Utafiti wa Kisayansi katika Ustaara...

Egypt's Dar Al-Ifta

Utafiti wa Kisayansi katika Ustaarabu wa Kisasa

Question

Ni zipi sifa za utafiti wa kisayansi katika ustaarabu wa kisasa?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Hakika utafiti wa kisayansi ni nguzo ya kwanza kwa kila ustaarabu, na huo ni msingi wa lazima kwa kila jengo, na kuna dalili nyingi zinazothibitisha hayo katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea, na haifai kuchanganya baina ya wingi wa idadi ya wataalamu na baina ya uhakika wa utafiti wa kisayansi. Baadhi ya nchi zina wasomi wenye shahada nyingi lakini nchi zao zina umasikini na kuchelewa. Kupata shahada ya elimu ni kitu, na ubunifu wa kisayansi ni kitu kingine. Hapa tutazungumzia mustkbali wa utafiti wa kisayansi katika ustaarabu wa kisasa..

Zifuatazo ni baadhi ya sifa anazopaswa kuwa nazo mtafiti wa kisayansi :
• Kuamini thamani ya elimu: imani ni utulivu, mtafiti hapaswi kuwa na shaka, bali analazimika kuamini thamani ya elimu, na mtaalamu si tu mfuatiliaji mwaminifu na shujaa mwenye kiwango cha utamaduni, bali ni mwenye imani kabla ya kitu chochote, kwani elimu ni jambo tukufu na haliwezi kuwa kama ni kazi tu.
• Kutoamini sadifu: sadifu inayokataliwa na elimu ya kweli ni ile inayooana na bahati, kitu hakiitwi cha ghafla isipokuwa kwa yule mwenye upungufu wa maarifa ya kitu hicho, na ghafla haifasiri kitu chochote, nacho ni kipimo cha ujinga kwa mambo ya dhahiri.
• Mshangao: elimu huzaliwa na mshangao na kupenda kudadisi, lakini mtu anatakiwa awe makini katika kutenganisha kati ya kupenda kudadisi kwa ubaya ambako hulenga kushibisha matamanio, na kati ya kupenda kudadisi kwa uzuri, ambako hulenga heri, haki na uzuri.
• Elimu ni jambo la kibinadamu: miongoni mwa sifa za maarifa ni kwamba hugusia jambo bila ya kupatwa na upungufu, bali maarifa huwenda yakawa na kila fursa za ukuaji kwa njia ya ushirikiano na uhakiki mbadala, na kwa ajili hii elimu ikawa ni jambo la kibinadamu.
• Wingi wa kukusanya matukio: huu ni mchakato wa kwanza mtaalamu analazimika kuuendea, akisukumwa na mapenzi ya udadisi wa kisayansi, na anapaswa kukusanya kiasi kikubwa cha idadi ya mitazamo na matukio kwa undani, kwa hivyo, elimu ni nguzo ya matukio. Na maabara za baiolojia na kemia zimeweka jadweli zilizosajili sifa za maumbile zinazojulikana ambazo misingi yake inaongezeka kwa kiwango kikubwa, ambapo hakuna anayejua upeo wake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
• Usafi na subra: hali inapasa kuchunguza katika mazingira ambayo yanatupilia mbalini kila uwezekano, na kuondoa kila aina ya shaka. Na hali asilia haina udanganyifu ndio ambayo lazima isifiwe kwa uaminifu kamili, kwani kitendo cha mtaalamu kupenda udadisi ni jibu la hisia za ndani. Kwa hivyo mtaalamu anapaswa awe na sifa ya unyenyekevu na usafi, ili afanye kazi ya ufuatiliaji wa matukio ya ulimwengu, na kuyaelezea kama yalivyo, na sio kama atakavyo yeye yawe. Ufuatiliaji wa kitaalamu unahitaji subra isiyokwisha na kujitolea bila ya mipaka.
• Ushujaa: elimu huchochewa na hisia kali zinazomfanya mtaalamu awe kiumbe kisichojua hofu kwa vyovyote vile, kwani ufuatiliaji wa kitaalamu unaweza kuwa na hatari nyingi, kwa mfano pale mtaalamu anapogundua nguvu za kimaumbile au kikemia au baiolojia isiyojulikana, lazima atarajie kutokea kwa hatari nyingi.
• Ukanusho wa dhati; mtaalamu wa kweli hatarajii thawabu isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani wadhifa wa mtaalamu unapelekea kukanusha ubinafsi, na kujizuia kutumia elimu kwa ajili ya kupata utajiri, kwa hiyo jamii za kisasa zimetenga kiwango kikubwa cha fedha katika bajeti za serikali ili kusaidia utafiti wa kisayansi.
• Uhakiki: uhakiki ni hukumu, na roho ya uhakiki ni roho ya hukumu sahihi, na hii ina maana kuwa mtu achukue msimamo wa kiakili wa hakimu ambaye yuko tayari kutoa hukumu, na hakimu anatakikana asipendelee upande wowote na aweke pembeni mielekeo yake binafsi, na angojee kwa uvumilivu hadi hoja zote zimdhirihikie, na hatimaye achague hoja imara.
• Mawazo: mara nyingi husemekana kuwa mtaalamu hapaswi kuwa mtu wa mawazo, na sifa hii ndio inayomtofautisha na msanii kwa mfano, bali mawazo yana athari katika kisichojulikana kitaalamu, ni makosa kuamini kuwa mtaalamu haongezi kitu katika kile anachokifuatilia, na mtaalamu hukisia kwamba nyuma ya mawasiliano ya nje ya maumbile kuna idadi kubwa isio na kikomo ya chembe chembe na mjengeko wake, ukweli ni kwamba nafasi ya elimu inayotokana na mawazo ni sawa na elimu ya ushairi, isipokuwa tu ni kuwa mawazo ya mtaalamu yanahitaji kujitolea, kama ambavyo inakataa kukitia makosani kitu kwa hisia, na uzuri ambao anavutiwa nao uzuri wa idadi na mahusiano ya kweli, na pia mawazo hutazamwa kama ni njia isiyo na mwisho, ama kwa upande wa lengo la mshairi yeye hujizingira katika kuyachemsha mawazo ya msomaji au msikilizaji bila ya kujali ukweli wenyewe, wakati ambapo uchangamfu wa kitaalamu mwisho wake huunyenyekea ukweli wenyewe, na matokeo ya mawazo ya kitaalamu huungana na uhalisia mwanzo na mwisho, si lazima kwa malengo ya kimsingi ya elimu kuwa yatengeneze uzuri, lakini lengo lake ni kuufikia ukweli kwa kiasi cha nishati ya mwanadamu.
• Utamaduni mpana: utamaduni ni mkusanyiko wa maarifa ya kitaalamu ambayo mtaalamu huyafanya kuwa maudhui ya utafiti wake, na wala si ujinga wa mtu kwa kila kitu ndio unaomwezesha kupambana na uhalisia kwa moyo mkunjufu bila kuelemea upande wowote, na miongoni mwa mambo yanayokubalika bila pingamizi yeyote ni kuwa moyo wa uhakiki ni sifa nyeti, na kwa hiyo, imekuwa ikihitajia daima kutiwa nguvu na kuungwa mkono kutokana na kujipatia elimu, na wanachuoni wanatambua fika upeo wa mkanganyo wa uhalisia, na hasa hasa katika elimu ambazo zinachukua maudhui zake kutoka kwa viumbe hai kwa ujumla na mwanadamu kwa sifa maalumu, na ni bora kwa mtaalamu wa elimu fulani kujikita katika elimu maalumu ambazo zinaendana na elimu yake.

Chanzo: Prof./Dkt. Abdullatif Al Abd, Diraasaatu Fil Fikri Al-islaamiy, Maktabat Al Anglo Al Masriyah, Kairo, 1977, Uk. (12-17)

Share this:

Related Fatwas