Kuingia Majini Mwilini mwa Mtu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuingia Majini Mwilini mwa Mtu

Question

Tunazisikia sana habari kuhusu majini, kwani majini ni nini? Na vipi kuhusu ulimwengu wake? Je, majini wanaweza kuingia mwilini mwa mtu na kumdhuru?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ulimwengu wa majini ni moja ya aina ya ulimwengu ambao uanazungukwa na uwezo wa Mungu, na kuamini kwake ni sehemu ya imani ya ghaibu.
Ibn Hajar amesema katika (Tuhfatul Muhtaj 7/279, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy.): “Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa upepo au moto yaani wao wameumbwa kwa mambo manne kama malaika kwa mujibu wa mtazamo mmoja. Imesemekana kwamba: Majini ni roho tupu na Imesemekana kwamba wao ni roho ya binadamu ambayo ni mbali na miili yao. Hata hivyo, majini wana akili na wanaweza kuonekana katika sura mbalimbali, pia wanaweza kufanya kazi nzito katika muda mfupi sana, na habari sahihi iliyopokelewa ni kwamba wao ni wa aina tatu: wale wenye mbawa kwa ajili ya kuruka kwazo, nyoka, na wengine wanakaa mara moja na wanasafiri mara nyingine”.
Na kuwepo kwa majini ni ukweli usiokatalika, na kuridhiwa kwake ni kuridhia kwa Quraani na Sunna na makubaliano ya masahaba, na kukataa kuwepo kwa majini baada ya kujua kwamba wao wanatajwa katika Quraani na Sunna basi kuna hatari kwa Waislamu, nayo inaweza kumtenga mtu yeyote na imani yake kabisa.
Imethibitishwa kwamba majini wapo katika Quraani na Sunna, na wanavyuoni wa umma wameafikiana kwamba ni lazima kuamini kwao, na akili haikatai hivyo. Majini wana majukumu kama wanadamu na wataulizwa juu ya matendo yao, kama watakavyoulizwa wanadamu, kama ilivyoelezwa katika Qur'an katika aya hizi: {Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii.} [Al-Anaam: 130], nakatika aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema: {Tutakuhisabuni enyi makundi mawili} [AR-RAHMAAN: 31].
Mwenyezi Mungu alisema katika Quraani kwamba majini wanasema: {Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.} [AL-JINN: 11].
Imethibitishwa katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim katika Sahihi yake kwamba Mtume, S.A.W alienda kwao na akazungumza nao, katika Sahihi ya Imam Muslim R.A, anasema: "Akanijia mwitaji wa majini, hivyo nilikwenda naye mimi nikasoma Quraani kwao", na katika hadithi hii wamemwuliza kuhusu vyakula vyao, akasema: "Mnaweza kula kila mfupa ambayo jina la Mwenyezi Mungu limetajwa juu yake, na mnaweza kutumia kinyesi kwa ajili ya kulisha wanyama wenu", kisha Mtume S.A.W, akawaambia masahaba wake kwamba: "Msitumie vitu hivi kwa ajili ya kujisafisha kwa sababu vitu hivi ni chakula cha ndugu zenu (miongoni mwa majini)".
