Kubadili Jina Baada ya Kusilimu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadili Jina Baada ya Kusilimu

Question

Je, Hukumu gani ya kubadili jina baada ya kusilimu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Kwa kuwa majina yana maana, inatakiwa mtu aitwe kwa jina zuri, lenye maana nzuri, ili awe na hadhi kutokana na jina lake. Kwa hiyo Mtume S.A.W. Alikuwa akibadili majina mabaya kwa majina mazuri, basi imepokelewa kutoka na Ibn Omar R.A. "Ni kuwa mtoto wa kike wa Omar alikuwa akiitwa: Aswia, basi Mtume S.A.W. akamwita Jamila." Na ilitolewa na Abu Dawud katika sunna yake (Kitabu chake) kutokana na Abi Adardaa amesema: Mtume S.A.W Amesema: "Hakika nyinyi mtaitwa siku ya Kiama kwa majina ya wazazi wenu, basi itaneni kwa majina mazuri".

Ibn Al Qaiym alisema: "Kwa kuwa majina yanabeba maana, na yana mweleweko wa maana, basi hukumu yake imepelekea pawepo kati yake mfungamano na mnasibiano, na wala maana isiwe pamoja nalo katika hali ya ugeni mtupu ambao haunasibiani nalo, hakika busara kwa aliye na busara hulikataa jambo hili. Na hali halisi inashuhudia kinyume na hivyo, bali majina yanaathari kwa muhusika, na muhusika wanaathirika kwa majina waliyoitwa katika uzuri, ubaya, wepesi, uzito, na upole". [Zaad Elmauaad fee Hadiy Khair Al Ebaad, 336/1, Ch. Muasasat Al Resalah]

Na hisia nzuri hutokana na neno zuri, Mtume S.A.W. Alikuwa anapenda jina zuri na anajihisi vyema kuwa na kheri kutokana na jina zuri, na huchukia jina baya sio kwa sababu ya hisia mbaya na iliyozuiliwa, hakika mambo yalivyo ni kwa kuleta hisia mbaya kwa kulitamka jina hilo na kuitaja maana yake ambayo anaikwepa, imepokelewa na Al Bukhariy na Muslim na Abu Dawud (na lafudhi yake) kutoka kwa Abi Hurairah amesema kwamba amesema: Mtume S.A.W "Napenda hisia nzuri" ilisemwa kwake: Hisia nzuri ni nini? Akasema: "Neno zuri", Na miongoni mwa majina hayo ambayo Mtume S.A.W. alitaja maana yake na akahisi zuri kwa maana yake, na akatahadharisha shari katika maana yake, na hisia yake nzuri na mbaya na uhalisi ulioafikiana na hisia yake nzuri na kutahadhari kwake tamko lake S.A.W. katika yaliyopokelewa na Ahmad na Muslim kutoka kwa Abi Hurairah: "Aslam, Mola atamweka katika hali ya usalama, na Ghafaar Mola atamsamehe makosa yake, Uswiyat, amemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake."

Na Sira imesema kwamba Aslam na Ghifaar na makabila mawili yalisilimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na watu wake wakaja kwa Mtume S.A.W. wenye kutii na wenye uongozi, Ama Uswiyat likapiga likawa dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na likashirikiana na Raiel na Zakwaan katika kuwaua masahaba wa Mtume S.A.W.

