Kufanya Dhambi kwa Walii

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufanya Dhambi kwa Walii

Question

Je, walii anaruhusiwa kuzini?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Maana ya Walii katika lugha ni: ufuasi, na Walii piani: ukaribu, au kuketi karibu na. Imesemwa kwamba: Walii ni: kuwawa pili baada ya wa kwanza pasipo na kuondolewa. Na Walii ni: Mlinzi, Mwewnyezi Mungu anasema: {Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walioamini.} [AL BAQARAH: 257], na maana yake katika upande wa waja ni yule anayeendelea kutii pasipo na kufanya dhambi lolote. Na uwingi wake ni Mawalii.Na Walii ina maana ya mtendewa kwa upande wa mtiifu, Husemwa kuwa: Mwaminifu ni mtiifu wa Mwenyezi Mungu, yaani ni yule anayeendelea kumtii Mwenyezi Mungu. (Rejea: Al-Misbah Al-Munii, uk 672, kidahizo: WALII, Al-Maktaba Al-Ilmiyah, Al-Taarifaat kwa Al-Jirjani,uk 329, Dar Al-Kitab Al-Arabi.).
Walii: ni jina la mpenzi, mlinzi na rafiki. (1/1344 Al-Kamus Al-Muhit, Kidahizo: WALII, Muasasatul Resala.).
Walii katika istilahi ni:yule amjuaye Mwenyezi Mungu na sifa zake, atendaye matendo mema aepukaye madhambi, aachaye kushiriki katika raha na tamaa (Rejea: Al-TarifaatkwaAl-Jirjani uk. 329, Sharhu Al-Saad Al-Taftazani LellAqaaid Al-Nasfih uk. 92, Maktabat Al-kuliat Al-Azhariya).
Al-Shawkaani anaelezea maana ya Walii akisema katika tafsiri ya aya hii: {Jue ni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.} [YUNUS: 62]: “Walii katika lugha ni: mtu ambaye yu karibu. Maana ya mawalii wa Allah ni: wateule miongoni mwa waumini kwa maana ya wale walio karibu na Mwenyezi Mungu kwa kumtii na kwa kujiepusha na dhambi” (Fathu AlQadiir kwa Al-Shawkani 2/660, Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy).
Ibn Al-Qayim ameugawa uwalii kwa aina mbili: uwaliijumla, ambao huwa kwa waumini wote na uwalii maalumu ambao huwa ni ule unaokusudiwa watu wateule. anasema: Kwa upande wa uwaliiya teule ni ule wa kutekeleza na kuzitimiza haki zote za Mwenyezi Mungu, na kumpendelea kuliko kila kitu kingine katika hali zote, mpaka radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ndizo shughuli yake kuu, na huhusiana na mawazo yake, asubuhi na jioni. Kazi yake ni kuomba radhi za Mwenyezi Mungu hata kama watu hawaridhiki. (Badaa'i Al-fawaida kwa Ibn Al-Qayim 3/106, Dar Al-kitab Al-Arabiy).
Mwenyezi Mungu anasema kuhusu mawalii wake: {Jue ni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.* Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Mungu * Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.} [YUNUS: 62-64]. Na pia Mwenyezi Mungu anasema: {Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu.} [AL BAQARAH: 257]
Mtume S.A.W, anasemakama ilivyopokelewa na Al-Bukhari kutoka kwa Abu Hurayrah R.A, kwamba: “Mwenyezi Mungu anasema: yeyote anayemwudhi walii wangu basi nitampiga vita, mja wangu yeyote anayenikaribia zaidi mimi kwa utendaji wa ibada kama nilivyomlazimisha, mja wangu bado anaendelea kusogea kuwa karibu nami kwa suna za Mtume mpaka ninampenda, kama nikimpenda, nitakuwa masikio yake anayoyasikia kwayo, macho yake ambayo anayaona kwayo, mkono wake ambao anaukamatia, na mguu wake na ambao anautembelea”.Katika hadithi ya Hakim Al-Tirmidhi katika kitabu chake muhuri wa mawalii: “Anasikia nami, anaona nami, na anashikia nami,anatembea nami, kama ataniuliza nitamjibu, kama akiniomba kumlinda nitamlinda,sijasita kufanya kitu chochote kama ninavyosita kumkufisha mja wangu ambaye mwamini, anachukia kifo na ninachkiakumwudhia”, na Al-Tabaraaniy akaongeza: “ni lazima kwake”.
