Maadili – kwa Mtazamo wa Kiislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Maadili – kwa Mtazamo wa Kiislamu

Question

Ni mambo gani ya maadili yanayozingatiwa kwa mtazamo wa Kiislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

1) Hapana shaka kwamba wasomi wengi na waandishi wa kiisilamu wanaogopa kuchukua hatua ya kutatua matatizo ya kisasa na kuleta ufumbuzi wa Kiislamu. Kama zisemavyo aya za Quraani na Hadithi za Mtume S.A.W. na makubaliano ya wasomi wa umma, na huenda sababu ikawa ni hofu ya wasomi hao kutuhumiwa kwa kutoendelea au kuwa na mawazo ya zamani au kutoweza kutumia zana za kisasa za kisayansi katika kuleta suluhisho la matatizo na matukio ya kisasa pindi waamuapo kutafuta utatuzi kupitia marejeo ya kiisilamu.

2) Mzozano wa kifikra kati ya miaka ya hamsini na sabini katika karne ya ishirini, umepelekea kutenganisha siasa na dini kwa ujumla, na kati ya sayansi na dini kwa kukusudia hasa. Na ni wajibu wetu kuelewa ufahamu wa wamagharibi na mifumo ya maisha ya ulaya kwa mtazamo wa kiisilamu. Bila shaka zitakuwepo wazi sababu muhimu za kutafautiana kati ya mifumo miwili nayo ni mifumo ya kibepari na kikomunisti pamoja na matawi yao na ule mfumo wa kiisilamu. Na hiyo ni kwa kuzingatia mambo ya kimaisha mfano, maadili, malezi, uchumi, sheria na saikolojia kwa mtazamo wa wamagharibi na kwa mtazamo wa kiisilamu wa kisasa. Hakika uchumi kwa mtazamo wa kiisilamu unatafautiana na ule wa kikomonisti na wa kibepari. Hivyo hivyo falsafa ya maadili ya kiisilamu inatafautiana katika miundo, njia na mwelekeo wake katika maisha na kwa jamii, ukilinganisha na falsafa ya maadili katika taasisi nyengine za kilimwengu. Pamoja na kuwa upo mlingano katika matawi au sehemu ndogo ndogo, isipokuwa katika muundo tafauti ni kubwa sana.

3) hivyo hivyo katika saikolojia, kuna tafauti kubwa kati ya mtazamo wa wasomi wa kisasa, na chuo cha wasomi waliojitenga, pamoja na saikolojia ya kiisilamu ambayo imeanza kuisoma nafsi kwa mtazamo wa kupitia Quraani, nayo (nafsi) inabeba ujumbe wa aina mbili; wema na uovu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu {Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake} [AShams, aya ya7- 8.]

4) Na pia kuna tofauti kati ya sheria za kiisilamu na kanuni za kutunga, pamoja na utaalamu wa viumbe, kwa kuwa (sheria za kiisilamu) zimethibiti katika asili yake, pamoja na kuwepo uwezekano wa wepesi na uwezekano wa kwenda sambamba na matukio ya maisha yote.

5) Kwa namna hiyo, tunaona tofauti ya wazi kabisa kati ya ufahamu wa maadili na tabia pamoja na utambuzi wa maisha kwa mtazamo wa kiisilamu na kwa mtazamo wa wa kimagharibi wa kisasa. Na wala haiwezekani kamwe kuwa yafaa kuchanganya kati ya mfumo wa kiisilamu na mfumo wa kimagharibi wa kisasa. Na pindi ikitokezea basi matatizo mengi tata kati ya ustaarabu wa kimagharibi na wa kiisilamu ambao unakusanya utashi wa roho na mwili kwa wakati mmoja katika kuleta uwiano, yatatokea.

6) Hali ya kutojielewa iliyowafika baadhi ya wasomi wa kiisilamu kuhusu elimu ngeni za tamaduni za kimagharibi, hii ni kwa ajili ya jaribio la kutaka kuondosha itikadi ya dini aliyo nayo muisilamu na kuweka mahala pake fikira za kimagharibi badala ya imani ya Mwenyezi Mungu. Na wanashikilia hawa ambao wamesoma katika nchi za magharibi, kutaka kuishi kwa akili zao, ama ndani ya nyoyo zao, wanataka kuishi kwa muonekano au kwa mwenendo wa kidini.

7) Hapana shaka kuwa matatizo ya maisha ya vijana waliosoma sio ya kijamii pekee, bali yamekuwa ni ya kijamii kwa ujumla, kiasi ambacho hakuna nyumba isipokuwa ina matatizo ambayo haiwezekani kuondokana nayo au kuyanyamazia. Na hapana budi iwapo tunataka kuyaondosha ni lazima tupitie mtazamo wa maadili ya kiisilamu katika kukuza tabia njema ndani ya jamii. Tabia ambazo chanzo chake ni kiigo chema. Ambapo hizo ni tabia njema zilizo muhimu na za msingi. Na kuachana na kiigo chema –kama wanavyojaribu wengi– kuwatelekeza wazazi, kwanza. Pili, kuitelekeza familia, na kisha, tatu, kueneza wito wa kuhalalisha tabia na maadili mabaya. Ama mazungumzo kuhusu kiigo chema yatahitaji muda wake maalumu.