Na Al Haithamiy alitoa katika kitabu cha [Majma' Al Zawid] kutoka kwa Umu Salama R.A. alisema: "Al Husaien aliposhuka na jamaa zake mji wa Karblaa, akauliza jina lake, akaambiwa jina lake ni Karbalaa, akasema: Sunhaan Allah, (Kar) kera na balaa, na kweli hayo yalitokea. (Ya balaa)

Ali Bin Borhaan ametaja katika kitabu cha [Al Sira Al Halabiyah] "Halima Al Sa'adiyah aliposimama kwa Abdulmutwalib anaomba kumnyonyesha Mtume S.A.W. Alipokuwa mtoto mchanga akasema: wewe ni nani? Halima akasema: mimi ni mwanamke kutoka Bani Sa'ad, akasema: na jina lako nani? Akasema: mimi ni Halima, abdulmutwalib akasema: "Uzuri ulioje kwako ewe Saad, wapwa/wajomba hawa wawili wana maisha marefu". Na Al Baihaqiy na Al Dailamiy na Al Haakim wameitoa na wakasema ni hadithi sahihi kwa masharti ya masheikhi wawili na haina kasoro, kutoka kwa Aisha R.A. Alisema: Mwanamke mzee alikuja kwa Mtume S.A.W. basi akamwulizia jina lake, basi akasema mimi ni Juthamah Al Muzaniah, basi Mtume S.A.W. Akasema bali wewe ni Husanah (Uzuri)".

Al Bajiy amesema katika kitabu cha [Sharh Al Muwatta'] Tofauti kati ya hali hii na nuksi inayokatazwa ni kwamba nuksi si katika tamko lake wala katika mwonekano wake kitu chenye kuchukiza au kuudhi, isipokuwa inaaminika kuwa wakati wa kukutana naye kwa upande maalumu huwepo nuksi na kuzuilika kinachokusudiwa, na sio hivyo majina haya ni majina yenye kuchukiza mabaya hayapendezi kutajwa kwake na kuyasikia, na hutajwa kwa maana zinazokatazwa, kwa mfano jina Harbu lenye maana ya vita, hutajwa kwa kutaja kinachotahadharisha vita, na vile vile jina kama Murra, huchukiza ndani ya nafsi ya mtu kulitaja kwa sababu hiyo. Na Mtume S.A.W. alikuwa akipenda hisia nzuri, na ilipokelewa kutoka kwake kwamba alisema: "Napenda hisia nzuri, ikasemwa: basi ni nini hisia nzuri? Akasema: neno zuri". Nalo hutajwa kwa namna mtu anavyotazamia kheri ndani yake na nafsi ikafurahikia kwalo na huwenda ikawa ni kwa maana ya ishara njema kwa yale aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu katika mambo ya kheri. Kwa hiyo Mtume S.A.W. akasema katika siku ya Al Hudaibiah na Sohail Bin Amr ameonekana: "Amekufanyieni wepesi jambo lenu ikawa kama alivyosema Mtume S.A.W. [Al Muntaqa Sharh Al Muwatta', 295/7, Ch. Dar El Kitaab Al Islamiy].

Na Malik ameeleza katika kitabu cha [Al Muwatta'] kutoka kwa Yahiya Bin Said: "Kwamba Omar bin Khatwab alimuuliza mtu jina lake, na akasema: anaitwa Jamra, Omar akamuuliza, wewe ni mtoto wa nani? Akasema yeye ni mtoto wa Shihab. Akauliza, Shihabu wa kutoka wapi? Akajibu wa kutoka Alhuraqqa. Akasema: makazi yako ni wapi? Akajibu yako katika Haratu Naar. Akasema Omar: ni ipi? Akajibu: ni katika Ladhwaa. Omar akasema: wawahi ndugu zako, hakika wameangamia. Akasema: ikawa kama alivyosema Omar bin Khatwab. Al Baajiy akasema: Na hii iko katika maana ya kuwa na matumaini kwa kusikia kwake, na hii ilikuwa hali ya huyu mtu kabla ya hayo, ambaye watu wake waliteketea kwa moto, lakini hiki ni kitu ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu hukiingiza ndani ya moyo wa mja mwenye matumaini, pale anaposikia habari za kufariji katika mambo ya kufurahisha, na nguvu za matumaini yake katika matumaini yake juu ya jambo hilo, juu ya kutahadharisha kwake kutokana na kitu hicho anadhani hivyo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajalia juu ya ulim wake na kwenda sawa na aliyo yakadiria Allah Mtukufu na baadhi ya watu wanakuwa ni wenye kukubaliwa zaidi kuliko wemgine. Na ilipokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kwamba yeye akasema: "Watakuwa wahadithiaji/wasemaji, bila ya wao kuteremshiwa wahyi, basi kama wapo katika Umma wangu basi Omar ni miongoni mwao." [Al Muntaqa Sharh Al Muwatta', 295- 299/7, Ch. Dar El Kitaab Al Islamiy].

Wasio waislamu labda wanaitwa kwa majina mabaya na haramu au yenye karaha, au wanaitwa kwa majina mazuri, basi lazima wasio waislamu wakisilimu wabadilishe majina yao mabaya kama majina hayo yalikuwa haramu, na ilikuwa ni Sunna kubadilisha majina hayo kama yakiwa yenye karaha. Na miongoni mwa majina hayo yaliyoharamishwa ambayo lazima yabadilishwe baada ya mtu kuingia Uislamu, kama jina linamuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu kama vile Muumba, Mtakasifu, Mwenye kutegemewa, Mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu, Mwenye Kibri, wa Mwanzo na wa Mwisho, au yakawa majina hayo kwa namna ambayo hailingani na mtu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama vile Mfalme wa wafalme, Sultani wa masultani, Mkuu wa Wakuu na mengineo. Na dalili ya hayo ni hiyo hadithi iliyotolewa na Al Bukhariy kutoka kwa Abi Huraira alisema: Mtume S.A.W. Amesema: "Majina yenye karaha zaidi kuliko yote siku ya Kiama mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mtu aitwaye mfalme wa wafalme."

Na katika kauli ya Muslim kutoka kwa Abi Huraira alisema: Mtume S.A.W. Amesema: "Mwenye kukasirisha mno siku ya Kiama kwa Mwenyezi Mungu na aliye mwovu zaidi ni yule aliyekuwa akiitwa Mfalme wa wafalme, kwani hakuna Ufalme isipokuwa ni wa Mwenyezi Mungu tu."

Al Ainiy Al Hanafiy alisema: "Na inazuiliwa kusema, Kadhi aliye juu ya Makadhi, kwani maana yake ni Muamuzi wa Waamuaji, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndie Mwamuzi wa Waamuzi wote." [Umdet Al Gaariy' Sharh Sahih Al Bukhariy 315/2, Ch. Dar Ihyaa Al Turaath Al Arabiy]

Al Bahutiy Al Hanbaliy alisema: "Inaharimishwa kuitana mfalme wa wafalme na mengineo ambayo ni sawa pamoja na majina ya Mwenyezi Mungu kama vile Sultani wa Masultani kama yalivyopokelewa na Ahmad: "Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu itakuwa kali zaidi juu ya mtu yule aliyekuwa akiitwa Mfalme wa wafalme, kwani hakuna Ufalme isipokuwa ni wa Mwenyezi Mungu tu."

Na ni haramu kuitana majina ambayo hayastahiki isipokuwa aitwe kwayo mwenyezi Mungu Mtukufu kama vile Mtakasifu, Mtenda wema kwa waja wake, Muumba au Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa; kwani maana ya majina haya inamfaa Mwenyezi Mungu tu. [Kashaaf Al Qinaiy kwa Al Bahutiy 26/3, Ch. Dar Al Kutub Al Ilmiyah].

Al Hattaab Al Malikiy alisema: "Na Inaharimishwa kwa mfalme wa wafalme kwani hilo ni jina baya zaidi kuliko yote mbele ya Mwenyezi Mungu, aidha alisema: "Mtume S.A.W. alibadilisha majina ya Azizi na Hakeem, kwani yanafanana na majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu". [Mawaheb Al Jalil kwa Al Hattwab 257/3, Ch. Dar Al Fikr]

Na miongoni mwa majina yaliyo haramu ambayo ni lazima yabadilishwe baada ya kuingia Uislamu jina lolote lenye kuabudia wasio Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile Abdulmaseeh (mja wa yesu), Abduluzi (mja wa Auzi), Abdulkaaba (mja wa Kaaba) na kadhalika kwa yaliyopokelewa na Ibn Abiy Shaibah katika kitabu chake: [Al Musanaf], na Al Bukhariy katika kitabu cha: [Al Adab Al Mughniy], kutoka kwa Bin Yazied kwamba alipofika pamoja na watu wake kwa Mtume S.A.W. Mtume S.A.W. akawasikia wanaita mtu mmoja miongoni mwao kwa Abdulhajar (mja wa jiwe) , basi Mtume [S.A.W]. alimuuliza: Jina lako nani? akasema: Abdulhajar, basi Mtume S.A.W. akasema: "Bali wewe ni Abdullaah".

Na katika kitabu cha: [Mustadrak Al Haakem] kutoka kwa Abi Hurairah akasema: "Jina langu lilikuwa katika Jahiliyah Abdushams (mja wa Jua) Bin Swakhr, basi Mtume S.A.W. akaniita Abdulrahmaan"
Na Shehaabu Edeen Al Ramliy akasema: "Na ni haramu kuitana Mfalme wa Wafalme kwa kuwa haifai kwa siye kuwa Mwenyezi Mungu, na vile vile kuitana Mja wa Kaaba, Nyumba tukufu, au Mja wa Ali, au Husein, kwa kuweza kufikirika kuwepo ushirika na Mwenyezi Mungu, na mfano wake ni Abdu Nabiy kama waitavyo wengi. Na kuna mielekeo ya pamoja na kuchukiza kufanya hivyo na hasa pale panapokusudiwa kunasibisha na Mtume S.A.W. na huchukuliwa kutokana na kasoro iliyopo kuwepo uharamu wa kumwita mja Jarullwah (jirani wa Allah) au Rafikullwah (rafiki wa Allah), na mfano kwa kuwepo uwezekano wa kufikirika ushirika ulioharamishwa pia." [Nehayat Al Muhtaaj Sharh Al Menhaaj 148/8, Ch. Dar Al Fikr]

Al Bahutiy Al Hambaliy alisema: "Ibn Hazm Akasema: waliafikiana kuharamisha jina lolote lenye kuabudia wasio Mwenyezi Mungu Mtukufu, hama vile, Abduluzi (mja wa Auzi), mja wa Amro, mja wa Aliy na Abdulkaaba (mja wa Kaaba) na yanayolingana na hayo, na mfano wake mja wa Anabiy, mja wa Al Husaein na mja wa Jesu. Ibn Al Kaiym alisema: "Ama kwa kauli yake Mtume S.A.W. aliposema: mimi ni Ibnu Abdul Mutwalib, haikuwa kwa lengo la kuasisi uitaji jina, bali ilikuwa ni kwa lengo la kutoa maelezo ya jina ambalo alijulikana kwalo mwenye kuitwa kwa jina hilo. Na kutoa maelezo kama hayo kwa ajili ya kumtambulisha mwenye jina sio haramu, kwa hivyo mlango wa kutoa maelezo ni mpana zaidi ya mlango wa kuasisi. Amesema: kundi la wafuasi wa Dini lilikuwa linachukua tahadhari ya kuita jina la Kadhi wa Makadhi na Hakimu wa Mahakimu, kwa kufuata kigezo cha yale yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuliko kuita kwa jina la Mfalme wa Wafalme. Ni hiki ndicho kipimo chenyewe." [Kashaaf Al Qinaa' kwa Al Bahutiy 26/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].

Na inachukuliwa kipimo hichi kwa majina yathibitishayo Akida potofu kama vile "Shenuda" ambalo kwa kiarabu jina hili lina maana ya mtoto wa Mwenyezi Mungu. Na majina mengine mengi ambayo lazima yabadilishwe. Au yale majina maalumu kwao ya wanaume wao na wanazuoni wao na wazee wao kama vile Paulo, Patrick au Butros, Yohana na Matayo. Haya majina yameharamishwa kwa upande wa kujifananisha na Mayahudi na Wakristo.

Na kuna majina ambayo ni Sunna kuyabadilisa kutokana na kuchukiza kwake, na miongoni mwa majina haya ambayo yanachukiza kuitana kwayo na inapendeza kuyabadilisha, majina ambayo yanatuchukiza ndani ya nafsi na kuudhika nayo ni majina kama vile; Vita, Chungu, Mbwa na nyoka. Na Malik ametoa katika kitabu chake: (Al Muata') kutoka kwa Yahya Bin Saied, kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Nani anamkama huyu? "Basi mtu mmoja alisimama, basi Mtume S.A.W. akasema kumwambia: Jina lako nani? Akasema mimi ni Harb (vita), basi Mtume S.A.W. akasema: simama! Halafu akasema: "Nani anamkama huyu?" Basi mtu mmoja akasimama, na Mtume S.A.W. akasema: "Jina lako nini?" Mtu akasema mimi ni "Yaishi" (huishi), basi Mtume S.A.W. akasema: "kamua!"

Na Abukhariy alitoa kutoka kwa Saied Bin Al Musaib kutoka kwa baba yake kwamba baba yake alikuja kwa Mtume S.A.W. basi Mtume S.A.W. akasema: Jina lako nani? Akasema "Huzuni", basi Mtume Akasema: bali "wewe ni Sahil" basi akasema: Siwezi kulibadili jina aliloniita kwalo baba yangu. Akasema Said Bin Al-Musiib: bado tunaendelea kuwa na Hazuni (wenye huzuni).

Swahib wa kitabu cha: [Mawaheb Al Jalil] Amesema kwa yaliyokuwa mabaya kama vile Harbu (Vita) Huzuni na Dhwarari yamekatazwa" [Mawahib Al Jalil Sharh Mukhtasar Khalil 256/3, Ch. Dar Al Fikr]
Na Swahib kitabu cha: [Mughniy Al Muhtaaj] akasema: majina mabaya, kama vile, Shetani, Dhalimu, dhwarari yamekatazwa Shehabu, Punda, Mbwa na mfano wake yanachukiza. [Mughniy Al Muhtahaaj Sharh Menhaaj Al Twalbeen 294/4, Ch. Dar Al Fikr]

Na wanavyuoni wa Madhehebu ya Hambali walisema kwamba inachukiza uitaji kwa majina ya majabari, kama vile Firauni, na majina ya shetani, Al Rahaibaniy alisema: "Na pia inachukiza kuitana majina ya Shetani kama vile; Murra, Walhaan, wal-aur na walajidah na pia inachukiza kuitana kwa majina ya mafarao na wafalme waovu kama vile Firauni na Hamana, Qarun na Alwaliid. [Matwalib Uliy An Nuha katika Sharh Ghayat Al Muntaha 495/2, Ch. Bairuut]

Na Al Bahutiy Al Hambaliy alisema: "Na katika majina yanayochukiza ni Harbu, Murra, Huzuni, Naafiu, Yasaar, Aflah, Najiihu, Barakah, Yaalaa, Mukbil, Raafiu, Rabaahu, Alaaswi, Shihaabu, Mudhtwajiu, Mtume na mengine mfano wa haya kama vile Rasuulu." [Kashaaf Al Qinaa' kwa Al Bahutiy 26/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].

Na Mtume S.A.W. alikuwa akichukia majina mabaya kwa watu, mahali, makabila na milima. Abu Dawud amesema katika Sunna zake: "Na Mtume S.A.W. alibadilisha jina la ardhi iliyokuwa ikiitwa Afra na akaiita Khadhra yaani kijani kibichi, na Shaabu dhwalaalah akaita Shaabul hudaa na Banuu Zanniyah akawaita Banuu Rishda na akawaita pia Banuu Mughwiya kwa jina la Banuu Rishda." Pia ilipokelewa katika kitabu cha [sira ya nabii] kwamba Mtume S.A.W. alipita katika moja ya vita vyake kati ya majabali mawili na kisha akaulizia majina ya majabali hayo; wakamwambia ni Faadhihun na Mukhzii (yaani moja linaitwa Fedheheshaji na jingine laitwa Tiaji aibu) akabadilisha kati yake na wala hakuelemea upande wowote. Na Mtume S.A.W. alipofika Madina na jina lake ilikuwa ni Yathrib na haijulikani Ila kwa jina hilo basi alilibadilishia kwa Twebah.

Na miongoni mwa majina haya ambayo ni vizuri kuyabadilisha kwa kuchukiza kwake ni kila jina linalochukiza ukanusho wake Kama vile Rabaahu na Yasaar lau mtu aliyemwita mwanae kwa jina la Rabaahu akiulizwa; Rabaha yuko ndani? Na akajibu Rabaahu hayuko hakika ni kwamba kwa mtu huyo huleta msikiko mbaya wa jina hilo. Na Muslim ametoa katika kitabu chake sahihi kutoka kwa Samrah Bin Jandab alisema: Mtume S.A.W. amesema: "Usimwite mtoto wako wa kiume kwa jina la Yasaar au Rabaha. Wala Najiihu au Aflah: kwa kufanya hivyo hakika wewe wasema kuwa yeye ni kosa au dhambi". Kwa hiyo huwenda ikawa ni njia ya kuwa na hisia mbaya na kwa hiyo, katazo linagusa kila kinachopelekea kuwa na kuagua isipokuwa na haliharamishi kwa Hadithi ya Omar, "Kwamba mtoa idhini wa manyweo ya Mtume S.A.W. anaitwa; Rabaah" [Kashaaf Al Qinaa' kwa Al Bahutiy 26/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].

Na miongoni mwa majina ambayo ni vyema kuyabadilisha kwa sababu ya kuchukiza kwake na vile vile kila jina lenye utukuzaji wa nafsi na kuikweza. Na asili katika hayo ni yaliyopokelewa na Al Bukhariy na Muslim kutoka kwa Abi Huraira: "Kwamba Zainabu jina lake lilikuwa ni Burrah, basi ilisemwa anajitukuza, basi Mtume S.A.W. alimwita Zainabu", na Mtume S.A.W. Akasema: "Msijitukuze nafsi zenu, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi wa watu wema kuliko nyinyi."

Ibn Abdeen alisema: "Na inakatazwa kuitana majina ambayo ndani yake kuna utukuzo kama vile: Muhyu Diin, Shamsu Diin pamoja yale majina yenye uongo ndani yake, na baadhi ya Wafuasi wa Madhehebu ya Maliki wameandika kuhusu kuzuia majina ya aina hii, na Aqurtubiy alitaja katika kitabu cha: [Sharh Al Asmaa Al Husnua] Kitabu na Sunna iliiashiria kwa kuzuia mtu hujitukuza, na imenukuliwa kutoka kwa Imamu Anawawiy alikuwa akimchukiza mtu yeyote anaemwita kwa Muhiy Al Diin na kusema: Simuweki aliyeniita kwa jina hilo katika uhalali, na mfano wa hayo Amjuae Mwenyezi Mungu Mtukufu Sheikh Sanani katika kitabu chake cha: [Tabyiinu Al Mahaarim], na akazua mgogoro mzito kwa wenye kuitana kwa majina kama haya, na kwamba hii ni katika utukuzo unaokatazwa katika Quraani tukufu, na miongoni mwa uongo". [Hashiyat Ibn Abdeen 412/8, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]

