Viza ya Kuingia Nchi Nyingine

Egypt's Dar Al-Ifta

Viza ya Kuingia Nchi Nyingine

Question

Je, viza ya kuingia nchi nyingine “ina hukumu” ya mkataba wa usalama katika Uislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Amani katika lugha ya kiarabu: ni kutotarajia kutokea chukizo (jambo la kuudhi katika muda ujao), amani muda mwingine hukusudiwa kama jina la hali anayokuwa nayo mwanadamu kutokana na utulivu, na muda mwingine mkataba wa amani au hati ya fedha au kitu kingine. Maana yake ni kuomba usalama. Kuwa chini ya himaya yake. [Al-Mufradat, Al Raghib El asfahaniy uk.90, chapa ya Dar al qalam, na Taj El arous 34/184, Dar Elhidayah, na El Misbaah El Muniir uk.24, mada ya: Amina, chapa ya Al Maktabat El ilmiyah].
Ama katika istilahi, amesema El Khatib El Sherbiniy: “amani, ni kinyume cha hofu, na hapa imekusudiwa kuacha kuuwa na mapigano pamoja na makafiri, nayo ni katika vitimbi vya vita na maslahi yake, na mikataba inayofidisha au kumaanisha usalama ni miatatu: Usalama, kodi na kusimama vita kwa muda mfupi au suluhu baada ya vita; Kwa kuwa ikihusiana na jambo maalumu ni usalama, au kinyume na hivyo, ikiwa ni katika kufikia lengo ni kusimamisha vita na kama sio hivyo basi inakuwa ni kodi, navyo vinahusika na imamu kinyume na usalama”. [El Mughny El muhtaj 4/236, chapa ya Dar ihyaa El turath el Araby}.
Na mwenyekutafuta usalama: Ni mwenye kuingia jimbo la mtu mwingine kwa ajili ya kuomba usalama kwa muislamu au hata kwa yule anayeupiga vita Uislamu. [angalia: Al Dur ElMukhtar 3/247 chapa Dar Ihyaa el Turath].
Uislamu ni dini iliokuja na kila jambo bora au zuri, na Mtume S.A.W. akabainisha kwamba ametumwa ili kutimiza tabia njema, na Quraani tukufu ikabainisha kuwa miongoni mwa sifa za waumini na kwa kuwa wao wanatekeleza ahadi na hawavunji mikataba, na kuvunja mikataba ni katika sifa za watu waliolaaniwa, anasema Allah Mtukufu: {Je! Anaye jua ya kwamba yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Wenye akili ndio wanaozingatia, Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji maagano, Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanaiogopa hesabu mbaya, ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na wakashiki Sala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika tulivyo wapa; na wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata malipo ya Nyumba ya Akhera. Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na walio wema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanaingia katika kila mlango. .(Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera. Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya ufisadi katika nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya.} [ AR-RAA'D 19-25].
Kizazi cha kwanza kilifahamu maana hii na kuitekeleza hata katika zama za fitna, kutoka kwa Said Ibn Al Musayyab ya kwamba Muawiyah aliingia kwa mama Aisha R.A. mama Aisha akasema kumwambia: hukuhofia kukaa na mtu ambaye anaweza kukuuwa? Akasema: je, ungekuwa ni mwenye kufanya hivyo nami nikiwa katika nyumba ya amani, na nimemsikia Mtume S.A.W. akisema: "Imani inazuwia kuuwa baada ya kuwa katika usalama". Vipi, itakuwaje shida iliyopo kati yangu na kati yako wewe? Akasema mama Aisha: vizuri. Akasema: tuache sisi na wao mpaka tukutane na Mola wetu Mtukufu. [Ahmad katika Musnad]
Na kutoka kwa Rifaa Ibn Shaddad amesema: Nilikuwa nasimama kwenye kichwa cha Al- Mukhtar, uliponibainikia uwongo wake wallahi nikaanza kuuchomoa upanga wangu kwa ajili ya kulipiga shingo lake ili kumuuwa, mpaka nilipoikumbuka hadithi aliyonihadithia Amru Bin Al Humq aliposema: Nilimsikia Mtume S.A.W. anasema: "mwenye kumpa usalama mtu yeye mwenyewe kisha akamuua siku ya Qiyama atapewa bendera ya usaliti". [Ameitoa Hadithi hii Ahmad na Ib Maajah na wanazuoni wengine]. Na katika riwaya iliyofupishwa –Hakikutajwa kisa ndani yake- Na kwa Ibn Hiban: "Mtu yeyote amempa mtu usalama juu ya damu yake kisha akamuua, basi mimi niko mbali na muuwaji, hata kama alieuwawa atakuwa ni kafiri".
