Kundi la Wabahai
Question
Siku hizi kuna ongezeko la sauti za upotoshaji na kuibuka kwa makundi ambayo yalikuwa yakifichika hapo zamani, na miongoni mwa makundi haya ni Wabahai, basi maswali ya watu kuhusu kundi hili, itikadi na misingi yao yameongezeka, tukawauliza wanavyuoni wa Ofisi ya Fatwa ya Misri, kwa ajili ya kuuonesha ukweli wa kundi hili, kuonesha hukumu ya kulifuata, na hukumu ya wanaoongoka kwa itikadi zao, kwa ajili ya kuwatahadharisha, kutoa nasaha na taarifa kwao. Kwa hivyo, tunatarajia kutoka kwenu ufafanuzi mzuri wa jambo hili utakaotuondoshea utata.
Answer
Ubahai umetokana na “Baha’u llah” ambalo ni jina la Mirza Hussein Ali, ambaye ni kiongozi wa pili wa madhehebu ya wale waitwao Wabahai.
Asili ya kundi hilo ni mtu mmoja aitwaye Mirza Ali Mohammad ambaye jina lake ni “Al-Baab” katika karne ya kumi na tisa katika nchi za Uajemi, naye ni wa kwanza kuliunda kundi hilo, na kudai utume, na kwamba sheria yake inaifuta sheria ya Kiislamu.
Wanavyuoni wamekabiliana naye na kumjadili, na pia serikali ya Iran iliupinga wito wake wakati ule, basi alikamatwa katika mji wa Shiraz halafu katika mji wa Asfahan, na alinyongwa mwaka wa 1850 katika mji wa Tabriz, na mwili wake ukahamishiwa mji wa A’ka na kuzikwa huko.
Na kisha wafuasi wake wakaanza kukusanyika mjini Baghdad wakimzunguka Mirza Hussein Ali, aitwaye “Al-Bahaa”. Mtu huyu alikuwa mfuasi wa madhehebu ya Shia ya “Al-Baab” walinganiaji wa Dini yake hiyo, na baada ya baadhi ya matukio na fitna zilizosababishwa na Wabaha'i, serikali ya Utawala wa Othman, iliamua kuwaweka mbali na Iraq, kwa hivyo basi ikawahamisha kwa kuwapeleka mji wa Astana na kisha kuwahamishia katika mji wa Erdirn, na baadae kuwahamisha baadhi yao kwa kuwapeleka hadi kisiwa cha Syprus, Al-Bahaa na baadhi yaw engine wakapelekwa mji wa Akka huko Palestina, ambako kiongozi wao aliangamia mwaka 1892 AD, na akazikwa juu ya ardhi ya tambarare ya Mlima wa Al-Karmeli.
Baada yake mwanawe "Abbas Effendi," ambaye alifariki katika miaka ya ishirini ya karne iliyopita aliyeitwa "Abdul-Bahaa". Yeye aliilingania dini yao, akisambaza uongo, akiongeza uongo zaidi na makosa, kama alivyosema "Darwin" katika nadharia yake ya Asili ya Viumbe, na nadharia nyingine ambazo zilifanywa kwa ajili ya kuuridhisha ukoloni, kisha kundi hilo la Wabahai baadae likagawanyika na halikuwa na kiongozi yeyote wa wafuasi wake, lakini nyumba moja tu miongoni mwa nyumba zilizoasisiwa ndiyo ambayo ilikuwa ikiyapanga mambo yao. Na nyumba hizo zinaitwa vikao.
Na mwenye kuzingatia katika itikadi za Wabahai ataelewa kwamba ni madhehebu ya kubuni yasiyo na uhusiano wowote na Uislamu, limechanganya dini, na itikadi mbali mbali, kwa kudai kwamba ni za Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa itikadi zao ambazo ni batili na zilizoandikwa katika vitabu vyao na machapisho yao ni:
- Kiongozi wao amedai Utume, na kwamba sheria yake inaifuta sheria ya Kiislamu, na alizusha hukumu mpya tofauti na hukumu za Kiislamu, kama vile, kuifanya funga kuwa siku za kumi na tisa kuanzia kupambazuka hadi magharibi. Na iwe katika majira ya vuli. Kisha akaja baada yake Al-Bahaa akafanya sala ni rakaa tisa kila siku, na upande wa Kibla yao ni pahala alipokuwepo Al-Bahaa na kaburi lake.
- Kisha wakapotoka zaidi na Kiongozi wao “Al-Bahaa” akadai uungu, na kwamba Mwenyezi Mungu akageuka binadamu, na kwamba ukweli wa Mungu inabidi uuteua mwili wa binadamu yeyote, na unakubali kuhama kutoka mwili wa mtu na kwenda kwenye mwili wa mtu mwingine mpaka unafikia ukamilifu mkubwa katika muundo wa binadamu ambao ni miongoni mwa miundo mikubwa, ambapo kwa mujibu wa itikadi yao ni Mirza Hussein Ali, ambaye jina lake la kupewa ni “Al-Bahaa”.
- Wana itikadi kwamba unabii haujaisha bali unaendelea.
- Kupinga miujiza ya manabii na kuipa miujiza hiyo maana za kuchekesha.
- Itikadi yao ni ya zamani sana, kwa maana kwamba ulimwengu hauna msingi wa ratiba, nao uliotolewa na Mwenyezi Mungu kama walivyosema baadhi ya wapotofu wa zamani ambao wamebobea katika falsafa.
- Kunyima kufufua na kukana kuwepo kwa pepo na moto, na wanatafsiri Siku ya Kiyama kwa kuja kwa Al-Bahaa, na wanatafsiri pepo na moto ni kwamba haki ambayo inaashiria kuishi na kufa kiroho.
Na wana itikadi nyingi ambazo ni batili, Mwanachuoni Al-Alusi alisema alipofasiri aya hii: {Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye sema kweli, naye ndiye anaye ongoa Njia} [AL AHZAAB: 4]: “imeibuka katika enzi hii kundi la Washia waliojiita wenyewe Al-Babih na wenye akili wanahukumu kwa ukufuru wa itikadi yao”.
Inatosha hapa kuashiria makosa yao na kuwaonya watu juu ya uovu na madhambi yao, na pia juhudi zao kwa ajili ya kufanya ufisadi, na anayetaka kusoma maelezo zaidi arejee majibu ya wanavyuoni kwa kirefu ambayo yanaonesha ukafiri na upangaji wa njama zao dhidi ya Uislamu na Waislamu; Watu hawa walikawa chombo kizuri sana kwa Ukoloni na Uzayuni wa kimataifa, na miongoni mwa wale ambao wamewajibu ni mwanachuoni, mtaalamu wa tafsiri ya Al-Alusi, Sheikh Al-Islam Silim Al-Bishri, Imamu Muhammad Abduhu, mwanafunzi wake Rashid Ridha, Sheikh wa msikiti wa Azhar, Sheikh Mohammed Al-Khader Hussein, Mohamed Farid Wajdi, Kamati ya Fatwa ya Azhar, iliyoongozwa na Mufti wa zamani Sheikh Abdul Majid Silim, Sheikh wa Msikiti wa Azhar Sheikh Jaadu l-Haq, na wengine wengi.
Kanuni namba 263 ya mwaka wa 1960 ilipitishwa kwa ajili ya kupiga marufuku Ubahai katika nchi ya Misri na kukomesha vikao vyake na kutunga sheria za shughuli zao, na hukumu ya Mahakama ya utawala wa Baraza la Taifa ilitolewa kwaajili ya kubatilisha ndoa ya Wabahai na kuwazingatia kwamba wao ni wapotofu, na ilithibitisha uharamu wa kundi hili na ukiukaji wao wa utaratibu wa umma na usalama wa kijamii, na kwamba Katiba haiyalindi madhehebu yaliyozushwa na ambayo yanajaribu kukwea iliyaifikie hadi ngazi ya dini ya Mwenyezi Mungu, wakati ambapo kundi hili ni uzushi mtupu.
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu, imebainika wazi kwamba kundi la Wabahai ni miongoni mwa makundi ambayo yako mbali sana na Uislamu na ambayo inapaswa kuwatahadharisha watu wasiyafuate, na inabidi wahusika katika nchi watekeleze wajibu wao katika jambo hili.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.