Kama ilivyothibitishwa kwamba miongoni mwao ni wasioamini na wanaoamini, na miongoni mwao niwatiifu na wenye dhambi, kama ilivyoelezwa katika aya hii: {Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo.} [AL JINN: 11], basi akili haikatai kwamba majini wanaweza kuwadhuru wanadamu, na hakuna dalili yoyote ya kweli ambayo inazuia madhara hayo, lakini madhara huwa yanafanywa na majini. Na mifano ya madhara hayo; ni katika Hadithi iliyopokelewa na Bukhari na Muslim katika hadithi yao iliyopokelewa na Abu Hurayrah kwamba Mtume SAW amesema: "Shetani miongoni mwa majini amenijia jana kwa ajili ya kukata sala yangu, lakini Mwenyezi Mungu akaniwezesha kuepukana naye, nilitaka kumfunga katika mlingoti wa msikiti; mpaka niamke asubuhi na kumwangalia, lakini nilikumbuka maneno ya ndugu yangu Suleiman, “Ewe Mola wangu nipe mali haipaswi kuwa kwa mtu mwengine baada yangu mimi, Rauhu alisema: basi akamwacha". Imepokelewa vilevile na Al-Nasaai kwamba "Kutoka kwa Abu Huraira R.A., alikuwa akisimamia tende za sadaka, na akakuta athari za kiganja kana kwamba kuna aliyechukua katika tende hizi, akataja hivyo kwa Mtume S.A.W., akasema: Je, unataka kumchukua? Sema: Ametakasika aliyempa Utume Muhammad S.A.W., Abu Huraira akasema: nimesema, basi yeye alikuwa katika mikono yangu, nilimchukua ili niende naye kwa Mtume S.A.W., alisema, lakini nimemchukua kwa watu maskini miongoni mwa majini na sitarudi...", tunaona kwamba shetani amejigeuza katika sura ya mwizi alitaka kuiba katika sadaka ambayo ililindwa na mmoja wa masahaba, na wakati alipomwambia Mtume S.A.W. akamwambia kwamba yeye alikuwa ni shetani, na hii ni miongoni mwa aina za majini zenye madhara kwa mwanadamu. Na Mtume S.A.W. ametuhimiza tutaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula, wakati wa kuingia katika nyumba, na hata wakati wa kutaka kulala na mke, ili majini washirikiane nasi katika jambo hilo.
Si ajabu, basi, kuwa majini wawe na uwezo wa kumdhuru mwanadamu, kama anavyoweza mwanadamu kuwatumia majini na kuwadhuru wanapojigeuza na kuwa na sura za wanyama, na miongoni mwa mifano hii, ni Hadithi iliyopokelewa na Imam Muslim kwamba "Abu Al-Saibmtumwa wa Hisham ibn Zahrah alisema: niliingia nyumbani kwa Abi Sa'eed Al-Khudry, nikamkuta akisali, nikakaa kumsubiri mpaka amalize sala yake, nikasikia sauti ya kitu fulani katika matawi ya mtende, upande wa nyumbani, nikageuka na kuona nyoka, nikaruka kwa ajili ya kumwua, Abu Sa'eed Al-Khudry akaniashiria niketi, nikaketi, alipoondoka akaashiria nyumba ndani ya nyumba, akisema: Je, unaweza kuona nyumba hii, nikasema: Ndiyo, akasema kijana mmoja miongoni mwetu alikuwa bwana harusi mpya, akasema, tulikwenda nje pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kwa Al-Khandaq (shimo), kijana huyo alikuwa akiomba ruhusa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. nusu ya siku, akarejea kwa familia yake, siku moja akamwomba ruhusa, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akamwambia: Chukua silaha yako, nina hofu juu yakokutokana na watu wa Qurayza, kijana akachukua silaha yake kisha akarudi. Mkewe akiwa kati ya milango miwili amesimama, akaja haraka kwa mkuki kwa ajili ya kumpiga, na akasikia wivu, mkewe akamwambia: Acha mkuki wako na uingie katika nyumba ili uone nimetoka nje kwa nini?! Akaingia akaona nyoka mkubwa akikaa juu ya kitanda, kijana huyo akaenda kwake haraka akamwua kwa mkuki. Kisha akatoka katika nyumba, basi nyoka akamshambulia, basi haijulikai nani alikufa haraka sana kuliko mwengine kijana huyo au nyoka?! Akasema: tulikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., tukamwelezea hivyo, na kumwambia: umwombe Mwenyezi Mungu amfufue kijana huyo, akasema: mwombe msamaha kwa rafiki yenu, kisha akasema: katika Madina wapo majini wameongoka kwa Uislamu, kama mmewaona miongoni mwao yeyote muwape ruhusa ya siku tatu, na akionekana yeyote miongoni mwao baada ya hapo mwueni, kwa sababu yeye ni shetani tu".
Kwa Imam Ahmad "Imepokelewa na Yaala ibn Morrah, kwamba mwanamke alikuja kwa Mtume S.A.W., akiwa na mtoto wake ambaye alingiwa na majini mwilini mwake, Mtume S.A.W., akamwambia: Toka nje adui wa Mwenyezi Mungu, Mimi ni Mjumbe wa Allah, alisema, mtoto huyo akapona".
