Kugongana Maoni ya Wanavyuoni Kuhusu Mapinduzi ya Kisasa
Question
Maoni ya wanachuoni yamegawanyika na kugongana juu ya mapinduzi yaliyopo katika baadhi ya nchi za Kiarabu kwa wakati huu, na neno Fitina limekuwa likisemwa na wengi mara kwa mara, miongoni mwa wanachuoni na mamufti wakiliongelea jambo hili. Kwa hivyo basi, ni ipi njia ya kuzuia Fitina? Na nini kukumu ya mapinduzi hayo? Na nini sababu ya kutofautiana baina ya maoni ya wanachuoni juu ya matukio hayo ya mapinduzi?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Fitina katika lugha ina maana nyingi: miongoni mwake: balaa, mtihani na jaribio. Na miongoni mwa maana zake ni katika tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je, watu wanadhani wataachwa (wasitiwe katika msukosuko) kwa kuwa wanasema "Tumeamini?" Basi ndio wasijaribiwe (wasipate mtihani?} [AL ANKABUUT 2], yaani na wao hawatahiniwi?, na husemwa pia: na wao hawajaribiwi ili kubainisha uhakika wa imani yao. Na kadhalika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hapana; bila shaka tuliwatia katika taabu wale waliokuwa kabla yao} [AL ANKABUUT 3], yaani tuliwatia katika mtihani na tuliwajaribu.
Na miongoni mwake ni upotofu na dhambi, kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala usinitumbukize katika Fitina} [AT TAWABA 49]. Na Fitina ni yale yanayotokea baina ya watu miongoni mwa ugomvi, na inasemekana kuwa yale yaliyotokea baina ya Ali na Muawia Radhi za Allah ziwafikie wote wawili ni Fitina. Na Fitina ni kuua, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Iwapo mnaogopa wale waliokufuru watakutaabisheni.} [AN NISAA 101], na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa sababu ya kumwogopa Firauni na wakuu wao, ili asiwatese} [YUNUS 83]; yaani anawaua, [Rejea: Lisaan Al Arab Li Ibn Mandhuor, 317/13, Ch. Dar Ssader, na Tahdheeb Al Lugha Li Al Azhariy 211/14, Ch. Dar Ihiyaa Al Turaath Al Arabiy, Ch. ya kwanza, 2001, na Bassair Dhawi Al Tamaiyez Li Al Fairuzabaadiy 167/4, Ch. Baraza kuu la Mambo ya Kiislamu].
Ama Fitina iliyotajwa na Sheria inasemwa kuwa: "Anayeilalia Fitina hiyo ni bora zaidi kuliko anayeikalia macho, na anayeikalia macho ni bora zaidi kuliko anayeisimamia na anayeisimamia ni bora zaidi kuliko anaeihangaikia. [Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Abi Huraira R.A]
Kwa hivyo basi, Fitina ina udhibiti wake, nayo hutokea kwa kumwaga damu bila ya haki. Na hadithi ya Mtume S.A.W. inathibitisha hivyo: "Siku ya Kiyama haiji mpaka pande mbili zipigane, na yatokee mauaji makubwa kati yao huku pande hizo zikiwa na wito mmoja..... na mpaka elimu itoweke.... na Fitina zikadhihirika na utani ukaongezeka". Na katika riwaya nyingine: walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Hii Fitna ni nini? Akasema: "Kuua kuua", [Imepokelewa na Al Bukhariy].
Na si lengo kufasiri neno utani kwa maana ya kuua, na kwamba kisicho mauaji si utani, bali hayo ni kama kauli yake aliposema: "Hija ni Arafa" yaani ni sehemu kuu ya Hija na nguzo yake kuu ni Arafa, basi maana inayodhihiri kwa kutumia neno utani ni kuua. Kwa hivyo basi, utani katika lugha ni hitilafu na mgongano -na hiyo inaafikiana na maana ya kilugha ya neno Fitina - na nyakati nyingine hitilafu na mgongano hupelekea kuua.
