Tatizo la Kimaadili na Njia ya Kutibu katika Uislamu
Question
Ni ipi njia ya kutibu tatizo la kimaadili kwa mtazamo wa kiislamu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuna masuala mengi ambayo elimu ya kimaadili imejaribu kuyajibu: Ni vipi unatakiwa mwenedo wetu uwe katika maisha? Namna gani tutawalea vijana katika malezi mema? Ni kitu gani kinalazimu kwa kiongozi na raia ili wawe katika njia sahihi?
Hakika jawabu la maswali haya kwa upande wa wasomi wa elimu ya falsafa na hasa elimu ya kimaadili –ambao ni tawi la elimu ya falsafa– nayo ni mhimili wa elimu ya kimaadili, imejaribu kujibu maswali haya.
Katika mambo yenye kusisitizwa ndani ya fikira za kiislamu ni kuwa, kwa upande wa elimu ya kiroho na kimaadili – ni kuwa – hazitegemei hisia wala akili kuifanya akili kuwa ndio chimbuko na kuwa ni chanzo, lakini chimbuko lake ni wahyi uteremshwao na Mwenyezi Mungu katika ulimi wa amchaguaye ili kubeba ujumbe kwa waja wake.. haya ni katika mambo anayoyaweka wazi Mwenyezi Mungu kwa kupitia ulimi wa mitume yake. Na akili hapa huwa haielewi kitu katika mambo yaliyofichikana isipokuwa kutaka kujaribu tu kufahamu. Kwani maamuzi na uwekaji wazi huwa si kazi ya mwanadamu na huwa hahusiki nayo.
Na katika mambo yasiyo na shaka ndani yake ni kuwa, akili imeweza kuleta matunda mengi katika asili ya vitu na hesabu. Imeweza kuweka kanuni madhubuti na mipango sahihi. Hivyo, akili kwa upande wa nyanja hizi mbili imefanikiwa kufanyakazi katika kile kinachohusika nacho hasa. Vitu ambavyo ni: Vyenye kushikika na vyenye kuhisika. Ila kwa mshangao mkubwa, baadhi ya watu wamehadaika na kudhani kuwa akili inaweza kujua kila kitu katika nyanja zote. Wakaizonga akili kwa kutaka kujua kilichopo nje ya asili (mazingira ya asili). Hapo ikawa ndio falsafa ya uungu wa kiakili na ikawa akili haiwezi tena kufanya katika nyanja hii (kujua vilivyo nje ya mazingira ya asili). Na mtazamo huu ni mpya kiasi Fulani –kwa kulinganisha na umri wa mwanadamu katika ardhi– umeanza wakati wa uwepo wa Wagiriki na falsafa zao zikiongozwa na Arosto ambaye baadhi ya wanahistoria wamemjaalia kuwa ni akili kubwa sana ya falsafa ambayo haijawahi kuwepo katika dunia, lakini wale ambao waliokuwa wakitafuta vilivyo nje ya asili waliporomoka na hapa ikawa ni kufeli kwao kukubwa kwa akili ni ishara ya wazi ya kuwa ulimwengu wa nje ni mkubwa zaidi ya kuweza akili yenye mapungufu kuudiriki.
Na pia haimpasi muislamu kutaka kujaribu kujua ulimwengu wa nje,kwa maana ulimwengu wa nyuma ya kitabia, au kuudhania kiakili, na kwa hiyo ni lazimza juu ya waislamu wote wafanye kwa bidii, na wanapaswa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu na kutotafautiana.
Na madhehebu ya akili yalipoanza nchini Ujerumani mwanzoni mwa uongozi wa kidini, haraka sana ikabainika kwa upande wa itikadi ya kidini kuwa haiwezekani kutoa ushahidi kwa njia ya hisia, ikawa njia pekee ni kuifuta itikadi ya kidini katika madaftari matukufu. Na ikadhihiri pamoja na kufutwa itikadi ya madhehebu ya falsafa ya kimaadili. Hivyo, madhehebu ya kiakili yaliweza kuongoza itikadi hiyo, na hivi ndivyo ilivyokuwa hali ya Wajerumani. Na alipokuja Kant na kuandika kitabu “Akili tupu” juu ya mapungufu ya mwanadamu, akavunja hoja juu ya wafuasi wa madhehebu ya kiakili
Na hivihivi ndivyo alivyofanya imam Ghazali, kwa kupitia njia za wasiwasi wa wana falsafa akafikia matokeo yaleyale ambayo yapo katika ulimwengu wa kiislamu. Na akaweza kumaliza madhehebu ya kiakili ambayo yalikuwa ndio yanaaza kuchomoza (tena) pamoja na kuwa yalikuwa yamefifia. Na Imamu Ghazali alipowakatasha tama katika fikira za kichambuzi wakaelekea upande wa kiroho na maadili, na kwa upande huu wakakuta kuwa dini tayari imeshajitosheleza kielimu juu ya nyanja hii na falsafa ya kimetafizikia
Na katika makosa ya kimitaala –kwa kipimo cha kiisilamu- somo la elimu ya jamii na elimu ya nafsi na elimu ya maadili na mfano wake katika elimu za kijamii kuwa ni elimu zenye kuhusika na matukio ya kijamii au ya wanadamu, na wakafasiri elimu kuwa ni misingi ambayo inazingatia majaribio na uchunguzi. Na wakawa wanaelezea haya katika elimu ya kijamii na ya kibinadamu. Na elimu hizi kwa mtazamo huu haziendani na dini, kwa sababu hiyo watu wasio na dini wakaenea sehemu tofauti ulimwenguni. Kwani elimu na maadili kwa mtazamo wa mitaala iliyochanganyika ni ule ukuaji wa mwanadamu katika jamii, na watu wamejijenga katika njia maalumu wakaiita tabia njema na njia nyingine wakaiita tabia mbovu. Na kwa kuisoma dini na maadili kwa mtazamo huu itafahamika kuwa mwelekeo wa ukuaji na kuendelea na kuonekana kwake hakuna uhusiano –juu ya somo hili– na yale yateremshwayo kutoka mbinguni
Na kila chenye kuwepo na chenye kuhusika na masomo haya huwa ni ya kudhaniwa na yenye kubadilika ambayo hayathibiti na wala hayadumu katika hali moja.
Hakuna budi kutenganisha kati ya ulimwengu wa ujuzi: ulimwengu wa vinavyoshikika mfano, utabibu, asili na kemia … n.k. mambo haya yanakwenda sambamba na majaribio na wala hayapingani na dini na wala hakuna hitilafu yoyote. Na ulimwengu wa kifikira pekee ndani ya dini, maadili na jamii.
Hivo, tutaona athari kubwa kwa mfano - “Driem Kame” na mwanafunzi wake “Leafy Bruhon” ambao mafunzo yao, uchunguzi wao kuhusu jamii na maadili kwa upande wa tabia wamemili kuzungumzia tabia za mwenendo wa kisasa (zaidi) – ambayo hauendi sambamba kwa upande wa ufahamu wa kidini na kimaadili na kujaribu kuharibu kila kilicho kizuri.
Na mbinu za wasiwasi katika kuzungumzia tabia, vigezo, itikadi na maadili hakuna kitakachopatikana zaidi ya kuiharibu jamii na kuichanganya kimaadili ya kidini.
Sasa wacha tufanya mlimganisho kati ya yale waliyoyasema waliotangulia zamani kuhusu tatizo la maadili na aliyoyasema msomi mkubwa wa kiislamu Alharith Binn Asad Almuhasibi. Utaona katika maelezo yake kuna upole wa nafsi, utulivu wa kiroho pamoja na kuwa amejiingiza mwenyewe katika vita ya matatizo yenye kuleta utata, na kuanza kujadiliana kiupole na kiustadi hali ya kuifanya Quraani na hadithi za Mtume kuwa ndio chanzo cha tegemeo lake na njia anayopatia hekima kwa kila alisemalo au alitendalo.
Hivyo basi, inapasa kwa muislamu kuwa na hisia za wazi na thabiti: kwani muongozo wa maisha ya muislamu ni kufuata, na muongozo huu ni ule aliotuwepesishia msomi Abdallah Bin Masuud Mwenyezi Mungu amwie radhi katika maneno yake mafupi yenye ujumbe mkubwa aliposema “fuateni wala msizushe kwani kwa hakika mumetoshelezewa”
Nalo ni neno la haki na kweli lenye maana nyingi na ndefu na pana zaidi, mwanzo wake ni ushahidi na mwisho wake pia ushahidi, ikimaanisha “ fuateni kwani hakika Mwenyezi Mungu yeye ndiye wa kutosheleza, na ndiye aliyeteremsha vyanzo vya misingi na nguzo zake, na hayo yote yakafanywa kimatendo na kuwekwa wazi na Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake). Na ikawa katika uwekaji wazi wake ni marejeo ambayo waliotafautiana huwa wanayarejea. Na aliposema “msizushe kwani kwa hakika mumetoshelezewa”. Kwa kuwa anayezusha huwa hatosheki, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya kuikamilisha dini na kutimiza neema zake pakawa hapana mwanya wala kuwepo haja ya kuzusha.
Kwa namna hii msomi mkubwa Profesa Abdul Halim Mahmoud anatuelezea kuhusu kutibu tatizo la kimaadili kwa muono wa kiislamu, kwa kusema, haitopatikana isipokuwa kwa namna moja nayo ni kufuata.
Muongozo wa kiislamu (kufuata) Una athari kubwa sana katika nyenendo za kimaadili ya mtu. Kwa upande wa wanamaadili wasiotumia sheria – lengo lao ni kufikia ladha ya “kuiridhisha tabia” tu na “kuitia aibu dhamiri”. Kwa upande wa muislamu huwa na pupa ya kutaka ridhaa za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujiweka mbali na yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na hufanya kimbilio la kumridhisha Yeye na kujiepusha na yamkasirishayo, hii ndio tabia ya muislamu. Na si kutaka kuiridhisha nafsi yake na kukimbilia kuiaibisha na kuilaumu.
Basi ni kwa kipimo gani cha maadili kilichothibiti cha kuiridhisha nafsi, ilivyokuwa nafsi yako inaridhika na kitu na nafsi za wengine haziridhishwi na kitu hicho. Ibn Atwaa Lah Sakandari anaona –naye ni katika watu maarufu sana wa maadili ya kiislamu katika hekima yake maarufu– kwamba (chanzo cha maasi yote na kughafilika na matamanio ni kuiridhisha nafsi, na chanzo cha kila utiifu na uamsho na upole ni kutoitii nafsi.) muamko wa dhamiri ya muislamu haurejei kwake yeye mwenyewe bali kw kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuogopa kwa ajili yake.
Mwanadamu alipoendekeza dhamiri yake ndio vita vya dunia vikasimama kila mahala, mauaji ya kutisha, maangamizo ya mali na miji, na watu wakaingia katika ufisadi na hasara ambayo haiwezi kufidiwa.
Marejeo muhimu: Prof, AbdulHalim Mahmoud. Katika utangulizi wake wa tafsiri ya kitabu cha “ Tatizo la kimaadili na falsafa” cha Andrew Krison. Cairo. (ukurasa 67-69. 155)