Mfumo wa Kielimu wa Kiislamu
Question
Je, Maulamaa wa Kiislamu waliweza kutoa mfumo ulio kamilika katika utafiti wa kielimu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1) Wanavyuoni Waarabu hawakuwa wakishughulika tu kunukuu elimu ya kiyunani ya zamani kama wataalamu wa mambo ya nchi za mashariki walivyojaribu kusema hayo, lakini waliitumia wakizidisha mambo mapya yenye umuhimu mkubwa sana, mpaka ikawa wana fikra wa Kiislamu wakifikia tatizo linalokuwa na umuhimu zaidi katika elimu ambalo linaambatana na asili yake nalo ni wazo la mfumo. Kwa kuwa, maendeleo ya utafiti wa kielimu yanahusiana zaidi na mfumo, ilhali utafiti wa kielimu unajengeka juu ya mfumo, na mfumo kama hautapatikana,basi utafiti wa kielimu utaharibika. Tena ni sharti la kusimamishwa elimu, iwe na njia iliyo kamilika ya kukusanya masuala madogo madogo ili kuyafasiri mahusiano yanayokuwa baina yao kufikia misingi ya kiujumla.
2) Hivyo, tunaweza kuiangalia misingi ya kiujumla ya mfumo wa kielimu wa Kiislamu katika Aya mbalimbali za Quraani Tukufu zilizotakaswa ambazo zinakuwa ni wigo unaotawala akili timamu ya Mwislamu pamoja na fikra, maadili na dhamira yake, miongoni mwa misingi ya KiQuraani ni kama ifuatayo: ufalme wote ni kwa Mwenyezi Mungu, Akhera ni bora kuliko maisha ya dunia, Mwenyezi Mungu Amevidhalilisha kwa ajili yenu vilivyomo ardhini, na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya, kutumia akili, kutafakari, kuzingatia, uyakinifu, elimu, unenaji na uongofu … na nyingi nyingine zaidi kutoka katika maadili ya kiQuraani yaliyotakaswa ambayo Mwislamu lazima aongozwe nayo, mfumo wa Waislamu wa kielimu uliathirika na Quraani Tukufu na misingi ya kiujumla na ambao unakuwa msingi wa mfumo wa kielimu wa Kiislamu, ni miongoni mwa misingi ya kisheria ya kiujumla ni:
a) Elimu na kutumia akili, Mwenyezi Mungu Amesema: {Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua} [AZ-ZUMAR, 9], naye Mwenyezi Mungu Amesema: {Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate nyoyo, (akili) za kufahamia, au masikio ya kusikilizia?} [AL-HAJJ, 46], kadhalika Quraani Tukufu iliwakaripia wale wasiotumia akili.
b) Uhuru, kwani uhuru na akili ni misingi miwili ichipuayo licha ya kuwa uhuru ni jambo la lazima kwa binadamu, Mwenyezi Mungu Amesema: {Na sema: huu ni ukweli uliotoka kwa Mola wenu, basi anayetaka naamini na anayetaka naakufuru} [AL KAHF, 29].
c) Suala la kutegemea hoja na dalili lazima liwe msingi wa kila dai na nadharia, Mwenyezi Mungu Amesema: {Na walisema: “Hataingia Peponi ila aliye Myahudi au Mkristo”. Hayo ni matamanio yao tu (si hukumu ya Mungu). Sema: “Leteni dalili zenu, kama nyinyi ni wasema kweli”} [AL BAQARAH, 111], kadhalika Amesema Mwenyezi Mungu: {Na anayemuabudu – pamoja na Mwenyezi Mungu – mungu mwingine, yeye hana dalili ya (jambo) hili; basi bila shaka hisabu yake iko kwa Mola wake. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi}[AL-MUMINUN, 117].
d) Kutegemea yakini na kutofuata dhana ni njia ya kuelekea maarifa, Mwenyezi Mungu Amesema: {Na wengi wao hawafuati ila dhana tu (sio ujuzi na maarifa). Na dhana haifai mbele ya haki hata kidogo. Hakika Mwenyezi Mungu anajua yote wanayoyatenda} [YUNUS, 36].
e) Kuelekeza kwa kutumia hoja za kiakili pamoja na hoja za kunukuliwa ili fitra (maadili ya asili) yashirikiane na fikra, kwa hiyo Quraani Tukufu ilitumia mbinu mbalimbali za kuwaelekeza watu wafahamu; balagha, utukufu wa umbo la Mwenyezi Mungu, umbile asili la watu katika kumwamini Muumba wao, pamoja na kuziangalia kanuni za kilimwengu na za kijamii, Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala hutapata mabadiliko katika kawaida (desturi) ya Mwenyezi Mungu (Aliyoiweka) wala hutakuta mageuko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu} [FATIR, 43], halikadhalika Quraani Tukufu ilitumia mfumo katika mjadala ambao ni lazima uwe msingi na kanuni katika uwanja wa fikra ya kifalsafa.
f) Mwito wa kushikamana na Uislamu kwa hekima na mawaidha mema, Mwenyezi Mungu Amesema: {Waite (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora}[AN NAHL, 125].
g) Kutambua hali halisi pamoja na kutumia akili, kuangalia na kuzitazama siri za ulimwengu na mambo ya ajabu ya viumbe na hayo ni mojawapo ya sifa za mfumo wa Kiislamu ambazo tunazikuta katika Quraani Tukufu k.v. maneno ya Mwenyezi Mungu: {Amemuumba mwanadamu kwa tone la manii. Tahamaki amekuwa mshindani dhahiri (wa kumkataa Mwenyezi Mungu) * Na (pia) Amewaumba wanyama. Katika hao mnapata (vifaa vitiavyo) joto na manufaa (mengine); na wengine mnawala * Na mnaona raha mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi * Na (wanyama hao pia) hubeba mizigo yenu kupeleka katika miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka na taabu. Hakika Mola wenu ni Mpole sana (na) Mwenye rehema nyingi * Na (Amewaumba) farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) mapambo. Na Ataumba (vipando vyengine) msivyovijua. (Nayo ndio haya mamotokari, meli, ….) * Na ni juu ya Mwenyezi Mungu (kuonesha) njia (iliyo sawa). Na zipo (nyingine zisizo sawa). (Basi nyinyi fuateni hiyo njia ya sawa Anayokuonesheni Mwenyezi Mungu). Na kama Angalipenda bila shaka Angalikuongozeni nyinyi nyote (mkitaka misitake. Lakini kakupeni uhuru wa kuchagua mtakalo) * Yeye ndiye Anayekuteremshieni maji kutoka mawinguni; kwa hayo mnapata kinywaji, na kwa hayo (inatoa) mimea ambayo humo mnalisha (wanyama) * (Na kwa hayo) hukuotesheeni mimea (ya kila namna) na mizeituni na mitende na mizabibu na kila matunda. Na bila shaka katika hayo imo ishara kwa watu wenye kufikiri (kuwa yuko Mwenyezi Mungu)} [AN NALH, 4: 11].
h) Kukataza jambo la kufuata kiupofu na kutojisalimisha kwa mawazo yasiyo na msingi, Mwenyezi Mungu Amesema: {Na katika watu wako wanaojadiliana juu ya Mwenyezi Mungu bila elimu wala uongozi wala Kitabu chenye nuru}[AL-HAJJ, 8], aidha Mwenyezi Mungu Amesema: {Na wengi wao hawafuati ila dhana tu (sio ujuzi na maarifa). Na dhana haifai mbele ya haki hata kidogo. Hakika Mwenyezi Mungu Anajua yote wanayoyatenda} [YUNUS, 36], na Aya nyingi nyingine zinazoamrisha uhuru, rai safi pamoja na kukataza kitendo cha kufuata dhana na mawazo yasiyo na msingi, na kujisalimisha kwa maarifa.
