Mfumo wa Vyama Vingi Vya Kisiasa

Egypt's Dar Al-Ifta

Mfumo wa Vyama Vingi Vya Kisiasa

Question

Je mfumo wa vyama vingi unafaa katika nchi ya Kiislamu?

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W, watu wake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:

Maana ya mfumo wa vyama vingi vya kisiasa ni wingi wa maoni ya kisiasa yanayotokana na wingi wa vyama vya kisiasa.

Na kila chama kinaundwa kwa fungu la watu wana maoni yanayokaribiana kuhusu masuala ya umma, na kila chama kinajaribu kuyafanyia kazi maoni haya kwa njia ya uwakilishi wa bungeni au wizarani au hata kwa njia ya kufikia madaraka ya ngazi za juu katika nchi iwapo watapata njia ya kufanya hivyo.

Hitilafu:
Utofauti ni jambo la kidunia, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Lakini hawaachi kukhitalifiana} [HUUD 118]. Na watu si sawa, ni kama duara tupu halijulikani ncha zake, kwani maumbile ya watu ni kutofautiana, na hitilafu ilitokea kati ya mitume. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaja hayo katika kisa cha Dawud na Sulaiman walipotoa hukumu kuhusu kilimo, na katika msimamo wa Nabii Mussa na Haruon katika kisa cha ya wana wa Israel kuabudia ndama.

Na kama watu wangekuwa na rai moja basi Mwenyezi Mungu Mtukufu asingeruhusu kushauriana na asingemwaamrisha Mtume wake S.A.W kwayo. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika kuwasifu waumini: {na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao} [ASHURA 38], na Akamwambia Mtume wake: {Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo} [AALI IMRAAN 159].
Na hitilafu inapokuwa ndani ya baraza la mashauriano/bunge hapana shaka kuwa inajuzu, na ni yenye kwenda sambamba na bunge ambalo linaendeshwa kwa misingi ya sheria ya Kiislamu. Na Mtume S.A.W alikuwa akishauriana na masahaba wake, na ushauriano huo ulikuwa wakati fulani unakuja bila ya kuomba, kama vile, katika kisa cha Al Habab Bin Al Mundher katika vita vya Badr, na kisa cha Umm Salama katika Sulhu Al Hudaibia, na ushauriano huwenda ukuwa bila ya kuomba lakini ulikuwa ukipingana na rai ya Mtume S.A.W kama vile rai ya Omar R.A. iliyopinga Sulhu Al Hudaibia, na pia kumsalia Abdullah Bin Ubay Bin Salul kiongozi wa wanafiki, na rai baina ya timu mbili au makundi mbalimbali ya waislamu zilikuwa zinapingana, basi Mtume S.A.W anachagua moja kati yao, na mfano wa hayo ni kisa cha mateka wa Badr, kisa cha kukabiliana na makuraishi siku ya Uhud, na kisa cha kushauriana pale msafara wa makuraishi ulipokimbia kabla ya kukutana siku ya Badr. Na baadhi ya wakati ushauriano ulikuwa kwa kuomba lakini mtazamo wa wenye ushauri unatofautiana na mtazamo wa Mtume S.A.W kama vile katika kisa cha kushauriana kwake na Saad Bin Muaadh na Saad Bin Ibaada kuyapa baadhi ya makundi theluthi ya tende za Madina ili kuondosha mzingiro wa Madina siku ya Khandak, wakakataa rai hiyo basi Mtume akachukua rai za watu hao wawili.

Na ama hitilafu ikiwa inatokana na baraza la mashauriano (bunge), basi kuna mitazamo kadhaa; miongoni mwayo: ni kundi la waislamu liwe na rai ambayo kwayo maslahi ya watu yanaweza kufikiwa, na jambo hili linajuzu kwani hakuna kizuizi chochote cha kisheria kinachomzuia mwislamu kuyafikia masilahi yake, ikiwa masilahi hayo yanalihusu kundi la watu na wala si mtu mmoja, basi hapana shaka katika kuthibitisha kujuzu kwake, lakini anaweza kuja mtu kutoka nje anayepinga kujuzu kwake.

Na mwenye kutazama njia ya uhamishaji wa madaraka katika zama za mwanzo, ataona kuwa Sheria ya Kiislamu haikuweka wazi kitu chochote kuhusu jambo hili, namna lilivyo ni kama vile mambo mengine ambayo yana uwezekano wa kubadilika, na haya yanaonekana wazi katika uhamishaji wa madaraka katika zama za Mtume S.A.W na makhalifa walioongoka; Mtume S.A.W hakutaja khalifa wake baadaye, kwa hiyo mjadala ulifanywa ukumbini, na waislamu wakamchagua Abu Bakar R.A., kisha Abu Bakar akamteua Omar Bin Al Khattaab awe khalifa wake, kisha Omar akateua watu sita ili waislamu wachague mmoja kati yao. Na hii inaonesha upana wa njia ya uteuzi, na kwamba inajuzu kuonesha njia nyingine mpya ambazo hazitoki nje ya Hukumu zenyewe za Kisheria katika jambo hili.

Njia ya kumteua khalifa wa kwanza, wa pili na wa tatu inadhihirisha kwamba hakuna nidhamu maalumu ya kisheria katika jambo hilo, na wanachuoni wakaunda maoni yao ya kifikhi kutokana na yaliyotokea na hawakuchupa mipaka.

Dalili za Mfumo wa Vyama Vingi Vya Kisiasa:
Hakuna hukumu iliyokuja kukana mfumo wa vyama vingi vya kisiasa bali iliyokuja inaunga mkono, na miongoni mwa hayo: msimamo wa Answaaru katika ngawira siku ya Hunain, na kisa cha Saad Bin Ibada; basi kutoka kwa Abi Saiyed Al Khudri amesema: "Na pale Mtume S.A.W alipotoa kile alichokitoa kwa makuraishi na makabila ya Waarabu, na Answaaru hawakupata chochote katika mgao huo, Answaaru hawakulifurahia jambo hilo, na baadhi yao wakathubutu kusema: Mtume S.A.W amekutana na watu wake". Basi Saad Bin Ibaada akaingia kwa Mtume S.A.W akisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika baadhi ya watu hawa wameudhiwa katika nafsi zao kwa kile ulichokifanya katika ngawira uliyoipata, umewagawia watu wako na ukawapa watukufu wa makabila ya kiarabu zawadi nono, na Answaaru hawakupata chochote katika zawadi hizo. Akasema Mtume Ewe Saadi, nini msimamo wako katika hili? Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi si chochote isipokuwa ni sehemu ya watu wangu, kwani mimi ni nani? Akasema Mtume: Basi wakusanye watu wako katika eneo hili, akasema: basi Saad akatoka na akawakusanya watu katika ukumbi akasema: basi wanaume Muhaajirina akawaacha na wakaingia, na wakaja wengine lakini akakataa kuwaingiza, basi walipokukusanyika Saad akaja na akasema: watu wa mtaa huo Answaaru wamekusanyika kwa ajili yako, akasema: Mtume S.A.W. akaja ... "akataja hadithi nzima kama ilivyotajwa katika Musnad Ahmad [76/3].

Na uthibitisho uliopo hapa ni kuwa Answaaru walikuwa na msimamo, na Mtume S.A.W, akawakubalia na kuupitisha msimamo wao huo kisha akazungumza nao kuhusu kiini cha jambo hili.
Na katika hadithi ya Bukhariy kutoka kwa Al Meswar: "Hakika watu waliopewa vyeo na Omar walikusanyika, kisha wakashauriana, na Abdulrahman akawaambia: mimi si mtu anayeshindana nanyi katika jambo hili, lakini iwapo mtataka basi mimi nitakuchagulieni miongoni mwenu. Wakatoa nafasi hiyo ya kuchaguliwa Abdulrahman, na Abdulrahmani alipopewa madaraka ya kuwa kiongozi wao, basi watu wote wakamili kwake mpaka ikawa sioni mtu yoyote anayewafuata wale watu waliopewa vyeo na Omar isipokuwa wanamfuata Abdulrahmani, na watu wote wakamili kwa Abdulrahman wakishauriana naye kwa siku hizo mpaka ilipofika ile siku tulioikusudia, na tukamuunga mkono Othman."

Basi kauli yake: "Basi watu wote walimili kwake mpaka ikawa sioni mtu yoyote anayewafuata wale watu waliopewa vyeo na Omar bila ya kumfuata Abdulrahman," ni dalili ya kuwepo mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, unaodihiri kwa viongozi hao sita. Kisha watu wakagawanyika miongoni mwao, na kila kundi likawa linafuata mmoja kati ya viongozi sita, na kufuata athari yake, au kwa kuwasikiliza kwa namna ambayo inazalisha uamuzi wa kupiga kura baada ya utambuzi na umakini.

-Na katika Sahihi mbili, katika kisa cha Sulhu Al Hudaibia: "Omar Bin Al Khattaab R.A. amesema: nimemwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W nikasema: Je wewe si Mtume wa Kweli wa Mwenyezi Mungu? Akasema: ndiye. Nikasema: Je sisi hatuko katika Haki, na adui yetu yuko katika batili? Akasema ndio: kwa nini basi sisi tunapewa kilicho duni katika Dini yetu? Mtume akasema: Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na mimi si mwenye kumuasi na yeye ndiye mwenye kuninusuru. Nikasema: Je wewe hukutuambia kuwa tungeliiendea nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kuitufu? Akasema ndio. Je mimi nilikwambia kuwa tutaijia nyumba hii mwaka huu? Nikasema: hapana. Akasema: hakika utaijia nyumba hii na kuitufu. Akasema: nikamjia Abu Bakari na nikamuuliza: Ewe Abu Bakar: hivi huyu si Mtume wa Kweli wa Mwenyezi Mungu? Akasema: ndio. Kisha mimi nikasema: Je sisi si ndio wenye haki na adui yetu yuko katika batili? Akasema ndio. Akasema kwa nini basi tunapewa kilicho duni katika Dini yetu? Akasema: Ewe mwanaume! Hakika yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W na hamwasi Mola wake, na Yeye anamnusuru, basi shikana na mafunzo yake, basi Walahi! yeye yuko juu ya haki, nikasema: hakuwa anatuzungumzia kwamba sisi tutaijia Nyumba Tukufu na twaitufu? akasema: ndiye, lakini je alikuambia utaitufu mwaka huu? Nikasema: Hapana, basi akasema: basi utaijia na tutaitufu ".

Basi msimamo wa Omar R.A na Mtume S.A.W siku ya Al Hudaibia, inaonesha wazi kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, kwa kushauriana na mwenye madaraka kisha wa chini yake, lakini bila ya kwenda kinyume na mtawala, kwa hivyo basi, mfumo wa vyama vingi vya kisiasa unahitajika kupitia baraza la mashauriano (bunge), au kinachofanana na bunge na kuchukua nafasi ya bunge.

- Na katika kitabu cha Bukhariy, katika kisa cha kuuliwa Omar: "Basi Abdulrahmaan akawasalisha waislamu Sala hafifu basi walipoondoka akasema: Ewe Ibn Abbas! Tazama nani aliyenipiga? Akazunguka kwa muda wa saa nzima kisha akaja na kusema: Kijana wa Mughiira! Akasema: fundi? Akasema: Ndio. Mwenyezi Mungu amuangamize, nimearisha kumfanyia wema, Ninamshukuru Mwenyezi Mungu ambaye hakujaalia kifo changu kuwa katika mikono ya mtu anayejidai kuwa ni mwislamu, wewe na baba yako mlikuwa mkipendelea watu wenye nguvu wawe wengi Madina – na Abbas ndiye aliyekuwa na watumwa wengi kuliko yoyote miongoni mwao.

Na katika kitabu cha [Sharh Al Hadeeth] cha Ibn Hajar: "Kauli yake: Wewe na baba yako mlikuwa mkipendelea kuongezeka kwa wanaume wenye nguvu katika mji wa Madina". Na katika riwaya ya Saad kutoka kwa Muhammad Bin Sereen kutoka kwa Ibn Abbas: "Basi Omar akasema: Hii ni kazi ya watu wako, nilitaka mji usiingiliwe na mateka wengi wenye nguvu nanyi mkanishinda." Omar akasema: Nani aliyenishambulia? Wakasema: Abu Lu'lu'a -na jina lake ni Fayruz- akasema: nimekukatazeni kwamba msilete Madina wanaume hao wenye nguvu lakini nyinyi mliniasi", na pia hayo katika riwaya ya Mubarak Bin Fadhalah, na Omar Bin Shaiba amepokea kwa njia ya Ibn Sereen amesema: Imenifikia kuwa Abbas alimwambia Omar aliposema: Msituingizie mateka isipokuwa wawe watumishi wadogo: hakika kazi za Madina ni ngumu na haziwezi kufanyika isipokuwa kwa vijana wenye nguvu" [Fateh Al Bariy 64/7].

Na huu ni mfano tu wa imamu kuyaangalia upya yale yanayozingatiwa kuwa yana masilahi, na pia imamu kuwakubalia iwapo rai yake itamili zaidi katika usahihi wa yale ambayo baadhi ya makundi yanayataka miongoni mwa uwekaji wa sheria kwa namna ambayo inaleta masilahi.

Na anayepiga kura anapaswa kumcha Mwenyezi Mungu katika kuchagua na achunge masilahi ya taifa kwa kiasi awezacho, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa!} [AZ ZUKHRUF 19]. Na lazima ajue kwamba jambo hilo ni nasaha, na katika Hadithi Tukufu kutoka kwa Tamim Adariy: "Mtume S.A.W. amesema: Dini ni Nasaha. Tukasema: kwa nani? Akasema: kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na viongozi wa waislamu na watu wote." [Imetolewa na Muslim].

Al Manawiy amesema: "Baadhi ya Kaamiliyna wamesema: mwelekezaji na mtoaji nasaha wanahitajia elimu nyingi kubwa, kwanza anahitajia elimu ya sheria, na hiyo ni elimu ya umma inayoambatana na hali za watu, elimu ya mahali, elimu ya wakati na elimu ya kutazama lililo bora zaidi. Na utakapokubaliana na mambo haya basi huwa yale yanayofaa kwa zama fulani huvuruga hali fulani au eneo fulani, na hivi ndivyo ilivyo, hutazamwa katika kuangalia lililo bora na kisha likafanywa kwa mujibu wa usahihi wake kwa imamu. Mfano wake: Muda ukiwa finyu kufanya mambo mawili yaliyosababishwa na hali, basi aashirie lililo muhimu zaidi, na iwapo hali ya mtu itajulikana kwa kukiuka kwake na kwamba anapoelekezwa kufanya jambo hufanya kinyume chake, humuashiria kwayo kwa namna ipasavyo ili afanye ipasavyo.

Na hiyo huitwa elimu ya siasa. Kwani hali ilivyo ni kuwa huongoza nafsi zenye kufuata matamanio na zilizopoteza mwelekeo wa masilahi yao, kwa hivyo wamesema: mwelekezaji na mtoaji nasaha, wanahitajika kuwa na elimu, akili, fikra sahihi, muono mzuri, hisia zilizotulizana na utaratibu wa kutenda, na kama hawatakuwa na sifa hizi basi kukosea ni haraka zaidi kuliko kupatia, na mtu wa namna hii hatakiwi kuelekeza wala kutoa nasaha. Wamesema : na hakuna katika maadili mema jambo lililo nyeti, lililofichika na tukufu mno kuliko nasaha. [Faidh Al Qadeer 268/6, Al Maktabah Al Tojaria Al Kubra, Misr].

Na kwa kuwa jambo hili linafikia katika Uimamu (Uongozi), na lina vidhibiti maalumu katika Fiqhi ya Kiislamu, basi ni vyema tuweke wazi vidhibiti hivyo maalumu ili tusije tukavivunja, na kisha baada ya hapo, tuvilingaanishe kati yake na mfumo wa vyama vingi vya kisiasa.

Na asili katika Uimamu ni wajibu, kwani zimo miongoni mwa kazi za sheria ambazo hazifanywi isipokuwa kwa nguvu,, kama Jihadi, Uadilifu, kurudisha udhalimu, na hizo zinahitaji Imamu aongoze watu ili kufanikisha hayo, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na pale Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa}[ BAQARAH 30], Al Qurtubiy amesema: "Aya hii ndio chanzo cha uwekaji wa Imamu na Khalifa anayesikilizwa na anatiiwa ili pawepo na tamko moja na kutekelezwa kwayo Hukumu za Khalifa."
Na hakuna hitilafu katika wajibu wa hayo baina ya Umma, au baina ya wanazuoni isipokuwa katika yale yaliyopokelewa na Al-Aswammu, kwani kwa hali ilivyo, yeye ni kiziwi wa Sheria, na pia kila mtu aliyesema kwa kuyatumia maneno ya Al-Aswammu, na akaifuata Rai na Madhehebu yake, (ambayo inasema Ukhalifa si wajibu), na dalili yetu ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi)}, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wa kabla yao}[AN NUUR 55], yaani anawajaalia makhalifa miongoni mwao.[Al Jamee' La'hkaam Al Quraani 264/1, Ch. Dar Al Kitaab Al Arabiy]

Na inatajwa katika Sunna; kutoka kwa Abdullahi Bin Amru, kuwa Mtume S.A.W amesema: "Si vizuri (halali) kwa watu watatu walio katika ardhi ya jangwa isipokuwa watamteua mmoja awaongoze." Imepokelewa na Ahmad, na kutoka kwa Abi Said, kwamba Mtume S.A.W amesema: "Wanapotoka watu watatu kwa ajili ya safari basi wamteue mwenzao mmoja wa kuwaongoza". Imepokelewa na Abu Dawud na ana mfano wake kutoka kwa Abu Huraira.

Al Shaukaani amesema: "Na ndani yake kuna dalili ya kuwa inatakiwa kisheria kwa kila idadi inayoanzia watatu na kuendelea wamchague mmoja wao awe kiongozi wao, kwani katika kufanya hivyo ni njia ya kujiepusha na tofauti inayoweza kupelekea uharibifu, kwa hivyo, kwa kutokumtanguliza wa kuwaongoza, kila mtu hung’ang’ania msimamo wake na kufanya anavyotaka kwa mujibu wa matamanio yake na kusababisha wote waangamie, na kwa kumchagua mmoja awaongoze tofauti hupungua na watu huwa na kauli moja, na iwapo watu watatu watafanya hivi wakiwa popote ardhini wanasafiri basi ni bora zaidi kufanywa na watu wengi zaidi waiishio vijijini au katika miji mbali mbali na wanahitaji kuwazuia watu kudhulumiana na kuamua gomvi mbali mbali, kwa dalili ya aliyesema: Hakika ni wajibu kwa Waislamu kuwa na Maimamu, Watawala na Viongozi". [Naili Al Auttar 265/8, Ch. Al Halabiy]

Ibn Taymiya amesema: "Sura ya nane, uwajibu wa kufanya Uongozi, na inapasa kujua kwamba Uimamu wa watu ni miongoni mwa wajibu mkubwa wa dini, bali dini haiaimrishi isipokuwa kwayo, kwani masilahi ya wanadamu hayatimii isipokuwa kwa kukutana kwa ajili ya haja zao wenyewe kwa wenyewe, na wanapokutana lazima awepo kiongozi, hadi Mtume S.A.W amesema: "Wanapotoka watu watatu kwa ajili ya safari basi wamteue mmoja wa kuwaongoza." Abu Dawud ameipokea hadithi kutoka kwa Abi Said na Abi Hurairah, na imepokelewa na Imamu Ahmad katika Musnadi yake kutoka kwa Abdullahi Bin Amru, kwamba Mtume S.A.W amesema; "Si halali kwa watu watatu walio katika ardhi ya jangwa isipokuwa watamteua mmoja awaongoze." Basi Mtume S.A.W amewajibisha kuwa na kiongozi mmoja katika mkusanyiko wa wachache walio safarini, kama ni uzinduaji kwa aina nyingine zote za mikusanyiko, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amewajibisha kuamrishana mema na kukatazana mabaya, na haya hayawezi kufanyika isipokuwa kwa kuwepo nguvu na Uongozi.

Na vile vile mengine aliyoyawajibisha kama Jihadi, Uadilifu, Hija, Sala ya Ijumaa, sherehe za waislamu, kumnusuru mwenye kudhulumiwa, na kusimamisha mipaka ya Allah, haya yote hayafanyiki isipokuwa kwa kuwepo nguvu na Uongozi, na kwa ajili hii, imepokelewa kuwa (Sultani ni kivuli cha Mwenyezi Mungu ardhini). Na inasemwa: "Miaka sitini ya sultani jeuri ni bora kuliko usiku mmoja bila ya sultani". Na jaribio linabainisha hayo, kwa hiyo, Salaf kama Al Fodhail Bin Ayaadh na Ahmad Bin Hambal na wengineo walikuwa wakisema: "Kama sisi tungelikuwa tuna dua inayokubaliwa basi tungelimuombea Sultani".

Na Mtume S.A.W amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu anakuridhieni matatu: Mumwabudu na wala msimshirikishe na kitu chochote, na mshikamane katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyinyi nyote na wala msigawanyike, na muwape nasaha viongozi wenu wanaoifanya kazi ya Mwenyezi Mungu", Imepokelewa na Muslim. Na Mtume S.A.W amesema: "Mambo matatu moyo wa Muislamu hauyapuzii: Ikhlas kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kuwanasihi waliopewa madaraka, na kuwa pamoja na waislamu, kwani maombi yao huwazunguka sehemu zote." Imepokelewa na Ahlul Sunan, na katika sahihi kutoka kwake amesema: "Dini ni Nasaha, Dini ni Nasaha, Dini ni Nasaha,. Wakasema masahaba: ni kwa ajili ya nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na viongozi wa Waislamu na watu wote."

Kwa hivyo Uimamu ni sehemu ya Dini na njia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumtii yeye na Mtume wake kwa njia bora za kujisogeza kwake Mola. Na hali za watu huharibika kwa sababu ya uchu wa madaraka kwa ajili ya cheo na mali. [Al Siasa Al Share'ia, Uk. 129, Ch. Wizara ya Wakfu ya Saudia Arabia].

Na asili yake ni kuwa Imamu hutiiwa na watu wake, na haramu kumgeuka, dalili ya hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi} [AN NISAA 59]. Na kutoka Sunna, kauli ya Mtume S.A.W.: "Yoyote atakayetoka katika utiifu na akaenda tofauti na wenzake kisha akaiaga dunia, basi atakuwa amekufa kifo cha zama za Ujinga/kabla ya Uislamu." Ameitoa Muslim. Na kuna hadithi nyingi katika mlango huo. Imamu Bukhariy ametaja katika mlango wa kauli ya Mtume S.A.W: "Mtaona baada yangu mambo myachukiayo", na Abdullahi Bin Zaid akasema: Mtume S.A.W amesema: "Basi vumilieni hadi mtakapokutana nami katika hodhi (la Kauthar)".

Kisha akataja hadithi ya Ibn Masuud, Mtume S.A.W anasema: "Mtaona baada yangu watu kujipendelea na mambo myachukiayo, wakasema unatuamrisha nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Wapeni haki zao na mumuombe Mwenyezi Mungu haki zao!". Na hadithi ya Ibn Abbas: Mtume S.A.W anasema: "Yoyote atakayechukia kitu cha Amiri wake basi avumilie, kwani atakayemgeuka Sultani kwa hatua moja basi atakufa kifo cha Kijahili.".

Na hadithi ya Ubada: "Tulimuunga mkono Mtume S.A.W kwa kumsikiliza na kumtii kwa raha zetu na shida zetu, kwa uzito wetu na wepesi wetu, na kumpenda kuliko kujipenda, na tusigombane na watu katika madaraka yao isipokuwa kwa kuuona ukafiri wa waziwazi kwa dalili kutoka kwa Mwenyezi Mungu".

Na hadithi ya Usaid Bin Hudhairi: "Kuna mtu alikuja kwa Mtume S.A.W basi akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu umemtumia fulani, na wala hujanitumia mimi katika madaraka, akasema: hakika nyinyi mtaona baada yangu mimi watu kujipendelea, kwa hivyo kuweni wavumilivu hadi mtakapokutana nami".

Na katika maelezo ya hadithi hizo; Ibn Battaal amesema: Katika hadithi hizi kuna hoja ya kuacha kwenda kinyume na viongozi waovu, na kuwajibika kuwasikiliza na kuwatii, na wanazuoni wote wanakubaliana kuwa kiongozi mwenye mabavu lazima afuatwe, iwapo atasimamisha Sala za Ijumaa na Jihadi, na kwamba kumtii ni bora kuliko kwenda kinyume naye: kutokana na kuzuia umwagaji damu na kuleta utulivu wa watu wengi. Je huoni kauli ya Mtume S.A.W. kwa wenzake, "Mtaona baada yangu watu kujipendelea na mambo myachukiayo", Basi akaelezea kuwa watakuwa na viongozi watakaochukua haki kutoka kwao na wakajipa wenyewe haki hizo na kuwapa wale wasiostahiki kupewa na wala hawafanyi uadilifu ndani yake, na akawaamrisha kuwa wavumilivu kwa viongozi hao na kuwajibika na utiifu kwao kutokana na kuwa kwao viongozi waovu.

Na Ali Bin Maabad, kutoka kwa Ali Bin Abi Twalib amesema: Lazima pawepo kiongozi, awe mwema au mwovu. Akaambiwa: hapana budi kuwa na mwema, je vipi kuhusu mwovu? Akasema: sheria ya Mwenyezi Mungu itatekelezwa kwayo, na pakawekwa usalama wa njia, na ngawira igawiwe na jihadi ifanyike dhidi ya adui, je huoni kauli ya Mtume S.A.W katika hadithi ya Ibn Abbas: "Yoyote atakayemgeuka Sultani kwa hatua moja basi atakufa kifo cha Kijahili."

Na Katika Hadithi ya Ubada: "Tulimuunga mkono Mtume S.A.W kwa kumsikiliza na kumtii" mpaka kauli yake "Tusigombane na watu katika madaraka yao isipokuwa kwa kuuona ukafiri wa waziwazi kutoka Mwenyezi Mungu". Haya yote yanamaanisha kuacha kwenda kinyume na viongozi, na ili waislamu wasigawanyike na wala isisababishe umwagaji damu na uvunjaji wa heshima, isipokuwa kwa kukufuru imamu na kudhihirisha kwake kinyume na ulinganiaji wa kiislamu, basi hakuna utiifu kwa kiumbe yoyote juu ya hil, na hayo yalitangulia katika kitabu cha Jihadi na kitabu cha Al ahkaam. Na ni juu ya umma kuwa tiifu na kumnusuru kiongozi wake kama tu hajaamrisha maasi kwa matini zilizopita.

Na Abu Yaaliy amesema: Na imamu anapotekeleza haki za umma basi ni wajibu wa watu kumtii na kumnusuru, iwapo hakuna jambo lolote kwa upande wake linalopelekea kumtoa madarakani, na mambo yanayomtoa imamu madarakani ni mawili: kutokuwa kwake na uadilifu na upungufu wa uadilifu wake kwa namna inayohitajika kusihi uongozi wake. Na tumelizungumzia jambo hili kuwa kuna udhuru unaozuia kuuzingatia uadilifu wakati wa kuweka mkataba, kama ambavyo ulivyokuwa udhuru unaathiri kwa mbora. [Al Ahakaamu Al Sultania Li Abi Yaaliy, Uk. 28, Ch. Dar Al Kutub Al-ilmiya].

Na Al Mawardiy amesema: Na imamu anapotekeleza haki za umma tulizozitaja basi ametekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika haki zao na wajibu wao. Wajibu wao kwa imamu wao ni haki mbili: kumtii na kumnusuru iwapo tu hataibadilisha hali yake. [Al Ahakaamu Al Sultania Li Al Mawardiy, Uk. 19, Ch. Dar Al Kutub Al-ilmiya].

Na asili katika Uimamu ni kudumu, basi wala haijuzu kugombana na imamu, kwa kauli ya Mtume S.A.W "Tusigombane na watu wa madaraka”. Na wala kiongozi haondoshwi madarakani isipokuwa atakapokiuka masharti ya uongozi, na kama kuna uwezekano wa kutokea fitna kwa kuenguliwa imamu madarakani, basi haitajuzu kufanya hivyo; kwa kujulikana kuwa kutakuwa na fitna, shari na uharibifu ambao anaujua Mwenyezi Mungu pekee, kwa hivyo ni bora kutegemea uwepo wa madhara madogo kwa ajili ya kuondosha madhara makubwa. Na wala hatutarefusha jambo hili kwa kuwa liko nje ya maudhui yetu.

Lakini iwapo kutakuwepo muda maalumu katika katiba na ukamalizika basi uimamu utabatilika. Kwa hiyo basi, jambo hili linatazamwa, ikiwa kipengele hiki kilikuwepo kabla ya Imamu kuingia madarakani kwa kuungwa mkono kwa masharti yaliyowekwa, basi atalazimika kuyatekeleza masharti haya, na ushahidi wa hayo ni Hadithi: "Waislamu hutekeleza masharti yao"

Na ikiwa yeye ndiye aliyeweka baada ya kuingia madarakani basi kuyafanyia kazi si kumgeuka kwa sababu yeye ndiye aliyeweka na kuridhia, lakini hii inaingia katika kuwa kwake yeye ndiye aliyejiengua mwenyewe madarakani na kilicho sahihi ni kujuzu kwake, kwani Uimamu ni uwakilishi wa waislamu, na inajuzu kuuacha kwa kuomba hivyo na watoa maamuzi wakakubaliana na hilo. Na dalili ya hayo, ni kitendo cha Al Hassan Bin Ali R.A na wanachuoni kumnyamazia, bali kuna ishara kwa hayo katika hadithi, nayo ni hadithi: "Hakika mwanangu huyu ni bwana mkubwa, na Mwenyezi Mungu anayasuluhisha makundi mawili kupitia mtoto huyu." Ameipokea Bukhariy.

Ibn Aabidiyn amesema: "(Na tamko lake, Usultani wa mtu aliyelazimishwa unasihi) kwa maana kwamba mtu amechukua madaraka kwa nguvu na kwa uamuzi wa wengi bila ya kuwepo mfumo wa uungaji mkono wa wenye kupewa jukumu hilo na iwapo atatekeleza masharti yote na akaonesha kuwa asili ndani ya madaraka hayo ni kwa kupewa. Amesema katika Musaayarah: Uimamu unapatikana ima kwa khalifa kumpa mtu madaraka hayo, kama alivyofanya Abu Bakar R.A, au kuungwa mkono na kundi la wanachuoni au watu waliopewa jukumu la kutoa rai. Na kwa upande wa Ash-ariy: mmoja miongoni mwa wanachuoni wajulikanao anatosha miongoni mwa waliopewa jukumu la kutoa rai, kwa sharti la kuwa kwake katika muonekano kwa waonao kwa ajili ya kuzuia upingaji kama utajitokeza. Na Muutazila wameweka masharti matano.

Na baadhi ya wanachuoni wa Hanafiy wakataja sharti la kuunga mkono kundi la watu bila ya idadi maalumu, na tamko lake aliposema (kwa dharura) ni kwa ajili ya kuondosha fitna, na kwa tamko la Mtume S.A.W "Sikilizeni na mtii hata kama kiongozi wenu atakuwa ni mtumwa wa kihabeshi aliyekatika pua".

Na tamko lake aliposema, (na pia mtoto) kwa maana kuwa inajuzu kumpa madaraka ya Uongozi kwa ajili ya uwepo wa dharura inayopelekea kufanya hivyo, lakini kwa uwazi wa kiutendaji ni kuwa hakuna uhakika. Amesema mwandishi wa kitabu cha Ashbaah: kuwa ni wazi kuwa inasihi kumpa usultani mtoto mdogo. Akasema mwandishi wa [Al Ashbaah]: Usultani wake uwe sahili kidhahiri, akasema katika [Al Bazaziyah]: Sultani amefariki na raia wakakubaliana kuwa mtoto wake mdogo achukue madaraka yake basi madaraka hayo lazima yawe chini ya liwali (mtawala aliye chini ya mfalme), na mtawala huyo ajiandae kwa ajili ya kuwa mfuasi wa mtoto wa Sultani kwa heshima yake na usultani kwa kuwa yeye kiofisi ni mtoto wa Sultani, na mtawala huyo kiukweli yeye ni kiongozi wa muda tu kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kutoa idhini ya hukumu yeyote au kusalisha Sala ya Ijumaa, kwa kuwa yeye ni katika wasio kuwa na jukumu la kufanya hivyo.

Kama mtawala huyo wa muda aliye chini ya mfalme mtoto huyu sio Sultani, basi idhini yake ya kutoa hukumu na kusalisha Ijumaa haisihi, na mtoto ataitwa Sultani atakapofikia umri wa kubaleghe, ili isihitajike mtawala huyo wa muda kuondoshwa madarakani pindi mtoto wa marehemu mfalme anapochukua mamlaka baada ya kubaleghe.

Na Hamawiy akasema kuwa upangaji muda maalumu wa mtoto wa Mfalme kuchukua madaraka baada ya kubaleghe kwake hautokei isipokuwa pale mtawala wa muda atakapong’atuka madarakani yeye mwenyewe, kwani Sultani hajiuzulu isipokuwa kwa kutaka mwenyewe, na jambo hili halipo. Nimesema, pengine inasemwa: Hakika madaraka ya liwali huyo sio madaraka yasio na mipaka, bali yanafungamana na muda wa udogo wa mtoto wa sultani, akikuwa basi madaraka ya liwali huyo yataishia hapo kama tulivyosema hapo juu. [Rad Al Muhtaar Ala Al Durr Al Mukhtaar 368/1, Ch. Ihyaa Al Turaath]

Na Al Rohaibaniy amesema: (Na wala Imamu hawezi kung’atuka madarakani) kwa sababu ya (ufuska wake), kinyume na Kadhi, kutokana na kuwepo uharibifu ndani yake wala (haondoki madarakani) kwa kifo cha aliyemuunga mkono kwani yeye si mwakilishi wake bali anawawakilisha waislamu, na analazimika kuendelea na uimamu kwa kuteuliwa kwake kuwa hivyo. Kwa sababu waislamu wanalazimika kuwa na kiongozi ili haki za watu zisije zikapotea. Na Imamu ni mwakilishi wa waislamu na ana uwezo wa wazi wa kujiengua yeye mwenyewe kama walivyo wawakilishi wengine. Na watu wa maamuzi wana uwezo wa kumng’atua madarakani iwapo ataomba ang’atuliwe: Kwa maana ya kutengwa na madaraka na wala sio kutengwa na Uimamu kwa tamko lake Asidiik: “niondoeni madarakani nitoeni madarakani” wakasema: hatukutoi madarakani (laa sivyo) anaomba atolewe madarakani (hawatamtoa madarakani). [Mattalib Uli Enuha Fiy Sharh Ghaiyat Al Muntahiy 265/6, Ch. Bairuut]

Ama hukumu ya kuomba uimamu, basi ina maelezo mengi, basi chama kikiwa kinaomba madaraka katika uchaguzi wa urais, basi hiyo inaambatana na hukumu ya kuomba uimamu mkuu, na hiyo ni Faradhi Kifaya (kutosheleza), na kama hakuna isipokuwa mtu mmoja mwenye ujuzi basi analazimika kuomba madaraka, na umma unalazimika kumkubali na kumuunga mkono, na anawajibika kuukubali kama vile Faradhi Kifaya zingine, na kama kuna watu wangi wenye sifa, inajuzu kwa kila mtu miongoni mwao kuomba mamlaka, na umma utalazimika kumchagua mmoja wao, basi wote wakikataa kuchukua uimamu, wote watapata dhambi kama vile katika Faradhi Kifaya zingine, na haipendezi mtu yoyote kumtangulia mwenye ujuzi zaidi kuliko yeye, na ni haramu kuomba madaraka ikiwa mtu hafai na hana sifa.

Sheikh Zakariya Al Ansariy amesema: (Mlango wa Uimamu Mkuu) Uimamu Mkuu ni Faradhi Kifaya kama Ukadhi; kwani Umma lazima uwe na Imamu anayesimamisha Dini, anaeinusuru Sunna ya Mtume, anaewatendea haki waliodhulumiwa, anayetekeleza haki na kuziweka katika sehemu zake. Na iwapo hatafaa kwa hilo isipokuwa mmoja na wakawa hawakumuomba basi atalazimika yeye kuomba Uimamu ili aweze kuteuliwa, na atalazimshwa kuchukua uongozi ikiwa atakataa kukubali kwa hiari. Na ikiwa watu watafanikiwa kwa uongozi huo basi hukumu yake ni hukumu ya kama watu wangelifanikiwa kutokana na ukadhi, na itakuja hukumu yake katika mlango wake. [Asniy Al Mattalib Sharh Raudh Al Ttalib 108/4, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy].

Na akasema katika mlango wa Ukadhi: Na ikiwa mtu mmoja katika kundi la watu atafaa basi faradhi hiyo itakuwa imeanguka, lakini wote wakikataa kuchukua uongozi basi watapata dhambi kama ilivyo katika Faradhi Kifaya zingine. Kwa hivyo imamu amlazimishe mmoja wao kuchukua uimamu ili masilahi ya watu yasiharibike. [Asniy Al Mattalib 278/4].

Sasa linakuja swala la kuchagua mtu bora na mtu bora zaidi; kwani kila chama kitatoa mgombea wake, na pia watu watachagua na kuwapigia kura wagombea. Kama kila chama kitawasilisha mgombea wake wa urais, basi kinapaswa kumtanguliza mtu bora zaidi. Ama watu wa maamuzi wanalazimika kumchagua mbora wao. Kutoka kwa Ibn Abbas R.A amesema: Mtume S.A.W amesema "Na atakayemtumia mtu (Asieridhiwa na Mwenyezi Mungu) miongoni mwa watu wa kikundi fulani wakati katika kikundi hicho kuna mtu anayeridhiwa zaidi na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amemfanyia hiana Mwenyezi Mungu na amemfanyia hiana Mtume wa Mwenyezi Mungu na amewafanyia hiana waislamu", ameitoa na ameisahihisha Alhaakim katika kitabu cha [Al Mustadrak 7023]. Na kutoka kwa Yazidi Bin Abi Sufyaan amesema: Abu Bakar Swidiyq R.A aliniambia aliponituma Shaam: Ewe Yazidi hakika wewe una ndugu huwenda ukawaathiri kwa Uongozi na hilo ndilo jambo ambalo mimi nalihofia zaidi kwako, basi Mtume S.A.W amesema: "Mtu aliyepewa jukumu la kufanya kitu na waislamu kisha akawachagulia mtu kwa upendeleo basi ni juu yake laana ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hamkubalii chochote kutoka kwake, iwe ni kutoa sadaka au Uadilifu hadi atakapomwingiza katika moto wa Jahannamu." Ameisahihisha Alhaakem katika kitabu cha [Al Mustadrak 7024]

Lakini iwapo atachaguliwa mtu anayependwa, je uteuzi huo unakubalika? Jamhuri ya wanazuoni wanasema kuwa unakubalika, na wanautumia ushahidi wa tamko la Swidiyq siku ya Mkutano wa Sakiifah “Mimi nimekuridhieni mmoja kati ya watu wawili”. Naye Omar akaufanya Ushauri uwe katika watu sita.

Almawardiy amesema: Na iwapo wataalamu watakutana kwa ajili ya uchaguzi, basi watalazimika kuangalia vyema masharti ya hali za wenye uwezo wa Uimamu waliopo kwa wakati huo, kisha wanamtanguliza kwa kumuunga mkono yule mwenye kukamilisha masharti zaidi, na yule ambaye watu wataharakisha kumtii na wala hawatasita kumuunga mkono, na iwapo atateuliwa miongoni mwa watu wao yule ambaye amepatikana kwa jitihada zao basi watamuunga mkono, na uungaji mkono wao utakuwa sahihi kwa ajili ya Uimamu, na watu wote watalazimika kumuunga mkono imamu huyo na kumfuata kwa kumtii, na iwapo ataukataa Uimamu na kutoitikia wito hatalazimishwa kufanya hivyo, kwani Uimamu ni mkataba unaofanyika kwa ridhaa na kwa utashi usioingiliwa na ulazimishwaji wa aina yoyote ile, na atachaguliwa mwingine miongoni mwa wenye kustahiki kuwa kiongozi. Na ikiwa watu wawili watalingana uwezo kwa kutimiza masharti yote ya Uimamu basi atatangulizwa mwenye umri mkubwa zaidi kati yao hata kama ukubwa wa umri na ukamilifu wa kubaleghe si sharti la Uimamu, na iwapo mdogo kati yao ataungwa mkono awe imamu basi itajuzu.

Na kama mmoja kati ya wawili hao atakuwa na elimu zaidi, na mwingine akawa shujaa zaidi basi pataangaliwa na kuchungwa katika uchaguzi hali ya wakati huo ilivyo, kama haja itakuwa kupendelea shujaa zaidi na ndio jambo linalohitajika zaidi kutokana na kuenea majambazi basi shujaa atafaa zaidi, na iwapo itakuwepo haja ya kutanguliza elimu kwa sababu ya kuwepo watu wajinga na kudhihiri kwa wazushi basi mwenye elimu atakuwa ni bora zaidi kuliko shujaa. Na iwapo atachagualiwa mmoja kati ya wawili na wote wawili wakagombania uongozi huo, basi baadhi ya wanachuoni wamesema hakika ya ugomvi wa madaraka hauwi kizuizi chenye kuvuruga, na wala kuutaka uimamu si jambo lenye kuchukiza, kwani watu wa ushauri waligombana na hakuna yoyote kati yao aliyemrudi mwingine katika ushauri wala hakuna yoyote aliyezuia ushauri kwa utashi wake.
Na wanachuoni wamehitilafiana kuhusu ugomvi wa watu wawili wenye uwezo sawa, baadhi yao wakasema: Watapigiwa kura baina ya wote wawili na atatangulizwa mmoja wao kutokana na kura hiyo. Na wengine wakasema: watu wa busara watamchagua mmoja wao, na iwapo mmoja atachaguliwa, na baadae akatokea aliye mbora zaidi basi uungaji wao mkono utakuwa sahihi kwa yule wa kwanza na haitajuzu kumwengua kwa kumpa huyo aliye mbora zaidi ya aliyekwishachaguliwa.

Na kama watu walianza kumuunga mkono mtu anayependwa pamoja na kuwepo aliye bora zaidi basi jambo hili litaangaliwa vyema, na iwapo hatua hiyo imefanyika kwa kuwepo udhuru uliopelekea hivyo kama vile kutokuwapo au kuumwa kwa aliye bora zaidi au kwa kuwa yule anayependwa na watu ni mtiifu zaidi katika watu, na yu karibu katika nyoyo zao basi uungaji mkono wa anayependwa utakubalika, na Uimamu wake utakuwa sahihi, na iwapo ataungwa mkono bila ya udhuru wa aina yoyote basi wanachuoni wametofautiana katika uungaji mkono wake lakini Uimamu wake utakuwa sahihi. Baadhi ya jopo la wanachuoni akiwemo Aljaahidh wanaona kuwa uungaji wake mkono hautimii. Na wanachuoni wengi na wataalamu wa masuala ya Imani wamesema: Uongozi wake utajuzu na Uungaji mkono utasihi. Na kuwepo aliye bora si kizuizi cha uimamu wa aliyefadhilishwa na watu iwapo tu hajazembea masharti ya uimamu.

Na pia inajuzu kwa uongozi wa Ukadhi (Mahakama ya Kiislamu), kuiga kinachoonekana kuwa bora zaidi kuliko kilicho bora, kwani ongezeko lolote la Ufadhilishaji ni zidisho katika kuchagua na wala si lenye kuzingatiwa katika masharti ya kusaka haki, na lau alikuwa peke yake wakati fulani kwa masharti ya uimamu na hakumshirikisha katika hilo mtu mwingine yeyote uimamu utakuwa umetimia, na haitajuzu kuufanyia marekebisho yoyote kwa ajili ya mtu mwingine. [Al Ahkaam Al Sultania Li Al Mawardiy, Uk.8, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]

Ufupisho: Hakika Mfumo wa vyama vingi vya kisiasa unajuzu ndani ya Dola la Kiislamu, lakini kwa vidhibiti vilivyotajawa hapo juu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas