao ni watu wa Ulimwengu ulio mbali na hisia, na maneno yajayo (kutoka katika Ulimwengu huo) huwatawala mpaka wakatamka kutokana nayo, yale wasioyakusudia. Na mtu wa Ulimwengu usioonekana si wa kuzungumza nae, na anaetenzwa nguvu ana udhuru (unaokubalika kisheria).

Na yule wa miongoni mwao anayejulikana kwa fadhila na kufuatwa kwake, atahukuliwa kuwa alikuwa na lengo zuri kutokana na jambo hili na mfano wake. Na kwamba maana ya neno “Mawaajid au mazuri” ni ngumu (kueleweka) kutokana na kukosekana hali yake, kama ilivyotokea kwa Abi Yazid Albastwaamiy na mfanowe. Na mtu ambaye hazikujulikana fadhili zake na wala hakuwa mashuhuri, huchukuliwa yale yatokayo kwake miongoni mwa manenoiwapo hatutaweza kuona wazi kile kinachotufanya tuyafasiri maneno yake.

Na kwa upande wa yule atakaezunguma kwa mfano wa maneno hayo hali ya kuwa yuko katika hali ya kawaida ya hisia zake na wala hakutawaliwa na hali (ya kuleweshwa) maneno yake pia yatachukuliwa kama yalivyo” [Muqaddima Ibni Khalduun, kitabu cha Abdulrahman Bin Khaldun, ukr 587-588]

Kwa hivyo aliyoyasema Ibnu Khaldun yanaweza kuwa Mwongozo wa kufuatwa katika kuzifanyia kazi maana za Sufi, kutokana na manufaa mbali mbali yaliyomo ndani yake, kwani yanatupa nafasi ya kunufaisa kutokana na Urithi mkubwa, na yanatuunganisha. Na yatatuepusha tusije tukaangukia katika yale yanayomuudhi Mwenye Mungu miongoni mwa maneno yao. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe kwa ajili ya uongofu na kuwa mbali na kila jambo ovu. Ewe Mola wetu tukubalie dua yetu hii.
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu zaidi na ndiye Mjuzi wa kila kitu.
 

Share this:

Related Fatwas