8) Muongozo wa kiislamu ambao asili yake inapatikana katika Quraani na katika mwenendo wa Hadithi za Mtume S.A.W. ni muongozo bora ambao mwanadamu anaweza kuuchagua katika ulimwengu huu. {Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini} [AL MAIDAH 3]

9) Na vitu muhimu vyenye kupambanua uongofu wa kiisilamu ni utulivu wa nafsi ya mwislamu, kwani hatahitajika kuacha mwelekeo wa Mwenyezi Mungu na kuogopa vikwazo, kuwa na wasiwasi juu ya msongo wa mawazo, kukata tamaa juu ya matukio ya mpito, kwani hakika ya muumini wa kweli, humfanya Mwenyezi Mungu Mmoja, mwenye kukusudiwa kuwa ndiye tegemeo lake pekee, na anamuhisi ipasavyo na kuwa Yeye pekee ndiye atakaemsaidia, pia ndiye atakautia nguvu moyo wake. Mwenyezi Mungu anasema {Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.} [QAF 16].

Na ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamuacha pekeemja wake katika ulimwengu huu bila ya kumpa upendo wake, na kumuacha apotee bila ya kumuonesha njia, na kumuacha awe dhaifu bila ya kumpa nguvu, na atakapokosea basi atamwelewesha njia sahihi, na atakapoteleza atamuinua, na atakapoghafilika basi atamkumbusha. {6.Kwani hakukukuta yatima akakupa makazi? 7. Na akakukuta umepotea akakuongoa? 8. Akakukuta mhitaji akakutosheleza?} [ADHUHA 6-8].

10) Mipango, wito mkubwana majigambo ya uongo ya aina yoyote ayafanyayo kiumbe kwa wengine kuwa kwamba watapata furaha pindi wakiyafuata, ukweli wa majaribio umethibitisha kuwa jambo hilo halikufanikiwa, na haya ndio matatzio ye viumbe wa kizazi hiki. Kwani uongozi sahihi wanao, isipokuwa wanafanya jeuri ya makusudi ya kuuacha na kuendelea kuupuuzia, mwishowe wanajaribu kuigiza kwa kupitia akili zao na njia wazionazo zinafaa.

11) Huyo hapo kiumbe, kila siku hubadilisha ngozi yake na kila tukio jipya likitokea hubadilisha kauli yake, huleta sheria mpya na kuifuta ya zamani, hubomoa mawazo yaliyotangulia na kuweka mapya. Hakika ukamilifu wa imani ya uongofu ni ule wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambao haufanani katu na huu wa viumbe kwa namna yoyote ile, kwani uongofu wa Mwenyezi Mungu unalenga katika haki, usawa na uzuri, isipokuwa tatizo ni kuwa wengi bado hawajaelewa uongofu wa Mwenyezi Mungu na hivyo, kutojua ukweli wa Kiungu, Imeelezwa katika kurani tukufu {Ishara yoyote tunayo ifuta au tunayo isahaulisha tunailetea iliyo bora kuliko hiyo, au iliyo mfano wake. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu?}[AL BAQARAH 106].

12) Mingoni mwa uzuri wa uongofu wa kiisilamu ni kuwa upo katika usawa na uadilifu ambao hauna ubadhirifu wala upungufu, pia hakuna isirafu wala kuvuka mipaka, ni uzuri ulio bora ambao unaleta kheri na mafanikio katika kila jambo, Mwenyezi Mungu anasema {Wala usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo} [ISRAA 110]. Na akasema {18 Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha. 19. Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda} [LUQMAAN 18-19). Pia akasema {Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi} [ISRAA 29).

13) Ukamilifu unaofahamika katika kufuata usawa na uadilifu unafahamika katika uisilamu kama ufuataji wa uadilifu, na sio kama inavyofahamika na Orosto kuwa ni ufuataji wa maadili hali ya kuwa upo kati na kati, na hivi ni kama walivyoelewa (baadhi) ya wasomi wa kiisilamu. Lakini ufahamu wa kufuata usawa kwa mtazamo wa kiisilamu ni kufuata njia iliyonyooka, na usawa wa uadilifu unakusudiwa pia katika nyanya zote za maisha na kwa umma wote. {Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani,)} [AL BAQARAH 143].

14) Uongofu katika uisilamu –kama walivyoweka wazi wasomi kwenye utafiti wao– una mambo yake maalumu ambayo yanatengana na mambo mengine yaliyomo katika mitaala ya masomo na katika majaribio yao, na njia ya kujua uongofu wa kiisilamu iko wazi na wala hakuna utata wala mtafaruku au hata kutofahamika ukilinganisha na mitaala mengine iliyopo sawa iwe ya majaribio, ya kihisia, ya kiakili, ya kiroho au hata ya kivitendo, na inatosha kuwa kila mtaala unatofautiana na mwengine na kuwa haufanani, hivyo basi, matokeo yake ni kutofautiana kwa matokea ya kila moja wapo. Kinyume na mitaala ya kiisilamu ambayo imekamilika na kuwa sawa kwa pande zake zote, na kujiepusha na hitilafu na migongano ya uchambuzi na ya kielimu, na hii yote ni kwa sababu, asili yake ni sheria ya Mwenyezi Mungu ambae neno lake halibadiliki na wala halipingiki, na wala halina hitilafu.

15) Kwa ujumla, uongofu wa maadili ya kiisilamu, unajitenga katika maumbile –yaliyo kamili– yaliyothabiti –ya ukweli – kwa hali zote-. Nayo tutakuja elezea kwa kina zaidi katika maudhui yake maalumu.

Marejeo:Profesa. Hassan Al-Sharqawy ,Maadili ya Kiislamu,Al-qahera: Shirika la Mokhtar kwa kuchapishaji,ch 1,1988,(ku,7-19-83-87)kwa muhtasari na baadhi ya maongezi kutoka kwa mhariri.

Share this:

Related Fatwas