Maadili kati ya mazoea na kujizoesh...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maadili kati ya mazoea na kujizoesha

Question

Mazoea ya maadili hujengeka namna gani? Na ni zipi elementi zake? Na ni sababu zipi au vitenda kazi ambavyo husaidia kuyajenga? Na yana umuhimu na athari gani katika mwenendo wa binadamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1-Kwanza kabisa, tuyajue mazoea: Ni hali ya nafsi ambayo hufanya nafsi hiyo itende vitendo vyake bila ya kufikiri wala kuzingatia. Au ni hali au sifa ya nafsi ambayo hudhihirika moyoni na athari zake zikajitokeza katika viungo vya mwili wa mtu kwa kusababisha vitendo bila ya uzito, uzingatiaji au fikra. Na huanza kwa kusababisha vitendo vinavyotokana nayo, kuanzia mwanzo bila ya uzito wowote wa kumalizia vitendo hivyo. Na Marehemu Prof. Dkt. Abdul-Maqsuud Abdulghina – mhadhiri na mkuu wa kitengo cha falsafa ya kiislamu katika Kitivo cha Darul-Uluum – anafafanua maama hizi mbili baada ya kuzinakili kutoka kwa Maskawiya na Alghazali, kuwa zinaashiria kwamba Mazoea hupitia njia mbili katika ujengekaji wake: njia ya kwanza ni ya jukumu la vitendo – na njia ya pili ni ya kutulizana na kuimarika kwake ndani ya nafsi kwa namna ambayo Mazoea hayo yanakuwa ni hali ya msukumo wa utendaji unaofuata mwenendo bila ya tabu au uzito wowote.

2- Na kwa upande wa ujenzi wa Mazoea: ili sisi tuweze kupata picha na namna Mazoea ya Maadili yanavyotengenezeka ndani ya binadamu mpaka yakawa ni kitu chenye mizizi na kutulizana ndani ya Nafsi yake, tunalazimika –kwa mujibu wa mwono wa Marehemu Prof. Dkt. Muhammad Dhiaau Diin Alkurdiy, Mhadhiri na mkuu wa kitengo cha Akida ya Kiislamu na Falsafa, Chuo Kikuu cha Azhar– tunalazimika kusimama na kuangalia vituo vya utendaji wa mwanadamu, na ambavyo huanzia pale anapokuwa na wazo, kisha kumili upande wa wazo hilo, kisha Hamu ya kutenda, kisha Utashi, na baadaye Mazoea.

3- Mawazo haya ni yale yanayokuja moyoni kwanza kwa muda wa mfupi hivi, na yanapotulizana kwa msukumo wa kile kinachoyazuia yasitoke na kukitia nguvu kile kinachoyasaidia basi huwa ni kumili. Na pale mwanadamu anapohangaikia matakwa yake, huku akitambua fika anayoyafikia miongoni mwa ladha au uchungu, na upeo na nafsi yake ikawa na mwelekeo huu, ikielekea kwa yale inayoyaona, na kutambua upeo wake kutokana nayo –na nalengo hutofautiana kwa kutofautiana watu kama vile tajiri, cheo kikubwa, na Ridhaa za Mola… n.k.– na moja kati ya aina hizi za kumili, huwa inazishinda aina zingine na kuwa utashi ambao mtu hufanya kazi ya kuufikia. Na anaetafuta mali kwa mfano, hukimbilia kipato na huweka mikakati kwa ajili ya kukifikia kipato hicho, na yule anaetafuta cheo hufanya juhudi ya kuyatekeleza yale yanayoidhihirisha nafsi yake, na anayemtafuta Mwenyezi Mungu Mtukufu humili katika kumtii Mola Mtukufu, na hivi ndivyo inavyokuwa. Isipokuwa ni kwamba lengo la mwanadamu halifikiwi kwa kuwa na utashi peke yake bali hapana budi pawepo kazi ya kuondosha vishughulishi na vizingiti vyote ambavyo vinazuia kuufikia utashi huo na kwa kutumia njia mbali mbali ambazo zitalifanikisha lengo hilo. Kwa hivyo nafsi inapoifanya kazi hii huwa imehamia katika ngazi ya utashi kisha huhamia kwenye ngazi ya utendaji, na iwapo hali hii itajikariri kwa basi itageuka na kuwa mazoea yake kufanya hivyo, na itakuwa ikijitokeza bila ya yeye kuzingatia wala kufikiri. Tunasema sisi luwa: baada ya hapo, hali hii huwa ni tabia yake. Na maelezo ya wale walioielezea hali hii kuwa: "Hakika maadili ni mazoea ya Uendaji" ni sahihi.

4- Na uchambuzi huu uliotangulia ndio aliouashiria Mtume S.A.W katika kauli yake: "hakika upole hupatikana kwa mtu kuwa mpole, na Elimu hupatikana kwa mtu kujifunza", na kauli yake Mtume S.A.W. "Wema ni Mazoea".

5- Haya ndio maadili katika kukua kwake kutoka katika hatua na kuelekea nyingine, ambapo huanza kwa wazo kasha huwa mazoea. Na hapa kuna swali linalojitokeza: Mazoea huundwa na vitu gani?

6- Moja kati ya vitu vinavyoyaunda mazoea ni: Maumbile ya Kibinadamu ambayo – kwa mujibu wa mtazamo wa Kiislamu –ndani yake kuna kumili Mtu katika heri kutokana na Maumbile yake ya Kiroho, na pia kuna kumili Mtu katika shari kutokana na yaliyomo ndani ya maumbile yake ya kimaada na namna yalivyojengeka ndani yake kwa kuwa na matamanio, hasira, mielekeo na aina mbali mbali za utashi wa Maada. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu {Na tukamuongoza njia mbili} [ALBALAD: 10], na anasema Mwenyezi Mungu {Hakika sisi tumemuongoza katika njia, ama mwenye kushukuru au mwenye kukufuru} [AL-INSAAN: 30], na kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amemrahisishia mwanadamu njia ya heri na shari, isipokuwa ameifanya Roho kuwa ndio chimbuko kuu, na akaipa uwezo wa kuidhibiti Maada iwapo tu mwanadamu huyu atafanya kazi ya kuitia nguvu Roho hiyo. Huu ndio mtazamo wa Kiislamu. Wakati ambapo wanafalsafa wameelekea katika mwelekeo wa mtazamo wenye matumaini kwa mwanadamu kwa kusema kuwa yeye ameumbwa kuwa ni mwenye tabia njema kwa maumible yake. Huku wengine miongoni mwa wanafalsafa hao wapo waliokuwa na mwelekeo mbaya kwa kusema kuwa mwanadamu ameumbwa kuwa na shari. Ukweli ni kuwa, mielekeo yote hii miwili ina makosa na si sawasawa, na ni hatari kwa maadili. Madhehebu ya wale wenye matumaini na ambao hawaoni chochote katika maumbile ya mwanadamu isipokuwa heri, kwanini basi wanajaribu kuyarekebisha! Ni heri hiyo. Sasa nini kinachohitajika baada ya hapo? Ama kwa upande wa madhehebu ya ubaya wao wanaona kuwa maumbile ya mwanadamu humuweka mwanadamu huyo katika kipindi cha chini kimaadili kuliko wanyama, kwani wao wanaona kuwa mwanadamu ndio shari yenyewe na wala hakuna uwezekano wa kuirekebisha. Na kati ya misimammo hii miwili ndipo inapokuja fikra ya Kiislamu kwa Uwastani wake, {Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini –ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndio Dini iliyonyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui} [AL RUUM 30]

7- Na miongoni mwa vinavyoyajenga mazoea ya Kimaadili ni: Urithi. Na Mtume S.A.W. ametuzindua juu ya umuhimu wa jambo hili akasema: "Watu ni kama madini, mbora wenu katika zama za Ujahili ndiye mbora wenu katika zama za Uislamu iwapo wanatambua". Na imepokelewa kutoka kwake S.A.W.: "Chagueni sehemu ya kuweka mbegu zenu za uzazi kwani asili hupenya na kuingia". Na watafiti wengi wa Falsafa wa nchi za Magharibi, wamepanua zaidi tafiti zao wakiuzunguzia umuhimu wa sababu hii, ambapo baadhi yao – kama vile August Kent, Spinoza na Schopenhauer – walipa jambo hili umuhimu usio na mipaka, na hata wakafikia kusema kuwa sifa za Urithi ndio kila kitu katika mwanadamu, na ukweli ni kwamba kuupa urithi umuhimu huu wa hali ya juu usio na mipaka katika utengenezaji wa maadili ni aina ya kuzidisha chumvi na kukiuka. Na hakuna shaka yoyote juu ya umuhimu wa vitu vinavyojenga maadili kama vile maumbile ya mwanadamu na mazingira. Na kilicho sawasawa ni kuwa tuthibitishe kuwa Urithi ni moja ya vitu vinavyojenga mazoea ya kimaumbile bila ya kuchupa mpaka, na tunufaike kutokana na ugunduzi huo katika pande mbali mbali za maisha bila ya kuziengua sifa zinazopatikana kwa kujifunza.

8- Na miongoni mwa vinavyojenga Mazoea ya Kimaadili: mazingira: yawe ya kimaumbile ambayo humuathiri mwanadamu kiakili kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano visababisho vya vinavyotokana na mazingira vina athari za wazi kwa maumbile ya wakazi wa maeneo yenye baridi na maeneo yenye joto. Au mazingira ya kijamii yanayotokana na familia na shule. Watafiti wengi wa kisasa wa nchi za magharibi –kama vile Luka, Stiwats Mill, Delag na Watson– wamezipa athari za mazingira umuhimu mkubwa sana usio na mipaka na wakawa n mwelekeo mwingine unaokabiliana na ule wa wanaosema kuwepo umuhimu mkubwa wa Urithi.

9- Kuna sababu nyingi mno na visababishisho –kama asemavyo Prof. Dkt. Abdulmaksuud Abdulghinaa– ambavyo vinausaidia ujenzi wa mazoea: miongoni mwavyo ni: kuwepo kwa vishawishi au vielemeaji ambavyo vinazingatiwa kuwa mazingira ya makuzi ya mazoea ndani yake. Kwa hivyo nafsi inaweza kujifunza kupenda kitu kwa njia ya mazoea mabaya, na kumili katika kitu hicho au katika mambo mabaya. Ingawa aina hii ya kumili katika vitu hivi si nzuri hata kidogo na inatoka katika tabia. Na hapo ndipo tunapoona kuwa mwanadamu analazimika kuzoea Ukweli na Heri ili viwe ni mazoea kwake. Na iwapo mwelekeo wake kwa vitu hivyo ni dhaifu basi atawajibika kuusisimua undani wake na kujenga utashi wa kuvifanyika kazi viwili hivi mpaka avizoee.

10- Na miongoni mwa vinavyoyajenga Mazoea: ni kukaririkariri jambo. Ni elementi muhimu katika ujenzi wa Mazoea kwani husaidia kupata umakini na kuufikia urahisi na kasi, na kusababisha utendaji unaojiendesha wenyewe bila ya kuwaza wala kuzingatia. Anayetaka nafsi yake ipate sifa ya unyenyekezu basi njia yake ni kuendeleza utendaji wa vitendo vya wanyenyekevu kwa muda mrefu. Na anayetaka kupata sifa ya uvumilivu analazimika kujikalifisha mwanzoni Uvumilivu huo mpaka uwe kwake ni wa kawaida. Kukariri huko kunapaswa kuambatane na mjongeleano wa muda, na jambo hili liwe na muda wa kutosha ili kuimarisha mazoea hayo na kuyafanya yatulizane. Kwa hivyo, mazoea hayapatikani kwa kukariri siku moja. Kwa mfano ibada, haiwezi kupatikana kwa kuikariri usiku mmoja tu. Na hapa haimaanishi kudharau uchache wa kazi, na hasa kwa upande Hasi. Kwa maana kuwa kuacha swala mara moja au mara mbili hakudharauliki kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea Nafsi iupende uzembe.

11- Na miongoni mwa vinavyoyajenga mazoea: Kuiga. Kwa maana ya kuwa na ufuasi wa kufanya mema. Kwa hivyo mazoea hupatikana kwa kuwaona watu wenye kutenda vitendo vizuri na kuambatana nao na kuwaiga. Kwani tabia hupatikana kwa tabia. Na hapo ndipo wanachuoni wanapousia daima kuwa mtu anapaswa kusahibiana na watu wazuri miongoni mwa wema na wenye adabu na maadili mema ili aweze kuyachuma mazuri yao.

12- Na mwisho kabisa, ni kuwa Mazoea ya Kimaadili yana athari nyingi katika Mwenendo wa Mtu: kwanza kabisa husaidia kuukamilisha utu wake, kwa kuunda mjumuiko wa mazoea mazuri kama vile upendo, utekelezaji wa ahadi, huruma, usamehevu, uadilifu na kufikiri vizuri, n.k. maadili mema kama haya yanapogeuka na kuwa ni mazoea ya mtu, basi ni vigumu sana mtu huyo kwenda kinyume nayo wakati ambapo yatakuwa yameukamilisha utu wake.

13- Na miongoni mwa athari zake: humpunguzia mtu kiasi kikubwa cha juhudi ya kibinadamu. Kwani mtu ambaye amejijengea mazoea mazuri ya kimaadili, basi huufuata mwenendo wake ulionyooka na aliouzoea kwa urahisi na wepesi bila ya uzito wowote wala kufikiri. Na kwa hiyo humpunguzia uzito wa kufanya mambo mazuri na ambao ulikuwapo, na kumfanya atumie juhudi zake katika nyanja au kazi nyingine.
14- Na miongoni mwa athari zake: husababisha kazi kufanyika kwa haraka na vilivyo. Kwani hufanyika kwa kujiendesha yenyewe bila ya hisia ndani yake. Na kwa ajili hii baadhi ya wanachuoni wameyaainisha Mzoea kuwa ni utendaji unaotoka katika hisia na kuelekea katika hisia nyingine.
15- Na bila shaka mambo haya yote yanatuashiria athari ya ada katika maisha yetu na mienendo yetu, na yaonyesha faida zinazohusika na mienendo na maadili, hususan kwa upande wa ada njema, na kwa hivyo lazima tusisitize na kushughulikia sana kwa upole wa ada zetu hasa ada nzuri,zilizoathari nguvu juu ya mwanadamu,kwa hivyo wanasema Ada ni tabia ya pili.

Chanzo:
1-Profesa Abdulmaksoud Abdulghany Khashabah, Nadharia ya kimaadili katika Islam-Darasa Linganishi, kairo: Dar Al Thaqafah Alarabiah, 1412\1991 (49-50 )
2-Profesa Mohamed dhiyaa addin Alkordy, Maadili ya kiislamu na SUFI, Kairo: Uchapishaji Alsaadah, 1409-1989, (24-35)

Share this:

Related Fatwas