Kwa mujibu wa hadithi hii, tunasema kwamba majini wanaweza kuingia mwilini mwa binadamu, na wanasababisha ugonjwa unaojulikana kama kifafa; kwa sababu hakuna dalili sahihi inayozuia hili, na baadhi ya watu walipinga, wakisema, kwamba inakatazwa hivi, kwa sababu asili ya majini ni moto hawawezi kuhusiana na asili ya udongo ya wanadamu au kuingia kwao na kuishi pamoja nao, au watachomwa moto tu, lakini maneno hayo hayakubaliwi; kwa sababu asili ya kwanza ya majini na wanadamu baadhi ya sifa zake zilitolewa, kwa mujibu wa hadithi iliyopokelewa na Al-Nasaai na Ibn Hibbaan katika Sahihi yake "Imepokelewa na Abu Huraira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: shetani amenijia msikitini mwangu, nikaikamata shingo yake na kumkaba roho; mpaka nikahisi baridi ya ulimi wake juu ya kiganja changu, lau kama ndugu yangu Suleiman asingeliomba dua mngekuwa mnamwangalia shetani huyo akifungwa)), lau kama asili ya moto ingelikuwa inabaki; basi ingeukumba mkono wake Mtume mtukufu S.A.W., na nyumba, mahali na mavazi yangeliwaka moto wakati shetani alipovaana na mtu ambae hakutaja jina la Mwenyezi Mungu anapoingia nyumbani kwake au anapokula chakula.
Al-Fakhr Al-Razi katika kitabu cha (Al-Matalib Al-Aliya 7/317, Dar Al-Kitab Al-Arabi.) alisema: “Wale wanaosema kuhusu uthibitishaji wa kuwepo kwa majini na mashetani inawezekana wakazungumzia kuwa kuna njia mbili:
Njia ya kwanza: Ni isemekane kwamba majini ni miili ya upepo, na inaweza kugeuka katika sura mbalimbali na majina wanaweza kupita ndani ya matumbo ya wanyama.
- Imamu Al-Razi anasema-: "Na hakuna umbali wowote, kwani pumzi inayovutwa huwa inafika ndani ya viungo, basi iweje pawepo na umbali kwa viumbe walioumbwa kwa upepo?”.
Miongoni mwa dalili pia, Mwenyezi Mungu anasema: {Wale walao riba hawasimami ila kama anavyosimama aliyezugwa na Shet'ani kwa kumgusa.} [AL BAQARAH: 275]. Nakuzugwa ni: binadamu kukosa hisia ya kitu chochote anachotaka kukifanya au kukifikiri, na miongoni mwa dalili ni hadithi ya Mtume SAW, iliyopokelewa na Ibn Abbas –R.A., alisema Ataa: "Unataka kumwona mwanamke miongoni mwa watu wa peponi? Akasema: Ndiyo. Akasema: mwanamke mweusi huyu alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., akasema: nina ugonjwa wa kifafa na nikiwa uchi, basi nimwombee Mwenyezi Mungu, Mtume Akasema: Ukitaka usubiri na utaingia peponi, au ukitaka nimwombe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako akuponye, akasema, nitasubiri. akasema, ninakuwa uchi, nimwombee Mwenyezi Mungu sitakuwa uchi, Mtume akamwombee dua".
Ibn Taymiyyah, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: “ugonjwa wa kifafa; yaani: majini wanaingia mwilini mwa mwanadamu, inawezekana kwa ajili ya tamaa, shauku na upendo, kama anavyoafikiana mwanadamu pamoja na mwengine, au inawezekana kwa ajili ya kuchukua na kulipa, kama vile: baadhi ya binadamu wanaweza kuwadhuru majini au wanafikiri kwamba wao wanakusudia kuwadhuru majini, ama kwa kukojoa juu ya baadhi yao au kwa kumwaga maji ya moto au kuwaua baadhi yao, ingawa binadamu huyo hajui hivyo, na majini wana ujinga na udhalimu –basi wanaadhibu binadamu zaidi kuliko anayastahiki, na inawezekana kutokana na ubatili na uovu wa wanadamu wapumbavu.” (Majmuu Fataawa Ibn Taymiyyah 19/39-40, Majmaa Al-Malik Fahd).
Ibn Al-Qayyim anasema: “Kuhus ugonjwa wa kifafa ni aina mbili: kifafa cha majini wabaya, na kifafa cha michanganyiko mibaya, na ya pili ni aina ambayo madaktari wanayoizungumzia na sababu ya matibabu yake, na kuhusu kifafa cha majini, maimamu wote na watu wenye hekima wanakubali, na wanakiri kwamba matibabu yake yanakuwa kwa majini wema kuwapinga majini hawa wabaya, wao wanalipa madhara na wanapinga vitendo vyao na kuvibatilisha". [Zaad Al-Maad kwa Ibn Al-Qayyim 4/66-67, Muasastul Resala].
Imepokelewa na Ibn Majah katika Sunan yake kwamba "Osman Ibn Abi Al-Aas, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alinituma Taif. Nilipokuwa ninasali, niliona kitu Fulani hata sijui nilisali nini, na nilipoona kitu hicho nikaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., akasema: Wewe ni Ibn Al-Aas? Nikasema: Ndiyo, akasema: umekuja kwa nini? Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimeona kitu fulani katika sala yangu hata sijui nimesali nini. akasema, huyo ni shetani, njoo karibu hapa. Nikaja karibu yake, nikaketi juu ya miguu yangu, Mtume akapiga kifua changu kwa mkono wake, akatema mate katika kinywa changu na akasema: Toka nje adui wa Mwenyezi Mungu, alifanya hivyo mara tatu, kisha akasema: nenda zako, Othman akasema: majini hawakuja karibu nami tena".
Na kuzuia kuzugwa na majini ni kwa kuhifadhi sala na dua zilizomo katika Quraani na za manabii, na kutekeleza amri za kisheria. Na mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani kabla ya kuingia chooni, na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia mahali pa faragha na penye giza, na mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani wakati wa kulala na mkeo, na kutokojoa juu ya mashimo na ndani yake, na kutomdhuru mnyama yeyote katika nyumba bila ya onyo; kwa sababu majini wanaweza kujigeuza katika maumbile ya wanyama hawa, na kuwazuia wavulana kutoka kucheza na kwenda nje baada ya jua kuzama, na kisha usiku ukiingia wavulana wanaweza kutoka nje, kwa sababu katika sahihi (kwa hadithi ya Jaber Ibn Abdullah Al-Ansari amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., amesema: usiku unapoingia -au wakati wa jioni-, wazuieni watoto wenu kutoka nje, kwa sababu mashetani huenea wakati huu, ikipita saa moja tangu kuingia kwa usiku, basi waachieni watoke, fungeni milango na mlitaje jina la Mwenyezi Mungu, kwa sababu shetani hafungui mlango unaofungwa, na mfunike bakuli la maji, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu, na mfunike vyombo vyenu, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu, hata mkiweka juu yake kitu chochote cha kufunikia, na mzime taa zenu". Na inakatazwa kumwaga maji ya moto katika maeneo ambayo inadhaniwa kuwa ni ya majini; kwa sababu maji hayo yanaweza kuwadhuru majini hao, na jambo hilo linawafanya walipize kisasi.
Kutokana na hayo yaliyotangulia, majini wanaweza kumdhuru mwanadamu; kwa sababu hakuna dalili sahili inayozuia hili, kama ambavyo akili haikatazi jambo hilo kutokea. Lakini inapaswa kujua kwamba wengi wa wale tunaowaona miongoni mwa wanaoamini kuzugwa na majini, wao wanadhani tu kwamba wanapaswa kwenda kutibu magonjwa ya mwili au ya akili. Vile vile wengi wao tunaowaona miongoni mwa wale wanaodai kuwa wana uwezo wa kutibu kutokana na majini, wao ni miongoni mwa wenye madai na wasiokuwa na ujuzi na ni waganga ambao ni lazima wadhibiwe na viongozi, ili wasije wakawaharibia watu misingi ya kufikiri vyema, na kuzorotesha ujenzi wa akili ya kisayansi.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas