Urithi wa Kiislamu – nyenzo za kuuf...

Egypt's Dar Al-Ifta

Urithi wa Kiislamu – nyenzo za kuufahamu na kuushughulikia.

Question

Msomaji wa Urithi wa Kiislamu hukabili matatizo mengi katika kuufahamu na kuushughulikia, je, kuna nyenzo zinazousadia kutatua matatizo hayo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Mwanzo ni lazima lengo liwe wazi, nalo ni umiliki wa chombo muhimu kinachotakiwa kuelezea taratibu za kuushughulikia “Urithi ya Kiislamu”, au tujiongoze kwa njia hiyo, pamoja na haja ya kuendelea kupambanua kati ya vyanzo viwili vitukufu (Quraani na Sunna), na kati ya aina zingine za Urithi ambazo ni kazi za bidii za Waislamu kama elimu, fikra, fiqhi, fatwa, mitazamo, na ukweli wa kihistoria.

Hakuna shaka kwamba kuna pengo linaloonekana kati ya vizazi vya watafiti wa kisasa katika elimu za kibinadamu na kati ya kinachorithiwa chenye thamani, mara nyingi tunasoma Quraani au Sunna au elimu za Urithi wa Kiislamu lakini hatuelewi maana ya kinachosomwa, na hatuwezi kufaidika navyo.

Kitu cha kwanza kinachotakikana ni “ufahamu”, ambao ni hatua ya kwanza kuliko zote, siwezi kuuhakiki Urithi huu au kuutekeleza bila ya kuufahamu. Mimi –kama mtafiti au mwanafunzi nimeipitia elimu ya kibinadamu au baadhi ya matawi yake - nataka kufaidika na niliyoyaona au niliyoyahisi katika urithi kutoka katika mfumo na maudhui katika utafiti wangu kwa elimu hii .

Na kwa hiyo – baada ya kufikia “ufahamu” –mchakato mkubwa zaidi unahitaji, na ambao tunaweza kuuita mchakato wa “kutenganisha akili”, kisha unafuatiwa na mchakato wa tatu ambao ni “kufahamu vizuri”; yaani kufahamu mbinu, misingi, na vyombo ambavyo vinatuwezesha kuendelea na kumaliza jambo hilo. Hatukusudii kupitia elimu hizo fikra na mbinu zilizo ndani yake kuziiga, kisha mwenendo wa elimu unasimama na tunakwenda safari ya kifo bali inakusudiwa tudondoe tunayoyahitaji.

Mara nyingi watafiti wanajiuliza kuhusu matumizi ya urithi huo katika nyanja zao za sasa za kielimu na kiutafiti, na kuhusu “Uhusiano” kati ya urithi na elimu hizo za kisasa, wakati kinachotakiwa mwanzoni –kabla ya matumizi- ni “kuelewa”. Hakika kuainisha lengo, hatua na kuzitekeleza hatua hizo vizuri, kunahitajika sana kwa ajili ya ufahamu na kufaidika.. lakini mtafiti ameangalia mbele zaidi, kiasi ambacho anataka kuchuma matunda kabla ya kuiva - na labda kabla ya kupanda na kuota - ni jambo ambalo linampelekea mtafiti atake kunyakua na kukosa udhibiti.

Mwanzoni tunasema:
Hakika urithi –kwa ujumla- ni ibara ya vitu viwili: zao la kiakili na ukweli wa kihistoria. Zao la kiakili lina “nafasi” fikra inafanya kazi ndani yake, nalo ni Quraani na Sunna ambavyo ni misingi miwili mikuu ya maarifa kwa Waislamu kwa kuwa ni ufunuo. Na zao la kiakili lina “matunda” anayoyapata binadamu kama rai, fikra, elimu, mitaala, hukumu na matendo kutokana na kutendeana kwayo.

Mhimili wa ustaarabu wa Kiislamu unajengwa na maandiko: Quraani na Sunna. Nini maana ya mhimili ? Maana ya mhimili ni kwamba elimu zote zinautumikia mhiili huo. Na elimu hizo zimeasisiwa kwa ajili ya kuutumikia mhimili huo. Nao ni kigezo cha kuzinyoosha elimu hizo, na pia ni mfumo wa rejea.
Mwislamu amesoma matini, na kama hakuifahamu anatafuta njia za kuielewa, ndio maana pakawepo kamusi na kudhihiri sarufi na maumbo.. anajiuliza: Je, maneno hayo ni ya kawaida au ya ufupisho? Je, kipi kilichofanya yawe tofauti? Ikadhihiri elimu ya balagha.. akajiuliza: ukiwa umefahamu dalili za semantiki ya maneno (msamiati na miundo), sasa vipi kuhusu dalili na kinachotolewa dalili?

Vile vile ikadhihiri elimu ya kunukuu na kurejea, nayo ni elimu ambayo hao kabla haikuwepo kama elimu nyingine duniani; lengo lake ni kuthibitisha matini, na migawanyiko ya elimu ikaendelea kati ya elimu mbalimbali kama tafsiri, hadithi, na elimu za kimadhumuni kama tawhiidi na fiqhi na pia ugavi mwengine unatokana na akili ya mwislamu kutendeana na matini.

Fiqhi –kwa mfano- imetokana na Quraani kiujumla, na machache yake yametokana na Quraani kwa njia ya moja kwa moja. Kuna maswala ya kifiqhi takriban milioni moja na laki mbili, ilhali aya za Quraani ni chache kuliko maswala hayo katika idadi na ukubwa, lakini Quraani ndio chanzo, na kwake ndio marejeo na ni kunyooka kwa huduma kwa ajili ya elimu ya Fiqhi na elimu nyenginezo ambazo tumezirithi.

Sehemu ya pili ya urithi – mkabala wa zao la kiakili- nayo ni ukweli, unaoundwa na ulimwengu wa aina tano: ulimwengu wa vitu, ulimwengu wa watu, ulimwengu wa ishara, ulimwengu wa fikra na ulimwengu wa matukio .. Nini maana ya matini ambayo ni mhimili wa ustaarabu wenye mchango katika kushughulikia ukweli wa aina hizi za ulimwengu? Inamaanisha kwamba wakati ninapotendeana na ukweli niweke matini mbele ya macho yangu.

Katika elimu ya falaki -kwa mfano- ili kuelewa vizuri, nahitaji kufuatilia kwa muda mrefu. Wanavyuoni walikuwa wakifuatilia katika jadweli kubwa na nyingi, zote ni nambari na alama kama jadweli za lugha ambayo haieleweki kama walivyofanya wanaanga wa kisasa.. Lakini watu wa urithi wamenufaika nini katika hilo? Wakati tunapopitia kazi ya mababu zetu tunawakuta wametoa wanavyuoni wenye uelewa wa kina sana kwa nyakati za sala, upande wa Qibla, nyakati za kufunga na hija ... nk. Mwislamu wa zamani ambaye amebobea katika utaalamu wa falaki –pasipo na wasiwasi– anapenda fani hii, bila ya kujali dini, lakini yeye kama Mwislamu pia anageukia ujuzi wa elimu hizi kwa ajili ya dini yake na kuihudumia.

Katika ulimwengu wa vitu vizuri tunakuta mapambo ya Kiislamu yaliyovichora viumbe hai, yameanza kwa michoro ya uhandisi na mimea kisha hati, halafu haya yote yakachanganyika ili kuonyesha sanaa ya Kiislamu na falsafa maalumu ya kisanaa. Hivyo kuna maendeleo na ustaarabu wa uzalishaji. Mtafiti akitafakari anaona mambo matatu yanaendesha uzalishaji huu: kumjua Mwenyezi Mungu, kumwogopa Mwenyezi Mungu na kumpenda Mwenyezi Mungu. Haya yalionekana katika Quraani katika zama za uadilifu.

Lakini baada ya karne ya saba, imeonekana kwamba herufi zinazoandikiwa Quraani zilianza kuwa mbaya, dalili ya hayo ni kwamba kumjua Mwenyezi Mungu kulianza kudhoofika, na waandishi wakaanza kusahau sababu ya kuibuka kwa herufi hizo, na mwingiliano wao na Quraani ukapungua, tofauti na kile kilichotokea kwa waziri anayeitwa ibn Muqlah.

Mpaka karne ya saba, mapambo katika msahafu yalikuwa machache, na hii inatokana na hofu (au uangalifu).. lakini baada ya hapo mapambo hayo yaliongezeka, hii ikiwa ni dalili ya kupungua kwa hofu... Katika karne za hivi mwishoni hati na mapambo yalififia sana, jambo ambalo liliashiria kupotea kwa mapenzi yenyewe, na hata kama leo hii kitatokea kitabu ambacho ndani yake kuna masharti haya matatu, tutakikuta kuwa ni kutoka kwa mtu ambaye ni mchamungu aliyeishi ndani ya jambo hili. Na hii ni katika ulimwengu wa vitu, je inakuwaje katika ulimwengu wa fikra?

Katika ulimwengu wa fikra, ibn Muqlah aliyetajwa hapo juu, kwa mfano, alikuwa waziri alisoma Quraani tukufu na ikamwathiri, lakini yeye alikuwa ni msanii na mwanachuoni.. alikuwa na sifa tatu ambapo alikuwa msanii, ana mawazo mapana, na mwanachuoni wa hisabati, licha ya hivyo, alikuwa Mwislamu anaeipenda sana Quraani. Kutokana na ujuzi wake wa hisabati aliweza kutumia vizuri kile tunachokiita [uwiano wa kimantiki 22/7], wakati ambapo aliuita “uwiano wa kiungu”. Ibn Muqlah anaona kwamba Quraani iliteremshwa kwa uwiano mzuri wa kiungu katika mpangilio wake, kisomo chake na maana zake, kwa hiyo anahisi kwamba ni lazima pia iandikwe kwa herufi za uwiano mzuri wa kiungu ili fani na maudhui zikubaliane, na amegundua njia ya kuandika kupitia uwekezaji wa uwiano huo wa kiungu, na kupitia njia hiyo aligundua misingi ya hisabati iliyo sawa sawa ya kuandikia herufi za Quraani.

Ustadi huu ulikuwa kwa ajili ya kuhudumia matini .. na sasa tunataka kusimamia hali hii .. kutambua kwamba matini ilikuwa chanzo cha fasihi na elimu zote ..

Katika ulimwengu wa matukio: Kuna historia na vitendea kazi vya harakati zake. Nataka - ninapogusia historia ya Waislamu- nione katika Urithi, lini yametokea maendeleo na ukuaji? Lini imetokea hali ya kurudi nyuma na kushuka chini? Na kwa sababu gani? Hadi karne ya nne Waislamu walikuwa wakizalisha elimu, kisha mchango wao ukawa unapungua mpaka ukasimama katika karne ya saba, na ustaarabu pia ulianza kwenda chini, jambo ambalo tunaweza kulichukulia kuwa ni fikra ya ujenzi wa mataifa na staarabu (kama alivyoashiria Ibn Khaldun).. Fikra ya vitendea kazi vya kuporomoka kwa ustaarabu na kuhusishwa kwake na kutozalisha elimu.

Hivyo, urithi ni vyanzo vya asili au zao la kibinadamu, na ukweli ni ulimwengu wa aina tano, na tunachotaka kwanza ni ufahamu – ufahamu sahihi- siyo uhakiki, kwa ajili ya kufanya kazi katika nyanja ya elimu ya jamii na macho yetu juu ya urithi. Kuhusu kutaja “ufahamu sahihi”, pamoja na wito kwa ajili ya kutafakari na kuchemshabongo kuhusu masuala mbalimbali, tunaonya hapa kwamba kuna kiwango maalumu cha ufahamu sahihi, ambacho haipaswi kukikiukwa. Kuna mambo matano ni lazima kuyaelewa na kuwajibika nayo katika urithi:

(1) Lugha ya Kiarabu, ambayo ni kinga ya mantiki ya Kiarabu inayofungamana na maumbile ya Kiislamu.
(2) Makubaliano, ambayo haipaswi mwenye kutafuta ufahamu kuyakiuka au kuyapuuza.
(3) Malengo Makuu ya kisheria, ambayo ni kuyalinda yafuatayo: Dini, Nafsi, Heshima ya Mazazi, Akili na Mali.
(4) Kigezo cha utambuzi - ambacho tunakiita imani au mtazamo uliokamilika.
(5) Misingi ya kifiqhi au misingi mikuu ya sheria: kwa kuutumia msingi usemao: hakuna kudhuru wala kujidhuru, hakuna atakayebeba mzigo wa mwenziwe...nk.

Jambo hili ambalo liko mikono mwetu kuhusu utaratibu wa kuelewa Urithi ni hatua barabarani, lakini ni hatua muhimu na ya kimsingi ili tufahamu Urithi wetu, na kutekeleza mabadiliko ya dhana yanayotakiwa; na ili tuurejeshe utengemavu wa akili ya Kiislamu; na ili watu kama ibn Muqlah, ibn Al-Haytham, Al-Birwani, ibn Khaldun na wengine kama hawa waibuke katika jamii.

Tunasisitiza kwamba kilicho muhimu zaidi kwetu katika urithi huu ni "mifumo" na njia za kufikiri: namna gani wenzetu walizitumia akili zao katika uhalisia wao? Hatujali “maudhui” au maelezo ambayo walikuwa wakiyafikiria.

Kama mfano: wakati tunapogusia nadharia saba za misingi ya fiqhi, itakuwa wazi kwetu milango ambayo elimu ya Urithi inaweza kuiwasilisha kwa ajili ya kuhudumia elimu mpya za kijamii na kiutu. Ama elimu ya misingi ya fiqhi ina safari yake katika akili ya wataalamu wake.

Mtaalamu wa elimu ya misingi ya fiqhi anajiuliza: vipi nitaipata dini yangu? Basi akafikiri matatizo na maswali mbalimbali: hoja ni nini? Akajibu: ni Kitabu na Sunna. Kisha alijiuliza: ziko wapi? Yaani uthibitisho? Basi akaanzisha elimu ili kuhakikisha kwamba kilicho mikononi mwake ni kweli Kitabu na Sunna, kisha akajiuliza kwa ajili ya kurekebisha ufahamu: unakuaje ushahidi? Ili majibu yapatikane kuhusu ya kweli na ya uongo.. nk. Kisha akajiuliza ikiwa matukio ni mengi na matini ni chache, ni jambo la lazima “kupima”! Akajiuliza: namna gani kupima? Yaani namna gani mambo ya zamani yalivyoyawahi mambo ya sasa? Na inakuaje wakati wa ukinzani baina ya matini? Akasema kwa kufadhilisha, kisha akajiuliza: vipi utafadhilisha wakati wa ukinzani? kisha akajiuliza: Nani anafanya hivyo? Masharti ya mwenye kujitahidi ni yapi? (au “mtafiti” katika kujieleza kulikoenea katika elimu za kijamii za kisasa)?

Na kwa kuunda muundo mwengine wa mambo haya saba, nitakuta kwamba mimi nilikuwa nikiangalia vyanzo, mbinu za utafiti, zana zake, mifumo ya uthibitisho na hoja. Na katika masharti ya mtafiti .. mambo ambayo ameyachukua Roger Bacon na kuyafanya misingi ya mbinu ya elimu ya kisasa, mambo hayo hayazidi ufafanuzi wa Al-Razi na Al-Baydhawi katika elimu ya misingi ya kifiqhi.
Wakati tunapouliza elimu ya saikolojia ya kisasa kuhusu “vyanzo” mwana saikolojia? Marejeo gani wakati wa kuhukumu mambo au kuyafikiri? Namna gani tunathibitisha mambo hayo kupitia marejeo? Je, kuna mambo yanayobadilika na yasiyobadilika? Ni upeo gani wa kweli na wa dhana? Na namna gani tunaweza kuufikisha ukweli kwa matini? Hakika mwana saikolojia ambaye ni mwislamu leo - katika hali ya mgawanyiko huu kati ya matini na kweli- hawezi kutoa jibu. Anayeangalia hazina hii ya urithi -leo- anashtuka kwa mbinu kubwa na maswali ya kimsingi labda hayana majibu isipokuwa katika urithi huo.

Miongoni mwa nyenzo muhimu sana za kuuelewa Urithi ni:
1. Kigezo cha utambuzi cha Kiislamu, kufahamu na kujua vipengele vyake na tayari tumeshagusia katika zaidi ya maudhui moja.
2. Akili ya Urithi, na kuvifahamu vipengele vyake.
3. Chombo cha kuushughulika na elimu za Urithi kwa ajili ya kuanzisha “ufahamu” wa kina wa vipengele kadhaa, labda vipengele viwili vikuu ni muhimu zaidi kuliko vyote: cha kwanza- vipengele vya mtazamo wa ulimwengu wa nje pamoja na waandishi wa Urithi ya Kiislamu, na cha pili- chombo cha kilugha ambacho kwayo tunaweza kuzielewa matini za Urithi.
Tayari tumeshagusia kila nyenzo miongoni mwa nyenzo hizo katika maudhui maalum.
Hatimaye, hii ni safari fupi katika akili ya mtu kutoka zama ya kile tunachokiita Urithi: Je, nyenzo gani ambazo alikuwa akizifikiria? Na namna gani alikuwa akifikiri? Alikuwa akiona nini? Namna gani alikuwa akifahamu .. na namna gani hali hiyo ilikiathiri chombo cha lugha au iliathiriwa nacho?
Chanzo: Njia ya kuelewa Urithi, Mufti wa Misri, Profesa Ali Juma.

 

Share this:

Related Fatwas