Na huyu tabii (Aliyekuja baada ya Maswahaba) mkweli Rifaa, umembainikia uwongo wa Al-Mukhtar na kwamba yeye alikuwa akidai utume mwisho mwa umri wake, akakaribia kumuuwa lakini kwa kuwa usalama wa Al Mukhtar ulikuwa katika damu yake, katika hali hii hakuweza kumuuwa.
Katika ufafanuzi uliopita, inabainika kwamba Salaf walikuwa wakichukua tahadhari iliyopokelewa katika Hadithi mfano wa Hadithi ya Abdallah Bin Umar aliposemea: alisema Mtume S.A.W. "Hakika msaliti, Mwenyezi Mungu atamnyooshea bendera siku ya Qiyama, itasemwa: eleweni, huu ni usaliti wa Fulani". [Bukhar na Muslim].
Uislamu umekuja ukiwa umekusanya mambo yote ya maisha, haukulifanya jambo la kutekeleza ahadi kwa wafuasi wake tu, bali umelipangilia swala la usalama kati ya waislamu na wengine, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi}. [AL MAIDA:1]
Na hii inakusanya kuyatekeleza yale yaliyopo kati yao, na yaliyopo kati yao na wengine, na akawaamrisha kutofuata hisia za ndani, na kufanya uadilifu hata kama itakuwa ni pamoja na adui, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda}.[ AL MAIDA:8]
Akawaamrisha kutowafanyia watu uadilifu kwa sababu tu ya chuki zao kwa watu hao, na hakuna shaka kuwa katika misingi muhimu ya uadilifu ni kutekeleza ahadi pamoja na watu wengine. Kama ambavyo pia Uislamu ulishuka ukiwa ni rehema kwa walimwengu wote, na hii inahitaji watu kuufahamu kwa kusikiliza Quraani tukufu, na kuzijuwa hukumu za Usilamu, anasema Allah Mtukufu: {Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu}. [ATAWBA:6].
Akiingia yeyote asiyekuwa Mwislamu katika miji ya waislamu kwa amani kwa lengo la kusikiliza Quraani au kwa lengo lingine inafaa kama vile biashara na mfano wake, ni wajibu kwa waislamu wote kumlinda yeye mwenyewe, mali yake na utu wake mpaka afikie mahala pake pa amani.
Na usalama ukiwa ni pamoja na taifa lisilokuwa la kiislamu haifai kulipiga vita isipokuwa baada ya kutangaza kwake kwa waislamu kuacha mkataba wakihofia miongoni mwao usaliti, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini}. [AL-ANFAAL:58].
Na kutoka kwa Sulaim Ibn Amir amesema: Kulikuwa na mkataba kati ya Muawiyah na Warumi, na alikuwa anakwenda katika nchi yao mpaka ulipomalizika mkataba akawavamia akatokezea mtu mmoja akiwa juu ya mnyama au juu ya farasi akiwa anasema: Allahu Akbar ahadi na sio usaliti. Kuangalia akawa ni Amrou Ibn Absah, Muawiyah akamuuliza kuhusu hilo, akasema: nilimsikia Mjumbe wa Allah S.A.W. anasema: "Atakaye kuwa kati yake na watu kuna mkataba wa amani basi asiubadilishe wala kuutengua mpaka limalizike lengo lake au wao kutupilia mbali mkataba au kuwaambia kuwa amevunja mkataba huo kwa kuhofia usaliti na ili awe mgomvi wake pamoja naye sawa katika kuuvunja mkataba huo". Akasema: Muawaiyah akarejea pamoja na watu waliokuwa naye. [Abou Dawud na El Tirmidhiy na akasema: Hadithi hii ni Hassan na ni sahihi].
Na usalama ukiwekwa na mwislamu basi ni wajibu kwa waislamu wote kuyafanyia kazi yaliyomo ndani yake, sawa sawa uwe unatokea kwa mtu dhalili au mtu mkubwa, mwanaume au mwanamke. Na zimepokelewa Hadithi katika hayo, kama ilivyopokelewa kutoka kwa mama Haniy mtoto wa Abi Taalib aliposema: "Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mtoto wa mama Ali Ibn Taalib alidai kuwa alipigana na mtu aliye msaidia fulani Ibn Hubayrah. Akasema Mtume S.A.W. tumemsaidia uliyemsaidia ewe mama Haniy". [wamekubaliana Maimamu wawili Bukhari na Muslimu]. Na kwa Abi Daud: "Tumemsaidia uliyemsaidia na tumempa usalama uliyempa usalama".
Na kwa Al Tirmidhiy: "Tumempa usalama uliyempa usalama". Akasema Al Tirmidhiy: Hadithi hii ni (Hassan) nzuri na Sahihi. Na katika kuifanyia kazi juu ya jambo hili kwa wanachuoni, wamejuzisha kumpa usalama mwanamke, na hii ni kauli ya Ahmad, na amejuzisha Is-haaq kumpa usalama mwanamke na mtumwa….
Imepokelewa kutoka kwa Umar Ibn Khatab R.A. kuwa yeye alijuzisha kumpa usalama mtumwa. Na imepokelewa kutoka kwa Ali bin Abi Twalib R.A. na Abdillahi bin Amru kutoka kwa Mtume S.A.W. alisema: "Mkataba wa mwislamu mmoja unaenea kwa wote". (Maana yake mwislamu mmoja akiwekeana mkataba na mtu basi ni wajibu kwa waislamu wote kuufuata mkataba huo). Akasema Al Tirmidhiy: Na maana ya hili kwa wanazuoni ni kwamba atakaye toa usalama katika waislamu basi inajuzu kwa wote kuufuata.
Na akasema Al Badru El-ainiy: Na katika fiqhi iliyomo ndani yake ni kujuzu usalama wa mwanamke na kwamba aliyepewa usalama na mwanamke ni haramu kumuuwa, na Zyanab bint ya Mtume S.A.W. alimpa ujirani Aba Al A’a si bin El Rabii, na hayo ndiyo wanayokwenda nayo kundi kubwa la wanachuoni wa Hijaz na Iraq, miongoni mwao ni Malik, Hanifah, Al shaafiy, Ahmad na Abu Thaur na Is-haak, nayo ni kauli ya El thauriy na El Auzaiyy. [Umdat Al Qaariy 15/93, Ch. ya Ihyaa El Turaath El Arabiy].
Na kutoka kwa mama Aisha R.A. anasema: Ikiwa mwanamke anauwezo wa kuwapa ujirani waumini basi inajuzu. [Abu Daud].
Na kutoka kwa Ali kwamba Mtume S.A.W. alisema: ((Waumini damu zao ziko sawa na wao ni kitu kimoja kwa mwengine asiyekuwa wao na mkataba wao unawaendea watu wengine, zindukeni, muumini hauwawi kwa kafiri na wala mwenye mkataba katika mkataba wake)). [Ahmad na Abu Dawud na Al Nisaiy, na ameitoa Hadithi hii pia Ahmad na Abu Dawud kutoka kwa Amru Bin Shuaib kutoka kwa baba yake na kutoka kwa babu yake].
Amesema Ibn Abdil Barr: “Maana ya kauli yake: "mkataba wao unawaendea watu wengine" ni kwamba kila mwislamu aliempa usalama mmoja wa wapiganaji basi unajuzu usalama wake, akiwa muovu au mwema, mwamume au mwanamke, mtumwa au mtu huru, na katika hili kuna hoja juu ya yule ambaye hakujuzisha usalama wa mwanamke na usalama wa mtumwa”. [al istidhikar 2/263, chapa ya Dar el kutub el aalamiyah].
Ikiwa kumpa mtu usalama inajuzu au kufaa kwa upande wa mtu mmoja raia akiwa mwanaume au mwanamke, mtu huru au mtumwa, itakuwa ni bora zaidi kujuzu kwa viongozi na wakuu wa nchi, na hata kwa Rais wa nchi yeye mwenyewe, na hiyo inakuwa kwa sasa ni sawa na kutoa viza ya kuingia kwenye hati ya kusafiria iliyogongwa muhuri wa nchi husika, na imeandikwa ndani yake kuwa nchi hiyo inamruhusu mwenye viza hii kuingia katika ardhi zake na kuishi humo kwa muda maalumu uliopangwa.
Amesma Al Nawawiy: “Maslahi ya usalama yanaweza kulazimu au kupelekea kujivutia kwenye Uislamu, au kulipumzisha jeshi, au kupangilia mambo yao, au kwa haja ya kuingia makafiri, au kwa fitna na vitu vingine, na umegawanyika katika ujumla nao ni ule unaohusiana na watu wa jimbo au mji, nao ni mkataba wa kusimamisha vita au kusuluhisha, na anahusika nao Imamu na magavana wake, maelezo yake yatakuja katika mlango wake inshaa Allah- na umegawanyika katika maalumu pia nao ni ule unaohusiana na mtu binafsi. Na inafaa kwa watawala na watu binafsi”. [ Raudat Taalibiyna ya Al Nawawiy 10/278, chapa ya Maktab Al Islam].
Amesema Al Buhutiy “Unafaa usalama (wa Imamu kwa washirikina wote) kutokana na kuenea kwa utawala wake , na unafaa usalama (kutoka kwa Amiri kwa watu wa mji aliyewawekea usalama mbele yao) kwa kuenea utawala wake katika kupigana nao. Ama kwa upande wa watu wengine ni kama vile mwislamu binafsi. Na inafaa (kwa kila mmoja) unaofaa usalama wake (kwa msafara na lindo dogo kutokana na mazoea). Na Ibn Al Banaa akachagua kwa kusema kama vile mia na chini ya hapo. Kama ikiwa kwa watu wa mji, kijiji au mkoa au mkusanyiko mkubwa haiwezi kufaa bila ya Imamu au makamo wake kwa kuwahifadhi. Kwa sababu inapelekea kuvuruga au kuzoretesha jihadi au kuwazulia uongo”. [sharhu muntaha el iraadaat 1/652, chapa ya Aalami al kutub].
Amesema Al Kassaniy: “Na pia kwa mwanaume hakuna masharti, unafaa usalama wa mwanamke, kwa kuwa kutokana na kuwa na akili hatashindwa kujua upande wa udhaifu na nguvu. Imepokelewa kuwa Bibi Zaynab binti ya Mtume S.A.W. alimpa usalama mume wake Aba Al Asi R.A., na Mtume akajuzisha usalama wake, na pia usalama kwa upofu, na kwa maradhi ya muda mrefu na maradhi ya kawaida, sio sharti, unakuwa usalama wa kipofu au mgonjwa wa muda mrefu au mgonjwa wa kaiwaida, kwa kuwa asili ni katika usahihi wa usalama ni kutoka kwake kwenye mtazamo katika mazingira yaliyofichikana kutokana na udhaifu na nguvu, na dalili hazichafui lolote, na haifai usalama wa tajiri katika Mji wa vita, na mateka akiwa ndani yake, na mpiga vita aliyesilimu huko, kwa kuwa kwao si wenye kusimama juu ya mazingira ya wapiganaji kutokana na uwezo na udahifu, hawafahamu kama usalama unafaida, kwa kuwa wanatuhumiwa katika haki za wapiganaji, kwa kuwa wao wametenzwa nguvu katika mikono ya makafiri, pia kundi la watu sio sharti, inafaa usalama wa mtu mmoja, kwa kauli yake S.A.W. (Mkataba wao unaenea kwa wote au wengine)), na kwa kuwa kusimamia katika mazingira ya uwezo na udhaifu hakuyategemei maoni ya kundi, inasihi kwa mtu mmoja na iwe usalama huo ni wa kundi liwe kubwa au dogo. Au watu wa mji au kijiji, pia inajuzu”. [Badaiu Al saaniu 6/107, Ch. Maktabat El Elmiyah].
Kama usalama utasainiwa na Imamu au na mtu mwingine kwa sharti, ni wajibu juu ya waislamu wote kuutekeleza. Haijuzu kuzifanyia uadui roho zao, mali zao na nafsi zao kinyume cha sheria. Amesema sheikh Al Dar diyr: “Na utakapo sainiwa usalama na Imamu au na mtu mwingine kwa sharti (Ni wajibu) kwa waislamu wote (Kuutekeleza) na haijuzu kuwateka wala kuchukua chochote katika mali zao ispokuwa kwa njia ya kisheria wala kuwaudhi kinyume cha sharia haisihi”. [Al sharh Al saghir 2/288, chapa. Dar el maarif].
Na akasema Al nawawiy: “Unapofanyika mkataba wa usalama, anakuwa muumini amehifadhika na kuuwa na kuteka, laiti akiuwa, amesema Imamu: Kwetu sisi tuonavyo atadhamini kile anachodhaminiwa dhimmiyu (Mtu aliyechini ya himaya yetu), nayo ni lazima kwa upande wa wailsamu”.
[Raudat al talibiin lilnawawiy 10/281, Ch.. Al Maktab Al Islamiy].
Ama mambo yanayotumika kuuandaa mkataba wa usalama ni yale yote yanayojulisha jambo hilo, kama vile matamshi ya wazi kwa mfano “Wewe uko katika usalama” au kinaya (fumbo) “ Wewe upo juu ya yale unayoyapenda”. Au ishara yenye kufahamika; kwa kuwa Uislamu umetilia mkazo ulinzi wa maisha ya watu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.} [AL MAIDA: 32]
Amesema sheikh Zakaria Al Answaariy “ (Unasihi mkataba) wa usalama (Kwa maneno ya wazi kama vile nimekupa ujirani, nimekupa usalama, na wewe ni jirani), wewe (Una usalama na hakuna shaka juu yako, usiogope, wala usifadhaike , usiwe na hofu, n,k. (Na kwa lugha ya mafumbo kama vile upo katika yale unayo yapenda, kuwa utakavyo, na mfano wake) kama aliyetajwa kwa kauli yake: (Na kwa kuandika) (Na kwa kumtumia) yaani mwislamu aliyetajwa ni mwenye kupewa jukumu (Na laiti akiwa kafiri na kutoa maoni yake kwa jeuri) kama kauli yake: Akija Zaid nimekupa usalama kwa kujenga mlango kwa kuupanua (Na kwa ishara yenye kufahamika hata kama ikiwa ni kwa mtu anayeongea) lakini itazingatiwa kuwa ni lugha ya mafumbo kutoka kwa bubu na mtu makini ahusike katika kumfahamu anachokikusudia, ikiwa atamfahamu yeyote Yule basi itafahamika kama ni maneno ya wazi…(Ikiwa mwislamu atamwashiria kafiri akahisi ni usalama wake) kwa kuashiria kwake (Akatujia na mwislamu akakataa) kuwa alimpa usalama (Au alimpa usalama mtoto na mfano wake) katika wale ambao usalama wao hausihi ( na akahisi kusihi kwake) yaani usalama (tutamfikishia au tutampatia usalama wake) wala hatumuuwi kwa kudharurika kwake….(Akifa mwenye kuashiria kabla ya kubainisha hakuna amani na hakuna kuuwawa) atapatiwa usalama wake”. [Asanaa Al Mataalib sharh Raud el taalib 4/203, Ch, Dar El Kitaab El Islamiy].
Amesema Ibn Qudamah:” Alisema Umar R.A. naapa kwa Allah laiti mmoja ameashiria kwa kidole chake angani kwa mshirikina akashuka kwa usalama wake na akamuuwa basi ningemuuwa, imepokelewa na Said. Na akifa mwislamu au akapotea hakika wao watarudishwa kwenye usalama wao, na haya ndiyo aliyoyasema Malik, Al Shaafii na Ibn El Mundhir, ikisemwa: Na vipi mmeufanya usalama kuwa sahihi kwa ishara pamoja na kuwa na uwezo wa kutamka tofauti na kuuza, kutoa talaka na kumuacha huru mtumwa? Tutasema: Ni kwa ajili ya umuhimu wa jambo la kuhifadhi damu ya mtu kama kuhifadhi damu ya mtu mwenye mfano wa maandishi ili kulinda maisha yake; Na kwa kuwa makafiri mara nyingi hawafahamu maneno ya waislamu, na waislamu hawafahamu maneno yao, mazingira yakapelekea kuongea kwa ishara kinyume na mtu mwengine”. [Al Mughniy 9/323, Ch. Makatbat El Qahirah, na Asanaa Al Mataalib Sharh Raud El Twaalib 4/203, Ch. Dar El Kitaab El Islamiy]
Na mwenye kuomba usalama atapewa usalama kwa sharti la kutoleta madhara au kuwepo maslahi kwa waislamu.
Amesema Al Buhutiy. “(na) Inashurutishwa katika usalama (kutosababisha madhara juu yetu) kwa kuwapa usalama makafiri”. [Kashaaf El Qinaa 3/104, Ch., Dar El Fikr]
Amesema sheikh Al Dardiir: “Kisha sharti la usalama (Ikiwa haikuwadhuru) waislamu kwa kuwa ndani yake maslahi au yako sawa maslahi yao na kutosababisha madhara, ikiwa atawadhuru waislamu ni wajibu kuuvunja mkataba huo wa usalama”. [ Al Sharh Al Kabiir 2/186, Ch. Dar El Fikr].
Haya yaliyoelezwa mara nyingi ni kwa ajili ya wapiganaji wa kivita wanapoingia katika nchi ya Kiislamu kwa amani, ni bora zaidi kwa ambao kati yetu na wao kuna mkataba, asili kwao itakuwa ni kuwapa usalama kabla ya kuingia, kwa ajili hiyo wao ni bora kwa hukumu hizi kuliko wapiganaji.
Na kwa mujibu wa hayo: Hakika viza ya kuingia ina hukumu ya mkataba wa usalama, ni haramu kuwaudhi wapiganaji watakapoingia kwa viza, na ni bora zaidi kwa mwenye mkataba. Kama ambavyo mahusiano ya kidiplomasia na kufungua balozi kati ya nchi na nchi nyingine ni sawa na mkataba, haihitajiki hapo baadae kuwekeana mkataba mwingine wa amani, na katika hali ya mataifa kuwa yanayopigana vita basi mkataba wa kusitisha vita ni aina ya mkataba wa usalama.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas