Maadili kwa Mtazamo wa Wasomi wa Ki...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maadili kwa Mtazamo wa Wasomi wa Kiisilamu – Mtazamo wa Kihistoria

Question

Wasomi wa kiisilamu wameyapa maadili umuhumi gani?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Hakika maadili hayajaacha kuwa ni sehemu kubwa iliyowashughulisha waisilamu pamoja na kutofautiana kwao kwa elimu na fani zao, kwa dalili, kama asemavyo Profesa Abdul-Hamid Madkur, Profesa na mwalimu mkuu wa sehemu ya falsafa ya kiisilamu katika Chuo Kikuu cha Cairo, Dar Uluum, anasema; "Tunakuta umuhimu wake upo katika sehemu tofauti za utamaduni wa kiarabu na kiisilamu, na yapo katika vitabu vya fasihi, vya mashairi, na mifano ya wanafasihi, kama ilivyo katika wanahistoria na wapokezi wa habari ambao walikuwa wakizungumzia maadili pale inapobidi. Si hivyo tu bali hata katika vitabu vya kisufi ambao walilipa umuhimu mkubwa jambo hili, kwa mfano Harith Muhasibiy na Hakim Tirmidhi."

Na wasomi wa elimu ya sheria za kiisilamu (Fiqhi) wamelipa umuhimu sana suala hili la maadili, kiasia ambacho katika uandishi wa Fiqhi – kama asemavyo Ibn Rushd unahitaji matendo mazuri. Na mmoja kati ya wanazuoni wa Fiqhi naye ni Imam Malik aliweza kuweka sawa kadhia nyingi zenye utata katika masuala ya maadili kwa kutumia moja ya marejeo ambayo yameandikwa na wasomi wa Usul Fiqhi na marejeo hayo ni (Masilahi yaliyoruhusika)

Na kama ilivyokuwa katika vyanzo vya sheria za kifiqhi, ambavyo wasomi wa elimu hiyo wamezoea kutumia kama (Usijidhuru wala kudhuru), Haya ni maneno (msemo) maarufu katika sheria, na kinachokusudiwa ni kuchunga maadili katika kukabiliana na wengine. Ili isije kutokea madhara kwa wengine. Pia msemo huu unakwenda sambamba na msemo mwengine ambao ni (Mambo–yote-ni kwa kuyakusudia). Nayo inaambatana na hadithi kuhusu kuweka nia katika kila chanzo cha kitendo. Na pia kuna msemo (ubaya hauondoshwi kwa ubaya) (Madhara hayaondoshwi kwa madhara).Haya ni miongoni mwa waliyoyazungumzia, ikiwa pamoja na utafiti wa mambo yenye kuchukiza ambayo yanashikamana na mitazamo ya kimadili.

Na katika mifano ya kuwa wanazuoni wamelishughulikia sana suala la maadili ni kule kukubaliana kwao juu ya kuharamisha ujanja ambao baadhi ya watu huutumia kwa ajili ya kuukwepa ukweli wa kutenda ya faradhi za kisheria, ambayo yatapelekea (kama hayatotendwa) kuwepo na ufisadi na uharibifu.

Na katika yenye kuingia akilini, ni kule kushughulikia wanazuoni wa hadithi juu ya uandishi wa hadithi na vitendo, maneno, na sifa za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) kwani yeye ni kigezo cha juu kabisa, na ni mfano mzuri kwa kuwa ni msambazaji wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu {Hakika nyinyi mnayo kigezo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana} [AL AHZAAB 21].

Kwa ajili hii tunaona katika sehemu nyingi za maadili zimezungumziwa kwenye hadithi za (Rehma na amani ziwe juu yake). Kwa mfano katika anuani za vitabu; kitabu cha wema, adabu, utumwa, na vipo vitabu vingi vilivyoandikwa ambavyo vinazungumzia maadili, kwa mfano Kitabu cha imam Bukhari, na vitabu tofauti vya Imam Zuhd, na vitabu vya Abi Dunia katika kitabu chake cha Al Kharait. Na Abi Abdulrahman Asalamiy. Na Abi Bakr na wengineo wasomi wa hadithi ambao walijali sana upande wa maadili kupitia hadithi za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake). Pia hata katika vitabu vyenye kutegemewa (vilivyokusanya maudhui tofauti) kama maudhui za fasihi, siasa na historia, kwa mfano kitabu cha “Uyun Akhbaar” cha Ibn Qutaybah. Ambaye ameweka sehemu maalumu akauita [kitabu cha tabia na maadili mabaya].

Na msimamo huu wa upande wa maadili unawafikiana na yale waliyoyaweka wazi wanazuoni kwa kuzungumzia hadithi zenye kuhusu maadili, amabayo ni wajibu wa kila msomi kuwa nayo na kila alie na nafasi katika jamii, pasi na kujali tofauti zao za kielimu, nafasi zao katika jamii. Kwa mfano yale aliyoaandika Abu Bakr Al Agri kuhusu tabia za wasomi (wanazuoni). Na aliyoaandika Al mawirdi kuhusu nasaha kwa watawala. Na waliyoyaandika wengine kuhusu adabu za kadhi, na aliyoyaandika Al khatib Baghdad kuhusu mjuzi wa elimu ya fiqhi na mtafutaji wa elimu ya fiqhi na tabia za mpokezi wa hadithi na adabu kwa msikilizaji. Na aliyoaandika Imam Nawawi kuhusu adabu za kuibeba Kurani Tukufu, na adabu za Mufti, na mwenye kujua kuuliza maswali. Na aliyoyaandika Ibn Qutayba kuhusu abadu za Mwandishi. Pia yaliyoandikwa na Al qalqashandiy kuhusu maadili katika “Subhi A`shaa”. Na imam Abu Bakr Al raziy Failosofi, ameandika sehemu maalumu katika kitabu chake “Twib Ruuhi” na baadhi ya uandishi wake kuhusu maadili.

Tunaweza kusema kuwa mazungumzo kuhusu maadili ya wasomi ilikuwa ni wigo wenye kufuatwa kwa wanazuoni wa kiisilamu, ambao walikuwa wakitenga sehemu ya vitabu maalumu (uandishi maalumu) au chapa inayojitegemea katika vitabu vyao, na walikuwa wakifanya hivi kabla hata kuanza kuzungumzia masuala ya elimu na yanayohusu elimu. Kuzungumzia maadili ilikuwa ni miongoni mwa mambo ambayo yalipewa kipaumbele katika elimu ya kiisilamu ambayo ilianza kuenea katika nyanja nyengine tangu vitabu vilipoanzwa kuandikwa. Kisha ukaanza utunzi na ufasiri kutoka kiarabu kwenda katika lugha nyengine, na kwa upande wa waisilamu hawakuona tabu kuhamisha elimu hiyo kwa lugha nyengine ilivyokuwa hapakuwa na pingamizi yoyote ya kimaadili ya kidini.

Zaidi ya haya, tunaona kuwa mtazamo wa wasomi wa hadithi sawa Ahlu Sunna au Ash a`ri kuhusu maadili uko wazi na wengine mfano Muutazila. Na hata jamaa wa Sufi wa kiisilamu suala hili liko wazi kabisa, na wanafalsafa. Ingawa kwa hawa (wanafalsafa wa kiisilamu) yanazingatia zaidi falsafa ya Kigiriki kuhusu maadili. Na kuweka nyongeza katika baadhi ya mambo na kuzidisha matokeo ndani ya falsafa ya maadili ya Kigiriki. Kwa mfano Farabi katika kuleta utatuzi juu ya maadili anawafikiana na Aflaton kwa upande mmoja na mara nyengine anakubaliana na Arosto. Na wakati mwengine huwapinga wote katika mtazamo wa kisufi na kiuchaji Mungu na hili naliweka wazi kupitia mtazamo wake wa kimaadili.

Sufi (wafanya ibada) wa kiisilamu mtazamo wao pia uko wazi kuhusu maadili, na wemeonesha mfano mzuri kwa waisilamu, na tunaweza kuonesha mfano wa maadili kwa kuangalia, kielelezo cha sufi (kina maana gani). ((tabia, atakaekuzidi kitabia, basi amekuzidi kwa usafi)). Pia tunaweza kusema kuwa, wanasufi wanajali sana maadili na yanatawala katika nyanja zote za kisufi, na yapo wazi kila sehemu. Kwa ajili hiyo, ni wajibu kufanya juhudi za kuwa na maadili kwa kumuwezesha mtu aweze kuwa na tabia za kicha Mungu, zikiwemo, kujua yakini ya majina ya Mwenyezi Mungu ambayo inambidi aambatane nazo kwa mujibu wa kila jina. Hivyo, wakafanya wigo wa kumuiga Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) kuwa ndio upeo wao na ni kigezo cha hali ya juu kabisa kilicho kamilika.

Pia wanasufi wapo wazi kabisa kuhusu msimamo wao wa kimaadili katika maelezo yao hasa wanapozungumzia kuishinda nafsi ambayo ni kiini cha uhai wa kisufi, na msingi wa ujenzi wao. Na kuipinga nafsi ni kwenda kinyume na matamanio yake na kuendekeza matakwa yake, ili isije ikawa nafsi ndio kizuizi kati ya mja na Mola wake. Na hapana shaka kuwa, jitihada hizi za kuipinga nafsi zinahitaji maadili ya hali ya juu na ya ukweli, kwa sababu kinachotakikana ni kuitakasa nafsi kutokana na maafa ya kimaadili kisha kuihalalishia maadili mema. Na wanasufi wanaipa maelezo kauli hii kwa kusema. Kujikinga na kujihalalishia, wakikusudia; kujiking na maadili maovu na kujihalalishia maadili mema.

Kama walivyoweka wazi kabisa wanasufi msimamo wao kuhusu maadili wanapozungumzia Upeo wa tabia, wakikusudia, kuwa na tabia zote za kisufi. Na wanasufi wamezingatia sana umuhimu wa mtu kujifunza maadili ili aepukane na kila litalopelekea kuwa na tabia ovu ambazo zitamwingiza katika matatizo mengi. Na katika kujiweka kiuchaji (ucha Mungu) kutapelekea kuacha kuipenda dunia na kuing`ang`ania. Na kwa kutegemea wengine itapelekea kumtegemea Mwenyezi Mungu, na ukimtegemea Mwenyezi Mungu kutaondosha uvivu na dharau katika mambo ya kutii na kutakukinga na kuingia katika maasi mbalimbali. Namna hii ndio upeo wa tabia huwa ndio njia ya kusifika mtu kuwa na maadili mengi mazuri ambayo yanashikamana na tabia itakiwayo na sheria.

Iwapo yote tuliyoyatanguliza mpaka sasa yana uhusiano na nafsi pamoja na mwenyezi Mungu, basi hakika wanasufi wametoa kipaumbela yote yenye kuhusu maadili ambayo inapasa kwa kila jamii kuwa nayo. Kwani wanasufi maisha yao wameyajenga katika hali ya mfumo wa kimaadili yaliyo mazuri, mtu asifikaye kuwa sufi wa kweli huishi na moyo usiojua chuki wala makero, huwa na moyo safi ndani ya kifua chake kwa waislilamu wote. Hivyo huwa amejiweka mbali na shari zao, hawaingilii katika mambo yao ambayo wanahangaika nayo. Sufi wa kweli huwa hamuudhi mtu si hivyo tu bali pia huvumilia makero ya wengine, na husamehe pamoja na kuwa ana uwezo wa kulipiza kisasi, na huitawala nafsi yake, kwa ajili hiyo wanasufi huwa ni kama jumuiko la amani na makazi yenye utulivu ndani ya jamii. Wanasufi wametoa mfano bora wa kuleta athari ya upendo wa kweli na wa dhati. Kama walivyoonesha roho njema na hisia zilizo hai. Na kwa sababu hii Sufi wa kweli huishi maisha safi katika sehemu zote na kwenye nyanja zote.

Wanasufi kupitia maadili yao ya kiisilamu husifika kwa kuwa ni fadhila za kimatendo zenye mazingatio kama yale waliyoyaleta wanafalsafa. Si hivyo tu, bali ni maadili ya kimatendo ambayo yanawezwa kuigwa, hivyo basi, kupitia maelezo ya wanasufi kuhusu maadili ni kuwa, wao wanaamini kwamba tabia inaweza kubadilika na kuwa nayo zaidi, na kama haiwezekani basi huwa hakuna haja ya kufanya juhudi.

Wanasufi pia wamezingatia sana umuhimu wa kuwepo nia. Nia ni chanzo cha matendo na roho yake, na kuweka umuhimu wa nia huanza mwanzo wa tendo na hutakiwa kwa mtu awe na nia safi siku zote. Na wamesisitiza umuhimu wa nia kwa kuwa, kuna matendo ambayo huwezi kuyapambanua isipokuwa kwa nia. Na kama ilivyo nia hubadilisha tendo na kuwa ibada, na huisalimisha nafsi kuepukana na maafa ya kila siku, kwa ajili hiyo, tunaona pupa yao ya kuwepo kwa nia siku zote. Na kwa ajili hiyo ya kusisitiza uwepo wa nia kuna athari kubwa ya kuisafisha nafsi isifuate tu kiupofu. Na hakika kuna uchunguzi mwingi umefanywa kuhusu kuitakasa nafsi, ingawa njia walizopitia ni tofauti.

Wanasufi katika kuzungumzia suala la maadili wamegawanya upande ambao wanauita, upande mwema ulioshikamana na mazuri na kutaka kuyatendea na upande mbaya ulioshikamana na maovu na unaobidi kuyapinga. Ama kuhusu upande mwema inaonekana wazi kupitia maelezo yao kuwa inahitajika kushikamana na subira, shukurani, kuridhia, upendo na mifano yake. Na kwa kuzungumzia upande wa pili – upande mbaya – wamezungumzia aibu za nafsi na maradhi yake ambayo huwa ni kizuizi cha kufikia katika maadili yaliyokamilika, kwa mfano tabia ya husuda, kiburi, kujiona na kuhadaika.

Na kwa kuzingatia matendo wamejali sana upande wa mtazamo wa maadili ya kinadharia, kwa kuwa yametangulia na nadharia na mwenendo wa fikra, ndio wakaweka pamoja mtazamo wa kimatendo na kinadharia, na hivi ndivyo walivyoweka viongozi wa kisufi katika kuzungumzia nyanja za maadili, nayo ni matunda ya kielimu na kifikra, na ni uchaguzi wa vielelezo, asili, hatua na shuruti. Na yote haya, yanashikamana katika kufikisha lengo litakiwalo nalo ni la kuwepo kwa maadili. Pia, kwa upande wa nadharia kama walivyotafsiri kwa mujibu wa mtazamo wao na uwekaji wazi wa maarifa yao kuwa asili ya nadharia huwa haina kikomo maalumu, lakini inakusanya pia nadharia zote zilizopo kwa ujumla, na elimu zote. Na kwa upande wa elimu tunawaona kuwa wakizungumzia kuhusu njia zake, na mnmna yake, shuruti zake na mfungamano wake na elimu nyengine kwa namna ambayo zinalingana – kwa upande wa mbinu – na maneno ya wanafalsafa hata kama wametofautiana njia na kupishana katika matokeo na vyeo.

Na kwa upande huu maelezo yao kuhusu madili yanaonekana kuwa yamekuja kutokana na kuwepo kwa nadharia na uanzilishwi wa fikira. Kwa wanasufi wanafananisha kazi ya kiongozi au mwalimu kuwa kama kazi ya daktari, ambaye hafai kutibu mgonjwa bila ya kuwa na ujuzi, kisha awe na utambuzi wa ugonjwa na kujua mazingira, na sababu ya ugonjwa, muda wake na hali nyengine, pia kujua namna inayofaa ya kumtibia.

Hakuna shaka kuwa maadili ya wanasufi (wacha Mungu) ni nyanja kubwa sana yenye pande nyingi, historia kubwa na madhehebu mengi na wasomi, na ni tabu sana kuzungumzia pande zote hizi, na kwa tuliyoyasema si chochote ila ni kidogo tu kuhusu upande wa maadili kwa upande wao.

Mwisho, maadili kwa upande wa Wacha mungu yamesifiwa na baadhi ya watafiti kuwa yamemili katika tabia isiyo sawa. Lakini kwa kuangalia maelezo yaliyopita tutagundua kuwa, rai hii sio sahihi na haiwezekani kukubalika hata mara moja.

Kwa mtazamo huu tunaweza kuhakiki upande waliopita baadhi ya watafiti ambao hawapo katika mtazamo wa fikira za kiisilamu na hauna asili ya mahehebu ya kiisilamu. Na ukweli tunaweza kufasiri mtazamo huu kwa kusema kuwa umesimama katika fikira isiyo madhubuti kwa kutaama matokeo ya kiakili kwa mtazamo wa falsafa ya Kigiriki, ambayo hauzingatiwi kwa kuwa matokeo yake yamekwishadhihiri tokea mwanzo wa kuanza falsafa hii huko Ugiriki. Kwa kuzingatia hili itakuwa tunawatukuza Wagiriki na hii haina maana kuwa tunaidharau nafasi yao au kutojali cheo chao kwa kuwa wamejitahidi kuisimamia elimu ya maadili na falsafa. Isipokuwa tunachotaka ni kueleza kuwa isije ikadhaniwa kuwa kuendelea kwa mwanadamu kunatokana na fikira za Kigiriki pekee na hasa tukizingatia kuwa fikira hii haijazingatia kwa uwazi zaidi katika upande wa dini.

Marejeo Pro. Abdul Hamid Madkur. Somo katika maadili, Cairo, Dar Al hani. 1426H. 2005 A.D. (Ukurasa 127 – 178)

Share this:

Related Fatwas