Na Al Hatwaab Al Malikiy alisema: "Ibn Al Hajaj amesema katika kitabu cha: [Al Madkhal]: Aqurtubiy amesema katika kitabu cha: [Sharh Al Asmaa Al Husnua]: Kitabu na Sunna imeeleza kuzuia mtu hujitukuza, halafu akasema: wanazuoni wetu wamesema: Na yanatokea kama haya katika nchi kama vile Misri na nchi za Uajemi, Iraki, watu walijipa sifa ambazo zinapelekea kujitukuza na kujisifu kama vile Zakiyu Diin, Alamu Diin, Muhyu Diin, na majina mengine yanayofanana na haya. Kisha akasema: kama majina haya yangekuwa yanajuzu basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na haki zaidi ya kuitwa kwayo kuliko maswahaba wa Mtume S.A.W.." [Mawaheb Al Jaleel kwa Al Hatwaab 257/3, Ch. Dar Al Fikr]

Na Al Bahutiy Al Hambaliy alisema: "Na pia jina lenye utukuzaji kama vile Takiyyu, Zakiyyu, Ashraf, Afdhwalu na Burrah. Amesema Kadhi: na kila jina lenye ukwezaji na utukuzaji ndani yake". [Kashaaf Al Qinaa' kwa Al Bahutiy 26/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].

Na kwa ujumla, inapendeza kwa mtu aliyeingia Uislamu kubadilisha jina lake liwe na Uja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ili autangaze Uislamu wake kwa jina hilo na iwe alama ya kujiengua kwake na ukafiri na alama ya kusilimu kwake, Ibn Abdeen Al Hanafiy alisema: "Majina yanayompedeza zaidi Mwenyezi Mungu Mtukufu na Abdullah na Abdulrahmaan, hilo ni tamko la hadithi ilipokelewa na Muslim, Abu Dawud, Al Tarimiziy na wengineo kutoka kwa Ibn Omar Al Menaawiy alisema: Na Abdullahi ni bora kuliko yote hata kuliko Abdulrahmaan, na yaliyo afadhali/Bora baada ya hayo ni Muhammad, halafu Ahmad kisha Ibrahimu. Na pia akasema katika mahali pengine: Na yanafuatia na majina hayo ambayo ni Abdullwah na Abdurahman,na yale yanayofanana nayo kama vile Abdul Rahiim na Abdul Malik, na kupendekezwa zaidi kuyatumia majina haya kunategemea na atakayetaka kuita kwa Unyenyekevu (yaani kwa kutanguliza Abdu kabla ya jina la Mwenyezi Mungu) kwani wao walikuwa wakijiita Abdul Shamsi na Abdu Daar, na hali hii haizuii kuwa jina Muhammad na Ahmad ndio yanayompendeza zaidi Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko majina mengine yote. Kwani Mtume hakuchaguliwa jina isipokuwa ni zuri zaidi kwake na hivi ndiyo sahihi. Na wala haijuzu kulichukulia [jina la Muhammad katika hali ya kawaida tu. Na imetajwa kuwa: "Na yeyote atakaeruzukiwa mtoto wa kiume na kumwita kwa jina la Muhammad basi yeye na mwanae wataingia peponi". Ilipokelewa na Ibn Asaaker kutoka kwa Umamah, Al Syutiy amesema hadithi hiyo ni ya afadhali zaidi kulio zote zilizotajwa katika mlango huu, na Asakhawiy amesema: "Na kuhusu kauli yao (Hakika majina mazuri ni yale yenye Abdu na yenye Muhammad sifahamu kuhusu hayo)" [Hashiyat Ibn Abdeen 418/6, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].

Na Al Hatwaab alisema: "Al Baajiy akasema: Majina yaliyo bora kuliko yote ni yale yenye Uja ndani yake kwa Hadithi ya Mtume S.A.W. "Hakika majina yenu yaliyo bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullahi na Abdul Rahmaan". Na Mtume S.A.W. amewaita Hassan na Husaen, na Al Utaibiy amesimulia kwamba wakazi wa Makkah wanazungumza wakisema kuwa hakuna nyumba yoyote ambayo ndani yake kuna jina la Muhammad isipokuwa huona ndani yake kheri nyingi na hujaaliwa rizki. [Mawaheb Al Jaleel kwa Al Hatwaab 257/3, Ch. Dar Al Fikr]

Na Al Bahutiy Al Hambaliy alisema: "Ni Sunna kutoa majina mazuri kwa kauli yake Mtume S.A.W. "Hakika nyingi mtaitwa siku ya Kiama kwa majina yenu na kwa majina ya Baba Zenu, kwa hivyo basi peaneni majina mazuri". Imepokewa na Abu Dawud. Na hadithi ya: "Majina yapendezayo zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kama Abdullahi na Abdul Rahmani. Hadithi hii imepokewa na Imamu Muslimu. Na jina lolote litakaloegemezwa katika jina miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu basi ni zuri. Kama vile; Abdul- Rahiim, Abdul-Razaaq na Abdul-lkhaaliq n.k. vile vile majina mazuri ni yale ya Mitume kama Ibrahim, Nuhu, Muhammad, Swaleh na yanayofanana na hayo, kwa Hadithi ya Mtume S.A.W. jiiteni kwa jina langu na wala msijipe ubini kwa ubini wangu", ilipokelewa na Abu Naiem, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Kwa utukufu wangu na cheo changu cha utukufu sitamuadhibu yeyote motoni aliyeitwa kwa jina lako" [Kashaaf Al Qinaa' kwa Al Bahutiy 26/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].

Ibn Al Qaiym amesema: "Kwa kuwa jina lina kwenda sambamba na anaeitwa kwalo na linamuathiri, basi majina yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni yale yenye kuambatana na sifa nzuri kama vile Abdillahi na Abdulrahmani, na kuegemeza abdu au unyenyekevu katika majina ya Mwenyezi Mungu kama vile Allwahu au Arahman, ni bora zaidi kuliko kuegemezwa kwa yasiyokuwa hayo kama vile Alqaahir au Alqaadir.

Kwa hivyo, jina Abdulrahmani linapendeza zaidi kuliko Abdulq-aadir, na Abdullahi ni bora zaidi kwa mtu kuliko Abdu-rabuhu, Na hii ina maana kuwa mfungamano uliopo kati ya mja na Mola wake jinsi ulivyo ni wa uchaji mungu mtupu, na mfungamano uliopo kati ya Mola na mja wake ni wa rehema tupu, na kwa rehema zake ndivyo ulivyo uwepo wake na ukamilifu wa uwepo wake. Na lengo ambalo ameufanya uwepo wake kwa ajili hiyo waja wamtukuze Mola yeye peke yake kwa upendo na kwa woga, kwa kumtukuza na kumuadhimisha na akawa mja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na awe anamuabudu kwa jinsi jina lake la lilivyo na maana yake ya kiuungu ambayo ni muhali kuwa nayo mwingine. Na kwa kuwa upole wake unaishinda hasira yake na upole wake anaupenda zaidi ya ghadhabu zake, hivyo Abdul Rahman ni jina bora kuliko Abdul Qaahir. [Zaad Al Meaad fee Hadiy Khair Al Ebaad 305/2, Ch. Muasasat Al Resaalah.]

Kutokana na yaliyotangulia: Basi inajuzu kisheria kubadili jina la mtu baada ya kuingia katika Uislamu iwapo kuna sababu za kufanya hivyo, na huenda ubadilishaji huu wa jina ukawa wajibu, na unaweza kuwa sunna au unapendeza, kama ilivyoelezwa kwa mapana na marefu

Share this:

Related Fatwas