i) Kutolea maoni kwa uwazi hata yakiwa yanapinzana kama Quraani Tukufu ilivyotolea mifano mingi wakati wa kuzungumzia upinzani wa washirikina juu ya Utume wa Mtume Muhammad S.A.W.
j) Kumfanyia usawa mgomvi ambapo tunaweza kuona wazi kwamba Quraani Tukufu inasisitizia ulazima wa kisheria wa kumfanyia usawa mgomvi na ikiwa kushikamana na uadilifu ni maadili ya Kiislamu yenye hali ya juu, basi Quraani Tukufu ilisisitizia ulazima wake kwa upande wa mgomvi na katika wakati huo huo ilisisitizia uhuru wa mdahalo na uhuru wa kutoa maoni.
3) Hizo ni baadhi ya sifa za mfumo wa kielimu katika Quraani Tukufu unaozungumzia fitra ya mwanadamu, maumbile yake, hisia zake, uelewa wake, akili yake, nafsi yake ili kutambua hali halisi na utohoaji (uchomoaji) wa hakika, hivyo tunatambua kwamba Uislamu unajumuisha baina ya dini, maisha, elimu na kazi licha ya kuzingatia zaidi uhuru wa kifikra, haiba (utu) wa kibinadamu pamoja na kulazimisha kutumia akili, uhuru ulio kamilika katika kufahamisha, kutochelewesha mwelekeo wa kifikra au kuelekea dhana na mambo yasiyo na msingi. Kwa sifa hizo (za kutambua hali halisi, kutumia akili na kuwepo uhuru, jitihada na fikra) mfumo wa kielimu katika Quraani Tukufu unajengeka.
4) Maulamaa wa elimu ya misingi ya fiqhi - hasa Imamu Shafii - walikuwa na fadhila ya kuanzisha mfumo wa Kiislamu wanaosimamishwa juu ya kusoma kwa ufahamu, jaribio, utohoaji wa hukumu pamoja na kuuweka katika sehemu ya misingi na vidhibiti na kuweka katika nyanja za kielimu, kutokana na hali hiyo Ulaya katika zama za kati ilichukua elimu ambapo maendeleo yake ya kisasa yalijengeka.
5) Hali kadhalika tunaweza kutokana na kuzingatia utekelezaji wa Maulamaa wa Kiislamu kwa mfumo huo na yaliyotokea katika midahalo yao tufikie baadhi ya mambo mengine:
- Rai safi za kielimu zinalazimishwa kisheria zikiwa katika kutafuta elimu, kuelimisha au kuitumia katika midahalo.
- Inalazimishwa kusoma mambo yenye miono(mitizamo) kwa ufahamu kwa masuala yake tanzu na utohoaji unaohusiana na kusoma kwa ufahamu pamoja na kuhakikisha na kufanya bidii katika jitihada.
- Kuelekea mtazamo wa kuelimu na kujiepusha na kushikamana na rai binafsi.
- Kuepukana na dhana na mambo yasiyo na msingi ambayo hayana dalili.
- Kupata dalili kutokana na kinachokuwepo juu ya kisichokuwepo k.v. kupata dalili kutokana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu juu ya kuwepo kwake na uwezo wake s.w.t.
- Ulazima wa kuwepo kanuni za kilimwengu.
6) Kwa upande mwingine, mfumo wa Kiislamu uliathiri kwa uwazi katika wanafalsafa na wanafikra wa zama za maendeleo ya kiulaya, hasa Francis Bacon aliyejaribu kufuta athari za kielimu za Waarabu, ingawa hajaficha kuathirika kwake na Rogar Bacon ambaye alitangaza kufaidika kwa elimu za Kiarabu.
7) Umuhimu wa Francis Bacon haurudi tu umuhimu wa nadharia zake za kimantiki bali umuhimu ulio mkubwa zaidi unarejea vitendo vyake vilivyokuwa na athari zake juu ya akili ya kibinadamu kama ni mfano mpya ulio juu wa utamaduni.
8) Athari hizo zinaonekana wazi zaidi kwetu kwa kulinganisha mfumo wa Francis Bacon ulio maarufu na mfumo wa Kiislamu, na hapo tunaweza kutaja muhtasari wa mfumo wa Bacon alioutaja ustadhi Al A’kad katika nukta zifuatazo:
- Maarifa ya kibinadamu yana lengo moja nalo ni kuainisha maumbile na kuelekeza kanuni zake kuhudumia masilahi ya mtu na jamaa.
- Mtazamo wa kupima kwa kutumia njia ya Arosto unajengeka juu ya dhanio, na dhanio ni maneno, na maneno yanakuwa ni alama na dhana, basi dhana ikivurugika, msingi wa dhanio utavurugika.
- Mtindo wa Arosto unaweka msingi kwa kutegemea kipimo na haya ni mambo ya kiujumla, kisha unajaribu kuhakikisha ukweli wake kutokana na matukio ya kimaumbile na mtindo wa mwalimu wake Aflatun unafanya ulimwengu wa kuhisika ulimwengu unaofuata dhana.
- Kuifanyia mtihani hali halisi ni njia iliyo fupi zaidi kwa elimu sahihi na kufanya hisabu ya mambo yote yenye muonekano haiwezi kutokea kwa kufikia matokeo.
- Inalazimishwa kuachana na athari za masanamu ya itikadi za jadi: itikadi za kikabila (makindano ya akili ya kimaumbile) – masanamu ya pangoni (fikra za zama zilizotangulia) – masanamu ya soko (fikra zinazokuwa mikononi mwa watu wa kawaida) – masanamu ya ukumbini (masuala ya wanafalsafa na makosa yao).
9) Mshauri Al Gendiy aliona kwamba muhtasari uliotolewa na ustadhi Al A’kad kuhusu mfumo wa Bacon unakuwa ni msingi wa mfumo wa Kiislamu unaotofautiana na mfumo wa kimantiki wa kiyunani ya kiarosto.
10) Hilo ni jambo alilolisisitiza Rogar Bacon alikuwa akisema kwa uwazi: “ningalikuwa na uwezo, ningevichoma vitabu vyote vya Arosto, kwani kuvisoma kunapoteza muda na kunaleta makosa licha ya kueneza zaidi ujahili”,licha ya kutangaza kwamba: “falsafa inatokana na Kiarabu, kwa hiyo mlatini hataweza kufahamu Vitabu Vitakatifu na vitabu vya kifalsafa ila baada ya kujua na kusoma vitabu vilivyonukuliwa navyo”. Kwa hivyo, Brevolet alisisitiza kwamba Rogar Bacon au Francis Bacon walikuwa hawana fadhila katika kugundua na kuanzisha mfumo wa kimajaribio katika Ulaya akisema: “Rogar Bacon alikuwa anasoma Kiarabu na elimu za Kiarabu katika shule ya Oxford na walimu waliohama kutoka Al Andalus, hivyo Rogar Bacon au Francis Bacon walikuwa hawana fadhila katika kuanzisha mfumo wa kimajaribio kwani Rogar alikuwa tu mwanafunzi wa elimu na mfumo wa Waislamu waliohamia Ulaya ya Kikristo. Naye alitangaza mara nyingi kwamba jambo la kujifunza wenzake lugha ya Kiarabu pamoja na elimu za Waarabu ndiyo njia pekee ya kufikia maarifa sahihi”.
11) Kutokana na mtazamo uliotangulia wa mfumo wa kielimu wa Kiislamu, tunaweza kusema kwamba mfumo wa kusoma kwa ufahamu (kufuatilia mambo madogo madogo kufikia matokeo ya kiujumla) au mfumo wa kielimu, au mfumo wa kusikia na kuona, au mfumo wa kuangalia, ni mfumo wa Kiislamu ambao Uislamu uliufuata na Waislamu waliufuata kabla ya kuanzishwa ustaarabu wa Ulaya wa kisasa, ule ustaarabu ambao ulitegemea katika kuanzishwa kwake ustaarabu wa Kiislamu.
12) Elimu ilikuwa picha mojawapo za nguvu za Umma wa Kiislamu, kwani Uislamu uliipa elimu cheo pekee kuliko dini yoyote au utawala wowote, bali inawezekana kusema kwamba elimu kwa mujibu wa mtazamo wa Uislamu na sifa zake inakuwa na cheo cha juu zaidi kuliko mtazamo wowote katika historia ya ustaarabu wa kibinadamu; maana elimu ni sifa mojawapo miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu Akiwapa baadhi ya viumbe vyake, basi jambo hilo linakuwa kwa mujibu wa fadhila na ukarimu wa Mola kwa viumbe vyake, kwa hiyo elimu haiwezi kugongana na uwezo wa Mwenyezi Mungu au kupinzana na matakwa yake kama hali ilivyo katika baadhi ya staarabu k.v. ustaarabu wa kigiriki ambapo maarifa yanadhaniwa kuwa yalikuja kinyume na matakwa ya miungu. Halikadhalika, elimu katika Uislamu siyo kazi, bali ni utiifu unaofikisha hali ya kukurubia kwa Mwenyezi Mungu tena elimu siyo anasa wala sunna (kufanya ua kutokufanya),bali baadhi ya wakati elimu inaweza kufikia cheo cha faradhi inayolazimishwa anayeiacha anakuwa mwenye kufanya madhambi, kwa hiyo elimu katika Uislamu haihusishwi na tabaka maalumu, aidha haiwezi kuhusishwa katika nyanja za elimu za kidini tu, bali kila elimu zenye manufaa zikiwa za kidini au za kidunia zinakuwa ni aina za elimu zinazolazimishwa kujifunza.
13) Suala la kuizingatia elimu kwa sifa hizo lilielekea kuanzisha harakati ya kielimu inayoleta vitabu asili ambavyo vinastahiki kuchunguzwa na kusomwa.
Marejeo:
- Abdel Halim Al Gendiy (Mshauri): QURAANI TUKUFU NA MFUMO WA ELIMU WA KISASA, Cairo, Dar El Maarifa, 1984.
- Abdel Halim Hefniy (Dkt): MTINDO WA MAJADILIANO KATIKA QURAANI TUKUFU, Cairo, Al Haiya Al Masriya Al A’ama lil Kitab, 1995.
- Abdel Halim Hefniy (Dkt): KUMFANYIA INSAFU MGOMVI KATIKA QURAANI TUKUFU NA ATHARI ZAKE, Cairo, Al Haiya Al Masriya Al A’ama lil Kitab, 1997.
- Abdel Halim Mahmoud (Prof. Sheikh Al Azhar): MFUMO WA KIISLAMU WA KUIREKEBISHA JAMII, Cairo, Al Haiya Al Masriya Al A’ama lil Kitab, Mak-tabat Al Usra, 2003.
- Abdel Hamid Madkur (Prof.): FIKRA YA KIISLAMU YA KISASA, Cairo, Dar Al Haniy lil Tiba’a, 2003.
- Abdel Latif Muhammad Al Abd (Prof.): UCHUNGUZI KATIKA FIKRA YA KIISLAMU, Mak-tabat Al Anglu Al Masriya, 1977.
- Muhammad Al Anwar Al Sanhutiy (Prof.) & Abdel Al Hamid Madkur (Prof.): UCHUNGUZI KATIKA FALSAFA YA KIISLAMU, Cairo, Dar El Thaqafa Al Arabiya, 1990.