Sheikh Taqi Al-Din Ibn Taymiyyah amesema, kuhusu hadithi hii: “Hadithi hii ni sahihi zaidi kuliko zote kuhusu mawalii,Mtume SAW ameeleza kwamba: yeyote anayemwudhi walii wa Allah basi atampiga vita Allah, (Al-Farq Baina Awliyaa AR-Rahman na AwliyaaA-Shaitan kwa Ibn Taymiyyah uk. 50, Dar Al-Fadhilah) .
Imepokelewa na Al-Baghawi katika Sharhu Al-Sunna kutoka kwa Anas Ibn Malik kwamba kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW kutoka kwa Mwenyezi Mungu: “nalipiza kisasi kwa mawalii wangu kama anavyolipiza kisasi samba mwenye hasira”maana kwamba Mwenyezi Mungu hulipiza kisasi kama anavyolipiza kisasi samba mwenye hasira.
Abu Jaafar Al-Tabari alisema: “Walii wa Mwenyezi Mungu ni: yule ambaye ana sifa maalum kama alivyomweleza Mwenyezi Mungu, naye ambaye ameamini na amemcha Mwenyezi Mungu kama alivyosema: {Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Mungu} [YUNUS: 63]”. (Tafsiri ya El-Tabari 15/123, Muasasat AR-Resala).
Imamu Al-Fakhr AR-Razi alisema: “Imeonekana katika taaluma ya unyambuliko kwamba miundo ya herufi za Wa-li-i inaonyesha maana ya ukaribu, na ukaribu na Mwenyezi Mungu katika mahali na upande hauruhusiwi, lakini ukaribu naye utakuwa wakati moyo ulipozama katika mwanga wa ujuzi wa Mwenyezi Mungu, kama moyo ukiona, ukaona ishara za nguvu ya Mwenyezi Mungu, kama moyo ukisikia, ukasikia aya za Mwenyezi Mungu,kama moyo ukitamka, ukatamka kumsifu Mwenyezi Mungu, kama moyo ukienda, ukaenda katika utumishi wa Mwenyezi Mungu, kama moyo ukijitahidi, ukajitahidi katika utii wa Mwenyezi Mungu, wakati huu moyo utakuwa karibu sana na Mwenyezi Mungu, na mtu huyu atakuwa walii wa Mwenyezi Mungu, na kama hivyo ndivyo Mungu Mwenyezi atakuwa walii wakepia kama Mwenyezi Mungu alivyosema: {Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani} [AL BAQARAH: 257], na ni lazima iwe hivyo, kwa sababu ukaribu haukutokea isipokuwa kutoka pande zote mbili” (MafatifuAl-Ghaibu kwa AR-Razi 17 / 275, Dar Ihyaa Al-TurathAl-Arabi).
Walii amehifadhiwa lakini siyo hana makosa kama mtume, uhifadhi maana yake ni kutosisitiza juu ya dhambi, na kutokosea maana yake ni kuiba uwezo wa asiyekosea katika dhambi amablo anaweza kulifanya (Sharhu Al-Kawkab Al-Muniir kwa Ibn AN-Najaaruk.12-13, Al-Sunnah Al-Muhammadiya), Imamu Al-Qashayri anasema katika barua yake: “Miongoni mwa masharti ya Walii ni kwamba huhifadhiwa kama kwamba hali ya nabii awe asiyekosea” (AR-Risalatu Al-Qashayriah 2/416, Daru Al-Maarifa).
Akasema: “Je, walii huwa mtu asiyekosea? Ikasemewa: kwa uwajibu unaosemwa kwa mitume kuwa wanalindwa, hauwezekani kuwa kwa mawaliii. Lakini hali ya walii kulindwa na Mwenyezi Mungu mpaka akawa hang'ang'anii kufanya makosa, ikitokea makosa au kuponyoka au dosari zozote basi hayo yote hayazuiliki kwa jinsi walivyo. na Al-Junaid aliambiwa kuwa: Ewe baba wa Al-Kasim inawezekana mtu amjuaye Mwenyezi Mungu akazini? Akasubiri kidogo kisha akasema: {Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyo kwisha kadiriwa} [AL AHZAAB: 38]” (AR-Risalatu Al-Qashayriah2/416).
Al-Kalabadhi anasema: “Neema za Mwenyezi Mungu kuhusukutokosea kwa manabii na kuwahifadhi mawalii wake na fitna, ni nyingi sana na hazihesabiki, na uwezo wake hauwezekani kufungamanana kitendo kimoja au kingine” (Al-Taruf li-Madhab Ahlu Al-Tasawufuk. 130, Daru L-Kutub Al-Lmiyah).
Imamu Al-Shawkaani anasema: “Kutokosea ni kwa ajili ya manabii tu, na mtu mwingine yeyote anaweza kukosea. Omar R.A, pengine alikuwa na maoni fulani, basi baadhi ya masahaba wakaweza kumwambia maoni mengine, Omar R.A, akaweza kufuata maoni hayo na kuacha maoni yake”. (QatruAl-Walii Ala Hadiith Al-Walii uk. 428, Daru Al-Kutub Al-Hadiithah).
Kisha akasema kwamba yeyote anayesema kuwa mawalii hawafanyi makosa basi anakwenda kinyume na makubaliano ya wanavyuoni. akaendelea na kusema: “Hakuna shaka wala wasi wasi wowote kwamba yeyote aliyejaaliwa kuwa katika wale waja wema waliopewa neema za Mwenyezi Mungu ni wale wanaotekeleza sunna za Mtume S.A.W, kwa wingi, katika hadithi hii kutokana na upendo wao, na yale yaliyotokana nayo, kwamba eti wana kinga kama ya mitume, ni kosa linalokiuka makubaliano ya wanazuoni wa Kiislamu, kwani maana hasa ya kinga hiyo Mwenyezi Mungu ameiweka maalumu kwa mitume na malaika wake tu, na wala hajaijaalia kwa yoyote katika viumbe vyake, kwa hiyo hali hii ni ya Unabii tu na wala siyo ya uwalii, na hasemi kinyume na hivyo isipokuwa hajui au mpotofu. (Qatru Al-Walii Ala Hadiith Al-Walii uk.430).
Jambo hilo halina maana ya kuthubutu juu ya kutenda madhambi na haramu au kusisitiza juu ya madhambi madogo madogo, lakini hilo ni haramu katika Uislamu, uzinzipia ni miongoni mwa madhambi makubwa zaidi kuliko mengine na Mwenyezi Mungu anasema kuhusu madhambi hayo: {Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.} [AL ISRAAU: 32], na katika hadithi iliyomo katika sahihi mbili imepokelewa na Abu Hurayrah inasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW, alisema: “Jiepusheni na mambo saba yaangamizayo; masahaba wakasema: Ewe Mtume wa Allah, ni madhambi gani? Akasema: kumshirikisha Allaah, uchawi, kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza kuiua isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, kukimbia siku ya vita, nakuwatukana wanawake ambao ni waumini”.
Na imepokelewa kutoka kwaIbn Massoudalisema: nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW: Dhambi yoyote kubwa zaidi kuliko madhambi mengine? Alisema “kumshirikisha Mwenyezi Mungu naye ndiye aliyekuumba”, nikasema,halafu nini? Akasema: “kumwua mtoto wako kwa hofu kwamba huna cha kumlisha”, nikasema, halafu nini? Akasema: “kuzini na mke wa jirani yako”. Na imepokelewa Abdul Rahman, kutoka kwa baba yake alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, amesema: “Je, niwaambieni kuhusu dhambi kubwa zaidi kuliko madhambi mengine? Akasema hivi mara tatu. Tukasema: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: kumshirikisha Allah, uasi kwa wazazi wawili. Na alikuwa akiegemea, basi akaketi na kusema: Je kusema uwongo, kusema uwongo, akafanya hivyo mara kwa marampaka tukasema: laiti angelikaa kimya”.
Kwa mujibu wa yaliyotangulia inaonekana kwamba mawalii wa Mwenyezi Mungu wanalindwa na hawana kinga ya madhambi kama ile walionayo manabii. Walii anaweza kutenda dhambi yoyote miongoni mwa madhambi kama; vile uzinzi na mengineyo, bila ya kuhalalisha au kutenda dhambi hiyo kama walivyo waliomuasi Mwenyezi Mungu na mafisadi, na hiyo ni hekima ya Mwenyezi Mungu ambayo hawezi kuijua isipokuwa mtu aliyefundishwa na Mungu na kuruzukiwa uelewa wa maajabu ya Mwenyezi Mungu.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas