Kuapa kuoa katika uchumba

Nimemchumbia binti na shughuli ya uchumba ilihudhuriwa na ndugu wa pande mbili, kisha nikasafiri kwa sababu ninaishi katika mji mwingine. Na tumepanga tarehe ya ndoa mwezi wa tano, na inshaa Allah nitahamia kuishi huko moja kwa moja, na sisi wawili tumeapa kwamba tutaoana na sote tunajua, NK … lakini msichana amebadili msimamo wake ghafla akidai kuwa hana uhakika, hataki matatizo, hataki kuolewa bado. Nimejaribu kumkinaisha hasa kwa sababu sisi tumeapa kwa Mwenyezi Mungu, akaachana na msimamo wake kwa mwezi mmoja, kisha akajaribu tena kuvunja uchumba, na tumeachana kwa njia ya simu, amesema kuwa yeye ameghairi kiapo chake, na tangu kipindi hicho nimekuwa siwezi kuwasiliana naye yeye wala baba yaje. Mama anataka nikachukue zawadi zangu ambazo nilimpa, lakini mimi ninaamini kuwa hilo si katika adabu. Swali: je, niendelee kujaribu kumnasihi na kung’ang’ania kuwa nae au la? Na je, niombe kurudishiwa zawadi zangu? Na je, watu kama hawa wanahesabiwa kuwa ni Wanafiki? Na je, wanatoka katika Uislamu?

Soma zaidi....

Atakapofariki Mchumba Zawadi za Uchumba Zinakuwa za nani?

Muulizaji anasema: Binti yake amechumbiwa na kijana mmoja miaka miwili iliyopita, na amempa zawadi za uchumba na baadhi ya zawadi, na amefanya sherehe ya uchumba na ametoa gharama zote, na kijana huyu amefariki, naomba kujua hukumu ya kisharia katika zawadi za uchumba?

Soma zaidi....

Zawadi za Uchumba

Ni ipi hukumu ya zawadi za uchumba ambazo mchumba wa kiume humpa mchumba wake kipindi cha uchumba?

Soma zaidi....

Zawadi za Uchumba na Gharama za Kuandaa Nyumba ya Wanandoa

Binti alikuwa amechumbiwa na kijana mmoja, na huyu kija akavunja uchumba, ipi hukumu ya zawadi ya Uchumba aliyoitoa? Na tulikuwa tumeshanunua samani za nyumba ya ndoa, kwa kumjulisha na kumshirikisha, sasa hivi tunalazimika kuviuza, jambo ambalo litapelekea kupungua kwa thamani yake. Je, hasara hii niibebe peke yangu?

Soma zaidi....