Na inawezekana kuwa kwamba Fitina inaweza kuhusika na baadhi ya sifa nyingine -na hiyo fitina ikitokea basi hakuna wa kusalimika nayo isipokuwa watu wachache sana, na kwamba matokeo yake hayajulikani. Na ilipokelewa kutoka kwa Ibn Al Mubarak: "Aliyeleta sababu ya Fitina katika nafsi yake mwanzoni hatasalimika nayo mwishoni mwake hata akijitahidi".
Na miongoni mwa sifa zake pia; kuwa watu wenye kutegemewa kielimu na wenye ujuzi wanatumbukizwa ndani yake. Kwa hiyo imesemwa kuwa; "Katika Fitina, hekima na busara hukosekana".
Na kuhusu matukio yanayotokea katika eneo la nchi za Kiarabu hivi sasa, yamesambaa katika nchi kadhaa, na kila nchi ina hali maalumu inayotofautiana na nchi nyingine, kwa hiyo basi, kutoa hukumu moja kwa nchi zote za Kiarabu bila ya kudadisi kweli kweli na kuijua hali halisi ya kila nchi ni jambo lisilo sahihi. Na kwa hiyo, wanachuoni wa kila eneo, wao ndio wajuzi zaidi wa hali halisi ya eneo lao na wao peke yao ndio wanaoweza kutoa hukumu ya kisheria juu ya mapinduzi hayo.
Lakini kuna mkusanyiko wa vidhibiti vikuu ambavyo vinavyodhibiti mtazamo wa kina, na ambavyo haviwezi kujiepusha na ufuatiliaji wake pale mtu anapotaka kutoa fatwa ya jambo hili. Navyo ni kama ifuatavyo:
Kwanza: Sheria tukufu imeharamisha kumwaga damu na kulitilia mkazo. Kwa hivyo basi imepokelewa na Al Bukhariy kutoka kwa Ibn Omar R.A. amesema: Mtume S.A.W. alisema: "Mwislamu ataendelea kuwa katika hali nzuri kwenye dini yake iwapo hata mwaga damu ya haramu."
Na imepokelewa na At Tarmeziy kutoka kwa Abdullahi Bin Omar Radhi za Allah ziwafikie wote wawili, kwamba Mtume S.A.W. anasema; "Kutoweka kwa dunia ni rahisi zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko kumwua mtu aliye mwislamu." Na imepokelewa na Abi Huraira R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Kama lau viumbe wa mbinguni na ardhini wangelishirikiana katika kumwaga damu ya muumini basi Mwenyezi Mungu Mtukufu angeliwatupa motoni." Na imepokelewa na Ibn Majah kutoka kwa Ibn Omar R.A. amesema: "Nilimwona Mtume S.A.W akitufu Alkaaba na huku akisema: ni uzuri ulioje wa harufu yako! Ubora ulioje wa utukufu wako! Na naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhamad iko katika mikono yake, utukufu wa mwislamu ni mkubwa sana kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko huruma kutoka kwako; mali yake na uhai wake, na tusimdhanie isipokuwa mazuri tu.
Pili: Mikusanyiko na mapinduzi kwa njia ya amani, ni moja kati ya aina za kuamrishana mema na kukatazana mabaya. Na hiyo ni miongoni mwa njia za kushinikiza kisheria, kama zikifuatwa na kutokea kwa njia ya kisheria, na kuingia katika matahadharisho ya kisheria; kama vile, kudai kwake jambo lililo haramu au lililozuiliwa kisheria, au kuzorotesha masilahi ya watu au kutokea mchanganyiko kati ya wanaume na wanawake kwa namna iliyo haramu au mfanowe.
Na dalili ya uhalali wa mikusanyiko hiyo, ni yale yaliyopokelewa na Al Haakem katika kitabu cha [Mustadrak] kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa mtu mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W. na akamshitaki jirani yake, kwa kusema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! jirani yangu ananikera sana." Basi Mtume S.A.W. akasema: "Itoe mizigo yake na iweke njiani," basi mtu huyo akaitoa mizigo yake na kuiweka njiani. Basi ikawa kila anayepita kando yake anasema: "Kwa nini umefanya hivyo? Mtu huyo akasema: "Mimi nilimshitaki jirani yangu kwa Mtume S.A.W, Mtume akaniamuru nitoe mizigo yangu na niiweke njiani. Kwa hivyo basi, watu wakaanza kusema: Ewe Mola wangu mlaani, ewe Mola wangu mdhalilishe. Mtu huyo akasema: "Jirani yangu alisikia hayo, basi akaja haraka sana na akasema irudishe mizigo yako na mimi kamwe sitakuudhi tena.". Ama kuhusu maandamano, basi asili yake ni halali kama ilivyo kwa mkusanyiko wa watu na wala hakuhitaji dalili maalumu ya jambo hili.
Tatu: Asili ya kisheria ni kuwa haijuzu kuandamana dhidi ya mtawala mwislamu, hata kama ni dhalimu, isipokuwa akiangukia katika ukafiri, basi tunamtanguliza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuendelea kubakia kwake madarakani kusisababishe uovu mwingine mkubwa zaidi ya huo.
Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Hudhaifa Bin Al Yamaan R.A. alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sisi tulikuwa wanadamu basi Mwenyezi Mungu akatuletea heri, na sisi tumo ndani ya heri hiyo sasa, na je, baada ya heri hiyo itakuja shari? Akasema: "Ndiyo", nikasema: Je, baada ya shari hiyo itakuja heri? Akasema: "Ndiyo", nikasema: Je, baada ya heri hiyo itakuja shari? akasema: "Ndiyo", nikasema inakuaje hivyo? Akasema: "Baada yangu watakuwapo maimamu wasioongoza kwa mwongozo wangu, na wala hawafuati Sunna yangu, na miongoni mwao watu watakuwa wenye mioyo kama mioyo ya mashetani katika mwili wa mwanadamu." Mtu huyo akasema: nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nitafanyeje kama nitawahi hali hiyo? Akasema: "Sikiliza na umtii kiongozi (wa waislamu), hata kama atakupiga mgongoni na kuchukua mali yako, basi umsikilize na umtii."
Na maandamano yanayokatazwa ni yale yanayofanyika huku watu wakiwa na silaha. Shekh Ibn Taimia amesema katika kitabu cha [Minhaaji Al Sunna 391/3, Ch. Chuo Kikuu cha Al Imam]: Inafahamika katika madhehebu ya Ahlu Sunna ni kwamba wao hawaoni kuwa watu wanapaswa kuandamana dhidi ya kiongozi na kupambana nae kwa silaha hata kama ni dhalimu, kama zisemavyo hadithi nyingi na sahihi kutoka kwa Mtume S.A.W.; kwani uharibifu unaotokana na kupambana nao pamoja na Fitina ni mkubwa zaidi kuliko uharibifu unaotokea kutokana na dhulumu yao bila ya kupigana nao, na pia bila ya kuwepo Fitina. Kwa hivyo basi, Uharibifu mdogo ni bora kuliko uharibifu mkubwa. Na huwenda uharibifu unaotokana baada ya kundi kumpinga kiongozi ukawa mkubwa zaidi baada ya kumwondosha kiongozi.
Na kwa kunukuu huku, inadhihirika pia kuwa kuzuia kumwasi mtawala mjeuri si kwa ajili ya utawala mwingine au kwa ajili ya kuvunjika moyo, bali ni kwa ajili ya kutenda madhara madogo zaidi kati ya madhara mawili. Na wanachuoni wengine wameyasema hayo pia, Al Haafidh Ibn Hajar amesema katika kitabu cha [Tahdheeb Al Tahdheeb 288/2, Ch. Dai'rat Al Maarif Al Nidhami bilhindi]: Kuwapinga maimamu majeuri kwa upanga ni madhehebu ya waliotangulia kale. Lakini maamuzi yaliyofikiwa baadae ni kuliacha jambo hili; walipoliona kuwa linapelekea hali mbaya zaidi ya iliyokuwepo kabla: Kwa hivyo basi, katika tukio la Al Hura na tukio la Ibn Al Asha'ath na mengineyo kama haya, ni fundisho na ni somo kwa wenye busara.
Na Al Khadimiy amesema katika kitabu cha [Bariqat Mahmoudiah 124/3, Ch. Al Halabiy]: kumpinga sultani dhalimu kwa udhalimu wake kunapelekea umwagikaji wa damu nyingi kwa pande zote mbili zinazogombana, na kwa kawaida vita vina madhara zaidi kuliko udhalimu wa sultani." Na katika maana nyingine ya kupinga kwa silaha: ni mambo yote yanayopelekea matokeo yanayotakikana kuepukwa, ambayo ni haramu.
Nne: Kudai marekebisho ya utawala ni jambo lenye kuingia akili, ama kutaka kuzing'oa tawala hizo na kuziteketeza kabisa ni jambo lisilokubalika kabisa kwa kuwa tawala hizo zinaweza kurekebishika na kutangamaa, si tu kwa ajili ya kuzibadilisha, au kwa ajili ya malengo mengine yasiyo ya kisheria.
Tano: Udharura wa kuwa na uthibitisho wa maelezo na kutokimbilia tetesi, kutojenga misimamo na kutotoa hukumu ambazo zinatikisa usalama wa kijamii na kuchafua majina ya watu bila ya dalili ya wazi. Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Abi Huraira R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Inatosha kwa mtu kuwa mwongo pale atakapozungumzia kila jambo analolisikia."
Imamu Al Nawawiy katika kitabu cha [Sharh Muslim 76/1, Ch. Dar Ihiyaa Al Turaath Al Arabiy]: anasema: Na ama maana ya hadithi na athaari zilizopo katika mlango huu; ni kuwa zinakemea na zinakataza kulizungumzia kila jambo ambalo mtu hulisikia; kwani kwa kawaida mtu husikia ukweli na uongo. Kwa hivyo basi, kama akilizungumzia kila jambo analolisikia basi yeye ni mwongo, kwa sababu yeye hulizungumzia jambo lisilokuwepo."
Na imepokelewa na Abu Dawud kutoka kwa Ibn Omar Radhi za Allah ziwafikie wote wawili kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Anayemsema mwislamu mwenzake kwa yale ambayo hakuyafanya basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamkalishi katika maangamio mpaka atakapojitoa katika yale aliyoyasema".
Sita: Kuiachia haki yako, kujiepusha na ubabe na kutowashambulia raia hata kama wao walishambulia, ili kuzuia mmwagiko wa damu na kuitupia mbali Fitina ni jambo jema linalozingatiwa, na mtu yoyote anaefanya hivyo hushukuriwa. Kwa hivyo basi, suala la kutenda madhara yaliyo madogo kati ya mawili halifanywi kwa raia wa kawaida tu, bali pia hufanywa kwa watawala. Mtume S.A.W. alimsifu Al Hassan Bin Ali kwa kuachia madaraka ili kuzuia umwagikaji wa damu, kama ilivyokuja katika kauli ya Al Hassan Al Bassriy: Wallahi! Al Hassan Bin Ali alimpokea Muawia kwa vikosi vya jeshi kama milima, basi Amru Bin Al Aas akasema: Mimi naona vikosi ambavyo havirudi mpaka viwaue maadui wake, basi Muawia akasema Wallahi! Alikuwa ni mtu mwema zaidi kati ya watu wawili: ina maana Amru kama hao watawaua hawa, wale wakawaua wale ni nani anaweza kunisaidia katika mambo ya watu hawa, ni nani anayeweza kunisaidia mimi kuhusu wanawake wao, ni nani anayeweza kunisaidia mimi kuhusu nini cha kufanya kuhusu mashamba yao. Kwa hivyo basi akawatuma wanaume wawili wa Kikuraishi kutoka kwa Bani Abdu Shams: Abdulrahmaan Bin Samrah, na Abdullahi Bin Aamer Bin Kreez. Kwa hivyo basi, akasema nendeni kwa Mtu huyo, na mumwonyeshe mapendekezo yenu, na semeni naye; na kisha mwombeni. Basi wakaja mpaka mahali pake, na wakaingia kwake kisha wakaongea naye; basi Al Hassan Bin Ali akawaambia kwamba: sisi ni watu wa Abdulmuttalib, tumekumbwa na mikasa kutokana na mali hiyo, na kwamba umma huu umezama katika dimbwi la damu yake, wakasema: kuwa yeye anakupendekezea hivi na hivi, na anakuomba na anakuulizia, Akasema ni nani anayeweza kunisaidia kwa jambo hili, wakasema sisi tutakuwa nawe katika kila jambo, basi kila alipowaulizia jambo walisema sisi tutakuwa nawe katika jambo hilo, kisha akaamua kuelewana naye. Na Al Hassan akasema: Nimesika Abu Bakara akisema: nilimwona Mtume S.A.W. akiwa juu ya membari na Al Hassan Bin Ali akiwa kando yake, na yeye anawatazama watu mara moja na kisha anamtazama Al Hassan mara nyingine na anasema: "mwanangu huyu ni bwana mkubwa, na huwenda Mwenyezi Mungu atamjaalia aweze kusuluhisha baina ya makundi mawili makubwa ya waislamu." Imetolewa na Al Bukhariy.
Ama kuhusu hitilafu ya wanachuoni juu ya mapinduzi yaliyotokea katika baadhi ya nchi za Kiarabu hivi karibuni: basi hakuna shaka kwamba hitilafu ni jambo la kawaida, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Kwa hivyo wataendelea tu kuhitalifiana} [HUD 118], kwa hivyo basi, watu kuhitalifiana ni jambo la kimaumbile, na hitilafu iliwahi kutokea baina ya manabii ukiongezea na kutokea kwake kati ya wanachuoni. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyataja hayo katika kisa cha Dawud na Sulaiman walipokuwa wakitoa hukumu ya makonde; {Na (wakumbushe) Daudi na Sulaiman walipokata hukumu juu ya konde, walipolisha humo mbuzi wa watu usiku. Nasi kwa hukumu yao hiyo tulikuwa Mashahidi, (tunaona tunasikia), (78). Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na elimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tuliofanya hayo. [AL ANBIYAA 78-79]. Na katika kisa cha Mussa na Haruni katika kisa cha kuabudu ng'ombe dume wa Bani Israiel: {(Musa aliporejea) alisema. "Haruna ni nini kilichokuzuia (usinifuate) ulipowaona wamepotea," (92). "(Kilichokuzuia) usinifuate Je! umeasi amri yangu? (93). Akasema: "Ewe mwana wa mama yangu usinishike ndevu zangu (kuzivuta) wala kichwa changu (kukikokota kwa ghadhabu). kwa hakika mimi niliogopa (kuondoka na baadhi na kawaacha baadhi) usijesema: "Umewatawanya wana wa Israili na hukungojea kauli yangu."} [TA HA 92-94].
Na kama watu wangelikuwa katika rai moja basi Mwenyezi Mungu Mtukufu asingewawekea sheria ya kushauriana, na wala Mtume wake S.A.W. asingeamrisha watu wafanye hivyo. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema katika kuwasifu waumini: {Na wanashaurina katika mambo yao.} [ASH SHUURA 38], na Akasema kumwambia Mtume wake: {Basi wewe wasamehe na uwaombee msamaha (kwa Mwenyezi Mungu) na ushauriane nao katika mambo} [AALI IMRAN 159]. Na masahaba na wanachuoni, baada yao walihitalifiana katika matawi mengi ya kifiqhi.
Na kutokana na hayo, basi hitilafu ya wanachuoni kuhusu mapinduzi haya yanayotokea kwa sasa, si uzushi, bali ni jambo ambalo lipo kama ambavyo lilikuwepo hapo kabla katika mambo mbali mbali
Na sababu za hitilafu hizi ni nyingi, miongoni mwazo: hitilafu yao katika kufahamu hali halisi na namna ya kuiwaza hali hiyo. Na uhalisia wa hali unatokana na ulimwengu wa vitu, ulimwengu wa watu, ulimwengu wa matukio, ulimwengu wa mawazo na ulimwengu wa nidhamu. Na huwa unatokana pia na aina mbali mbali ya mahusiano yenye nguvu baina ya aina zote za ulimwengu. Na hitilafu hii huwa inajenga hitilafu katika kuleta taswira ya mambo mbali mbali, na kisha hitilafu katika kuyaweka mambo hayo katika hali ya kisheria. Na hii labda ndio sababu iliyozaa hitilafu katika hukumu kwa kila mtazamaji.
Na miongoni mwake: Ni ufahamu wa hadithi zinazotajwa katika uzuiaji wa kuingia katika Fitina na uwajibikaji wa makundi, na usikivu na utiifu, na kuyapeleka haya katika uhalisia, na wataalamu wa misingi ya dini wanaliita hili kuwa ni "Ufikiaji wa Lengo"; na ni namna ya kuthibitisha sababu kuu katika kuangalia picha zake kila moja peke yake kwa mtazamo na kwa kujitahidi katika maarifa na kuwepo kwake katika picha kila moja ikiwa peke yake baada ya kuielewa kama ilivyo. [Rejea: Sharh Al Kawakab Al Muneer, uk, 532].
Na miongoni mwake: Ni hitilafu yao katika kuainisha kama masilahi yanayotazamwa, yanazingatiwa au yamefutwa, na je, uharibifu maalum ni uharibifu halisi au wa kuwazika?. Kisha hitilafu yao baada ya hayo ni katika ukinzani wa masilahi na uharibifu, ni lipi kati ya mawili hayo lililo sahihi na bora zaidi kuzingatiwa.
Na katika kisa cha bwana wetu Mussa pamoja na mja mwema wa Mwenyezi mungu kuna mfano wa hitilafu katika Fiqhi ya ulinganishaji baina ya masilahi na uharibifu; basi Nabii wa Mwenyezi Mungu, Mussa A.S, alichukizwa na huyo mtu mwema pale alipoitoboa meli, kwani kufanya hivyo ni uharibifu unaopelekea kuzama kwa meli na abiria wake. Kwa hivyo basi, yule mtu mwema akamjibu Mussa kuwa uharibifu huo ni kwa ajili ya kuepusha uharibifu mkubwa zaidi, ambao ni kuchukuliwa meli hiyo na mfalme dhalimu, na ili meli ibakie kwa wenye kuimiliki, kuitoboa ni bora zaidi kuliko kuipoteza kabisa.
Na kadhalika kumwua kijana; Yule Mja mwema alijua fika kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba kijana huyo atakuwa mwasi na kafiri, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atawapa wazazi wake kijana mwema na mwenye heri zaidi kuliko kijana huyo aliyeuliwa. Na pia kutochukua ujira kwa kuujenga ukuta uliokuwa unakaribia kuporomoka ni uharibifu, lakini masilahi ya mayatima wawili yako katika kuujenga ukuta huo kwa ajili ya kuhifadhi mali yao iliyowekwa chini ya ukuta huo, ili baadae watoto hao waitoe ardhini baada ya kubaleghe kwao, na vitendo hivyo vyote ni ulinganishaji baina ya masilahi na maharibifu.
Na ni lazima kuzinduka katika hali kama hii na kutambua kuwa mapinduzi ya kisasa yote hayakuwa ya aina moja, bali mapinduzi haya yalifanya marekebisho ya matakwa yake maalum, jambo ambalo limesababisha kutokea mageuzi ya kudumu ya Fatwa.
Kama ambavyo watawala hawakuwa katika kiwango kimoja kinachofanana ili kuwahukumu, je, kuwapinga kunakatazwa au ni wajibu kufanya hivyo? Na mtaalamu mwenye sifa ya kutazama, anapaswa kufanya taratibu na kuzingatia mno pole pole katika mambo mazito kama hayo, kisha yeye mwishoni hatatakiwa isipokuwa kwa yale aliyoyaona kwa mtazamo wake na kwa jitihada zake, na tunatumaini kuwa atalipwa na Mwenyezi Mungu kwa hali zote, kwa ukweli wa tamko la Mtume lenye kusadikisha hayo pale aliposema: S.A.W.: "Mtawala akitawala na kisha akajitahidi na akapatia basi atakuwa na malipo mawili, na akitawala kisha akajitahidi na akakosea basi atakuwa na malipo ya aina moja tu. " (Bukharin a Muslim).
Na kigezo chake katika hilo pia ni masahaba Radhi za Allah ziwafikie wote; ambapo kila kikundi miongoni mwao kiliyafanyia kazi yale yaliyotokana na jitihada zao katika mambo ya Fitina; Imamu Al Nawawiy katika kitabu cha [Sharh Muslim 110/8] anasema: "Na ujue kwamba damu zilizomwagika baina ya masahaba R.A. haziingii katika onyo, na madhehebu ya Ahlu Sunna na Haki yanataka kuwa na hisia nzuri za kuwadhania kwa wema na kujizuia na yale yaliyotokea baina yao, na namna walivyoyatafsiri mapigano yao, na kwamba wao walijitahidi na kujaribu kutafsiri na wala hawakukusudia maasi au dunia kama dunia, bali kila upande ulifikiria kuwa ndio wenye haki na anayekwenda kinyume ametoka katika uongofu na ni wajibu kupigana naye ili arudi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na baadhi yao walipatia, na baadhi yao walikuwa na makosa na wenye udhuru katika kosa lao hilo; kwani ni jitihadi ya mwenye kujitahidi akikosea hana dhambi.
Na Ali R.A. alikuwa na haki, na alichokifanya katika vita hivyo ni sawa. Haya ni kwa mujibu wa madhehebu Ahlu Sunna, na mambo haya yalikuwa yanafanana, mpaka ikafikia kwamba kundi miongoni mwa masahaba likatahayari katika mambo hayo na kujikuta kuwa linachukua uamuzi wa kujitenga na kila upande kati ya pande mbili za masahaba na wala hawakupigana vita, na wala hawakuwa wakijua usahihi uko wapi na kisha wakachelewa kumsaidia Ali kwa msaada wao.
Ama mwenye kulalamika na mwenye mzigo wa dhambi basi yeye ni mjinga asiyekuwa na uwezo wa kuona mbali, au ni mzembe anayeharakisha kudhihirisha maoni yake kabla ya kukamilisha yanayotakiwa katika utafutaji wa maoni hayo, basi huyo na yule wote wawili wana makosa na hata kama kauli yao itafikiana na haki kama ilivyo, na hawa wana fungu la mzigo katika damu zinazomwagika na uharibifu wa kila aina unaotokea; na katika hadithi "Aliyeanzisha jambo baya katika Uislamu, na kisha likafanyiwa kazi baada yake, basi ataandikiwa dhambi mfano wa uzito wa yule aliyelitumia jambo hilo, na wala hatapunguziwa katika mizigo ya dhambi ya watu waliolifanyia kazi jambo hilo," [Imepokelewa na Muslim].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.